Kifo cha MC Joel Misesemo ni changamoto ya afya ya akili

Lukumba

Member
May 24, 2023
35
91
Ndani ya wiki hii kumekuwa na matukio mawili ya kushtusha ndani ya Kijitonyama yote yakihusiana na majengo aina ya ghorofa ambapo moja limepelekea kifo cha MC Joel kwa kujirusha toka ghrofa ya kumi na tano na lingine kufeli kwa lift ya kupandisha na kushusha na kupandisha watu ghorofani ndani ya Millenium Tower.

MWISHO WA ANDIKO HILI TUANGALIE VIDEO CLIP YA HUYU MTU JINSI ALIVYOJIRUSHA PAMOJA NA WATU KUMUOMBA HASIFANYE IVYO , YOTE YA YOTE TUNACHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI , HAKUNA WA KULAUMIWA.

Binafsi najikita katika issue ya MC Joel alieamua kukatisha uhai wake kutokana na changamoto zake za kimaisha zilizopelekea afya ya akili kutokuwa sawa , toka kifo kimetokea kumekuwa na maneno mengi sana hasa wengine wakihusisha kifo hicho na imani za kishirikina kama kutupiwa majini , wengine wanasema kauwawa kutokana na mazingira ya kifo kuwa mtu hawezi kutoka nyumbani kwake akawasaha gari akaendesha na akapanda juu kutoka ghorofa ya kwanza mpaka ya 15 na kujipoteza binasfi nasema hii inawezekana na akili ya binadamu inapanga vitu vingi kwa muda mrefu .

Kumfahamu mtu pamoja na kazi zake , biashara zake , familia yake , ucheshi wake hivi vyote sio sababu ya kusema kuwa kwanini fulani kafa vile wakati alikuwa mtu poa nikuambie ndugu changamoto ya afya akili kwasasa ni kubwa kuliko hata changamoto vya virusi vya ukimwi binadamu anaweza kukuonesha kila kitu lakini kile alichosema hapana hauwezi kujua na akiamua kufanya hivyo jua hiyo ni siri yake na maamuzi yake.

Jiulize kwanini kwa sasa mauaji ya kikatili yamekuwa makubwa sana , Jiulize kwanini Binadamu kwasasa anaogopeka kuliko hata huyu mnyama Simba , ukisha jiuliza hivyo unaweza kujua kinachoendelea juu ya changamoto ya Afya ya akili inavyotumaliza kwasasa.

Magonjwa ya Akili ni Nini na husababishwa na Nini?•
Magonjwa ya akili ni matatizo yaubongo ambayo humfanya mtukuwa na hisia, fikira na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii na kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha ambazo mwisho zinampelekea ugonjwa wa afya ya akili.

• Magonjwa ya akili yanaweza kusababishwa na sababu za kibaiolojia au kisaikolojia;Sababu za kibiolojia
• Kurithi vinasaba kutoka kwawazazi.
• Magonjwa ya muda mrefu kamadegedege, malaria kali, UKIMWI
• Matumizi ya dawa za kulevya ,
• Majanga, ubakaji, uvamizi, ajali,utekaji nyara, kukosa elimu,kukosa ajira
• Kufiwa, kutengana,talaka, ugoni,kufungwa
• Kufukuzwakazi,kukosamishahara,kustaafu kazi .
• Kutokufanya vizuri kwenyemasomo na Kufukuzwa chuo/shule
• Matatizo yanayowaathiri watoto

Dalili za Kiakili
• Kukosa umakini wa shughuli zakeza kila siku
• Kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu
• Kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti
• Kutokujali
• Kuwa na imani zisizo za kawaida kama vile; Kuwa mtu maarufu au Nabii , Kupokea taarifa kutokakwenye redio au mitandao ya simu , Imani ya kuwasiliana na watu maarufu Kuamini kuwa na nguvu ya ziada kutoka nje ya mwili Imani kuwa kuna watu wanamfuatilia au wanataka kumdhuru.
• Mawazo yake hayana mtiririko unaoeleweka.

Dalili za Kihisia
• Kusikia sauti ambazo watuwengine hawazisikii
• Kuona vitu ambavyo watuwengine hawavioni
• Kuhisi kufuatiliwa na watu
• Wivu uliopitiliza
• Kuhisi mawazo yake yanajulikana na watu wengineau yanazungumzwa kwenye vyombo vya habari
• Kuhisi kuwa mtu anatumia mawazo yake kufanya mambo Fulani
• Kuhisi harufu ambayo watu wengine hawaisikii
• Kuhisi maisha hayana thamanina kuona bora kufa kuliko kuishi.

Dalili za Kimwili
• Kukosa furaha au kuwa na furahakupita kiasi
• Kuwa na wasiwasi au wogakupita kiasi
• Kupunguzakuongeaau kuongeakupita kiasi
• Hasira za haraka na kufikia hatuaya kudhuru watu au kuharibuvitu.
• Kuwa na msongo wa mawazo
• Kujitenga na watu na kupendakukaa mwenyewe muda mwingi
• Kutokuwa na ari ya kufanya kaziau kufanya kazi nyingi kwa wakatimmoja bila ya kuzikamilisha
• Kutokuonyesha hisia yoyote usonimwake [furaha au huzuni].

EBU TUANGALIE HUYU MTU JINSI ALIVYOJIRUSHA PAMOJA NA WATU KUMUOMBA HASIFANYE IVYO , YOTE YA YOTE TUANCHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI ,HAKUNA WA KULAUMIWA
 

Attachments

  • picha.jpg
    picha.jpg
    104.2 KB · Views: 13
  • kajirusha.mp4
    4.7 MB
Suluhisho ni lipi ukijihisi unapitia changamoto za Afya ya Akili ?

Tiba Ya Magonjwa Ya Akili:

Matibabu ya changamoto ya akili hutofautiana kati ya ugonjwa mmoja na mwingine.

Matibabu hayo ni pamoja na;

1) Elimu kwa jamii kuhusiana na magonjwa ya akili ni kitu cha muhimu sana katika kuzuia kujirudia au kupata ugonjwa wa akili, juu ya matibabu na msaada anaohitaji mgonjwa ili kuendelea na maisha yake ya kila siku.

2) Kupatiwa uchunguzi mapema ili apatiwe tiba sahihi na ya mapema.

3) Tiba ya kisaikolojia (kujitambua aliko, anapotaka kuwa na kuamua kufanya mabadiliko kwa kutegemea uwezo wake mwenyewe).

4) Tiba kimwili kutumia dawa za hospitali.

5) Matibabu kwenye nyumba za upataji nafuu (sober house).

6) Ushirikiano kati ya mgonjwa, familia na wataalamu wa tiba huleta mafanikio makubwa sana katika matibabu.

7) Kutokutumia madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na vilevi.

8) Kupata muda mrefu wa kupumzika.

9) Fanya mazoezi.

10) Usijitenge na jamii zungumza na watu bila kuona aibu.

11) Kujibidisha kwenye shuguli za kuleta kipato.
 

Tiba Ya Magonjwa Ya Akili:

Matibabu ya changamoto ya akili hutofautiana kati ya ugonjwa mmoja na mwingine.

Matibabu hayo ni pamoja na;

1) Elimu kwa jamii kuhusiana na magonjwa ya akili ni kitu cha muhimu sana katika kuzuia kujirudia au kupata ugonjwa wa akili, juu ya matibabu na msaada anaohitaji mgonjwa ili kuendelea na maisha yake ya kila siku.

2) Kupatiwa uchunguzi mapema ili apatiwe tiba sahihi na ya mapema.

3) Tiba ya kisaikolojia (kujitambua aliko, anapotaka kuwa na kuamua kufanya mabadiliko kwa kutegemea uwezo wake mwenyewe).

4) Tiba kimwili kutumia dawa za hospitali.

5) Matibabu kwenye nyumba za upataji nafuu (sober house).

6) Ushirikiano kati ya mgonjwa, familia na wataalamu wa tiba huleta mafanikio makubwa sana katika matibabu.

7) Kutokutumia madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na vilevi.

8) Kupata muda mrefu wa kupumzika.

9) Fanya mazoezi.

10) Usijitenge na jamii zungumza na watu bila kuona aibu.

11) Kujibidisha kwenye shuguli za kuleta kipato.
Nice
 
Back
Top Bottom