andate
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 2,651
- 1,028
Sasa Jirani yetu KENYA chini ya MZEE JOMO KENYATTA alikuwa na MISINGI MAALUMU YA KUONGOZA? kumbuka kulikuwa na Mwanaukombozi kwa JINA LA DEDAN KIMATHI aliyekuwa na uhamasisho mkubwa kudai ARDHI yao iliyochukuliwa na MABEBERU wa kizungu ndio walioanzisha MAU MAU WAR; Kenyatta akapandikizwa
Kenya ikapata uhuru sababu ya Huyo Jamaa na Land Issue, Lakini Kenyatta land kidogo aliyopewa na wazungu aligawana na vizito wenzake wachache; wengine akawapa vibaraka Dedan Kimadhi akafa bila ARDHI
Kwa Nyerere Tanganyika ilitawaliwa na Wakoloni wawili MJERUMANI halafu MWINGEREZA wakati wa MWINGEREZA hakuwa anaijali sana Tanganyika na Maendeleo yake alikuwa anajua iko siku ataikosa atanyangány´wa kwahiyo pamoja na Tanganyika kuwa na Utajiri haikuendelezwa
Tanganyika ilikuwa na Makabila MENGI; DINI KIBAO;
Kwanza ukiangalia katika MAKABILA; Ni Mengi zaidi ya 250 lakini kuna 5 ambayo ni Makubwa na yana Machief na hayo pia yameendelea kielimu na yana mifumo bora sana ya ELIMU ukilinganisha na MAKABILA MENGINE
PILI DINI kulikuwa na Dini kuu kusema kuu ni Maana well established nchini ambazo zilikuwa tayari zina SHULE kuanzia PRIMARY HADI VYUO VYA UALIMU... Ukiangalia Shule za Utawala wa Mkoloni ambaye ni Mwingereza zilikuwa hazina huo mkondo Murua kama hizo shule za dini ni dini kama ya ROMAN CATHOLICS
LUGHA kwasababu ya makabila kibao. ingekuwa vigumu sana kuwasiliana kwenye nchi kubwa kama Tanganyika; South Africa hawana Makabila mengi kama sisi lakini wana 7 official national languages
ÆÆÆÆ Sasa Nyerere alipochukua UHURU kwanza alipendekeza LUGHA ya TAIFA kuwa KISWAHILI hivyo basi kila mtu lazima awe anaongea na ni lugha inayoongelewa Maeneo ya Pwani; kwahiyo haina mwenyewe... Pili kwasababu ya VYAMA VYA USHIRIKA enzi hizo vilikuwa na NGUVU kwa UPANDE wa hayo MAKABILA MAKUBWA akavunja Uongozi wa MILA --- Machief na Watemi wakaondolewa hii ilisaidia sana, sababu enzi hizo walikuwa na sauti kuliko hata Governor wa kikoloni sasa kama wangeachwa nchi ingekuwa labda bado Marais wanabadilishana toka Makabila Makubwa pekee... tusingeona Nyerere, Mkapa, Mwinyi na Kikwete wote toka Makabila Madogo wakiiongoza nchi hii...
Nyerere alitaifisha shule nyingi tu za DINI ili wanafunzi waweze kusoma bure elim ya msingi na walifanikiwa.... na UNAPOSEMA KUWA NYERERE ALIWEKWA MADARAKANI ni only yeye??? kwasababu alikuwa na watoto 9 watoto wake wooote walisome elimu ya Tanganyika hawakusomea ELIMU iliyokuwa inatolewa na SHULE za DINI. Watoto wake hawana Ma-Ph.D na hawafanyi kazi kwenye hizo kampuni zilizomuweka baba yao madarakani
Mwl Nyerere ni wa BUTIAMA; yeye na hao wanae hawakujenga International Airport Butiama; International PORT; au kupafanya BUTIAMA INTERNATIONAL FREE TRADE ZONE... Nyerere hakuwajengea Mahekalu wanae MBEZI BEACH; sasa kama kweli hao waliomweka madarakani walimtakia mema kwanini waliiacha familia yake OMBA OMBA???
Hakuna hata visenti USWISI kama wengine? Sasa kweli ni misingi gani Imara hadi leo unataka aiweke?
THE BEST PEDAGOGIST He did AZIMIO LA ARUSHA... lakini kila mtu aliyekua chini yake aliichambua kidogo kidogo kwasababu hawakulipenda...
wakaondoa nguzo 5 za uongozi, sasa ukaona viongozi wanamiliki makampuni na wanaingia nayo maofisini mwao; wanaajiri wake zao, wanauziana Majumba, hawakuishia hapo ikaishia kuwa it is not a police state... unaingiza madawa ya kulevya... wewe ni tajiri, wanaua viwanda wananchi wanakosa kazi kwahiyo ndio wateja wa hayo madawa ya kulevya
Lakini Mnaogopa kulaumiana.... Mnamkimbilia Mwl. Nyerere oh alikuwa akiendeshwa na waliomweka MADARAKANI!!! kweli hamuoni AIBU???
&&& Yaani ni kwanini Mwarabu wa Furniture Center katupiwa KEMIKALI...??? na nani kaenda kumuangalia South Africa --- Rais Kikwete... watu hawamuongelei vizuri huyo jamaa... ni jinsi anavyo operate jijini Dar...
Lakini wote mwafunga Macho.... Mwamwangalia Nyerere ati????
Mkuu una moyo wa chuma, wewe unaweza hata ukajitolea muda wako kuandika aya ndeeefu kuwapa somo ng'ombe. Keep it up mkuu labda wataelewa.