Ndio nini hicho? au Kiswahili ni lugha adimu kwako?
Unatakiwa kujibu hoja, kama unataka kufundisha lugha badili kichwa (title cha hoja yako) mjinga wewe
Ndio nini hicho? au Kiswahili ni lugha adimu kwako?
Siyo kweli! Mwalimu was right,hata kama alifanya makosa ni madogo kulinganisha na huyu chekibobu!
marekebisho yake ni azimio la zanzibar?kama sikosei!
...kwa hiyo tangu Nyerere aondoke watanzania tunachagua mafundi paa wakato hata msingi wa nyumba hakuna? mnaanza kuropoka taratibu mtajikuta mnajitukana wenyewe.Mkuu, unaelewa maana ya MSINGI lakini?
Fundi paa anaweza kuweka msingi?
Oh .. kumbe leo Ijumaa .. the day of rage!
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.
Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.
How many people had access to right information?
Kulikuwa na magazeti mangapi? Yalikuwa yanamilikiwa na nani?
Usiposikia kitu haimaanishi kuwa hakipo, wake up.
Sio kwamba alikuwa hana muuono; baada ya 9/12/1962 Baba wa taifa alikuwa na muuono wa kuendelea lakini sio kwa Tanganyika tu bali kwa kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa Ujumla (Umajumui wa kiafrika) ambapo yeye alikuwa tayari hata kutumia rasilimali za nchi yake kupigania muungano wa Afrika Mashariki na hatimaye Afrika kitu ambacho wenzake hawakunacho na daima hakukiona kwao yeye alizidi kutumia rasilimali zetu kupigania wengine wakati taifa likiwa halina cha kututosheleza kitu ambacho kilituangusha sana hasa pale ambapo hata lile soko dogo la bidhaa zetu lilipoanguka hatukuwa na namna ya kufanya biashara yoyote kwa ufanisi na vita iliyofuata ambayo ilitumaliza kabisa kiuchumi ambapo inasemekana aliposema miezi kumi na nane ya kufunga mkanda alificha uhalisia ambapo ilikuwa ni miaka 18 ya kufunga mkanda!
Kiukweli Mwalimu alijenga misingi thabiti ya uongozi katika nchi hii na kuisimamia vilivyo kuliko kiongozi yeyote katika historia ya nchi hii hadi leo. alituunganisha watanzania wote akiwa na nia ya kutengeneza taifa la Tanzania na sio vitaifa vidogo vidogo ndani ya Tanzania. Alisimamia thabiti upatikaji wa elimu hadi kwa watu wazima kiasi kwamba Tanzania ikaongoza Afrika kwa watu wanojua kusoma na kuandika na mengineyo mengi...
Kwa namwona Nyerere kama kiongozi jasiri mwenye kukemea pasipo kujali wewe nani na aliye kiri wazi kuwa anaondoka madarakani baada ya kuona kuwa sera zake zimeshindwa na hakuwa tayari kuzipa nafasi sera kandamizi za kimagharibi akiwa yeye madarakani akaona bora apishe mtazamo mpya.Ni kiongozi gani Afrika anayeweza leo kufanya hivi?
Kimapungufu Mwalimu alibana sana uhuru wa kujieleza hadi ikafika mahali kukosoa serikali ilikuwa kama kufuru, aliweka kizuizini waliotofutiana na mitazamo yake, na hakuweza tambua haki za binadamu katika katiba ya nchi, aliifanya serikali na viongozi wake waogopwe na watu na hakuruhusu juhudi binafsi na ubunifu katika kutafuta maendeleo.
Zaidi ya yote ndo maana kaitwa Mwalimu anatufundisha na sisi tunaiga kwake; hivyo tuyaige yale yake mazuri na kuachane na yale mabaya aliyotenda enzi za utawala wake!
NAWASILISHA HOJA!
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
ZeMarcopolo
1. By that time what was the level of technology and can you distinguish this with reference to other African nations? especially nearby countries? otherwise your argument is not balanced
2. With question one above are we still in the same level with the countries you have mentioned above if not why?
Can you discuss this with reference to Kenya, Uganda and Rwanda to support your argument if is valid and was not the same?
Things and events happen with time, as the result civilization and development become the outcome, do not get fool at a fixed position as life and everything changes with respect to time subject to human level of adaptation to his/her environments
Nadhani umepoteza dhana halisi ya maisha yako, ya babu na babu wa bibi yako nadhalia asilia ya wapi ulikotoka na maendeleoa kiuchumi nk.
Je babu wa babu na babu yako alikuwa dini gani? uislam au ukristu umekuja hivi karibuni lakini babu zetu zama zile waliishi kwa imani zao na maisha yalienda.
Hebu tuambie kwanini hulalami kwamba
1. walikula matunda mabichi, mizizi na hawakuswali wala kutawaza nani aliweka misingi ya maisha yao? Nyerere?
2. kama walifanya makosa mbona FaizaFoxy umestaarabika na kumgeukia mtume? vipi hujabaki kulalama kwa wale wasiojuwa kutawaza wala kuenda misikitini?
Wewe mwanamke FaizaFoxy nimpumbavu unaendeshwa na kuwashwa na udini! chuki za kijinga
zisizo na base wala misingi yoyote zaidi ya unafiki na ufedhuli kufanya uchochezi watu waanze malumbano yasiyo natija.
Huwezi kujadili challenge za nchi zilizoko kwa sasa na kuangalia positive solution za miaka ijayo bila kuangalia historia ya matukio ya zamani na jinsi yalivyoshughulikiwa kwa sababu kutokufanya hivyo, kutakuwa na uwezekano wa kufanya makosa yaleyale.
Utawala wa Mwl. Nyerere ni mojawapo ya historia ya nchi yetu na katika utawala huo kuna mambo mengi mazuri na mabaya ya kujifunza ili tupate solution ya matatizo yaliyopo na yajayo. Maendeleo yoyote yale chanya mara nyingi yanapatikana kwa kujua udhaifu wa kilichoko na hasa tangu kilipoanzishwa na kutafuta solution ya kukibadilisha katika hali chanya.
Historia ya taifa letu ipo kwa ajiri ya kutuasaidia kujitambua wapi tumetoka na pia inatusaidia kufahamu mabadiliko yaliyotokea kama ni mazuri au mabaya. Ndiyo maana hata Katiba tunayohangaika kuitafuta kama taifa, misingi yake mikuu imekuwa based on our Nation history.
Mbona kuna watu huwa wanapandwa na midadi na hasira pale tu historia ya utawala wa Mwl. Nyerere inapoangaliwa katika macho hasi lakini ni hao hao pia wanapatwa na furaha sana pale inapoangaliwa katika macho chana.
Kama yeye mwenyewe alishawahi kusema kuwa hakuwa "malaika", kwa nini baadhi ya watu wanataka jamii imuone kama alikuwa "malaika" katika macho ya kinafiki. Tujenge nguvu ya hoja na siyo hoja za nguvu kama baadhi ya watu wanavyopenda iwe.
Jamii bado inaangalia na kuzichambua athari za vita vya dunia (1,2) na pia athari ya utawala wa Adolf Hitler kama ilivyo kwa watanzania ambao wanaangalia na kuzichambua athari za kikoloni katika dunia na hii ikiwa ni pamoja na Tanzania. Why not Mwl. Nyerere legacy?.
We can't have Mwl. Nyerere positive legacy without having negative legacy. Huu ndiyo ukweli. Let's talk openy as Jf motto.
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
kuna kitu nimejifunza hivi karibuni harafu nimekikubali sana kwamba raia wa kawaida hajali nani anatawawala ikulu anachojali ni mkate uwpo mezani. je nyerere alihakikisha kwamba hata yeye akiondoka madarakani watanzania wanapata mkate kama kawaida?. hapana aliweka maZingira kwamba mwinyi akija nae atumie utashi wake. hakuweka misingi imara na thabiti ambayo kama nchi tulitakiwa kufuata kama waLIvyfofanya china. ni kana kwamba alijua atatawala milele hivyo hakuandaa watu wa kuendeleza mawazo yake ambayo from my heart nakubali yalikuwa mazuri kwa nchi maskini kama yetu (nchi maskini zinafaa ujamaa lakini tajiri inafaa ubepariHebu fafanua tuijadili vizuri hapo kwenye red, mimi naanza halafu wewe pinga hoja zangu......tujadiliane.
-Madini
Alikuachieni tena kwa ahadi kwamba mtavuna mkiwa teyari
-Elimu
wakati wake JK Nyerere, japo walifaidika wachache lakini wote masikini kwa matajiri walisoma shule za aina moja na waliofaulu waliendelezwa mpaka mwisho, leo hii watu binadamu fedha, walalahoi shule za kata hakuna chochote....
-Dawa za kulevya,
Wakati wa nyerere mlipata kusikia ujinga wa madawa haya kama ilivyo sasa na jinsi watanzania wanavyoteketea?
-Afya,
Pamoja na uchache wa dhahati na vituo vya afya, ukienda kutibiwa unapata dawa za uhakika, bure wahudumu na madakitari walifundwa na walikuwa wazalendo wa kweli.
-Polisi, jeshi na usalama wa raia,
Wakati wa Nyerere vikosi hivi vilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, uzalendo na ushilikiano kwa raia, walihifadhi siri za serikali kwa umakini mkubwa leo hii kila kitu ni upuuzi tu
-Mbuga za wanyama na maliasili
Mliwahi kusikia meli kusafilisha meno ya tembo?, Ndege kubebe twiga, Loliondo kupigwa mnada na akina Katabalo kuuwawa?
-Udini na mshikamano miongoni mwa raia wa tanzania
Mliwahikusikia watu kugawanyika kama ilivyo sasa kwa mitazamo ya udini, ukabila na ukanda? (Tulisifika duniani kote kwa jina moja - tuliitana Ndugu FaizaFoxy, Ndugu Red Giant nk)
Mnataka misingigani nyinyi??? unaweza kumpeleka punda hadi mtoni lakini jukum la kunywa au asinywe maji linabaki kuwa hiari yake sio mchungaji.
Kimsingi siasa yetu imebadilika. Siasa za siku hizi zinahitaji kiongozi kuinvest kwenye kupendwa na watu.
Mwanasiasa wa leo can not afford too many enemies, anatakiwa kujenga kundi la "marafiki". Hapo ndipo mambo yanapoharibika, kwa sababu kwenye urafiki kuna "kuvumiliana" na kuoneana aibu. Nakumbuka Nyerere alisema mtu akienda Ikulu inabidi awaambie marafiki zake kuwa Ikulu ni mahala patakatifu,a. Kuwageuka marafiki hao baada ya kuingia Ikulu is a political suicide.that is not practical today kwa sababu bila kuwa na hao marafiki watakaompigania hata Ikulu mtu hawezi kuiwaz
Nyerere hakuhitaji "kambi" ndani ya chama ili aendelee kuwa kiongozi ili ashinde uchaguzi. Siku hizi bila kuwa na "kambi" mgombea haambulii kitu.
Kwahiyo si sahihi viongozi hawa kuwafananisha kwa kutumia jedwali. By the way, kifalsafa hawa wote ni viongozi wa mfumo uleule. Mfumo wetu wa uongozi tangu Uhuru kimsingi haujabadilika
Mkuu, umesema kweli.
Ninachoona mimi ni UNAFIKI kwa watu wetu. Mashabiki wa serikali tatu ndio haohapo wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Wanaonunua kura wakati wa uchaguzi ndio haohao wanajifanya kupigania legacy ya Mwalimu. Vinara wa kuomba misaada nje ya nchi ndio haohao wanaojidai kupigania legacy ya Mwalimu. Mabepari ndio hao hao wanaojifanya kupigania legacy ya Mwalimu.
Huu ni UNAFIKI.
Huwezi kusema ugombei Urais mpaka uahidiwe pesa nono kama mshahara wa mbunge halafu ukajifanya unapigania legacy ya Mwalimu.
Huwezi kusema chama chako hakihitaji wanachama Zanzibar halafu ukajidai unapigania legacy ya Mwalimu.
Lets be true,
Legacy gani ya Mwalimu tunaishi nayo leo?