Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.

Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.

Kwa hiyo kama mtu hajui Kiingereza na Kiswahili vizuri maanake hana fikra pevu?!
Hizi fikra zipo mahali kwingi hapa duniani na si kwako peke yako!
Ni mawazo ya watu waliokuzwa kwenye misingi ya RECIPROCITY....
Huwezi kueleweka kwamba Umaskini wetu hadi leo ni kwa sababu ya Nyerere.....
Amewaachia kila kitu mkakihamishia nje ya nchi!
Aliwafunza uzalendo mkawa mafisadi-japo mnazidiana viwango!
Nyerere ni mzazi bora ambaye kaacha urithi japo watoto wameanza kuutapanya!
Wanaishia kumlaumu kwamba ni heri angaliwaacha patupu!
Hayo ndo matunda ya kuongozwa na CCM!
No future!
 
We mpuuzi Muhamad amefikaje huku sio makosa yako una akili ya kuvuka barabara tu huna lazaidi :focus:

Ni mfano hai tuu wa watu walioshindwa weka misingi....kuongezea tuu .Muhamad was worse..hakuandaa warithi, nyerere alimuanda mwinyi, alisomesha watu, aliwaapa maelekezo mali zao wasiingie nazo duniani kw amanyang`au km hawajui ni cha kufanya na jinsi gani ya kukifanya...
 
Hauna akili wala hujui kilichokufikisha hapo ulipo wewe uliyesoma bure na umeshindwa kufanya kitu chochote unamlaumu nyerere aliyepokea nchi ikiwa haina wasomi wakusaidiana naye. Hata watoto wako siku moja watakukana kuwa na mzazi mbumbumbu kama wewe copy chama

Nyie maccm mnaanza kunyukana wenyewe kwa wenyewe....Kwani huyu Faizafoxy si kambi moja na wewe....Kwi kwi kwi ......Lumumba project bana...
 
Last edited by a moderator:
Hata wewe uwezo wako wa kufikiri ni mdogo Sana, sijui unafanwya makusudi au umeamua kujivalisha ujuha na kupost nonsense humu.
1. Tangu mwalimu aachie madaraka mwaka 1985 we we hujui tu ni matatizo gani yanayoikabili nchi yako? Zinakutosha kweli wewe?2. Unataka tumjadili mwalimu ili nchi hii iendelee? Kwani sisi wenyewe hatuwezi kujikndoa hapa tulipo? Nchi zinazokua kiuchumi kwa sasa unafikiri zina wanafiki wengi kama Tz?
3. Kama ulijengewa nyumba mbovu bomoa name jenga mpya acha kulia lia na kumsingizia marehemu.
sikubaliani na wewe.hapa ndipo watanzania wanapotea maboya.usipojua chanzo cha ugonjwa kamwe huwezi kuutibu!!!!hakika utakufa tu.huwezi kamwe kumtenganisha nyerere na matatizo ya nchi hii.ukoo wa panya ulitengezwa na nani???tuwe wakweli jamani.mficha uchi hazai.alikuwa na kawaida ya kusema :CCM INA WENYEWE.HAWA "WENYEWE" NI AKINA NANI???tafakari.

 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Mimi nilifikiri ccm zamani TANU ndio wameshindwa kufuata misingi yao ! Kumbe kulikuwa na chama kingine kunachoitwa Nyerere! Shukrani kwa kunijuza
 
Tumjadili kikwete ndo yuko madarakani kwa sasa. Kwanini tumjadili marehemu? Sababu zako ni finyu sana.
Yeye alikuwa kiongozi wa taifa letu. Kumzungumzia katika yale aliyofanya kupitia uongozi wake ndio kinachopaswa kuzungumzwa. Lengo likiwa ni kujifunza na kuchukua tahadhari alikoteleza tusijeteleza na alikopatia tuige ili kuendeleza nchi yetu. Uislamu umeweka wazi mlango huo wa kutahadharishana makosa ya viongozi ili watu wasijeshika njia isiyo sahihi. Jambo la muhimu ni kumjadili kiongozi kwa njia ya uadilifu. Usimzulie wala kupita mipaka ukamtukana. Ukifanya hivyo utakuwa umemdhulumu.
 
Wanaleta hasira kama siyo nyerere hata saa hii ucku uhuru wa kuchat ungetoka wapi. Watu wengine ni kama mafurushi tu wamejikuta hapo walipo hawajui chochote.

Umeamua kumkana mwana ccm mwenzako Faizafoxy...Leo kada anakera ehhh!!!! Pathetic!!!
 
Kati ya wanafunzi wangu wewe ndio mjinga kuliko wote. kimsingi wewe huna hadhi ya kumjadili NYERERE hata kidogo.wewe unajua kusoma na kuandika tu na hujaelimika. huwezi kumjadili mtu wa hadhi ile hata kidogo.hata wazungu walio leta hii organized education, wasomi wa sayansi ya jamii na philosophy wanamuona Nyerere kama PHILOSOPHER OF ALL THE TIMES! Waandishi wa habari wa dunia nzima walikuwa wanaona fahari kumhoji maswali NYERERE siyo tu ili wasikie majibu yake bali walitegemea kupata maarifa mapya kutokana na majibu yake.

kinacho kupa kiburi cha kujiona unaweza kumjadili NYERERE mimi sijakiona,labda kwakuwa uko ccm na unapitapita kwenye ofisi alizo kuwa anapita NYERERE umeona una hadhi ya kumjadili.huna,huna huna hadhi hiyo hata kidogo. NAKUSHAURI FUTA UZI HUU MARA MOJA.

Unajua huyo dada anajenga hoja zake kwa misingi ya udini....Hilo ndo tatizo lake..
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Ni theme ya shule yako au umetumwa bila kujua unachokitafuta? Huoni kama unaleta kejeli ya kukosa fadhila na uelewa? Hiyo misingi sahihi kama unaijua aliyotakiwa kuwajengea ni ipi?
 
Mamndenyi
Hebu niulizie kwa huyu Red Giant ni kiongozi gani aliyemuona yeye amefaa sana maana naona matatioz ya kiuchumi ya nchi za kiafrika yanafanana na ukiangalia kwa undani watanzania tuna nafuu; pamoja na kulalamika eti Nyerere aliacha msingi mbovu lakini bado hatujaachwa sana; kwenye theory za uchumi sio kila ulichoinvest leo unakivuna kesho matunda mengine yanaonekana baada ya miaka 30
hapa ndio tunakose sana. tunaweka malengo yetu huku nchi za kiafrika ndo zikiwa reference zetu .yaani hatufikiri tunataka nini ila tunafikiri tunataka kufanana na nani.
 
Maendeleo ni watu sio VITU, pengine kwa FIKRA zako ulitaka aache vitu. Jeshi la Wananchi( JWTZ), JKT, Usalama wa taifa wenye tija na ufanisi na Jeshi la Polisi lisilo kula rushwa, Mahakama yenye watumishi waadilifu, taasisi za elimu zenye kutoa wasomi wa kweli ( 92% ya wananchi walikuwa wanajua kusoma na kuandika. ''leo 69%). Taasisi za fedha imara(NIC,NBC). Aliwasaidia watu kujitambua na kutambua kazi ndio kipimo cha utu( UHURU NI KAZI). Amani na utulivu, alijitahidi kuutokomeza ukabila na udini, aliisadia tz na watz kuwa watu wenye kuheshimika duniani kimichezo(tuling'ara kwenye michezo ya riadha, ngumi na soka). Pengine una hasira binafsi na MWL ndio maana hukutufahamisha misingi ambayo hakuijenga ni ipi.
 
Mkuu unawasiwasi na utawala wa mwalimu? Kwa dhati ya moyo wangu ndiyoooo alitekeleza japoa kasoro ndogodogo

hazikosi, lakini mambo yalibadilika kwa kasi alipong'atuka madarakani.



Nimekata hii paragraph ya Mwanamutapa hapa chini nimeipenda kwa kweli tena sana tu.
mwalimu alikuwa na mawazo mazuri sana tena sana. ila hakuwez a kuhakikisha yanaendelezwa na kuoboreshwa leo nch i k am a ch in a , north korea na marekani zote zinasimamia misingi ya kuundwa kwao. ni sisi tu tunaoyumba yumba KAma bendera.
 
Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.

Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.

Ila Faiza kiingereza/kiswahili sre just medium of communication,someone can use signal not talk even a word ujumbe ukafika .Hivyo izo lugha mbili zisiwe issue kikubwa ni ujibu hoja zake sasa kama wewe mleta bandiko ndo unajibizana hivi unategemea nini kutoka kwa wachangiaji wengine?
 
Na awa makanjanja wanaoingia mikataba mibovu, walioficha pesa nje, wala rushwa, wauzaji madawa ya kulevya. Etc
Tumuache mzee apumzike
 
Unapotaka kufananisha mtu aliyekaa madarakani miaka 23 na aliyekaa miaka 8 unaonyesha ukosefu wa upeo, lakini hata utakapoamua kufanya hivyo kwa kutumia vitu vinavyopimika utaona aibu mwenyewe.

Mwalimu hayupo, lakini maadui zake bado wameendelea kumshambulia. Sasa hivi maadui wa Mwalimu wanataka kuleta serikali tatu ili kuangusha nguzo ya mwisho ya legacy yake. Sijui watu hawa wananufaika vipi na chuki waliyo nayo kwa Mwalimu!

wewe kweli janga!tunaweza kumfananisha wa 23 na 8 kwa kuangalia uyo wa muda mrefu kaleta faida/hasara gani na uyo wa 8 ambaye kwa kipindi kifupi tu kaleta majanga yasovumilika hadi tunaanza kuuana kwa misingi ya udini yaanai ndo unaemsifia poooooh!Hii miwili ilobaki ateleta ajabu zipi?Ila naona dalili kwamba mnaanza kunyundana wenyewe kwa wenyewe vita vyenu ni furaha yetu.
 
kwa mujib wa iman ya dini ya mnyaazmung tumeamrishwa kuwaombea marhun ili warehemike na kuiona pepo.
marhum jk alikuwa muasis wa chama chetu na alio waandaa ndo hao waliomtanguliza kuzim kabla maulana hajamkurubisha,naomba wana ccm haswa waumin wa dini ya mnyaaz tuungane kumwombea pepo.
 
Gharama ya kubomoa mtaiweza? Ni bora tukae kwenye nyumba yetu ya urithi ya udongo kuliko kubomoa bila kuwa na uhakika wa gharama ya kujenga mpya.

Tunaiweza. Kwani tuna kila rasilimali inayohitajika kujenga upya msingi na nymba. Suala lililobaki ni watanzania kuamua (kama kutakuwa na usawa na haki katika kuchagua mafundi) kama wako tayari kuanza kujenga upya msingi wa nyumba yao.
 
Huwa nasema kila siku, kuendelea kumlaumu Nyerere hakutusaidii kitu, cha msingi ni kuangalia wapi alikosea na turekebishe au tufanye tofauti kwa ubora zaidi.

Hata yeye mwenyewe alishasema, serikali yake ilifanya mambo mazuri lakini pia walifanya yakijinga tena mengi tu ila kilichomshangaza ni kuona waliomfuata wakiyaacha mambo mazuri ya msingi na kuendeleza ya kijinga.

Chifu, tatizo ni kwamba mafundi ya nyumba yetu wamechemsha mno sasa. Ili kujionyesha kwamba kuchemsha kwao hakujasababishwa nao; wanafanya kampeni ya kumchafua Mwalimu.
 
Back
Top Bottom