- Thread starter
- #1,961
Simba; Yupo mkoa gani kwa sasa?Kuna kisa kimoja Cha kweli kabisa naomba Arsis anipe ufafanuzi na Tiba:
Baba yangu ni mgonjwa (maradhi ya akili) wa muda mrefu sana. Maradhi haya yalimpata 1996 nikiwa na umri miaka ..... Kwa kipindi hicho alikua mjasiliamali mdogo huko kijijini na alikua anamalengo ya kuamia mjini Kwa wakati huokwa ajili ya kujitanua kibiashara.
Ugonjwa ulimpata akiwa polini anapasulisha mbao Kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mjini, ghafla akapatwa na hayo maradhi akiwa uko poloni!
Sasa huu ugonjwa una mkangnyiko kutoka na ulivyotokea tunaamini amefanyiwa ushirikina. Kwa kipindi hicho chote watitembea sehem mbalimbali walishindwa baadae wakampeleka hospital akawa anatumia Sindano Kila baadae ya miezi 3. Kuanzia 1998 Hadi 2012 hivi ikawa zile dawa hazisaidii akawa tena Yuko serious sana.
Mwaka 2020 nikazunguka nae Mimi bila mafanikio nikampeleka milembe akapatiwa dawa ambapo hizi dawa alizopewa sasa ni mtihani sana Kwa sababu anatakiwa ameze Kila siku asubihi 3na jioni 1, Hadi Maisha yake yatakapofika mwisho. Kikubwa zaidi zinaua nguvu za kiume.
Kikubwa zaidi sana ni yeye kutotumia dawa hizo na hili hata alipokua anatumia Sindano hilokua ni changamoto kubwa sana. Hii inatokana na kutojitambua kama yeye ana maradhi ya akili.
Sasa hali hapo zamani ilipokua inataka kumtokea alikua anafaham kua siku zijazo atapatwa na hilo tatizo hivyo kama anapesa alikua anampatia mama anamwambia hii ni Ada ya Chama hata kama nikikuomba vipi usinipatie na anaweza akampatia na Pesa nyingine. Sasa Ile hali ikimjia tu anakua na huruma na ukarimu mkubwa sana mtu akija dukani kununua kitu anampatia vingine zaidi au kama Kuna mtu anapita nje anmwita anampatia ama Pesa au Mali kutoka dukani ni hivyo. Ile Pesa aliyokupatia akirudi kwenye hali yake yakawaida anakumbuka vizuri ikipungua hata 100 atakuambia.
Kwa ufupi ugomvi unatokea na hasira zaidi pale anapodai zile Pesa anakua na vitisho vikali na hata kutia kukupiga au kukupiga kabisa. Nilisoma Kwa namna hyo Hadi nikamaliza.
Kwa ufupi Hadi Leo baba yupo ni mgonjwa naomba Arsisi aniambie huu ugonjwa nini chanzo chake na unatibika na kama unatibika anifahamishe wapi atapata tiba.
Nina mengi ya kuongea athari tunazozipata au tuzazopitia kutokana na huu ugonjwa wa baba kama famiia na ukoo Kwa ujumla.
Simba.