Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,480
- 40,480
Nawaza zawadi ya kumpatia mke wangu kama 'surprise' tu, kutokana na changamoto alizopitia mwaka jana, mwezi kama huu, mpaka ikafikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi.
Alifiwa na mzazi wake aliyempenda sana; aliyekuwa akimuuguza muda mrefu.
Kabla ya mzazi wake hajafariki, ndani ya wiki mbili hivi, 'wife' akafanyiwa upasuaji mkubwa, hajamaliza hata wiki, akatakiwa kufanyiwa tiba ya mionzi. Ile kuanza tu tiba ya mionzi, mzazi wake akafariki.
Ndani ya muda mfupi, vichwa vilikuwa vimevurugika sana; lakini tuliweza kuhimili ingawa changamoto zilikuwa nyingi.
Sasa nawaza, nimpe zawadi gani itakayomsababisha kutoa machozi ya furaha, iwe kama 'surprise'.
Kama gari, yeye siyo mpenzi sana, hata lililopo huwa halitumii; kama ni nyumba, anaweza asione kama zawadi, kwa sababu itakuwa kama sehemu ya familia (yeye na watoto).
Nawaza, zawadi ambayo yeye ataiona inamgusa yeye tu.
Karibuni kwa mawazo.