b; compared to us wananchi, na kipato cha nchi.
Hapana huko siyo kulinganisha kwa haki kwani kunafanywa based on vionjo. Tukifuata hilo, ni gari gani kiongozi anatakiwa awe nalo ukilinganisha na usafiri wanaotumia wananchi wengi? Je mtumishi wa umma anastahili kitu gani kulinganisha na mwananchi mwingine?
hofu yangu ni kuwa mtu ambaye amefanikiwa anapokuja kwetu kijijini anatakiwa avae marapurapu, atembee kwa miguu tena avae makubanzi ili
afanane na wananchi anaowaongoza.
Hivyo, msomi asijifanye msomi sana kwani kwa kufanya hivyo anakuwa tofauti na wananchi wengi ambao si wasomi. Mwenye uwezo wa kujenga nyumba ya kisasa asiijenge ikawa ya kutisha sana kwani haimfananishi na mamiliioni ya watu.
Suala la kipato cha nchi is debatable; je kipato cha nchi hakiakisi matumizi hayo ya ofisi ya Spika maana kwa kadiri nilivyosoma hiyo taarifa ni kuwa serikali ndio imeefanya iliyoyafanya ina maana wanajua kuna uwezo wa kufanya hivyo.
Kufanya hayo anayoyafanya huku akijtangaza kuwa naye yumo katika mapambano ya ufisadi ni KUFURU na UNAFIK kuliko maelezo.
Hilo si sahihi; ufisadi siyo mavazi, nguo, cheo, elimu au kuishi maisha ya fahari au afueni. Ufisadi NI vitendo. Ndio maana kwangu mimi kashfa hapa ingekuwa:
a. Nyumba yenyewe haistahili bei hiyo
b. Nyumba hiyo mmiliki wake ana uhusiano wa wa karibu na Spika na hivyo imepatikana nepotism ya aina fulani. Au ni nyumba yake mwenyewe!
c. Spika alijiamulia bila kuishirikisha serikali
d. Pesa zinalipwa kupitia akaunti yake binafsi na hazijulikani zinakwenda n.k
e. Kulinganisha na bei ya upangaji katika eneo lililoko nyumba hiyo haistahili kupangisha kwa zaidi ya dola 1000 kwa mwezi. Je katika eneo hilo (sijui wapi) nyumba nyingine zinapangishwa kwa kiasi gani kwa mwezi na baadhi ya wapangaji ni nani? - Kama nyumba nyingine katika eneo hilo hilo za watumishi wa kawaida zinapangishwa kwa kati ya dola 5000 na 12,000 kwa mwezi then sidhani kama itamshtua mtu.
f. kwamba utaratibu unasema kuwa gharama ya kumpangishia Spika au mtumishi wa serikali isizidi dola 5000 kwa mwezi na yeye ameenda mara mbili yake; so far sijaelewa ni taratibu gani imevunjwa.
Kwamba yeye ameikuta kwenye sheria na taratibu is a lame excuse kwa sababu yeye kama kiongozi alipaswa kuona kwamba hilo ni tatizo na angeanzisha mchakato wa kubadilisha ujinga huo aliuokuta.
Hilo hapo ni kweli kabisa; lakini ni wangapi ambao wako tayari kukata tawi ambalo wao wenyewe wamekalia? Ni wangapi ambao wanapewa magari ya serikali na wanajua ni ya gharama kubwa kuliko vinginevyo?
Lakini hapa kubwa ni kuwa kama Wabunge wanaona kuwa Spika hastahili nyumba hiyo au ni ya ghali ni wao ndio wabadilishe au kumpunguzia hayo yote. Kitu ambacho itabidi kitulete pia kwa waliowahi kuwa mawaziri wakuu, marais n.k
Hivi aliyekuwa Waziri Mkuu na Spika ni nani ana hadhi kubwa? Ni nani anastahili kupewa pecks za aina mbalimbali. Je Spika anastahili kuwa na msafara wa magari au ajiendeshe yeye mwenyewe? Je anahitaji ulinzi kwenye nyumba yake ? Je anatakiwa kukaa kwenye nyumba ya vyumba vinggapi? Je anapopata wageni wa kimataifa anaweza kuwakaribisha nyumbani kwake? na eneo la hiyo nyumba liwe na uwezo wa kuegesha magari mangapi? n.k
Kwa maelezo haya yote sasa yanaingia-so all items above-a, b, c, and d- are a problem.
maelezo yako ni mazuri lakini hayajagusa au kuonesha kiini cha tatizo hasa.