Waraka wa wazi kwa Watanzania kutoka kwa watumishi
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ufisadi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania
Ndugu zetu Watanzania. Sisi ni wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tunapenda kutumia nafasi hii kuwafikishia ujumbe huu muhimu kupitia waraka wetu huu wazi kwenu.
Tunaomba ifahamike kuwa, haikuwa nia yetu hata kidogo kutumia njia hii kueleza mambo ya siri sana yanayofanyika ndani ya Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Tumelazimika kuchukua hatua hii baada ya jitihada zetu za kufikisha taarifa hizi pamoja na malalamiko yetu ngazi husika kutokufanikiwa. Aidha, mbali na hayo hata juhudi za ziada tulizochukua kuwasiliana na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kueleza uvundo ulio katika taasisi hii hazikufanikiwa kutokana na nguvu ya pesa iliyotumika na ofisi ya bunge kuwafunga midomo waandishi wa habari na wahariri wao.
Lakini kikubwa zaidi kilichotusukuma kuandika waraka huu kwa Watanzania wote ni baada ya kubaini kuwepo kwa njama za kuchoma moto ofisi ya uhasibu ya bunge ili kupoteza kumbukumbu muhimu kabisa za matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi ya ofisi ya bunge yaliyofanywa Spika pamoja na marafiki zake. Tunaomba watanzania waelewe kuwa kuanzia sasa ofisi hizo zitaungua moto wakati wowote. Na kama jambo hili litatokea watanzania wote hasa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndivyo vinavyopaswa kulaumiwa zaidi kwa kushindwa kubaini ufisadi wa kutisha katika ofisi hii hadi njama za kuchoma moto ofisi.
Ndugu zetu Watanzania, tunapenda kuwafahamisha kuwa Ofisi ya Bunge, katika kipindi cha miaka mitatu na ushee, imekuwa ikikaliwa na mafisadi wanaojificha katika jina la vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi, na kiongozi wao wa Mkuu ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Tunajua kuwa wapo baadhi ya Watanzania wenzetu wanaoweza kuona kuwa tunasema mambo ya uongo au tusiyo kuwa na uhakika nayo. Kwa kuthibitisha haya tunayoyasema, tunaomba tueleze mambo machache machafu ya kifisadi yanayofanywa na Spika Sitta pamoja na wabunge kadhaa walio karibuni naye, wakisaidiwa na badhii ya watendaji wenye nyadhifa kubwa katika Ofisi ya Bunge.
*Tangu Spika alipoingia madarakani amekuwa akiiongoza ofisi ya bunge kidikteta. Analazimisha kupatiwa fedha kutoka katika ofisi ya bunge anapokuwa katika ziara zake binafsi katika Jimbo lake la Urambo Mashariki. Ushahidi wa haya upo katika vocha za malipo haya. Tunaomba wakaguzi waje wakague watakuta haya.
Fw: ufisadi ndani ya bunge la tanzania - Wanabidii | Google Groups