Je, hauna furaha kabisa na hujui chanzo chake na kila njia unatumia haileti matumaini kwako?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,518
14,383
Kukosa furaha kabisa kwa muda mrefu sana bila sababu yoyote ya msingi huwa ni kiashiria cha tatizo sugu ambalo unakuwa upo nalo kwa muda mrefu sana bila kulipatia ufumbuzi.

Kuna tatizo la kisaikolojia ambalo huitwa PTSD -KIWEWE CHA MATUKIO YENYE KUUMIZA, KUHUZUNISHA NA KUSHTUA SANA.

Ambapo kwa kiingereza huitwa PTSD - POST-TRAUMATIC STRESS DISORDER, ikiwa maana hali ya mfadhaiko wa akili, huzuni na msongo wa mawazo ambao hutokea baada ya mtu kupatwa na matatizo yenye kushtua,kuumiza sana na kuhuzunisha sana.

Matukio hayo yanaweza kuwa kupigwa, kutekwa nyara, kushuhudia mauaji, kushuhudia ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi, kubakwa au ulawiti, kufanyiwa unyanyasaji ndani ya familia,kupata ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu,kuugua kwa muda mrefu sana, kunusurika kuuawa, kushuhudia mapigano makali sana yenye kumwaga damu n.k.

Ambapo muhanga wa tukio anakuwa anatumia muda mwingi sana kufikiria sana Matukio hayo mpaka hawezi kufurahia chochote katika maisha yake.

Kujua kama upo na PTSD jibu maswali yafuatayo kuhusu historia yako ya utotoni chini ya miaka 10;

1. Je, mzazi wako au mtu mkubwa kwako nyumbani kwenu utotoni mwako mara kwa mara alikuwa anakufokea, kukutukana, kukukosoa kupita kiasi, kukulaumu sana, kukushambulia kwa maneno makali sana,kukufanya uwe na hofu ya kuumizwa kimwili?

2. Je, mzazi wako au mtu mkubwa kwako nyumbani kwenu utotoni mwako mara kwa mara alikuwa anakupiga, kukusukuma chini, kukubamiza ukutani, kukurushia vitu vyenye kudhuru mwili au alikupiga sana mpaka umepata makovu?

3. Je, mtu mkubwa kwako au mwenye kukuzidi umri wa miaka 5 au zaidi nyumbani kwenu mara kwa mara alikuwa anashika mwili wako kwa njia ya kukutaka kimapenzi?

4. Je, umekuwa ukiishi nyumbani kwenu na kuhisi hakuna mtu yeyote anaona fahari kuishi na wewe pamoja au hakuna mtu yeyote anakupenda? Je ndugu zako hawapendani, hawana ushirikiano, hawana mahusiano mazuri,hakuna mwenye kumsaidia mwenzake?

5. Je, mara nyingi ulikuwa hupati chakula,ulivaa nguo chafu, ulitembea bila viatu, ulikosa mtu wa kukulinda na kukutetea, ulikosa mtu wa kusikiliza maumivu yako, je wazazi wako walikuwa wagonjwa sana au ulipokuwa ukiugua mara kwa mara hukupelekwa hospitali?

6. Je, mama yako mzazi au mlezi mara kwa mara uliona anapigwa, kusukumwa chini, kutukanwa, kufokewa, kudhalilishwa hadharani, kupigwa ngumi, kupigwa kitu kizito mwilini,kutishiwa silaha, kubamizwa ukutani, kupigwa ngumi, kurushiwa vitu vyenye kudhuru mwili?

7. Je, ulipokuwa mdogo uliishi na mtu ambaye alikuwa mlevi kupindukia au mwenye kutumia bangi au dawa za kulevya?

8. Je, utotoni mwako umeishi na mtu nyumbani kwenu ambaye alikuwa na huzuni kupita kiasi,alikuwa mgonjwa wa akili,au ambaye aliwahi kupelekwa hospitali kwa matibabu ya ugonjwa wa akili, je kuna mtu nyumbani kwenu alitaka kujiua bila mafanikio?

9. Je, ulipokuwa mdogo wazazi wako walitengana au walikuwa wanaishi sehemu tofauti au walipeana talaka?

10. Je, nyumbani kwenu kuna mtu alifungwa jela au alikuwa anafungwa jela na kutoka kisha anarudi tena jela?

Kama umejibu NDIYO maswali kwanzia 4+ hicho ndio chanzo cha kuishi maisha ya upweke kupita kiasi,hasira kupita kiasi na huzuni kupita kiasi kwa muda mrefu.

Matukio ambayo huzidisha màumivu moyoni kama upo na historia yenye matukio yenye kuumiza ni pamoja na kupitia ubaguzi ndani ya familia au shuleni, kufanywa kichekesho, kubakwa au ulawiti,kupigwa sana, kufokewa, kutukanwa, kudhalilishwa hadharani, kuishi maisha ya upweke kupita kiasi na umasikini kupita kiasi, kupata ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu, kupata malezi ya mzazi mmoja au kukosa kabisa malezi ya mzazi labda kwa sababu ya kifo cha mzazi au kutenganishwa na wazazi, kutekwa nyara, kunusurika kuuawa, kuambukizwa ugonjwa usiokuwa na tiba.

MABADILIKO YA MWILI KAMA UPO NA PTSD-KIWEWE CHA MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA NA KUSHTUA SANA

a. Kujaribu kukwepa watu, mazingira au mazungumzo yenye kukumbusha tukio hilo,kujaribu kuwakwepa watu , sehemu au hali yenye kukumbusha tukio hilo.

b. Kupoteza kumbukumbu za matukio husika, kupoteza uwezo wa kufurahia vitu umezoea kufurahia,kushindwa kujenga mahusiano mazuri na watu wengine.

c. Kupoteza hisia kabisa,kukosa huruma kwa wengine. Kushindwa kupenda wengine, kupoteza hisia za kujumuika katika shughuli za kijamii, kuchanganyikiwa haraka sana, kuonekana mwenye hasira kupita kiasi muda wote.

d. Kushindwa kuhuzunika kwa jambo lolote baya, kupoteza hamasa ya kuwa na mwenza,watoto au kazi , kupoteza kumbukumbu mara kwa mara.

e. kuota ndoto za kutisha zenye kukumbusha tukio hilo,kushindwa au kujuta sana, kujilaumu, kujikosoa kupita kiasi,uchovu kupita kiasi,kukosa usingizi au kulala sana mpaka unachoka.

f. kujitenga na watu wa karibu, kupoteza hamu ya kula au kula sana vyakula bila mpangilio, kulala popote,kuacha kufanya usafi binafsi, kutetemeka sana, kuogopa sana baadhi ya sauti,harufu,mwanga mkali na sauti kali .

g. Kutafuna meno,hofu kupita kiasi,kujiona upo hatarini muda wote,kuhisi kitu kibaya kinataka kutokea ghafla,kukosa umakini na utulivu,kushindwa kutuliza akili sehemu moja.

h. Kushindwa kufikiria vizuri,kutaka kujiua,kufanya maamuzi kwa hasira mara kwa mara,kufanya makosa yenye kujirudia rudia,kushindwa kuamini watu.

i. kupata màumivu makali sana ya viungo, kupaniki, kuchanganyikiwa, tumbo kuvurugika, kuumwa kichwa na mgongo,moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kichefuchefu.

j. kupoteza hisia kwenye vidole, kubanwa kifua, pumzi kuwa ngumu, kuumia kooni, kutetemeka.

NJIA HATARI WATU WENGI HUTUMIA KUKABILIANA NA TATIZO LA PTSD-KIWEWE CHA MATUKIO YENYE KUUMIZA SANA NA KUSHTUA SANA

a.Kunywa pombe kupindukia, kuvuta bangi au dawa za kulevya, kutumia pesa nyingi sana, kubadilisha wanawake au wanaume mfululizo, kuendesha vyombo vya moto kwa kasi sana.

MADHARA YA NJIA HIZO

Madhara yake kiafya huchochea hofu kupita kiasi,woga, wasiwasi na hasira kupita kiasi yenye kuathiri mwili kwa kufanya mwili Kupoteza hisia za mapenzi mpaka watumie dawa za kusisimua, shinikizo la damu, kupooza, kuugua mara kwa mara, kisukari, madonda tumbo, uvimbe, matatizo ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

UFUMBUZI WAKE

Mtu mwenye tatizo hilo hawezi kujipa MSAADA yeye mwenyewe na wapo wangi hupoteza fedha nyingi na muda mwingi sana kwa kutafuta msaada kwa watu wasiokuwa na elimu ya kutosha wala hawana uzoefu wowote wa kukabiliana na matatizo hayo.

Ikiwa unatafuta msaada sehemu ambayo sio sahihi utatumia miaka mingi sana bila kuona nafuu yoyote na utapoteza fedha nyingi sana eneo hilo kwa sababu PTSD sio kitu rahisi kwa mtu yeyote kutoa ufumbuzi wake.

Kuna njia mbalimbali unaweza kutumia chini ya uangalizi wa mtaalamu kama vile kuandika historia yako kwenye karatasi kwa muongozo maalumu, kufanya mazoezi ya viungo, RELAXATION TECHNIQUES utapewa maelekezo, njia ya mazungumzo na mtaalamu, kuwa na mtu anaeweza kufuatilia mabadiliko ya hali yako mara kwa mara, kuwa na mtu anaeweza kuelewa undani wa tatizo lako kwa kina bila kukushambulia wala kukulaumu kwa jambo lolote.
 
Brother hujawahi kutana na wanaume ambao hawana kazi halafu age inazidi kwenda mbaya awe ana watoto,,,huwa hawana furaha kabisa halafu wana hasira kichizii!!!
 
Lakini
Brother hujawahi kutana na wanaume ambao hawana kazi halafu age inazidi kwenda mbaya awe ana watoto,,,huwa hawana furaha kabisa halafu wana hasira kichizii!!!
Brother hakuna kinachodumu hata hizo hasira huwa hazipo wakati wote sasa ukikutana na mtu mwenye hasira mwambie avute hewa kwa sekunde 5 halafu aanze kuitoa taratibu hasira zote zitaondoka na mapigo ya moyo yatakaa sawa.
 
Lakini

Brother hakuna kinachodumu hata hizo hasira huwa hazipo wakati wote sasa ukikutana na mtu mwenye hasira mwambie avute hewa kwa sekunde 5 halafu aanze kuitoa taratibu hasira zote zitaondoka na mapigo ya moyo yatakaa sawa.
kuondokana na iyo hali ni wao kupata kazi tofauti na hapo ni kuforce jabali kuzama kwenye maji.
 
Mashambulio ya kiroho pia ni chanzo kikuu Cha ukosefu wa furaha na kushuka moyo pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom