Nyakati ngumu huwa kwajiili ya kutufunza na nyakati za furaha ni kwaajili ya kumbukumbu nzuri za maana ya kuishi

boniuso

JF-Expert Member
Mar 13, 2013
680
852
UKIBADILI NAMNA UNAVYO TAZAMA VITU NA VITU UNAVYOTAZAMA HUBADILIKA
Kinachotokea sio tatizo ila tafsiri unayoweka juu yake ndio inaweza kuuwa tatizo

Kikwazo chochote kinachotokea huwa kinakuja kuboresha sehemu ya maisha yetu

Usitazame vikwazo kwa ubaya wake tazama vikwazo kwa mazuri yake

Kila kitu hutokea kwa sababu na ikiwa hujui sababu bado sababu ipo

Watu huwa wanahukumu matokeo badala ya kuuliza sababu ya matokeo husika

Ukiona matokeo yeyote yawe mazuri au mbaya tambua kuwa zipo sababu nyuma yake

Usipojua sababu ya matokeo fulani huwezi kurekebisha dosari za matokeo husika

Watu wengi huwa wanalaumu wenzao kwa maamuzi wamefanya au hawakufanya ila hawana muda kujua siri iliyopo nyuma ya pazia

Usiwe kama watu wengi ukiona matokeo huyaelewi uliza sababu ya matokeo hayo bila kutoa hukumu haraka

Kufikiri ni kazi sana ndio sababu watu wenye wanahukumu haraka

Usihukumu jambo kwa kuangalia upande wako limeathiri kiasi gani bali angalia jambo kupitia upande wa tatizo

Ukiangalia maumivu unayopitia utaona haustahili kupata maumivu lakini ukiangalia kosa lako au fundisho lenye kupatikana katika maumivu hayo utaona sehemu ya kurekebisha

Ikiwa huoni unapokosea huwezi kujirekebisha na utapata matokeo yaleyale

Binadamu hawezi kujifunza anapoamini anajua tayari

Unaweza kupoteza uwapendao,unaweza kupoteza fedha, unaweza kupoteza kazi,unaweza kutengwa,unaweza kunyimwa misaada katika dhiki,unaweza kupewa ahadi na zikavunjwa ila yote hutakiwi kusema kwanini napatikana na haya

Badala yake jiulize chanzo cha hayo yote ni kitu gani

Ukijua chanzo cha tatizo unaweza kukabiliana na tatizo

Usipojua chanzo cha matatizo ni vigumu kukabiliana na matatizo kwa sababu huwezi kujua wapi sahihi pa kuanzia

Wengi wakipata ugumu kwenye maisha huona kama hawastahili kupata ugumu huo

Ukweli ni kuwa matatizo huwa yanakuja yenyewe wala hayana mualiko

Furahia haiwezi kujileta yenyewe hivyo usipotafuta sababu ya kufurahi huwezi kufurahia maisha yako

Bila kujali nini umefanya au hukufanya mpaka umefika hapo ulipo huna sababu ya kujichukia kwa uamuzi ulifanya au hukufanya

Siku mbaya zinakupa kukupa masomo na siku nzuri zinakupa kumbukumbu za furaha

Huwezi kuthamini ushindi bila kushindwa

Huwezi kuthamini afya bila maradhi

Huwezi kuthamini upendo wa dhati bila kupata usaliti

Huwezi kuthamini akiba bila kuona madhara ya kutoweka akiba

Hivyo kila kitu hutokea kwa sababu

Usifanye siku mbaya kama vile maisha yako yote ni mabaya

Hakuna binadamu ambaye hafanyi makosa hivyo kukosea ni kawaida sana

Ikiwa unapitia kipindi kigumu kumbuka kuwa kuna mtu tayari amepitia nyakati ngumu hapo awali na aliweza kuvuka hivyo jiulize aliweza vipi kuvuka kisha na wewe vuka

Kurudia kumbukumbu za maisha ya zamani kila wakati mpaka unaona maisha ya zamani pekee ndio yalitakiwa kudumu ni kupoteza muda

Huwezi kufurahia maisha ikiwa unaona maisha ya miaka ya nyuma ndio mazuri huku ya sasa unaona hukustahili kuishi

Hakuna maisha yenye kudumu
Ukiona upo kwenye furaha ujue matatizo yapo njiani na ukiona maisha ni magumu sana ujue nafuu ipo njiani

Maisha siku zote ni mfululizo wa matatizo kama mawimbi ya bahari

Kwa maana mawimbi yapo makubwa kwa madogo lakini haiwezekani mawimbi kukosekana baharini

Fursa ni kama dala dala ikikupata moja nyengine ipo njiani

Ukitazama sana fursa umepoteza utaona wewe ni mbaya sana,mwenye mikosi,asiwe na jema n.k lakini kutazama mabaya tu katika maisha yako huzidisha maumivu

Huwezi kujisikia vizuri wakati muda wote unakumbuka matatizo yako badala ya mazuri yako

Hauna matatizo yote ya ulimwengu hivyo tabasamu

Wakati mwengine utapoteza watu ambao uliamini kuwa hao ndio wangefanya maisha yako kuwa mazuri

Kuna wakati unaweza kupoteza kazi nzuri ambayo unaona kama kazi pekee duniani ambayo bila kazi hiyo huwezi kuishi

Kuona maisha yako yatakuwa magumu sana kwa sababu huna kitu fulani au kwa sababu umepoteza mtu au kitu muhimu kutazidisha maumivu kwako

Huwezi kufurahia maisha ikiwa unaona matatizo yako muda wote

Tazama mafunzo katika kila ugumu usitazame kwa nini wewe ndio unapata ugumu huo

Hakuna mtu mwenye mahusiano yenye furaha saa 24,wala mwenye kujiamini kwa 100% kila binadamu huwa anatilia shaka uwezo wake na kipaji chake pale haoni matokeo mazuri huku juhudi ameweka kubwa sana

Kumbuka mafanikio hupimwa kwa mchakato sio matokeo

Ukipima mafanikio kwa matokeo utakata tamaa haraka sana

Huwezi kudhibiti matokeo bali unaweza kuongeza au kupunguza juhudi zako

Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)

6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
 
Back
Top Bottom