Nyerere hakua na "luxury" ya kuwa na watu wasomi wa kumsaidia, aliingia madarakani na "a handful" ya wasomi wa kumsaidia kutawala Watanzania Mil.9
Kumbuka hata madaktari wa liletwa kutokea Cuba, Ujerumani nk
Kulikua hakuna chuo kikuu hata kimoja, alirithi watanzania wasiokua na elimu kwa saana, bila elimu hata uwe na akili km "Einstein" ni ngumu lakini pamoja na hayo yote mpaka leo hakuna kiongozi atakaye weza aliofanya "leo akisimamia ujenzi wa barabara anasema yeye katoa hela halafu anatulazimisha wote tuamini barabara ni maendeleo na sio wajibu wa serikali" .... hata ujenzi wa mashule, na zahanati ni maendeleo lakini vinachangiwa na wananchi.... kwanini barabara hua hazina harambee? Iweje ujenzi wake uitwe maendeleo km si udhaifu wa viongozi wa sasa kutafuta sifa kwa migongo ya wananchi wao?
Nyerere hakuwahi kuelekezwa na mtu au kuwa mtumwa wa wakubwa kama alikua hivyo asingeweza kushirikiana na Cuba, au kuunga mkono PLO au Kupambana na wakoloni nchi jirani yaani Zambia, Msumbiji, Angola, Namibia na Africa ya kusini