Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Wanaleta hasira kama siyo nyerere hata saa hii ucku uhuru wa kuchat ungetoka wapi. Watu wengine ni kama mafurushi tu wamejikuta hapo walipo hawajui chochote.

Nakubaliana nawewe 100%, kunamambo yapo wazi kabisa hatuhitaji kukashifu vitu vinavyojieleza waziwazi.

Sisi tupingane na kuzodoana kwa vyama vyetu vya sasa na viongozi wetu wasasa ndiyo siazi yetu, mwalimu pamoja na mapungufu yake upeo, uwezo na misimamo yake haina wakumlinganisha na hawa wasasa, si waupinzani wala wa serikalini

Moja ya walimu wangu Prof. Masuha (marehem kwa sasa, mungu amlaze mahalapema peponi) - alimsimlia nyerere alivyowawezesha watoto wa maskini kupata elimu, yeye Prof. Masuha akiwa mmojawapo kwa hisia ya ajabu sana. Nakumbuka wakati wa msiba wa mwl JK pale mlimani maprof na maDr walilia sana tena hadharani, mmoja wapo namkumbuka ni Dr Mhiru, kilichowaliza si kingine ni uadilifu na utendaji wa mwalimu.

Nasikitika kusema kwamba tumekuwa na kizazi kisicho na shukrani wa aibu kwa kuzusha na kushuhudia uwongo kwa watangulizi wetu hususani mwl JK Nyerere.
 
  • Thanks
Reactions: ral
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Sasa Jirani yetu KENYA chini ya MZEE JOMO KENYATTA alikuwa na MISINGI MAALUMU YA KUONGOZA? kumbuka kulikuwa na Mwanaukombozi kwa JINA LA DEDAN KIMATHI aliyekuwa na uhamasisho mkubwa kudai ARDHI yao iliyochukuliwa na MABEBERU wa kizungu ndio walioanzisha MAU MAU WAR; Kenyatta akapandikizwa

Kenya ikapata uhuru sababu ya Huyo Jamaa na Land Issue, Lakini Kenyatta land kidogo aliyopewa na wazungu aligawana na vizito wenzake wachache; wengine akawapa vibaraka Dedan Kimadhi akafa bila ARDHI

Kwa Nyerere Tanganyika ilitawaliwa na Wakoloni wawili MJERUMANI halafu MWINGEREZA wakati wa MWINGEREZA hakuwa anaijali sana Tanganyika na Maendeleo yake alikuwa anajua iko siku ataikosa atanyangány´wa kwahiyo pamoja na Tanganyika kuwa na Utajiri haikuendelezwa

Tanganyika ilikuwa na Makabila MENGI; DINI KIBAO;

Kwanza ukiangalia katika MAKABILA; Ni Mengi zaidi ya 250 lakini kuna 5 ambayo ni Makubwa na yana Machief na hayo pia yameendelea kielimu na yana mifumo bora sana ya ELIMU ukilinganisha na MAKABILA MENGINE

PILI DINI kulikuwa na Dini kuu kusema kuu ni Maana well established nchini ambazo zilikuwa tayari zina SHULE kuanzia PRIMARY HADI VYUO VYA UALIMU... Ukiangalia Shule za Utawala wa Mkoloni ambaye ni Mwingereza zilikuwa hazina huo mkondo Murua kama hizo shule za dini ni dini kama ya ROMAN CATHOLICS

LUGHA kwasababu ya makabila kibao. ingekuwa vigumu sana kuwasiliana kwenye nchi kubwa kama Tanganyika; South Africa hawana Makabila mengi kama sisi lakini wana 7 official national languages

ÆÆÆÆ Sasa Nyerere alipochukua UHURU kwanza alipendekeza LUGHA ya TAIFA kuwa KISWAHILI hivyo basi kila mtu lazima awe anaongea na ni lugha inayoongelewa Maeneo ya Pwani; kwahiyo haina mwenyewe... Pili kwasababu ya VYAMA VYA USHIRIKA enzi hizo vilikuwa na NGUVU kwa UPANDE wa hayo MAKABILA MAKUBWA akavunja Uongozi wa MILA --- Machief na Watemi wakaondolewa hii ilisaidia sana, sababu enzi hizo walikuwa na sauti kuliko hata Governor wa kikoloni sasa kama wangeachwa nchi ingekuwa labda bado Marais wanabadilishana toka Makabila Makubwa pekee... tusingeona Nyerere, Mkapa, Mwinyi na Kikwete wote toka Makabila Madogo wakiiongoza nchi hii...

Nyerere alitaifisha shule nyingi tu za DINI ili wanafunzi waweze kusoma bure elim ya msingi na walifanikiwa.... na UNAPOSEMA KUWA NYERERE ALIWEKWA MADARAKANI ni only yeye??? kwasababu alikuwa na watoto 9 watoto wake wooote walisome elimu ya Tanganyika hawakusomea ELIMU iliyokuwa inatolewa na SHULE za DINI. Watoto wake hawana Ma-Ph.D na hawafanyi kazi kwenye hizo kampuni zilizomuweka baba yao madarakani

Mwl Nyerere ni wa BUTIAMA; yeye na hao wanae hawakujenga International Airport Butiama; International PORT; au kupafanya BUTIAMA INTERNATIONAL FREE TRADE ZONE... Nyerere hakuwajengea Mahekalu wanae MBEZI BEACH; sasa kama kweli hao waliomweka madarakani walimtakia mema kwanini waliiacha familia yake OMBA OMBA???

Hakuna hata visenti USWISI kama wengine? Sasa kweli ni misingi gani Imara hadi leo unataka aiweke?

THE BEST PEDAGOGIST He did AZIMIO LA ARUSHA... lakini kila mtu aliyekua chini yake aliichambua kidogo kidogo kwasababu hawakulipenda...

wakaondoa nguzo 5 za uongozi, sasa ukaona viongozi wanamiliki makampuni na wanaingia nayo maofisini mwao; wanaajiri wake zao, wanauziana Majumba, hawakuishia hapo ikaishia kuwa it is not a police state... unaingiza madawa ya kulevya... wewe ni tajiri, wanaua viwanda wananchi wanakosa kazi kwahiyo ndio wateja wa hayo madawa ya kulevya

Lakini Mnaogopa kulaumiana.... Mnamkimbilia Mwl. Nyerere oh alikuwa akiendeshwa na waliomweka MADARAKANI!!! kweli hamuoni AIBU???

&&& Yaani ni kwanini Mwarabu wa Furniture Center katupiwa KEMIKALI...??? na nani kaenda kumuangalia South Africa --- Rais Kikwete... watu hawamuongelei vizuri huyo jamaa... ni jinsi anavyo operate jijini Dar...

Lakini wote mwafunga Macho.... Mwamwangalia Nyerere ati????
 
acha hayo mawazo mkuu, mapebari manaseek for the best. wote tunataka elimu bora, ila mwalimu hakutuakikishia tunaipataje (mapungufu). tumeshagundua kwamba ili tupate elimu bora tunahitaji pesa. sasa tunapigania mgawanyo sawa wa pesa za tanzania

Sasa Mkuu mbona tena hujatowa majibu kiongozi! pale chini kabisa nimekupa fursa kwa kijisentensi kwanini....Eleza.

quote_icon.png
By adolay

Nitakujibu kwa swali ukilijibu utapata unachokihitaji.

Mtanzania wa kawaida anaishi kwa chini ya Tsh 1500 kwa siku.

Shule bora za kulipia ada kwa mwaka ni kuanzia 1.5 milion nakuendelea.

Swali watanzania wangapi wanauwezo wa kulipia ada hiyo?

a) wakulima na wafanyakazi wa kawaida

b) wa wafanyabishara za madawa ya kulevya, wabunge na mawazili

c) a, b, na c yote sawa?

Elezea kwanini?
 
Hiyo unayosema ni nadharia ambayo Mwalimu alikuwa anaitekeleza. Lakini sasa haipo.

Je, mama Anna Mkapa anaweza kudhurumiwa kiwanja kama alivyodhurumiwa mama Maria Nyerere?

anaweza akadhulumiwa na aende mahakamani kama watanzania wengine. sema mwalimu hakujenga nchi inayofuata misingi ya sheria na kwa hilo alikosea sana, tena sana .alitujengea taifa la kiemotion zaidi
 
Mmezoea kudhulumu. Sheria gani ulitaka wewe. Nyerere aliandika katiba bila wasomi wengi imeongoza nchi hadi leo. Nchi imejaza wasomi lakini mmeshindwa hata kuedit katiba ili muweke hiyo misingi ya hizo sharia zako unazotaka.
 
  • Thanks
Reactions: ral
Mabaya gani kujenga vyuo kujenga mashule elimu ya ubure hospital bure tulisafi kwa warant kwenda shule kakosea wapi. Wangeboresha ujamaa na kujitegemea wangeboresha azimio la arusha ili litekelezeke siyo kumlaumu nyerere kwani aliondoka na nini?

Mamdenyi sijui kama umenipata vyema. Binafsi sioni baya alilolifanya ila kama binadamu naamini huenda kwa wengine wanaona mabaya upande wao na ndio maana hata yeye mwenyewe alisema tatizo watu wanachukua mabaya wanayaacha mazuri, yeye mwenyewe alijua kuwa ni binadamu na hajakamilika.

Tatizo Mamdenyi watu wanataka wachukue maisha na mahitaji ya wakati ule wayafitishe kwenye wakati wa sasa kitu ambacho hakiwezekani.

Nyerere alianzisha viwanda kwa uchache vilivyokua vinatoa ajira akaja mtu mmoja hapa akaviuza sasa utamlaumu Nyerere? Tunapokuwa na watu kama mtoa mada wasiokuwa wakweli nafsini mwao hatuijengi nchi, yanayotokea sasa ni sawa na kuwa na watoto kadhaa ambao unawahangaikia wapate maisha mazuri halafu kati yao mmoja anashia kwenye makundi mabaya baadae anakuja kumlaumu mzazi kuwa hakumjengea msingi mzuri.

Nyerere haikushika nchi isiende na mabadiliko, aliipenda nchi wamekuja hawa wa sasa ndio wanaiuza sasa
 
Nakubaliana nawewe 100%, kunamambo yapo wazi kabisa hatuhitaji kukashifu vitu vinavyojieleza waziwazi.

Sisi tupingane na kuzodoana kwa vyama vyetu vya sasa na viongozi wetu wasasa ndiyo siazi yetu, mwalimu pamoja na mapungufu yake upeo, uwezo na misimamo yake haina wakumlinganisha na hawa wasasa, si waupinzani wala wa serikalini

Moja ya walimu wangu Prof. Masuha (marehem kwa sasa, mungu amlaze mahalapema peponi) - alimsimlia nyerere alivyowawezesha watoto wa maskini kupata elimu, yeye Prof. Masuha akiwa mmojawapo kwa hisia ya ajabu sana. Nakumbuka wakati wa msiba wa mwl JK pale mlimani maprof na maDr walilia sana tena hadharani, mmoja wapo namkumbuka ni Dr Mhiru, kilichowaliza si kingine ni uadilifu na utendaji wa mwalimu.

Nasikitika kusema kwamba tumekuwa na kizazi kisicho na shukrani wa aibu kwa kuzusha na kushuhudia uwongo kwa watangulizi wetu hususani mwl JK Nyerere.

Asante. Hata sie wakulima ambao hatukusoma tunamlilia mwalimu tunakumbuka vyama vya ushirika tuliuza kahawa tulikuwa tunalipwa pesa siku ya kuuza na kahawa ikishauzwa kwenye soko la dunia walikuja kutulipa mabaki ya hela zetu. Nalia loooh wapi ile Tanzania yangu Mamndenyi?
 
Last edited by a moderator:
Mamdenyi sijui kama umenipata vyema. Binafsi sioni baya alilolifanya ila kama binadamu naamini huenda kwa wengine wanaona mabaya upande wao na ndio maana hata yeye mwenyewe alisema tatizo watu wanachukua mabaya wanayaacha mazuri, yeye mwenyewe alijua kuwa ni binadamu na hajakamilika.

Tatizo Mamdenyi watu wanataka wachukue maisha na mahitaji ya wakati ule wayafitishe kwenye wakati wa sasa kitu ambacho hakiwezekani.

Nyerere alianzisha viwanda kwa uchache vilivyokua vinatoa ajira akaja mtu mmoja hapa akaviuza sasa utamlaumu Nyerere? Tunapokuwa na watu kama mtoa mada wasiokuwa wakweli nafsini mwao hatuijengi nchi, yanayotokea sasa ni sawa na kuwa na watoto kadhaa ambao unawahangaikia wapate maisha mazuri halafu kati yao mmoja anashia kwenye makundi mabaya baadae anakuja kumlaumu mzazi kuwa hakumjengea msingi mzuri.

Nyerere haikushika nchi isiende na mabadiliko, aliipenda nchi wamekuja hawa wa sasa ndio wanaiuza sasa

Nimekuelewa vizuri nilianzia juu kidogo. tuko wote viwanda hakuna tena vijana wanaishia kula na kuuza unga wafanye nini ajira hakuna. Naililia nchi yangu nakulilia mwalimu nyerere.
 
Una maono gani wewe hapo ulipo.

ninamaono kwamba wataanzania tuwe namaisha kama raia wa norway,new zealand,sweden and the like. lakini kufika hapo lazima tuwe na viongozi serious na wanaojua watu wao tunchataka.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Kati ya wanafunzi wangu wewe ndio mjinga kuliko wote. kimsingi wewe huna hadhi ya kumjadili NYERERE hata kidogo.wewe unajua kusoma na kuandika tu na hujaelimika. huwezi kumjadili mtu wa hadhi ile hata kidogo.hata wazungu walio leta hii organized education, wasomi wa sayansi ya jamii na philosophy wanamuona Nyerere kama PHILOSOPHER OF ALL THE TIMES! Waandishi wa habari wa dunia nzima walikuwa wanaona fahari kumhoji maswali NYERERE siyo tu ili wasikie majibu yake bali walitegemea kupata maarifa mapya kutokana na majibu yake.

kinacho kupa kiburi cha kujiona unaweza kumjadili NYERERE mimi sijakiona,labda kwakuwa uko ccm na unapitapita kwenye ofisi alizo kuwa anapita NYERERE umeona una hadhi ya kumjadili.huna,huna huna hadhi hiyo hata kidogo. NAKUSHAURI FUTA UZI HUU MARA MOJA.
 
FaizaFoxy nimewahi kuisikia hotuba moja ya Nyerere redioni aliitoa baada ya Mwinyi kuwa madarakani,

Unajua alisema nini? Alikuwa amekasirishwa kwa nini Watz wanajenga shule za sekondari kwa wingi....
Alitaka sekondari ziwe chache sana na za msingi ziwe nyingi, pia akadai kuwa Watu wengi wakisoma
eti wataenda maofisini na miti itakatwa yote kutengenezea fenicha za maofisini, pia akadai kua
watu wote wakisoma hakuna atakaye lima....
Hii hotuba ilinisikitisha sana na ilinifanya niamini kua kweli Nyerere hakupenda kuona watu wanaelimika...
Na ndio maana ameweza kuwafanya asilimia kubwa ya Watz kuwa mazuzu na kumuabudu
 
Bibie,
Naona umerudi kiaina. Kikwete nchi imemshinda. Kikwete ni janga la taifa. Lakini ninyi wafahidhina zimwi la Nyerere linazidi
kuwanyima usingizi.
 
Umewanunulia watoto kiwanja, ukakitengeneza; ukachimba msingi na kuupiga, tena ukaanza hata kuwainulia ukuta, na ramani ya nyumba umewaachia. Watoto wanakuja wanaamua kubomoa misingi uliyowaachia, kuvunja na nyumba na kuuza kiwanja; halafu wanapojikuta hawana kitu wanalalamika "baba hakutuachia"...

Mlitaka awaandalie hadi nini nyinyi mje na kukunja nne tu kama spoiled kids?
 
Mabaya gani kujenga vyuo kujenga mashule elimu ya ubure hospital bure tulisafi kwa warant kwenda shule kakosea wapi. Wangeboresha ujamaa na kujitegemea wangeboresha azimio la arusha ili litekelezeke siyo kumlaumu nyerere kwani aliondoka na nini?
Mamdenyi swala sio aliondoka na nini, swala ni alituachia nini?. mwalimu akutuachia misingi yake.
 
Last edited by a moderator:
Kati ya wanafunzi wangu wewe ndio mjinga kuliko wote. kimsingi wewe huna hadhi ya kumjadili NYERERE hata kidogo.wewe unajua kusoma na kuandika tu na hujaelimika. huwezi kumjadili mtu wa hadhi ile hata kidogo.hata wazungu walio leta hii organized education, wasomi wa sayansi ya jamii na philosophy wanamuona Nyerere kama PHILOSOPHER OF ALL THE TIMES! Waandishi wa habari wa dunia nzima walikuwa wanaona fahari kumhoji maswali NYERERE siyo tu ili wasikie majibu yake bali walitegemea kupata maarifa mapya kutokana na majibu yake.

kinacho kupa kiburi cha kujiona unaweza kumjadili NYERERE mimi sijakiona,labda kwakuwa uko ccm na unapitapita kwenye ofisi alizo kuwa anapita NYERERE umeona una hadhi ya kumjadili.huna,huna huna hadhi hiyo hata kidogo. NAKUSHAURI FUTA UZI HUU MARA MOJA.

Mwalimu kweli huyu mwanafunzi wako ni mjinga hata elimu uliyompa haitamsaidia maisha yake yote. asante kwa kuwa umeona.
 
FaizaFoxy nimewahi kuisikia hotuba moja ya Nyerere redioni aliitoa baada ya Mwinyi kuwa madarakani,

Unajua alisema nini? Alikuwa amekasirishwa kwa nini Watz wanajenga shule za sekondari kwa wingi....
Alitaka sekondari ziwe chache sana na za msingi ziwe nyingi, pia akadai kuwa Watu wengi wakisoma
eti wataenda maofisini na miti itakatwa yote kutengenezea fenicha za maofisini, pia akadai kua
watu wote wakisoma hakuna atakaye lima....
Hii hotuba ilinisikitisha sana na ilinifanya niamini kua kweli Nyerere hakupenda kuona watu wanaelimika...
Na ndio maana ameweza kuwafanya asilimia kubwa ya Watz kuwa mazuzu na kumuabudu

Na wewe ni sawa sawa na mwanzisha uzi akili za kushikiwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nakubaliana nawewe 100%, kunamambo yapo wazi kabisa hatuhitaji kukashifu vitu vinavyojieleza waziwazi.

Sisi tupingane na kuzodoana kwa vyama vyetu vya sasa na viongozi wetu wasasa ndiyo siazi yetu, mwalimu pamoja na mapungufu yake upeo, uwezo na misimamo yake haina wakumlinganisha na hawa wasasa, si waupinzani wala wa serikalini

Moja ya walimu wangu Prof. Masuha (marehem kwa sasa, mungu amlaze mahalapema peponi) - alimsimlia nyerere alivyowawezesha watoto wa maskini kupata elimu, yeye Prof. Masuha akiwa mmojawapo kwa hisia ya ajabu sana. Nakumbuka wakati wa msiba wa mwl JK pale mlimani maprof na maDr walilia sana tena hadharani, mmoja wapo namkumbuka ni Dr Mhiru, kilichowaliza si kingine ni uadilifu na utendaji wa mwalimu.

Nasikitika kusema kwamba tumekuwa na kizazi kisicho na shukrani wa aibu kwa kuzusha na kushuhudia uwongo kwa watangulizi wetu hususani mwl JK Nyerere.
hatuendeshi nchi kulingana na emotoins kuhusu walimu wako au walimu wa yeyote. tunaendesha kwa misingi ya sheria na sheria inategemea context.
 
Umewanunulia watoto kiwanja, ukakitengeneza; ukachimba msingi na kuupiga, tena ukaanza hata kuwainulia ukuta, na ramani ya nyumba umewaachia. Watoto wanakuja wanaamua kubomoa misingi uliyowaachia, kuvunja na nyumba na kuuza kiwanja; halafu wanapojikuta hawana kitu wanalalamika "baba hakutuachia"...

Mlitaka awaandalie hadi nini nyinyi mje na kukunja nne tu kama spoiled kids?

Mwambie huyo chotara hawezi kuwa mtanzania huyo mama.
 
Mamdenyi swala sio aliondoka na nini, swala ni alituachia nini?. mwalimu akutuachia misingi yake.

Alikuachia nini? ulitaka nini zaidi ya ardhi yenye miamba iliyojaa madini ameacha waalimu ameacha shule vyuo mali asili hivi mtu ukishindwa kuwa tajiri hapa tanzania utamlaumu nyerere au utajilaumu wewe na ubongo wako uliogandamiana.
 
Last edited by a moderator:
Umewanunulia watoto kiwanja, ukakitengeneza; ukachimba msingi na kuupiga, tena ukaanza hata kuwainulia ukuta, na ramani ya nyumba umewaachia. Watoto wanakuja wanaamua kubomoa misingi uliyowaachia, kuvunja na nyumba na kuuza kiwanja; halafu wanapojikuta hawana kitu wanalalamika "baba hakutuachia"...

Mlitaka awaandalie hadi nini nyinyi mje na kukunja nne tu kama spoiled kids?

Usimrithishe mtoto mali....

mpe elimu....

hapo chacha ndipo baba alipokosea
 
Back
Top Bottom