Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Inakuwaje kwa yule aliezaliwa na kujikuta ndani ya mchanganyiko huo kupitia wazazi (ie: Baba Islam, Mama Katoliki/Mkristo)?

Kama tulivyojikuta wengi wetu tukiwa Dini fulani/ Dhehebu fulani kwa sababu ya wazazi wetu?
Simba; Uislam unasisitiza hata ukizaliwa na wazazi wote wawili Waislam ni lazima usome ili ujitambue.

Nakushauri, soma bila kujiwekea mipaka.

Arsis; Swali zuri sana.

Wanatumia bila kujijua, wamekua "brain washed" na hawaelewi tofauti, kwa sababu wanafata tafsiri. Hivi visa na mafundisho ya biblia yaliingizwa miaka mingi sana kwenye tafsiri za Wur'an sio Qur'an yenyewe. Ilianza baada ya kufa Mtume Muhammad.

Mtume, hakuitafsiri Qur'an, wanamzushia eti katafsiri. Mtume hakuna aya zaidi ya 10 au ishirini ndizo alielezea maana yake. Tafsiri zingine zote ni za kutunga au kugtokea biblia au fantasy za waandishi wa tafsiri, kama alfu lela u lela tu.

Mkiependa kujua zaidi kuhusu historia ya hadithi na kuna majina makubwa ya watu wa hadithi kwenye vitabu vyao wanakiri kuna visa wamevielezea kutokana na biblia, hii ni kwa kutokujua ubora na umuhimu wa Qur'an au kwa kudhani watu wataelewa zaidi wakifanya hivyo. Na wengine ni kwa makusudi kabisa ili wapotoshe ubora wa Qur'an.

Pia mkipenda kujua zaidi elimu ya Qur'an bila kutumia hadithi za kujitungia, ulizeni maswali kama hili, yenye nguvu. Kuna njia nyepesi za kila mmoja wetu kuweza kutambua hii hadithi ya kwe;i au sio hya kweli.

Kama mnakumbuka kuna mtu kaleta mstari juu huko, kaupamba kwa Kiarabu nikamuuliza aya ipi hii? Akajibu hadithi, nikamwabia hadithi ipi hio? Hajajibu tena, sasa ananisoma kwa kunusa nusa tu. Namwambia usifanye hivyo, sio elimu hio. Kama yalikua ni maneno ya mshairi sema tu, ni mshairi, kama hujui yametoka wapi na uliyasikia tu, sema hayo nilisikia tu lakini sina elimu nayo yametoka wapi.

Tutumie hili jukwa hili kujua mengi sana. Ya dini, ya sayansi, ya ulimwengu. Ya dhahiri na siri za kidunia. Tusiwe na jazba, kama hatujui kitu au tunashaka nacho, sisi hatuwezi kujua kila kitu tuulize.

isipokua tunasema, umri huongeza maarifa na busara, ndio elimu yenyewe hio.

Hakuna zaidi ya Allah na mafundisho yake.
Arsis.
 
Arsis ni mswahili mmoja tu anae tafuta mazombi. Ana kona kona nyingi kwa mtu anae jielewa ina tosha kuona ni mweupe sana .labda kupaa tu ndo kitu ana jua

Mazombi ndio nini? Au ndio misukule au mashetani, misukule ya kishetani? Mimi nasoma tu "zombie" ndio hao uliokusudia kwa mazombi? Kiswahili chake sijui. Mwaga elimu ya kidevil.

Devil Kiswahili chake ni nini?
Simba.
 
My Life Experience 03

Vitabu vya dini vipo sahihi kwa kiasi isipokuwa watafsiri wa hivyo vitabu ndo wanapindisha mambo.

Djinn ambae wapo kwenye vitabu vya dini ni kweli wameumbwa kwa moto, Pia anaezungumziwa kwenye vitabu vya dini sio hawa ambao ni Chotara/Djinn/Soul/Nafsi bali ni hao ambao wapo kwenye Ulimwengu/Dunia/Sayari ya pili baada ya hii yetu.

Jiulize tu Kiumbe kimeumbwa kwa moto then inakuaje akaweza kukaa na kustahimili katika ulimwengu huu wa kwetu ambao viumbe vyake vimeumbwa kwa udongo?

Djinn wa kwenye vitabu vya dini hafungamani na binadamu, Hata kumuona kwake ni mtihani ingawa wanakuja mara chache na kukaa kwa muda mfupi usiozidi masaa matano katika ulimwengu huu.

Kuna nyota huwa zinachomoza ghafla angani na huwa zina ng'aa sana, Nyota hizi zinaweza kaa ndani ya wiki moja, mbili, tatu na mpaka nne ndio zinatoweka. Nyota hizi zina ashiria kuna binadamu amezaliwa ambae ana nguvu za kimungu ndani yake, Hivyo hawa Djinn halisi ndio huja ulimwengu huu kwaajili ya Binadamu huyo na watakuja mara kwa mara kumuona mpaka Binadamu huyo atakapo fariki.

Wanakuja kumpa Elimu ya Mafumbo, Alama na Maandishi. Hawatoengea nae neno hata moja kwasabau lugha yao na yetu ni tofauti.

Hakuna Binadamu mwenye uwezo wa kuwaita wala kuwa control isipokuwa kwa yule waliye mjia tu.
Arsis; Moja ya muujiza wa Qur'an ambao uliwashinda na kuwa-acha midomo wazi mabingwa wa lugha ya Kiarabu na washairi wa Kiarabu iliposhushwa Qur'an ni lisan zilizotumika kwenye maandiko yake, kuna lisan, kwa maana ndimi, ingawa watafasiri wengi wametafasiri lisan kua ni neno ugha. na style ya uandishi wake ni ya kipekee. Mifano na mingi sana tena sana.

Inawezekana kua kuumbwa kwa moto au kwa udongo au kwa nuru, imetumika lisan, ndimi fulani lakini haimaanishi moto, udongo au nuru?

Ndimi ni lexicon au locution kwa Kingereza. Mfano Kiswahili tunasema "mwanangu" kwa rafiki zetu, mtu asieijua lisan hio au locution hio anawez asielewe kua anamaaanisha rafiki yangu.

Tusome zaidi kuhusu lisan zilizotumika kwenye Qur'an ili tuna uelewa mpana zaidi.

Mfano tu; Tukisoma mama wa vitabu vyote, Umm al Kitab. haimaanishi hicho kitabu kina watoto vitabu, ni Lisan tu yenye maana tofauti na kilichoandikwa au kutamkwa.
Arsis.
 
Arsis siamini mpaka page hii Simba Kuna kilichofunguliwa, ngoja nione labda huko mbeleni
Simba; Mengi sana Arsis anaendelea kufunguka kidogo kidogo mara kwa mara. Kama una kitu fulani unakitarajia, hukukiona, uliza.

Au pia inawezekana anayofunguka yote wewe una ujuzi nayo kitambo, wengine mengi hatuna ujuzi nayo, tunayaona ni mapya kabisa kwetu na anafunguka kweli kweli.
Simba.
 
Lakini tunaambiwa zilipita dahar na dahari na binadamu hakuwa wa kutajwa kwa maana hakuwepo kabisa,sasa kotendo cha Allah kumuumba adam kwa udongo wenye kutoa sauti,inaonyesha lwa dalili kuwa hiyo ndo wa kwanza

Lau asingekuwa wa kwanza basi angezaliwa kwa maji ya kuchupa kama sisi na tusiongeonyeshwa asili yake

Ni dhahir adam ndio wa kwanza na Allah anajua zaidi
Simba; Watu je? Walikuwepo au hawakuwepo? Namaanisha , mfano wewe ni Etugrul Bey, atakuwepo bin Etugrul Bey kabla yako? Lakini wakati huohuo wanaweza kuepo bin Simba kabla yako.

Naomba kuuliza swali, yeyote anaweza kulijibu; Hivi Adam toka uwepo wake kwa jinsi mnavyosoma mpaka leo imepita miaka mingapi?
Simba.
 
Faiza nakupenda sana ila nakuogopa huchelewi kumpa mtu makavu kina muda kupitia comment zako najenga taswira ni mtu wa aina gani nafurahia uwepo wako JF Namuomba Mwenyeezi Mungu akubariki akulinde na akuongoze.

Bwana Arsis alisema wewe Simba Clan 😁 nimesoma story za koo za Simba bora ukatae Simba ushuzi 😂 wanajamiana kama wanyama baba mama watoto babu Dada kaka.
Anatisha, mimi kishaniita simba ushuzi, mara mbili tatu, naogopa hata ku comment.

Naamini jina lake sio FaizaFoxy, ni ID tu aliojipachika JF, lakini imemkaa kwa ujeuri wake, kina Faiza wengi niliokutana nao au kuwasoma ni jeuri sana. Huyo sio fox ni 100% lioness wa mkuranga.
Simba.
 
Naomba kufahamu jambo kama kuna mtu alistuka kama uko na hayo majini kuna viashiria gani vinavyomfanya ajue kwamba hao si watu bali ni majini yaani nini kinamtofautisha mtu halisi na jini aliyevaa taswira ya binadamu
Cha haraka kabisa kujua ni macho yake, jini hata afanane vipi na binadam macho yake lazima yacheze kwa haraka kulia na kushoto.

Na viashiria vingine vingi tu. Ukishawazoea, uwepo wao tu hata kama hujawaona unajua hapa yupo jini au wapo majini wangapi na wa aaina gani, kabla hata hujaaona.
Simba.


Kuchezaje? Ya binadamu hayachezagi je kuna sign nyingine zaidi japo moja tu pia humo masokoni na madukani huwa wanafanya nini hasa?

Simba: Ya binadamu hayachezi kama yao, labda albinoi kwa kiwango fulani, wengineo.

Masokoni na madukani, wapo wanaofanya biashara wapo wanunuzi, wapo wauzaji, wapo wanautumwa, wapo wachawi, wapo wema.

Ni kama binadamu, masokoni na madukani walivyo, sema majini wametuzidi idadi. Mgfano mzuri ni hapa JF, verified users ambao hao ndio sio majini, wapo wachache sana. Na wengine kinasisi yusiojulikana na kuonana na wsala hatutaki tujulikane, ndio majini wenyewe, na wewe ukiwemo, hata jina lako linaashiria hivyo.
Simba.
 
Hii ishu nakuwachia wewe sasa naona unaikwepa kijanja janja

Asante
Sina sababu ya kukwepa hoja, usiikimbie elimu ukatunyima raha, itoe uijuayo, isikutie unyonge au kuogopa kua itapingwa. Bila kuitoa hutopata nyingine ya ziada.
Simba.
 
Kuhusu mimi, Picha lilina anza nilipigwa na radi, baada ya miezi kazaa kupita nilipo amka asubuhi nakuta nimepakwa mafuta kama ya siagi kichwani, sijui walikusudia nini na hayo mafuta. hayo yote niliyachukuli pow tu, kumbe kuna kitu kizito kina kuja kwangu mpaka leo walimwengu wameshindwa kunijibu nitoke vipi
Ibada tu, rudi kwa Muumba wetu kwa kuzidisha ibada, kuacha maovu na kutenda mema.
Simba.
 
Arsis; Swali zuri sana hili. Ngoja niigie ndani zaidi kidogo ili watu wengi wapate kuelewa.Hio ni ibada ya kishetani.

Kama mnakumbuka mnaoufatilia huu uzi, wakati tunafafanua kidogo huko nyuma kuhusu Subian tukaelezea kua Subian linatokana na Saba, Sheba (Abysinia) au habashia Kiarabu. Waarabu wakisema Subian wanamaanisha mtu wa kutokea Saba au mwenye asili y Saba au ana nasaba ya Saba.

Sabb ndio utawala ambao wengi wanaamini wakati fulani ulikua na mtawala mwanamke (malkia), mwanamke mwenye nguvu, hakima, busara na mali nyingi sana. Huu utawala uliabudu nhota na moto lakini baadae wengi wakaamini vingine. Miaka mingi baadae wapo ambao wamekua Wayahudi, wapo ambao wamekua wakristoo, wapo ambao wamekua Waislam. Wapo ambao wamebaki kua ni Wasabai na Wapo wanaabudu nyota na moto.

Pia kuna ambao wamebaki na mila hizo za saba kwa kupitia mizimu (jini) ya zamani. mizimu na majini wengine ni roho ambazo hazijaingia kwenye umati. Watu wanaouliwa wengi wanakua wamekufa mwili lakini roho zi hai, hazijaigia kwenye umauti. Ndio hubaki kua mizimu, kua majini na wengine huita Qareen au wengine ruhani. Majini ni wengi ni roho za watu.

Hapa ielewedke zote ni roho, hakuna roho ya kibinadam au kijini bali miili ndio ipo ya kibinadam, na viumbe wengine. Roho inaweza kukaa kwenye mwili wowote.

Kwa bahati nzuri au mbaya hii Ardhi huko ziwa victoria, chanzo cha mto nile, ndio iikua moja ya njia kuu za kwenda na kurudi kati ya kaskazini na Kusini. Kuna makabila ya kando ya ziwa, yana mizimu ya kisaba "subian" ina nguvu na inadai watu waelewe nguvu yao na uwepo wao kwa kugtumia moto. Wanaoamini hio miziu inaweza kuwalina na kuwapa mafanikio ndio waliouanzisha huo mwenge.

Mwenge sio hapa kwetu, upo mpaka wanaoita michezo ya olympics. Upo mpaka makanisani, kanisa katoliki linaongoza. kwa kuwasha nwenge wa kuwatukuza ma Subian.

Pia ieleweke hawa masaba wanaamini wana kitabu cha Yahya kwa Waislam na Wayahudi, John kwa wazungu.

Hilo suala linagusia mambo mengi sana, nimejaribi ufanya kwa ufupi sana. Ni elimu kiubwa sana ya mtu kupata PhD kwa sabu yote utaweza kuitetea kwa ushahidi au wa moja kwa moja au wa kimazingira.

Binafsi naamini Yahya ni kaka yake Isa na mama yao ni mmoja Mariam, Meritaton.

Natumai imeeleweka.
Arsis.

So huu mwenge sio umetokea bagamoyo? Ni ziwa victoria! Na huo wa kikatoliki ni upi?
 
So huu mwenge sio umetokea bagamoyo? Ni ziwa victoria! Na huo wa kikatoliki ni upi?
Ingekua Kiongozi alieuanzisha mwenge Tanzania katokea bagamoyo ningefikiria mara mbili.

Sehemu nyingi tu, wakatoliki wana sherehe yao ya moto. t-Tena sio wakatoliki tu, na makanisa mengine pia.
Simba.
033024_Easter-Vigil-036.jpeg

Washington Cardinal Wilton Gregory presided at the March 30 Easter Vigil at the Cathedral of St. Matthew the Apostle, where people became full members of the Catholic Church as they received the sacraments of Baptism, Confirmation and Eucharist. (Catholic Standard photos by
 
Cha haraka kabisa kujua ni macho yake, jini hata afanane vipi na binadam macho yake lazima yacheze kwa haraka kulia na kushoto.

Na viashiria vingine vingi tu. Ukishawazoea, uwepo wao tu hata kama hujawaona unajua hapa yupo jini au wapo majini wangapi na wa aaina gani, kabla hata hujaaona.
Simba.




Simba: Ya binadamu hayachezi kama yao, labda albinoi kwa kiwango fulani, wengineo.

Masokoni na madukani, wapo wanaofanya biashara wapo wanunuzi, wapo wauzaji, wapo wanautumwa, wapo wachawi, wapo wema.

Ni kama binadamu, masokoni na madukani walivyo, sema majini wametuzidi idadi. Mgfano mzuri ni hapa JF, verified users ambao hao ndio sio majini, wapo wachache sana. Na wengine kinasisi yusiojulikana na kuonana na wsala hatutaki tujulikane, ndio majini wenyewe, na wewe ukiwemo, hata jina lako linaashiria hivyo.
Simba.
Arsis na wenzake kila siku wapo kwenye vita ya kupambana, kuwapiga na kuwaua majini waovu, wachawi na washirikina. Je hiyo vita ipo kwa kiwango gani? Majini wapi wapo wengi duniani ni wazuri au wabaya? Hiyo vita yako itaisha lini?
 
Inatokea post namba 2026.

Vionjo vya Arsis 4 Kumwokoa Msukule Unguja 4.

Tukatoka bandari tukachukua taxi nje pale, kumtajia dereva wa Taxi tunapokwenda akasema napajua, hata mimi nilikua mazikoni jana. Akatufikisha. Kijana akamlipa tukashuka.

Nyumba ilikua ya kizamni lakini kubwa na safi, inapendeza, watu wawili watatu walikua nje. Tukasalimia, tukaoneshwa baba na wajomba wa marehemu nikajitambulisha, wakasema ngoja gtukuitie mama'ko ypo ndani huko kwa kina mama, njoo huku. Nikanyayuka na mwenyeji, tukainga ukumbini, aknambia kaa nikamwite, wawaletee na chai,watu wameshakunywa chai. Yule mwenzako mliokuja nae na yeye tutamwita mje kunywa nae chai, akaingia ndani akatoka mothe na wife wangu tkasalimiana nae watu wanalia kama kawaida. Wakiona wageni, yule mwenyeji akaja, njooni njooni mnywe chai, najua mmeondoka boti ya aldajiri. Kaa hapa, akatoka kwenda kumuita kijana. Mara akarudi, hayupo hapo nje, wewe endelea tu, nikaanza kunywa chai, mama akaja tena, ngoja nikuigtia mama'ke yule binyti umsalimie. Nikamwabia usimuite mama, wacha ninywe chai baadae kidogo tutamsalimia. Mama akaondoka kurudi ndani.

Nilipomaliza kunywa chai nikatoka, nikakuta yule kijana na Jini 3 wamesimama pembeni wanaongea. Nikawafata.
MImi: Mbina mnaleta vituko tuka kwenye boti?
Kijana' Vituko gani mkuu?
Mimi; Wewe umefatwa hapa tunywe chai ukawa haupo, Jini 3 katoweka bandarini, nini kinaendelea ambacho sikijui?

Kijana: Iilibidi nionane na Jini3 anifahamishe hilo unalouliza. Kwa ufupi, mambo yote mazuri sana, baada yamuda mchache sana binti atatolewa hapa nyumbani, sisi wote tuage tunaondoka hapa mpaka baadae, lakini hatuchelewi tutarudi hakuna atakae tuona hata awe jini.

Kijana: haya twendeni tukaage.
Mimi Jini 3 twende ukasalimie na kuaga.
Jini3: Twendeni tu Mkuu, mimi mnaniona nyinyi tu hakuna anaeoniona.

Nikacheka kimoyo kimoyo, nikaona najisahu kabisa kama nafatana na majini.Moyoni najisemea hata huyu anaesema binadam ni jini tu.

Mimi nikaaa, nikawaambia natoka kidogo jamani, tutaonana baadae.
Mwenyeji; Mkumbuke chkula cha mchana hapa, kija a twebde ukanywe chai, naona ulitoka kidogo.
Kijana; Ahsante, nipo vizuri, mimim nilikunywa chai kwenye biti huyu mwenzangu alilala hajawahi kunywa. Tunatoka tutaonana baadae,

Mweneyeji: Sawa jamani, msichelewe chakula cha mchana.

Nilishi anavyosisitiza kama anatamani tusirudi kabla ya mchana.

Wala hatukwenda mbali ku[pinda kona tu, kuna kichochoro tukaingia, Jini 3 akatoa kitamba cheupe kikubwa tu, akanambia hiki vaa kilemba, wedwe mwatabiu mfunge kkilemba cha kikwenu huyu. Yule kijana akachukua kilemba akaanza kunifunga kichwani, nikahisi kimekaa sawasawa.

Kijana: Sasa na wedwe huonekanai kabisa, hata aje Jini wa wapi hakuoni,Sasa sikiliz kwa makini. Tutaingia ndani ya chumba kilichooshwa na kukafiniw mgomba, Chumba kimeshgasafishwa kisafi na binti yumo humo. Sasa hivi wataingia wale wachawi na majini yao lakini wapo chini ya ulinxi, Utachokiona utachokisikia, kaa kimya kabisa.

Mimi; Sawa.
Kijana; kamanda sfaisha njia sisi tunakufata nyuma.
Jini 3; Njia safi nyeupe haina tatio kabisa, twendeni msiwe na shaka lolote.

Tukawa tunarudi tukakuta watu wengine wameondoka wemgine waamekuja, katika waliokuja wawili nikajua haw wachawi lakini ni watu, walikua wanaongea na mwenyeji wetu. Tukaingia ndani, hapo hatuongei, zinatembea ishara tu.

Kuingia ndani tukapoita mpaka chumba walichoosha. Jini 3 akafungua mlango kama kawaida, aki-aingia akatrushiria tuingie, aktuonesha pembeni kwenye kona, tukamuona binti. Dah, binti mzuri kweli kweli, kigori wa haja kabisa, kutuona sisi akawa anatabasamu tu, nikajua anatuona.

Hatujakaa sawa, jini 3 aktuita pembeni upande mmoja, mara mlangoni wakaingia majini wawili wamevaa kama jini3 lakini wao sio warefu kama yeye, mmoja akaenda mkonoi wa kulia wa binti mmoja mkono wa kushoto, mara wakaingia watu watu watatu, mmoja mtu mmoja jini, mmoja mwanamke, kijana tu.

Mwanamke; haya jamani twendeni tukamalixane njia iko nyeupe.

Yule mchawi akaenda akamshika mkono yule binti kama anamuongoza amfate, na jini waliokuja nae yupo nyuma yao.
Mchawi: haya tangulia wewe, wewe mbona umezubaa t mlangoini hapo?
Mwanamke; hapatokeki mpaka mtoe vitu vyenu, tazama tutapita wapi hapa?

Yule mmchawi kutazama, na mimi nikaangalia mlangoni nikaona kitu kama bonge la nyuka limeuxiba mlango, pembeni yake yupo Jini 1 ndio anaongea na yule mwanamke, huku macho yake mekundi sijawahi kumuona namna ile. Hana tabasamu,hatishi kasoro macho tu.
Yule mwanamke akarudi ndani, akmwambia mchawi, nendeni nyinyi, mimi sitoki mpaka waturuhusu na wanasema mpaka mtoe vyote.
Jini 3: Nawapa nusu dakika mtoe kila kitu, lasivyo na nyinyi mtazikwa humuhumu ndani bila kuoshwa.

Jini la kichawi likajua hapa kasheshe tukichelewaa wanatuua kweli. Yule mchawi ndio alikua analeta kiburi. Jini la kichawi likamtandika kofi yule mchawi.
Jini Mchawi: Toa haraka.

Huku damu za poua zinamtoka yule mchawi akaanza kumwaga unga fulani kwenye kona chumbani.
Kijana: Wewe mbwa, futa matone yote ya damu yasionekana, tena yalambe kwa ulimi wako.

Yule mwanamke hajasita, akaanza kuyayamba, yale matone yalikua yanamtoka yule mchawi puani. alikua kiainama kila pembe, pembe ya kwanza aktoa kichupa kidogo, ya pili aktoa kitambaa cheusi kama fundo hivi, ya tattu akatoa kama mizizi midogo imefungwa pamoja, pembe ya nne akatoa chupi nyeupe, imekunjwa kunjwa nikajua ya yule mtoto wa kike.

Kijana: haya wewe mwanamke nenada nao hawa na mtoto katungoje nje mlangoni hawa tunaenda nao kutoa vigtu vingine, nyie mpeni huyo uchafu wenu abebe.

Akapewa yule mwanamke vile vitu alvyochimbua aktoka nje na wale majini wawili na jini! yupo nyuma yao wote tuaktoka nao ukumbini wakaenda mlango wa uani, wakamwaga mdawa yao yule mchawi akainama kati kati ya mlango akatoa kichupa kingine. Akaanza kwenda mlango wa mbele, nakao akatoa kichupa, akasema tumemaliza. Jini 1 akase haya twendeni hawa wamemaliza, tuwahi, tuukaondoka wote wao mbele sisi nyuma, tunakatiza mitaa nawaona viumbe wengi wanapoita oita hawana hata habari na sisi. Tukaingia nyumba moja si mbali sana na pale.

Itaendelea
Simba.
 
Arsis na wenzake kila siku wapo kwenye vita ya kupambana, kuwapiga na kuwaua majini waovu, wachawi na washirikina. Je hiyo vita ipo kwa kiwango gani? Majini wapi wapo wengi duniani ni wazuri au wabaya? Hiyo vita yako itaisha lini?
Tazama uwiano wa watu waliopo duniani, wengi ni wazuri aiu wabaya? Utapata jibu. Jini hafanyi kazi za kichawi bila ushirikiano na watu.
Simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom