Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Natamani kuanzisha thread nyingine kuuliza JF imekutwa na janga gani? Toka tumeanza huu mjadala, imechukua zaidi ya siku 2 kupata picha za nyumba ya Sitta inayojadiliwa. Pia hatuna undani wa mchakato mzima na hata mwenye nyumba hatujamjua. Mbaya zaidi hatuoni hata ka-inzi ka kutuletea data za jinsi viongozi wetu wengine wanavyofuja na kula nchi. Je JF imefulia?
 
Mkuu hapo ndipo wengi tunaposhindwa kuelewa. Kama value for money hakuna, basi si kosa kusema yafuatayo:
1. Wahusika wote walioshughulikia suala hilo wameibia serikali. Fedha ya walipa kodi imeibiwa na huo ni ufisadi. Kwa maana hiyo bunge kama taasisi lina kashfa ya matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.
2. Kwa vile hiyo nyumba haikuwa na samani, bei yake ilitakiwa iwe ndogo zaidi. Kwa hiyo wametumia mwanya huo kuiba pesa au kufanya matumizi yasiyo ya lazima kununua samani wakati wangedai mwenye nyumba aziweke kwa gharama zake mwenyewe. Hiyo ni kashfa ya pili kwa taasis.
3. Mhusika anayeishi humo (Spika, awe ni Sitta au mwingine) ana kosa la kimaadili (moral ofense) la kukubali matumizi mabovu ya pesa za umma hata kama sheria inatoa mwanaya wa namna hiyo. Kwa hiyo hawezi kukwepa lawama (binafsi) kwenye hii kashfa.
4. Hoja kwamba wengine wanalipiwa na kutendewa hivyo na kwamba haijavunjwa sheria haifuti kosa la matumizi mabovu ya pesa za umma. Inaonesha moral iresponsibility ya wahusika wote (Taasisi, yaani Bunge na Mzee wetu mpendwa Sitta).
5. Kwa hili Sitta amekuwa mfano na mahali pa kuanzia (stepping stone) katika mjadala mpana wa matumizi mabaya ya pesa za umma yanayofanywa na viongozi wa wetu. Tunaomba tupate data za wengine ili tuendelee. Labda siku moja dua za kuku zitampata mwewe😕.

HAPANA. Nimeangalia picha tu, naweza nisiwe sahihi.

Labda kuta zake hata ukipiga na SCUD hazivunjiki, hilo linaweza kuongeza thamani na nalikubali hasa ukizingatia kuna mijangili na ma jasusi wanaomwinda Spika Six kila siku!!

Pia doors zake na windows zinaweza kuwa bullet proof hili pia linaongeza bei.

Inaweza kuwa na kamera na mfumo wa ulinzi unaoonyesha kuanzia "NIA" ya mvamiaji au jasusi anapofikiri kuja kuvamia, leave alone kuanza kuja kuvamia. Hilo pia linaweza kuongeza thamani.

Ila bado nasema kwa Masaki.....sijuiiii.

Alamsik
 
Mijadala yetu watanzania wakati mwingine huwa ninapata nayo shida sana. Mara kwa mara tunaangalia mtu na kuachana na hoja kabisa. Hebu nije kwenu kwa kuangalia mtu. Lengo ni kupanua tu mjadala ili mjaribu kuona kuwa suala la malipo au stahili za dhamana ya kikatiba ni suala la kuliangalia kwa mapana yake.

Agalia mifano ifuatayo.

1. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania mshahara wake ni 16,000,000 kwa mwezi
2. Kamishna Mkuu wa TRA analipwa sh 18,000,000 kwa mwezi
3. Mkurugenzi Mkuu wa TBC analipwa sawa na Gavana wa Benki Kuu.
4. Orodha ni ndefu na hao wote mshahara wao (mshahara tu bila marupurupu mengine) ni zaidi ya ule anaopata Rais wa Nchi (Rais analipwa 5.4m kwa mwezi).

Turudi kwenye hoja, malipo ya nyumba ile yanaendana na soko? Taratibu zilifuatwa? Lakini kama lengo lenu ni kumsulubu Sitta, mnaweza kuendelea na wala hamtapata suluhisho maana kesho akiwa Spika Slaa au Hamad Rashid au Marmo nk, atalipiwa nyumba hivyo hivyo kama hatutamaliza tatizo la Nyumba kwa viongozi wa Kikatiba.

Fenicha za 200m zilizonunuliwa kwa ajili ya nyumba ya Spika, ndizo hizo hizo na thamani hiyo hiyo ambayo amenunuliwa Jaji Mkuu na ni zaidi ya hapo alizonunuliwa Waziri Mkuu amara alipoteuliwa maana PM anaetoka hutoka na kila kitu alichokuwa anatumia (wanasema ndio commonwealth tradition)

Hold on.......Mheshimiwa Zitto, hivi umesema kuna mtumishi wa umma kama kamishna wa TRA anapokea mshahara mkubwa kuliko wa Rais? Sasa inakuwaje kwenye maagizo? Rais anakuwa na 'nguvu' zipi dhifi ya kwa mfano gavana wa BoT nk? Mishahara imapishana mbali mno jamani! sasa ina maana mkuu wa TRA anapokea almost 216,000millioni kwa mwaka, bado marupurupu mengine, na hii ni sawa au zaidi ya wakubwa kabisa wa kule white house marekani.....

Something must be very wrong here!
 
sio very tu.
 
kwani spika kama anaishi nyumba ya thamani ya shilingi milioni kumi kwa mwezi anapokea mshahara wa shilingi ngapi kwa mwezi?itakuwa ni kichekesho kama gharama ya pango ni kubwa kuliko mshahara. wake

Zaidi ya hapo viongozi wawe wazaledno sio mambo yakijulikana wanarusha mpira kwa watu wengine . kwa upeo wa elimu yao na uazalendo wao wana wajibu wa kukataa mambo kila kitu wanachoshauriwa. Na kwa style hii unaweza kukuta hata hiyo nyumba ni ya mtoto au mwanafamilia wa kigogo fulani basi irimradi ilimradi utajiri unaendelea kugawanywa kwa matajiri.
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno...
 
Mimi nasema kuwa Samwel Sitta ni mbadhirifu kw kuwa nyumba yenyewe wameikodisha kisanii kw mkenya kupitia third party ambaye ni Rupia investment.....nafasi ya uwanja ni ndogosana hata gari 5 haziwezi kupaki yani hakuna hata eneo la kukaa nje ya nyumba...kutoka kwenye ukuta mpaka kwenye nyumba ni less than 3 metres.haina wimming pool wala nyumba ya nje ya walinzi na umbali wake kutoka bahalini ni zaidi ya mita mia 5
 
Kwani waajiriwa gani wa serikali wanalipwa mshahara wa mkia wa mbuzi ?
 
wa kulaumiwa hapa ni ROSTAM maana ndiye aliyempa hiyo kazi

hahaha! Ukimkamata mwizi utamlaumu mzazi wake?

Naona hapa tatizo sio Spika!!! Sujiulize, je malipo hayo yako kwenye Standing Orders or whatever? Kama Yapo basi Spika na watendanji hawana lawama wanatekeleza kilichopo kwenye vitabu, lawama sasa iende kwa bunge kama institution kwa kuweka rights na entitlements za namna hiyo, kama tunaona ni exhorbitant and unnecessary.
Tatizo linamwangukia spika kwa maana yeye ndio mtumiaji wa hizo pesa. Is he blind to notice such extravagant usage of money?
- Sheria ipi ya Jamhuri ambayo imevunjwa na hizo Millioni 10 za nyumba ya Spika? Na hata kama ningekuwa ninajua ninaweza vipi kuingilia sheria maofisa wetu nje wa ubalozi wanaishi kwenye nyumba za hela ngapi mpaka nishangae hizi hela ndogo sana?

- Spika wa bunge la kutunga sheria za taifa kisheria zetu anatakiwa aishi kwenye nyumba ya hela ngapi mbona maneno mengi bila facts? Wekeni facts Spika wa Kenya anaishi kwa hela ngapi? Wa Zambia anaishi kwa hela ngapi? as opposed na wetu ambaye anakiuka sheria ya Jamhuri kufungu kipi hicho na inasema nini hasa?

- Wakuu Tanzania tumeamua kufuata ubepari, katika ubepari serikali haimiliki nyumba za viongozi ikiwa ni moja ya sera za kuhakikisha hela zinazunguka katika kuboresha uchumi, kumilipia Spika na viongozi wote wa juu nyumba ni moja ya hatua muhimu sana katika kuboresha uchumi wa Taifa katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaingiza pesa mifukoni mwao huku serikali ikikusanaya kodi katika hela hizo zake yenyewe, unless kuna ishus zingine separate zinazomhusu Spika na ufisadi ambazo mwenye facts anatakiwa kuziweka hapa tuzichambue, lakini la Millioni 10 na nyumba wakati tuna maofisa nje ya nchi wanaolipiwa more than this amount tena on monthly bases, binafsi sioni kuwepo na ishu hapa, Spika hawezi kwenda kuishi kwenye chamba cha kupanga na besides si kuna bajeti ya ofisi ya Spika inayopitishwa na wabunge wetu wa CCM na upinzani sasa hizi kelele ni kwa sababu Spika amepitisha bajeti ya matumizi ya ofisi yake or what?

- Can we talk facts badala ya emotions? I mean some ishus zinahitaji pure facts na hii ni mojawapo! Yaani the third leader on line to run our Government hatakiwi kuishi on $ 10,000 House tena only monthly tu? Aaaaaghhhhhhrrr!

Repsect.

Kamanda FMEs!

Mkuu Kitila heshima yako kwanza,

- As a nation na taratibu za usalama wa taifa kwa viongozi wetu wa juu, ni taifa ndio tunampangia kiongozi namna ya kuishi haamui mwenyewe, ndio maana hawasafiri kwenye Economy ingawa wengi wao wangependa hivyo kwa sababu ni wajibu wetu taifa kuwalinda kwa kufuata sheria za Jamhuri, Spika hawezi on his own kuamua mahali pa kuishi ni taifa ndilo tunamuamulia, hata singetaka hawezi kwa sababu hatuwezi ku-compromise usalama wake kwa sababu tu ya kujaribu ku-save peanuts,

- Kumlaumu Spika kwa sababu ya gharama ya nyumba anayoishi either ni ignorance au ni kukosa hoja za kuikosoa serikali, ndio maana sometimes tunajiuliza kwa wananchi wanaichagua CCM tu, off ocurse kwa hoja kama hizi ni clear kuwa wananchi hawana alternative na kama ipo basi ni very weak au iko kwenye political lifesupport somehwere!

Respect.

Kamanda FMEs!

Naona kajijibu mwenyewe hapa...
Wakuu heshima sana na huu mjadala ni very educative, kuna mengi sana hapa yamesemwa ambayo ni valid na hayakwepeki, ni muhimu sana hii debate ikapanuliwa katika sekta nyingi za serikali yetu ukianzia na ofisi ya rais hadi chini,

- Pamoja na kwamba Spika indiviually hana makosa kisheria kwa kuishi kwenye hii nyumba, ni kweli he is obligated kuangalia matumizi ya ofisi yake, kwa sababu hata Obama alipoingia amebadili mengi sana ya matumizi ya ofisi yake ili kupunguza matumizi ambayo yako okayed na sheria.

- Bunge letu lianze kujiangalia upya, kama kweli linaishi within our national financial means maana reading between the lines hii thread inaonekana kuna some financial abuse huko kwa visingizio vya sheria na hili ni kwa wabunge wote kuanzia CCM na hata Upinzani,

- Kamati ya bunge ya mahesabu ianzishe utaratibu wa kuweka wazi matumizi ya ofisi mbali mbali za serikali na hasa mishahara ya maofisa wa serikali, I mean mimi sikujua kwamba tuna wananchi wanaolipwa mpaka Shillingi Millioni 18, garademiti that is 18,000 USD are you kidding me or what hivi unajua what it takes kwa US government kukulipa hela kama hizo tena monthly?

I mean nilitaka kuu'dissmis huu mjadala, kwa sababu ya kukosekana kwa facts, lakini damn this is a valid national debate Tanzania tunakuwaje na maofisa wa serikali wanaoweza kulipwa US Dollars 18,000 kwa mwezi hela za kodi za wananchi? That is insane, sasa hawa wabunge wanafanya nini huko bungeni zaidi ya kwenda kukusanya pay day tu, yes hili la nyumba ya Spika ingawa halina anything to do na yeye binafsi as a leader kisheria, lakini ni justified tena 100% kulijadili as a starting point against matumizi mbaya ya hela za kodi za wananchi.

Respect.

Kamanda FMEs!

Mijadala yetu watanzania wakati mwingine huwa ninapata nayo shida sana. Mara kwa mara tunaangalia mtu na kuachana na hoja kabisa. Hebu nije kwenu kwa kuangalia mtu. Lengo ni kupanua tu mjadala ili mjaribu kuona kuwa suala la malipo au stahili za dhamana ya kikatiba ni suala la kuliangalia kwa mapana yake.

Agalia mifano ifuatayo.

1. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania mshahara wake ni 16,000,000 kwa mwezi
2. Kamishna Mkuu wa TRA analipwa sh 18,000,000 kwa mwezi
3. Mkurugenzi Mkuu wa TBC analipwa sawa na Gavana wa Benki Kuu.
4. Orodha ni ndefu na hao wote mshahara wao (mshahara tu bila marupurupu mengine) ni zaidi ya ule anaopata Rais wa Nchi (Rais analipwa 5.4m kwa mwezi).

Turudi kwenye hoja, malipo ya nyumba ile yanaendana na soko? Taratibu zilifuatwa? Lakini kama lengo lenu ni kumsulubu Sitta, mnaweza kuendelea na wala hamtapata suluhisho maana kesho akiwa Spika Slaa au Hamad Rashid au Marmo nk, atalipiwa nyumba hivyo hivyo kama hatutamaliza tatizo la Nyumba kwa viongozi wa Kikatiba.

Fenicha za 200m zilizonunuliwa kwa ajili ya nyumba ya Spika, ndizo hizo hizo na thamani hiyo hiyo ambayo amenunuliwa Jaji Mkuu na ni zaidi ya hapo alizonunuliwa Waziri Mkuu amara alipoteuliwa maana PM anaetoka hutoka na kila kitu alichokuwa anatumia (wanasema ndio commonwealth tradition)

okay, point taken. Lakini i would imagine point of view yako na wewe imekuwa distorted kidogo kutokana na kuwa mmoja wa walaji wa pesa za umma - aka: mishahara iliyozidi kiwango. Sidhani kama watu wanamsulubu Sitta, bali wanasulubu ujinga wake. Ukisoma article inaanza kwa kuzungumzia statement zake za kupingana na ufisadi. Then it leads to lavish expenditure za pesa ya umma. Link the two, then there is your problem. Kamishna wa TRA kulipwa million kadhaa ingekuwa ishu kama na yeye angekaa na kudai anapambana na ufisadi. Lakini kakaa kimya, na hivyo tumemweka kando kwa sasa.
A good point uliyoweka ni hilo la kuangalia mfumo mzima. Hapo nakubaliana na wewe 100%. Sijui kama nyie Waheshimiwa mmeliongelea bungeni. Mishahara ya watumishi wa umma - ilingane na hali ya umma, that is the main cry from JF!

Zitto.. hivi Gen. Mboma amewahi kushika wadhifa wa Meremeta baada ya kutoka JWTZ?

I would have thought hii ingekuwa covered by the 50 paged report!!
 
Mimi nasema kuwa Samwel Sitta ni mbadhirifu kw kuwa nyumba yenyewe wameikodisha kisanii kw mkenya kupitia third party ambaye ni Rupia investment.....nafasi ya uwanja ni ndogosana hata gari 5 haziwezi kupaki yani hakuna hata eneo la kukaa nje ya nyumba...kutoka kwenye ukuta mpaka kwenye nyumba ni less than 3 metres.haina wimming pool wala nyumba ya nje ya walinzi na umbali wake kutoka bahalini ni zaidi ya mita mia 5

Kumbe nyumba yenyewe ipo Dar? My thought it is in Dodoma! Then where he is staying in Dodoma? In hotel? And its not the headquarter of Bunge in Dodoma?...
 
Tukishakubali kwamba tumeshatoka rasmi kwenye siasa za ujamaa na kujitegemea, itakua rahisi zaidi kuielewa hii picha. Hapa tunapiga kelele wakati tunayoyataka tunajua kabisa hayatawezekana, eti nini... mkuu wa TRA alipwe laki 5 kwa mwezi sababu nchi ni masikini...subuutu!

People lets stop dreaming... Kutambua reality of our times ni first step ya kuusuka upya mfumo mzima. Lakini hii ya spika, spika, spika napingaaa.
 
Lazima tukubali ya kuwa viongozi wetu ndio wanaotuangusha sisi wananchi, mimi nadhani hili la spika ni kipande kidogo sana cha ubadhirifu unaoendelea (It is just the tip of the iceberg). Kuna vitu vingi sana sisi wananchi hatuelewi especially inapokuja kwenye masuala ya malipo ya viongozi wetu walio madarakani na wale ambao wamestaafu. Ni lazima vitu viwekwe wazi jamani, kwani hapa tunazungumzia hela za walipa kodi wote wa Tanzania. Ni haki ya kila mtanzania kujua Rais, Waziri, Naibu Waziri au Jaji Mkuu et al wanalipwa kiasi gani , kiasi gani kinakuwa taxed, Posho zao wanalipwa vipi, Nyumba zao wanazokodiwa zinatakiwa ziwe kwenye price range gani and so forth. Wakati huo huo malipo yao ni lazima ya reflect hali yetu ya uchumi !

Kusema ya kuwa tutapigana na vita mnavyoita vya fikra, wakati sheria zetu pamoja na chombo cha kutunga sheria vimejaa ufisadi itakuwa ni naivety. Ukitaka kujua ni jinsi gani hii ishu imejaa ufisadi jiulize swali moja tuu, Mheshimiwa sana Spika amenunuliwa fenicha zenye thamani ya shilingi millioni 200. Per jumuia ya common wealth tradition (according to Hon. Zitto) hizi fenicha atapewa kama akistaafu au asipochaguliwa tena kuwa spika. Kwa maana nyingine spika alijua kabisa wakati akinunuliwa hizi fenicha ya kuwa hizi fenicha mwisho wa siku zitakuwa zake. Kwa hiyo Spika kama Mwanadamu mwingine angependa kununuliliwa kitu kizuri na chenye thamani, kwa maneno mengine ni kuwa indirectly tumempa spika open check tunamwambia kanunue kitu utakachopenda ambacho kitakuwa chako ! You don't have to be a neurosurgeon to realize this issue is encroached with ufisadi.

Sasa hapa tunazungumzia spika tu, bado hatujaenda kwa mzee mwenyewe wa Magogoni, tukisikia matumizi yake pamoja na waziri mkuu, Makamu wa Rais nadhani itakuwa hatari !
 
Hold on.......Mheshimiwa Zitto, hivi umesema kuna mtumishi wa umma kama kamishna wa TRA anapokea mshahara mkubwa kuliko wa Rais? Sasa inakuwaje kwenye maagizo? Rais anakuwa na 'nguvu' zipi dhifi ya kwa mfano gavana wa BoT nk? Mishahara imapishana mbali mno jamani! sasa ina maana mkuu wa TRA anapokea almost 216,000millioni kwa mwaka, bado marupurupu mengine, na hii ni sawa au zaidi ya wakubwa kabisa wa kule white house marekani.....

Something must be very wrong here!
Lakini hapa unasahau kuwa rais ana marupurupu kibao.
 
..nimesikia pia hiyo imeidhinishwa na Rais? ambaye aliutangazia umma kuwa kuna mtikisiko wa kiuchumi? Hii ni sawa na baba kutangaza matatizo ya kiuchumi nyumbani, nyama hakuna (kama nyumba ya wapenda nyama) wakati yeye anachoma nyama baa!! Kumbe siasa za kwenye majukwaa hazina ukweli wowote katika maisha halisi? Hiyo nyumba sio ya kulipiwa milioni kumi kwa mwezi nakataa kuamini kuwa ni kweli.
 
Tukishakubali kwamba tumeshatoka rasmi kwenye siasa za ujamaa na kujitegemea, itakua rahisi zaidi kuielewa hii picha. Hapa tunapiga kelele wakati tunayoyataka tunajua kabisa hayatawezekana, eti nini... mkuu wa TRA alipwe laki 5 kwa mwezi sababu nchi ni masikini...subuutu!

People lets stop dreaming... Kutambua reality of our times ni first step ya kuusuka upya mfumo mzima. Lakini hii ya spika, spika, spika napingaaa.
Kwani Ubepari maana yake ni Ufujaji? Au kuwa na mali bila daftari? china a former commuist with capitalism on Chinese "socialist" charateristics. USA and Eorpean capitalists. Sasa hapo unaiweka wapi Tanzania? Ufujaji hauna ideology!!
 
Hivi wakulu, heshima mbele, maadamu sisi ni 'mabingwa' wa kuiga 'sera' za wenzetu wa nje huko na kujilinganisha, hli la mishahara hawakumsikia Obama alivopunguza punguza mishahara/marupurupu ya watu wake wa ikulu? au hilo haliwezi kuigwa, maadamu na sisi 'mdororo' wa kiuchumi umetukumba? au hii hawakuisikia?
 
Kwani Ubepari maana yake ni Ufujaji? Au kuwa na mali bila daftari? china a former commuist with capitalism on Chinese "socialist" charateristics. USA and Eorpean capitalists. Sasa hapo unaiweka wapi Tanzania? Ufujaji hauna ideology!!

Now you are talking, manake umeshaanza kufikiria kimfumo mfumo badala ya ki Sitta Sitta. Tukishakubaliana tuna tatizo la kimfumo basi tunaelekea pazuri. Safi sana...
 
Ni kuushawishi umma wa WaTanzania kuingia mabarabarani kupinga mishahara hii mikubwa ya aina yake ,hii ni kazi ya vyama vya upinzani ,labda hilo itaonekana ni kutaka kuleta fujo.Ila ni njia muhimu kwa siku hizi katika ulimwengu wanyonge kupinga au kuipinga Serikali kutokana na ubadhirifu unaovuka mipaka.
Unajua watanzania sisi ni watu wa ajabu sana.
Vyama vya upinzani wakijaribu kulipeleka kwa wananchi hawa hawa wa Tanzania, utasikia wakibezwa kwamba hawana hoja nyingine bali hii hii tena wanabezwa na watanzania wenyewe hawa hawa.
Sijui tumelogwa!
 
...naomba kuuliza;

Iwapo spika anaishi kwenye hili jumba na marupurupu hayo, mkewe (Bi Margaret Sitta) anastahiki marupurupu na nyumba nyingine kwa wadhifa wake wa uwaziri wa jamii, jinsia na watoto au ndio serikali imejumuisha mafao yao wote wawili?
 
Back
Top Bottom