Kwanini baadhi ya watu huonekana kuwa na furaha sana huku wengine wakiwa na hasira sana muda wote?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,481
14,329
Sisi sote huwa tunakuwa na hasira baadhi ya nyakati za maisha ya kila siku lakini wapo watu wengine kwao ni tofauti kabisa wanakuwa na hasira kupita kiasi muda wote.

Kwanini watu wawili wanaweza kupatwa na matatizo yenye kufanana lakini mmoja anakuwa na matumaini ya kurejesha furaha wakati mwingine anakuwa na hasira kupita kiasi na kukata tamaa?.

Leo tuangalie tatizo la hasira kupita kiasi, viashiria vyake, vyanzo vyake,madhara yake na ufumbuzi wake.

Kisaikolojia hali ya mtu kuwa na hasira kupita kiasi huitwa Intermittent Explosive Anger .

VIASHIRIA VYA TATIZO LA HASIRA KUPITA KIASI :TABIA ZAKE (Intermittent Explosive Anger)
Mtu mwenye tatizo la hasira kupita kiasi (Intermittent Explosive Anger) huonyesha viashiria vifuatavyo
a.Kufoka sana ,kutoa vitisho, kufululiza matukio ya majibizano mara kwa mara na watu wa karibu,kutishia kujiua au kuua wengine,kupiga ngumi ukutani ,kuvunja vunja vitu,

b.kupigana kwa kutumia silaha,kufanya vurugu mara kwa mara ndani ya familia, kushindwa kuvumilia utani,kuibuka ugomvi baada ya kuambiwa makosa yake au mapungufu yake,kuwa mkali sana kwa vitu vidogo vidogo sana,kujihisi muda wote

VIASHIRIA VYA TATIZO LA HASIRA KUPITA KIASI: MABADILIKO YA MWILI
Kwa mtu mwenye hasira kupita kiasi yeye mwenyewe ataona mabadiliko mwilini mwake pale ambapo anakuwa na hasira kupita kiasi
a.Kupata msukumo mkubwa kutoka ndani ya mwili ili kufanya au kuongea kitu kibaya kwa wengine,kuumwa kichwa na mgongo,

b.Moyo kwenda mbio sana, kifua kubana, misuli kukaza sana, kutetemeka sana, miguu kuishiwa nguvu, kuchanganyikiwa, tumbo kuvurugika, kupoteza hisia kwenye vidole

c.Kukosa utulivu,kushindwa kutuliza akili sehemu moja,kuona aibu sana na kutamani kulipiza kisasi,kuumia sana kooni,moyo kuuma sana, kutamani kulia

d.Kizunguzungu,uchovu mwili mzima, kichefuchefu, kupaniki,fikra kuvurugika, kuhisi unataka kudondoka ghafla, kuhisi unataka kurukwa akili, kuhisi unataka kufa ghafla

e.Kupata mshtuko wa moyo,kuwa na huzuni kupita kiasi,kuanza kulia,kujiona mpweke sana, kujiona huna thamani, kujiona hueleweki ukianza kuongea

f.Kujikosoa sana, kujilaumu, kujichukia kupita kiasi, kutamani kujiua au kuua,kuumia sana kwa kumbukumbu za tukio,kukosa nguvu ya kufanya kazi

g.Kupoteza hamasa ya kufanya kazi,kuchukia mtu yeyote anataka ukaribu, kupoteza hisia za mapenzi, kupoteza hamu ya kula au kula sana vyakula bila mpangilio

h.Kukosa usingizi muda wote au kujilazimisha kulala sana mpaka unachoka, kujitenga na watu wa karibu,kuanza majibizano mara kwa mara na watu wa karibu

i.Kujiona unadharaulika,kujiona upo hatarini muda wote,kuhisi kitu kibaya kinataka kutokea ghafla, kupoteza kumbukumbu,kushindwa kuona na kusikia vizuri

j.Maumivu makali sana ya viungo, kupoteza matumaini,kushindwa kujenga mawazo kichwani.

VYANZO VYA TATIZO LA HASIRA KUPITA KIASI (Intermittent Explosive Anger)
Kuna vyanzo vitatu vya tatizo la hasira kupita kiasi ambavyo ni familia, mazingira na upungufu wa homoni za serotonin.

I.KURITHI KWENYE FAMILIA
Mtu mwenye hasira kupita kiasi anaweza kujenga tabia hiyo kwa sababu ya kurithi kwenye familia yake.Ikiwa umepata mzazi au wazazi wenye hasira kupita kiasi (Intermittent Explosive Anger) utakuwa hatarini kupata tatizo la hasira kupita kiasi kwa njia zifuatazo
Mzazi mwenye hasira kupita kiasi huonyesha tabia zifuatazo zenye kuathiri tabia ya mtoto

a.MANENO MAKALI
Mzazi mwenye hasira kupita kiasi mara kwa mara iwe kwa makusudi au bila kukusudia huwa anaongea maneno makali sana kwa mtoto anaweza kufoka sana, kumtukana sana mtoto, kumdhalilisha, kumtishia kumdhuru mtoto, kumuita majina ya aibu,kumtenga,kumbagua kwa maneno makali sana,kukataa ukaribu na mtoto,kumkosoa kupita kiasi kwa vitu vidogo vidogo sana,kukumbusha makosa ya zamani kila siku,kumtabiria mtoto maisha mabaya sana,

b.ADHABU KUPITA KIASI
kwa mzazi mwenye hasira kupita kiasi (Intermittent Explosive Anger) anaamini adhabu kupita kiasi ndio njia ya kujenga nidhamu kwa mtoto hivyo mara kwa mara

i. anakuwa anampiga sana mtoto, kumsukuma chini,kumbamiza ukutani,kumwagia maji ya moto,kuchoma na pasi ya umeme,kumpiga kwa vitu vyenye ncha kali,

ii.kumpiga kwa nyaya za umeme, kumfunga kamba,kumlaza chooni,kumnyima chakula,kumzuia kuongea wakija wageni

Ii.kumnyima mahitaji muhimu kama nguo na viatu kama adhabu baada ya kufeli au kufanya makosa,kumfukuza nyumbani

iii.Kumkaba shingo,kumfungia ndani,kumzuia kujumuika au kucheza na watoto wenzake,kumfanya kitu kibaya sana mbele ya wengine

iv.Kumshambulia kwa maneno makali sana mtoto akianza kuzungumza kuhusu matatizo yake binafsi,kumgeuzia kibao mtoto akijieleza kwa chochote

c.UGOMVI WA WAZAZI MARA KWA MARA
Kwa wazazi wenye hasira kupita kiasi ni hulka ya kawaida kabisa kuona wanapigana, kufokeana, kutukanana, kujibizana, kupeana vitisho,kupeana tuhuma za usaliti,kuitana majina ya aibu mbele ya wageni au watoto wadogo mara kwa mara.
Hali hiyo husababisha mtoto anakuwa na hasira kupita kiasi dhidi ya wazazi wake tangu akiwa mdogo sana

Matokeo ya ugomvi kupita kiasi ni pamoja na talaka, kutengana,kuishi sehemu tofauti bila mawasiliano hiyo husababisha upweke kupita kiasi kwa mtoto mpaka akiwa mkubwa anakuwa na hasira kupita kiasi.

d.MZAZI AU WAZAZI KUWA NA TABIA ZENYE KUTIA AIBU MTAANI
Kama mzazi au wazazi wamekuwa na tabia zenye kutia aibu mtaani na kila mtu anawasema vibaya sana wazazi wako ni rahisi sana kujenga tabia ya hasira kupita kiasi kwa sababu ya ile lugha ya kushambuliwa na maneno makali sana ya wakosoaji kila siku mtaani au shuleni.

2.MAZINGIRA
Mtu mwengine anaweza kujenga tabia ya hasira kupita kiasi kwa sababu ya mazingira yake wala sio tabia ya wazazi wake kwa mfano matukio yenye kuumiza labda ulawiti na ubakaji ambao mtoto anaweza kufanyiwa mtaani au shuleni unaweza kumfanya anakuwa katili sana kwa wengine.

Matukio mengine ni kupigwa sana, kufokewa sana, kutukanwa sana, kukosolewa kupita kiasi,kutengwa, kubaguliwa, kuzushiwa uongo,kutishiwa maisha,kufanywa kichekesho kwa muonekano kwa muda mrefu sana utotoni husababisha mtu kujenga tabia ya hasira kupita kiasi dhidi ya watu wengine.

3.UPUNGUFU WA HOMONI ZA SEROTONIN & DOPAMINE
Mtu mwengine anaweza kuonekana kuwa na hasira kupita kiasi kwa sababu ya upungufu wa homoni za serotonin kwenye ubongo.

Homoni za dopamine husaidia kupata usingizi,kupata hamasa ya kufanya kazi,kupata utulivu na hisia za mapenzi.

MADHARA YA TATIZO LA HASIRA KUPITA KIASI (Intermittent Explosive Anger)
Madhara ya tatizo la hasira kupita kiasi yapo sehemu mbalimbali
a.Kiafya
Mtu mwenye hasira kupita kiasi atakuwa hatarini kupata magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, madonda tumbo, uvimbe, shinikizo la damu, kupooza, kuugua mara kwa mara,kuumwa kichwa na mgongo,kupata maambukizo ya magonjwa yenye bakteria na virusi haraka sana kuliko wengine, kwa wanawake atakuwa na changamoto za hedhi kuvurugika, ujauzito kuharibika.

b.Kifedha
Atakuwa hatarini kupata madeni makubwa sana, kusababisha hasara kwenye biashara au ofisi,kuuza mali zake ghafla,kuingia kwenye michezo kama kamari,

c.MAHUSIANO
upo uwezekano mkubwa sana wa kuvunjika mahusiano yake mara kwa mara,kuzaa kila mtoto na mama au baba yake,kuishi katika mahusiano yenye migogoro na ugomvi miaka nenda rudi, kumsaliti mwenza wake kwa hasira au wivu au kisasi.

UFUMBUZI WAKE
Kwa mtu mwenye hasira kupita kiasi anaweza kukabiliana na tatizo hilo kwa njia zifuatazo
a.Kutafuta MSAADA wa kitaalamu wenye uzoefu eneo hilo ili aweze kupata misaada wenye uangalizi maalumu

Kwa wengine ambao hali sio mbaya sana jaribu njia zifuatazo

b.Vuta pumzi ndefu kisha hesabu 1 mpaka 5 kisha iache pumzi polepole itoke huku unahesabu 1 mpaka 5 kwa dakika 5 utaona mabadiliko mwilini

Njia nyingine ni kufanya mazoezi ya viungo,kutumia RELAXATION TECHNIQUES, kujiondoa kwenye tukio,kaa kimya kwa utulivu,tuliza mwili akili itatulia yenyewe,kunywa maji mengi,pata usingizi,kula chakula kizuri kiafya,

Epuka matumizi ya pombe kupindukia, kuvuta bangi au dawa za kulevya, kubadilisha wanawake au wanaume kila wakati,epuka kutumia pesa nyingi bila kufikiria.

c.MASWALI YA KUJITAFAKARI
1.Kipi chanzo cha hasira yangu?
2.Nifanye nini kubadilisha hali hii?
3.Naweza kujifunza nini kutokana na tukio hili?
4.Mimi sio mkamilifu kwanini nataka wengine kuwa wakamilifu?

5.Je mara ngapi nimekuwa na hasira kwa tukio kama hili?
6.Je ni hasira,njaa,uchovu au upweke wenye kunisumbua kwa sasa ?
7.Kwanini nakuwa na hasira dhidi ya mtu huyu je nachukia tabia zake au namchukia yeye ?
8.Je mara ngapi nimefanya au kuongea kitu kibaya kwa wengine je nilikuwa na kusudio gani kwao ?

Baada ya maswali hayo hasira yako itakuwa imeondoka.
 
Lakin hizo hasira hazilainishi huo ugumu wa maisha, kuna dogo kapoteza mia 2 mama yake amemshushia kipigo kikali na adhabu ya kutokula mchana, hayo maneno ya lawama kuhusu ugum wa maisha ni dhahiri hali n mbaya
Na hasira kubwa wanazo wamama...imagine
Na hata ukimpiga mtoto maisha hayatabadilika
 
Lazima wawe na hasira, familia kubwa alafu mume anamuachia hela haitoshi alafu kwenye hiyo hiyo mtoto anapoteza.
Na hyohyo kumbuka ana kikoba rejesho ambalo mume hajui..maybe hela ingetosha japo kwa tabu ila inakatwa hapo pasu kwa pasu...hasira lazima zidabo
 
Back
Top Bottom