Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Yani we umesema unajibu swali lolote lkn maswali magumu hutaki kujibu full yaeleweke unajibu kwa mkato Sasa sisi tukikwambia ukweli unajibu fyongo kama ulimvojibu huyo jamaa hapo sa sijui ndo maelekezo ya Babu Yako aliyokwachia ama nn mana alikeambia mtu akiwa na swali majibu and hamna shidakutumia herufi kubwa

Anaonesha msisitizo mtu akiuliza swali mjibu kamili na maelezo ya kueleweka sio nawe unaacha mafumbo au unajibu kwa swali
Ajibu mgundue hajui lolote kwa alivyo jinasibu 😀watu wenye D 3 tushajua hamna kitu hapa hana elimu hakuna cha jinn sheytwan tu 🤣😂wanakulana familia mama baba watoto bibi babu dada kaka.
 
Simba; Unauliza elimu inabadilisha nini kwenye maisha yetu? Pole sana ndugu yangu.

Point siyo hio, point ilikua kuelimishana na Waislam waache kubishana kwa kutumia biblia. Waelimishe kwa kitabu chao ambacho ni Qur'an. Ndio niwafahamisha wamefikia kuitafsiri Qur'an kwa kutumia visa vya kwenye biblia.

Katika kupeana nasaha elimu bora, sio bora elimu. Umeelewa?

Arsis ana njia za kipekee za kufundisha. Ni mtata sana.

Mkasa wa Unguja unakuja. Baada ya sala ya alfajiri.
Simba.
Wewe lete mkasa tusome ndo unakiweza hufurahia, elimu huna wala huyo Arsis wako, hakuna wajinga humu wa kupotoshwa na elimu sio 😀
 
Kuhusu mimi, Picha lilina anza nilipigwa na radi, baada ya miezi kazaa kupita nilipo amka asubuhi nakuta nimepakwa mafuta kama ya siagi kichwani, sijui walikusudia nini na hayo mafuta. hayo yote niliyachukuli pow tu, kumbe kuna kitu kizito kina kuja kwangu mpaka leo walimwengu wameshindwa kunijibu nitoke vipi
 
Arsis: Qur'an ni muujiza unaoishi. Hakuna dalil ya kukisia.

Weka hio aya tukufahamishe kilichokusudiwa. Kama huna haraka sana, baada ya kukiri kuwa huna aya naa kuleta aya biblia, sasaunatakiwa ulete Hawa, manesema ni mkewe Adam, Waislam mmemsoma wapi? ummmetowa wapi?

Tukimalizana na la Hawa, naahidi kuanza kuwa elimu kidogo kidogo ya adam ni nani. kwa mujibu wa Qur'an.

Unajua kua Adam wako wengi, sio mmoja tu?
Arsis.
Hii ishu nakuwachia wewe sasa naona unaikwepa kijanja janja

Asante
 
Arsis; Ujanja upi wa maneno? Umeleta aya za biblia hapo au hujaleta?

Mbona mpaka sasa wewe na Waislam wengine mmeshindwa kuleta aya za Qur'an zinazoonesha Adam ni mtu wa kwanza?

Hawa mmetoa wapi? Hili la Hawa naona wote mmeshindwa hata kujitetea japo kidogo.

Ushauri wangu, semeni ukweli kua hakuna, ili niwafundishe Qur'an bila kutumia biblia kuitafsiri Qur'an.

Bapo mpaka sasa mmedhihirisha ukweli nilipowaambia Waislam mnaijua sana biblia kuko Qur'an yenu na hamuitumia Qur'an amacho ni kitabu bora kabisa, kwa kua hamuispomi Qur'a mnasoma tafasiri za waliopotosha.

Nyie mmeona jina Adam basi moja kwa moja mkajua ni kisa cha Adam wa kwenye biblia. Qur'an haiendi hivyo, lakini tutaelimishina kidogo kidogo, wenye kuelewa wataelewa.
Arsis.
Wewe una porojo sana boss,aya tumekuletea za qur'an lkn naona sasa tunafanyana watoto wakati sisi ni watu wazima

Tumekuletea za biblia bado unaleta porojo,sasa unataka kuhamishia mambo kwa hawa,ebu acha porojo na utoto,kwa umri wako huo wa miaka 5000 bado unakuwa kama jini mwenye miaka 100

Pili waislamu tunaamini vitabu vyote na mitume wote,kwahiyo hakuna ubaya baadhi ya mambo kuyachek katika biblia,ingawa tunajua kuna mambo mengi yamechezewa katika hiko kitabu

Kwahiyo bakia kwenye hoja na usianze kuleta maneno ambayo sio hoja iliyopo mezani hapa

Binafsi hii ishu naachana nayo kwakuwa naona tunapotezeana mda tu hapa

Tutajadiliana mambo mengine lkn si ishu ya adam tena

Asante
 
Kama watu mko makini mtagundua Arsis anapenda kujibu kaswali kwa kuuliza Maswali. Hii ni njia bora ya kujibu kutoka kwenye unknown to known, yaan anataka ufaham kutokea pale usipoelewa, yaan ku unridle. Njiaa hii pia ilitumika ancient time na wanafalsafa kama akana Socrate, na Aristotle, kwenye reasoning.

Changamoto ni kuwa watu tumezoea majibu ya rahisi, hatutaki kufikilia. Arsis antaka ufikirie af uulize tena ukikwama uulize alternative. Ni niia bora ya kujifunza japo inahitaji mtu mwenye uharaka wa kutatua mtego na kurusha kete yaan kama Draft.
 
Kielimu inawezekana lakini hairuhusiwi. Wanaofanya hayo ni washirikina. Utakiona kisa chake kikifikia.
Umesema kuna majini wazuri na majini wabaya, je mgawanyiko huo upo pia kwa Malaika ikiwa ona maana kuwa kuna Malaika wazuri na Malaika wabaya?
 
Kuhusu mimi, Picha lilina anza nilipigwa na radi, baada ya miezi kazaa kupita nilipo amka asubuhi nakuta nimepakwa mafuta kama ya siagi kichwani, sijui walikusudia nini na hayo mafuta. hayo yote niliyachukuli pow tu, kumbe kuna kitu kizito kina kuja kwangu mpaka leo walimwengu wameshindwa kunijibu nitoke vipi
hiko kitu kizito kishakuja ? kama ndio ni kitu gani?
kama bado kwanini unahisi ni kitu kizito kinakija kwako?
 
Tukaondoka salama pale, Dada yangu akamwambia anti Sofia ukija Dar uje kunidfundisha kufanya visheti na kahawa yako, nimevipenda. Anti Sofia akaingia ndani akamtolea kopo zima la visheti, yale makopo ya biskuti makubwa. Akamwabia hii ndio biashara yangu kubwa hapa, navitengeneza kwa wingi wanaojua wananipa order, navipeleka sehemu nyingi sana, wewe ulikua hujui hii zawadi yako. Nakupa kwa sababu asingeolewa mamako unagekua mwanangu, kidogo babako anioe, huyo mdigo sijui akampa nini. Tukacheka tukaondoka.

Tulipoondoka kwenye gari nikajua dada yangu anamchokoza mama.
Dada; Anti Sofia anasema baba ilikua amuoe yeye wewe ukamt)roga kidogo akakuoa wewe, eti kweli? Ananesha alikua mzuri kweli?
Mama; Sofia anawatania, tu, amuoe miubwa kweli kwetu yule, kaolewa sisi bado tunasoma msimuone vile ana mwili mzuri. Lakini alikua mzuri mkweli, mpaka sasa mzuri .

Baba Sofia kajiweka pale kibiashara tu, pale anauza visheti Tanzania nzima, halafu hakuna Msomali anapita Chalinze bila kununua mirungi kwake, siku hizi haweki pale, anaweka kule uoande wa pili, kuna watu wake wanamuuzia, zinatembea simu tu, usimuone vile anapesa nyingi sana, yule muewe kamwachia Scania zaidi ya kumi, urithi wa wanawe. Huyomwanae mdogo wa kiume ndio anafanya kazi za kuzitrazama hizo. Hata wewe bwana mkubwa unazijua garizake, huwa zinakuja garage matra moja moja, zile anazokuja nazo Anko Abdi. Zile zote za Sofia na wanawe. Nikasema aaah, nimezijua na huto mwanae nimeshamjua, siku hizi wanzo benz moya mpya wamewachana na Scania kabisa.
Baba: ndio hizo hizo.
Mimi: Kweli ana pedsa, kwanini anakaa huku sasa?
Baba' Atahamia mjini hgivoi karibuni ana nyumba nyingi tu Dar. Hapa anatengeneza pesa nyingi sana, yule Waarabu wote wa Morogoro wanachukua kirungi kwake, magaru ya Wasomali na mengine mengi tu yanayopita hapa yanachukua miringi kwake. Yule kwa siku anafanya ya miilioni wo mpaka ishirini, usimuone vile.
Mama: Wasomali ni hodari sana kwa biashara.

Tukaneda mwndi mzuri tum hatukuchelewa sana tukawa tumeingia Dar, Vimbwanga vikaanzi mtaa wa Msimbazi, maana tulizunguka kupitia Kariakoo, kuna kitu mama alitaka kabla ya kwenda nyumbani. Ikabidi tupite Msimbazi.

Itaendelea.
Simulizi ni Nzuri, tatizo ni kwenye uandishi unachapia sana
 
Nijulishe bas wewe unayeyajua mkuu wangu. Maana nimeona hapa kuwa dunia sio duara so kuna tabu kuuliza vitu obvious ambavyo umekuta tu vinaaminiwa hivyo?
Hivi wanavyosema dunia ni duara maana yake kuwa ukichimba au kuingiza kitu kirefu sawa na diameter ya dunia kinaweza kutokea bara/Nchi/sehemu nyingine 🤔
 
Kwahyo mpaka angeita kwa kiarabu.....
Vitu vingi kwenye maswala ya kidini vimetoka kwenye lugha ya Aramaic (kwahyo nguvu halisi ya jina huwa ipo kwenye lugha yake ya asili...... Mfano Jibreel jina lake asili ni Gabriel 🤝

Jina ukiliingiza kwa lugha nyingine hupungua nguvu🤔
Maana unakuwa umelitafsiri

Mfano chukulia wakristo wanavyotoa pepo kwa jina la yesu..... Sasa wewe liingize jina yesu kwa kilugha cha kinyasa (mfano iwe Yesu = Kivumba)

Halafu nenda uanze mwambia pepo kwa jina pa kivumba.... Utaona kichapo chake mpk utatoka vumbi usoni


Kwahyo usikariri kwamba mambo lazima yaende kiarabu.... Nope Kuna lugha zingine zenye muujiza na nguvu kubwa kuliko Arabic🚶🚶🚶

(Kama nimekosea nipewe elim, maana mengi n mtizamo wangu tu)

Ndugu Arsis samahani kwa kutoa elim nisiokuwa na elim nayo.... Tusameheane vijana tunateleza🤝🤝
So ukienda nchi wanazoongea Kiingeeza ukasema toka kwa jina la Yesu pepo wa huko wanakupa kichapo? Vp kama pepo hao ni wa Kimasai utatumia jina gani?
 
Corazon Espinado.

Siyo utani. Kisa chako ni kizuri sana. Siyo kwa huo usimba ushuzi wako.

Kuna mengi yanaingia akilini. Ushauri wangu kwako, usiwe na haraka ya kupost ulichoandika. Andika post yako, tulizana, isome mara mbili tatu, rekebisha makosa ya kiuandishi kadri ya uwezo wako, kisha ndiyo post.

La pili ni ombi, naona kuna masuala ya dini yamejitokeza, natamani uniruhusu niyajibu ninavyoelewa mimi.

Mambo yako na majinni wako sikuingilii, nikiwa na swali huko ntauliza.

Ombi langu la mwisho kwako, tafadhali sana wachana na u foxy wangu na usimba wako. Tumekutana kwenye mtandao yaishie kwenye mtandao na mada zilizopo. Mjmi sikujuwi kabisa. Nikisema nakujuwa ni kwa kukutania tu. Ispokuwa, umemtaja mtu wa Shinyanga ambae nafahamiana nae toka utotoni, wamekuwa pamoja na mume wangu kwa ukaribu kabisa. Nawahamu ukoo wake wote. Ulichoelezea kijuujuu kuhusu huyo mtu wa Shinyanga ni ukweli mtupu.

Tafadhali nielewe, maana naona uzi umeshaingia watu wa jazba, wewe "remain cool" utupe kisa au visa vyako. Narudia, nimekipenda kisa chako, wachana na vile visa vyako vya usimba ushuzi.
Aisee, kumbe wakati mwingine huwa akili zako zinakaa sawa. Safi sana
 
Unataka nikujibu Arsis alisema nini kuhusu hilo? Sitaki jazba lakini, ni majibu ya Arsis.

Arsis aliwahi kusema"Yesu mwenyewe kajua siku hizi kua kuna watu wanamuita Yesu". Nikamuuliz kwanini? Akanambia Yesu hajawahi kuitwa hivyo duniani. mama yake Yesu alikua anaongea Kiaramu (Aramaic) na Kimisri. Nilipomuuliza zaidi akanambia "wewe hupendi kusoma. Hizo lugha zote mbili zinafanana sana na Kiarabu cha zamani".
Naona Arsis hana uelewa mpana kuhusu Ukristo...my first doubt
Mbona hujadaut uelewa wa Arsis kuhusu Uyaudi?
 
Simuoni ndugu mshana akitia neno kwenye huu uzi ! aidha siwaoni wadau wake wakimualika kuja kuona kama ilivyo sunna yao, kwa maana tumezoea kuona nyuzi zenye asili ya nguvu za asili basi zina mchango wake katika aidha utoaji wa maoni au uongezaji wa nyama. sina maana kuwa ni lazima awepo kwa vile JF ni kubwa kuliko Mshana na kwa kusema hivyo sina maana ya kumdogosha Mshana.

hii thread ni miongoni mwa zile nazoweza kuziita ni multifunctioning kwa maana ya kwamba kwanza ni burudani kwa vile ni simulizi lakini pili, ni kile nachoweza kusema ni elimifu na inaibua hisia kwa vile tumeweza kufahamu au kusoma habari ambazo tusingetegemea kuzisikia mahala kwingine kama tusingezisoma hapa. binafsi siwezi kutoa credit kuwa ni kweli au ni kinywaji cha wazee lakini i am there watching.

My attention kwenye thread hii ni kuwa khaa kumbe even spirits ie Arsis are or may put in application matumizi ya vitu vya kibinadamu kama vile simu na namna members wanavyojibizana na msadikika Arsis kupitia jukwaa ! hii inafanya nijiulize ni kwa vipi Simba anampatia kifaa cha mawasiliano ya kibinadamu rafiki yake wakati hawaonani ?. but whatever it may be.

Kitu kinachofanya niamini walau kwa mbaaali sana kuwa may be jamaa ni spirit kweli na ako hapa tunazungumza ni pamoja na uvumilivu wa kimazungumzo aliokuwa nao. anaambiwa maneno ya karaha lakini yeye hajibu karaha, ame relax sana anakutizameni mnavyorukaruka kuvitetea vitabu vyetu vitukufu. kwa mfano mtu kaambiwa alete maandiko yanayosema kuwa Adam ndiye mtu wa kwanza ndani ya Qur an, badala ya kusema kwanza hakuna then ndo alete excuse ya alternative verses ! and infact haipunguzi chochote katika imani yako kwani waislamu tunaelekezwa kuacha ujuaji pale tusipolielewa jambo kwa undani wake, lakini mtu huyo ataanza kuleta aya ambazo hazitoshi kujibu explicit question on table. na hakubali kuwa hakuna, and by the way kama haipo haipo tu na wala haibatilishi uhalali wa qur an kwa mujibu wa qur an yenyewe ukisoma sura ya kwanza aya ya pili.

Lakini pia ishara ndogo nyingine ya kwamba labda ni kweli jamaa ni spirit ni ; tabia ya utoto anayoionesha katika majibizano yake. binafsi sina elimu ya majini na watu wasioonekana kwa vile amesema yeye ni mtu, lakini ufahamu wangu mdogo katika dini yetu ni kwamba spirits wana ile inferiority complex juu ya mwanadamu ! wako na wivu juu vile mwanadamu ndio kiongozi wa dunia na hawakupenda kwahio, wherever they are in contact with us they want to show us that they are better than us na hivyo anachokisema yeye hataki kibishiwe, you don't have to reason before his or her eyes ,just say "yes sir", ndio kusema; badala waendelee na mazungumzo ya kuwa watu wengine ni kina nani before Adam, yeye anang'ang'ania ni lazima mkiri kwanza qur an haijasema kuwa Adam ndiye mtu wa kwanza na Hawa hajawa adressed ndani ya kitabu hicho. na nimeona mahala mtu akimpledge Arsis basi jamaa hufurahi sana. hahahaha ndo jamaa walivyo najua nyie mnafahamu watoto waking'ang'ania kitu how it appears, hususan wanaogombania nani mkubwa kuliko nani jaribu kuconnect.

Kuhusu juju wa majuju nilifurahi niliposkia wana dunia yao ya kujitegemea kutoka kwa mwamba huyu Arsis, lakini kuna fikra iliyopita kama umeme kwenye kichwa changu kwa vile nakumbuka when i was in my O level studies nilikuwa nimekwisha wiva kiasi kuhusu dini ya kiislamu[ nimesoma seminary ya kiislamu ilemela mwanza], sasa kuna kitabu kimoja kilichokuwa katika lugha ya kiarabu kilikuwa kinazungumza kuhusu dalili za kiyama, dini yetu inaeleza kuwa hao raia[AKINA JUJU] watakuja nyakati za mwisho kuifisadi dunia sasa, ndani ya kile kitabu sehemu inayowaeleza hawa wadudu wenye uzito wake palichorwa ukuta fulani hivi kama ngome na kwamba watakapokuja duniani kufanya ufisadi watapitia maeneo hayo.

hiyo ngome tuliisema kwa mengi na kimsingi yalikuwa ni mawazo yetu kama growing elites kwamba inawezekana ndio ule ukuta tulioambiwa na vitabu kuwa jamaa wanaula kuanzia asubuhi hadi jioni, kisha kitapobaki kipande kidogo kutoboa duniani basi jioni ingefika na wangerudi kulala huku wakisema aaah hapa tutapamalizia kesho bila kusema Allah akipenda[INSHAA ALLAH]. basi kesho wangeukuta hivyo na ikawa zoezi la kila siku mpaka siku watakapompa credit muumba wao basi watakuta mambo kama walivyotarajia na hatimae kuingia duniani.

kwa wale wapenzi wa movie ukuta huo umeoneshwa kwenye movie moja siifahamu jina lake kwa vile siyo mambo yangu hayo, ni movie ya kichina sasa kuna wanyama hao walikuwa na kazi ya kuvamia ngome ile ni wakali balaa na ni wengi kuliko walivyo hata ! najua umenilewa, so wanashambulia mpk watapoweza lakin badae wataondoka.

Sasa fikra zangu zinaniambia kwamba hahahaha eti kwa vile Qur an imeeleza kuwa hawa wadudu wapo lakini haikusema wapo wapi, na kwa vile Arsis anatuambia wapo dunia yao huko hapaendeki, na kwa vile wapo wanaojitahidi kusema kuwa hilo eneo hapo china ndo kuna mlango wao, basi najaribu kufikiri kuwa hapo kwenye hiyo ngome kuna mlango wengine mnasema cjui portal, ambayo inaweza kumtoa kiumbe hapa duniani kwetu kwenda dunia zingine ikiwemo hiyo ya kina juju, haya ni mawazo tu baada ya kula ugali sihitaji ligi pia mwenye mawazo au ufahamu zaidi basi tutaendelea kusomana.The story is telling kwa kweli , kuanzia kule sokoni chalinze, shinyanga, tabora, tanga na hata unguja huko,

Ushauri wangu kwa wasomaji, put away hizo fanatic feelings zote pembeni[udini], then open to learn utajifunza habari nyingi sana kwa vile walioishi kabla yetu hawakuswali swala tano wala kushika misalaba.

Mwisho niwaombe radhi kwanza kwa maneno mengi ilihali uzi sio wa kwangu, pili kwa makosa ya kiuandishi yatakayoonekana kwa vile sinaga kawaida ya kupitia mara mbilimbili nilichoandika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom