Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Kweli hawa viongozi wetu hawana uchungu na kodi zetu, hiyo nyumba ina nini hasa? Na kama unaworthy 10ml kwa nini wanunue na thamani tena za ml 200!?
Namna hii hatuendi popote

Sio thamani bali ni samani!
 
Kiongozi aliyepata kuwa mwadilifu katika nchi hii ni Nyerere na wengine wachache tu! Unategemea kiongozi aliyeingia kwa rushwa akapambane na hiyo rushwa? Na waliowachagua hao viongozi wasio waadilifu watakwepaje lawama?
 
Kwenye hii topic sijatia neno... Labda tuangalie kwa ufupi tu...

Nyumba ya zamani ambayo imegeuzwa kuwa Club ni hii hapa:

i576_kaikimbia.jpg


Na nyumba mpya inayolipiwa $8,000 kwa mwezi ni hii hapa:



i578_hekalu2.jpg

Mkuu kwa kurekebisha taarifa, hiyo nyumba ya juu haikuwa nyumba ya spika, nyumba aliyokua anakaa Msekwa na kuuziwa ipo mtaa wa Bongoyo. Hiyo nyumba inayooneshwa hapo alikua anakaa General Frish, ipo Haile selasie rd, opposite Jackies Pub na aliuziwa General kama wengine.

Ili kuwa fair, tunaomba na picha za mahekalu ya waziri mkuu, chief secretary na makamu wa rais. Kumlinganisha spika na nyumba za fullusuti za polisi tutakua hatumtendei haki na ni kupersonalize issue na haitatusaidia kitu in the long run.
 
Inaonekana kuna mgongano kati ufahamu na hapa ndipo tunapokwama katika kujadili ,ila ndi mjadiliano.
Hao akina Kikwete akina Sita Lipumba ,yako mambo ya kusemwa kwao na ni pale wanapozungumza ndio unaweza kuvaana nao ,kama tunavyomuona Sitta akikingia ubavu wanaoulizwa masuala ya papo kwa pao.

Hapa kunajadiliwa viwango vya mishahara katika vyeo vya kiserikali na si vinginevyo ,mfumo mzima wa mishahara ya serikali na viwango vyake ndio lengo kuu ,katika kuvijadili ,aidha hili halimhusi Kikwete wala Sita au Lipumba na wengine tele.

Vyeo na kima cha mshahara haviendani na hali ya WaTanzania walio wengi ,na hawa tunaowataja wameyakuta na wanayaendeleza pengine na kuyazidisha ,sasa faida ya majadala sio kwenda nao mbali sana ,kinachotakikana ni kujenga hoja nzito ambayo itakubalika kwa wadau ambao ni wananchi wapiga kura.Na nini wanatakiwa wafanye.

Pengine tukaona kwa upigaji kura itatuchukua muda mrefu kusahihisha na kuuondoa ufisadi huu kutokana na ukiritimba wa CCM (Hapa hakuna Kikwete hiki Chama kipo zaidi ya miaka 50 wanapokezana vijiti),nini kifanyike ?

Ni kuushawishi umma wa WaTanzania kuingia mabarabarani kupinga mishahara hii mikubwa ya aina yake ,hii ni kazi ya vyama vya upinzani ,labda hilo itaonekana ni kutaka kuleta fujo.Ila ni njia muhimu kwa siku hizi katika ulimwengu wanyonge kupinga au kuipinga Serikali kutokana na ubadhirifu unaovuka mipaka.

Jengine ni kufanya tathmini kwa nchi majirani hata za Ulaya namna watu kama hawa wanavyolipwa ,ikiwezekana tutafute mshauri muelekezi wa kutufanyia na kutuondolea mirija hii.Ila hili nalo litakuwa la ajabu.

La mwisho ambalo linaweza kuzua mvutano ni kwa upande wa vyama vya upinzani ambacho kitaweza kubeba jukumu la kubadilisha na kupitia upya mfumo wa kiwango cha lala salama kinachotumiwa na Sulatani CCM kulipa wafuasi wake wa ngazi za juu kuwarubuni ili ifanye itakavyo kama tunavyoona ,ukienda mabenki wanakwapua kwa ajili ya Uchaguzi ,wakienda kwenye vyombo vya dola tunaona vinavyotumika,wakienda mahakamani hata kama wanamakosa wanaibuka videdea ,bungeni wabunge wanaunga mkono na Spika anashangalia.

Ingawa bado fedha hio ukiibadilisha kwa dola si pesa kitu labda ile ya raisi kidogo inatia homa na akimaliza utamu wa Uraisi anafungiwa nyingine.Hata hivyo inabidi kwanza tujue International salari inasemaje ,sio tunakwenda mbio tu kama tunaozungumzia private busness,mnaweza mkapanga mkakuta Mkuu wa mkoa inabidi apokee laki moja.

Kama Dr. Slaa amekataa nyongeza za marupurupu kwa wabunge, basi kwa nini wengine wanashindwa kuona kuwa hizo pesa wamazopewa ni nyingi mno? Sita ni kiongozi wa Bunge, kapewa pango la Dollar 8000 kwa mwezi na furniture dollar 200,000 hivi kwa nini yeye mwenyewe hawazi kuona that is too much money? I am ver convinced kuwa Sita ndiyo yeye mwenyewe alitaka hiyo Nyumba ni hiyo cost ya furniture; and maybe if you go deep; utaona ile nyumba ni ya prominent guy who benefits from a certain position by renting his own house.

Mwiba, Kikwete alivyoingia madarakani ilikuwa ni sypmpathy ya watu kuwa huyu jamaa spoke sofly, he looked frank, and our hope was that he could tackle most of the existed problems during the past government. He spoke highly of the hungry and the poor. He promised to change. He ran all over the country getting sympathy from people from all sorts of life. The first thing to do after taking his presidency was supposed to sort such issues.

What he has done, he developed cronynism among the cadres. Hivi Mwiba unafikiri sijakuelewa nimekuelewa sana; what you are missing is one theory, these guys to clinge on power will continue to lie and if possible they will even use dubious methods. They know by getting the government is when they will control the money; and politics is the best business in this country! When you retire you become a dollar millionaire.
 
hizi biashara ya the bucket stops with people TZ hai-aplyy hata siku moja.kwa sababu hakuna DEMOKRASIA.

wangapi wanakufa kwa kukosa dawa?matibabu?polisi akikaa kwenye nyumba ya mabati no one talks about hadhi and dignity of our constitution's guards.lakini hiyo minjemba inayotuibia kila siku mnataka iwe na hadhi.kwa lipi la maana wanalolifanya?!hizo nyumba zote mbili,ya zamani na mpya in zaidi ya mara 10 ya ile ya mtanzania wa kawaida.zinatosha!mnataka waishi kama wako DC?!kwa lipi,kwa kipi?!we are soo proud of nothing.the day we learn to be humble may be things will change.
...Kaka upo right !!!

---Hii Kusema Spika anastahiki hadhi Fulani wakati Waalimu,..Polisi..Madaktari nao wanastahiki lkn Hawapati....Tuache Ujinga wa Kusema eti Sheria Inaruhusu....

kama SPIKA amekuwa Front kupambana na UFISADI ...na Anajua Hali Halisi ya watanzania Alikuwa hana haja ya Kukataa Nyumba aliyopewa Kuishi...Angeweza Kuhitaji Marekebisho Kadhaa tu..

Kwa Kitendo hiki Spika Haguswi na Shida za Wananchi...Bunge Letu Limejaa MAFISADI...!!!
 
Mkuu kwa kurekebisha taarifa, hiyo nyumba ya juu haikuwa nyumba ya spika, nyumba aliyokua anakaa Msekwa na kuuziwa ipo mtaa wa Bongoyo. Hiyo nyumba inayooneshwa hapo alikua anakaa General Frish, ipo Haile selasie rd, opposite Jackies Pub na aliuziwa General kama wengine.

Ili kuwa fair, tunaomba na picha za mahekalu ya waziri mkuu, chief secretary na makamu wa rais. Kumlinganisha spika na nyumba za fullusuti za polisi tutakua hatumtendei haki na ni kupersonalize issue na haitatusaidia kitu in the long run.

Hakuna ubaya mkuu kama tukipata picha za mahekalu ya waziri mkuu, chief secretary, makamu wa rais, mkurugenzi wa usalama wa taifa, IGP, mkuu wa majeshi na bila kusahau hizo nyumba za polisi pale Tazara ambazo ni full suit (mabati toka chini mpaka juu) ili tuache ku-personalize kama ulivyodai.
 
...Kaka upo right !!!

---Hii Kusema Spika anastahiki hadhi Fulani wakati Waalimu,..Polisi..Madaktari nao wanastahiki lkn Hawapati....Tuache Ujinga wa Kusema eti Sheria Inaruhusu....

kama SPIKA amekuwa Front kupambana na UFISADI ...na Anajua Hali Halisi ya watanzania Alikuwa hana haja ya Kukataa Nyumba aliyopewa Kuishi...Angeweza Kuhitaji Marekebisho Kadhaa tu..

Kwa Kitendo hiki Spika Haguswi na Shida za Wananchi...Bunge Letu Limejaa MAFISADI...!!!

Pamoja na kujenga hoja yako vizuri sana, lakini tusisahau huwezi kulinganisha spika wa bunge na watumishi wengine wa kifani, uspika si fani. Hivyo nchi itakua na spika mmoja tu at a time tofauti na watumishi wa kifani.

Mi naona kitu tunachomiss kwenye huu mjadala, ni kuona kuwa hili la spika ni kiashiria tu cha tatizo kubwa. Nalo ni watumishi wenye stahili za kupatiwa makazi ya hadhi kulazimika kupangishiwa nyumba. Na hii ni sababu serikali iliamua kugawiana nyumba kishikaji(ushikaji haukuanza na JK)watu ambao Mkapa aliwaita anawasaidia kuwapatia makazi bora, siku hizi wanazivunja to the ground zile nyumba na kunyanyua mablock of flats. Sasa unajiuliza, kweli hawa watu walikua wa "kusaidiwa makazi" kweli???...mtu kapewa nyumba anaivunja yote na kunyanyua mablock yakupangisha wakati watumishi kuanzia majaji na wengine wanapangishiwa nyumba kwa maelfu ya dola??

Hebu mtu apite pale CourtYard Hotel Seaview aone maofisa mbalimbali wa serikali(wengi) wanavyoishi hotelini na familia zao kwa miezi kwenye ile hoteli(kwa siku chumba dola 80) kwa sababu nyumba zote watu walipeana(oysterbay watu wameuziwa nyumba kwa 32m baada ya kufanyiwa renovations kwa pesa za serikali of 70m)

Mpaka TUTAKAPORUDISHA NYUMBA ZA SERIKALI KWA AJILI YA MAAFISA WAANDAMIZI, hili jinamizi la kutafuna maelfu ya dola kwa kupangisha nyumba TUNALO MPAKA KIAMA...Pakuanzia tunapajua tuache kulalama sasa.
 
Shekh tia bidii ramli zako za ulozi, ipo siku moto utakuwakia

Majimoto,

Ana ni ni basi huyo mpiga faraki?

Mi namsifu kuwa ni mjanja sana huyo Sheikh Yahya!

Anasoma alama za Nyakati za jambo, kisha anajifanya anatabiri, ..kisha na wenzangu na mimi wasiotumia hata sekunde kuwaza, wanajikuta wamechotwa nae, wanamwamini kwamba anawezea...aa wapi nyinyi?.

Huyu amesikilizia mjadala huu wa Kadhi weee, akiwa kimya..sasa ameona ni wakati muafaka, anaongea, baada ya kusikilizia misimamo ya watu wa jamii yake...!
Ha haa haaa ... Mjanja sana mganga huyu!
 
Wakuu heshima sana na huu mjadala ni very educative, kuna mengi sana hapa yamesemwa ambayo ni valid na hayakwepeki, ni muhimu sana hii debate ikapanuliwa katika sekta nyingi za serikali yetu ukianzia na ofisi ya rais hadi chini,

- Pamoja na kwamba Spika indiviually hana makosa kisheria kwa kuishi kwenye hii nyumba, ni kweli he is obligated kuangalia matumizi ya ofisi yake, kwa sababu hata Obama alipoingia amebadili mengi sana ya matumizi ya ofisi yake ili kupunguza matumizi ambayo yako okayed na sheria.

- Bunge letu lianze kujiangalia upya, kama kweli linaishi within our national financial means maana reading between the lines hii thread inaonekana kuna some financial abuse huko kwa visingizio vya sheria na hili ni kwa wabunge wote kuanzia CCM na hata Upinzani,

- Kamati ya bunge ya mahesabu ianzishe utaratibu wa kuweka wazi matumizi ya ofisi mbali mbali za serikali na hasa mishahara ya maofisa wa serikali, I mean mimi sikujua kwamba tuna wananchi wanaolipwa mpaka Shillingi Millioni 18, garademiti that is 18,000 USD are you kidding me or what hivi unajua what it takes kwa US government kukulipa hela kama hizo tena monthly?

I mean nilitaka kuu'dissmis huu mjadala, kwa sababu ya kukosekana kwa facts, lakini damn this is a valid national debate Tanzania tunakuwaje na maofisa wa serikali wanaoweza kulipwa US Dollars 18,000 kwa mwezi hela za kodi za wananchi? That is insane, sasa hawa wabunge wanafanya nini huko bungeni zaidi ya kwenda kukusanya pay day tu, yes hili la nyumba ya Spika ingawa halina anything to do na yeye binafsi as a leader kisheria, lakini ni justified tena 100% kulijadili as a starting point against matumizi mbaya ya hela za kodi za wananchi.

Respect.

Kamanda FMEs!

Mkuu Kamanda FMEs, this is a mindful U-turn in this discussion and I owe you a grand standing oversion! My great respect😀
 
Kwanini katika kupunguza matumizi na kuleta mantiki tusiamue kupunguza matumizi kwa viongozi wote wa umma kuanzia Rais, Makamu, Majaji, Wakuu wa majeshi, vyombo vya umma, Wabunge n.k Hiyo ndiyo movement ya kuungwa mkono; lakini hii ya kuchagua mtu mmoja tu...

Wakati wanafunzi wa Chuo Kikuu walipoandamana kwenda Ikulu ya Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 70 kupinga kulazimishwa kuingia JKT na wakidai kuwa kama wataenda JKT basi muda watakaokuwa kule walipwa kama watumishi wa umma, Nyerere aliamuru mishahara ya watumishi wote ikatwe kwani inaonekana ni anasa. Na mishahara yote ikakatwa ili kupunguza hisia kuwa kuna watu wanaishi kifahari mno kutokana na mishahara yao.

Kama tunataka kumkatia "Spita" matumizi ili kuonesha kuwa tunajali hali ya maisha ya watu na kuleta nidhamu ya fedha.. tukate matumizi ya serikali nzima. Lakini ili tujue tunachokata ni kiasi gani hatuna budi kujua viongozi wengine wote wanalipwa kiasi gani, mapango, na pecks nyingine.

Hapa tuwaangalie viongozi wafuatao tu na mtu yeyote mwenye data atumwagie hapa:

Rais
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Rais wa Zanzibar
Spika na Naibu wake
Mawaziri
Manaibu Waziri
Wakuu wa Majeshi (JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa, Magereza n.k)
Wabunge wote
Wakurugenzi wa taasisi za umma wanaoteuliwa


wanalipwa mshahara wa kiasi gani?
Je wanalipwa posho ya kiasi gani kwa safari ya ndani au ya nje?
Je mawaziri wanapopangishwa nyumba huwa wanalipa kiasi gani?
Pecks zao nyingine ni zipi?

Heshima yako Mkuu,

Nadhani huu mjadala umelenga kwenye hilo unaloliongelea. Hapa Sitta anatajwa kwa sababu ndiye tumepata data zake. Hilo nimelisema sana na wengine pia. Kupanua mjadala ndio lengo letu na sasa limeanza. Soma post yangu ya jana na ile ya FMEs. Zitto katupatia data za baadhi ya watu na sasa tungependa tupate za viongozi wakuu wote ili tusonge mbele. Niko tayari kusaini petition ya kuomba marupurupu ya viongozi wetu kwanza yasiwe siri na pia yaendane na kipato chetu. Hatuwezi kuendelea kuona mambo kama ya baadhi ya wazee wa mjini kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wakati nyumbani hakuna kipande cha muhogo. Ni uzezeta na hatutakiwi kuuruhusu hata kidogo.
 
By all means nyumba ya Spika Sitta ni gharama kubwa kwa taifa masikini kama letu. Kibaya zaidi hawa ndo madereva wa kutupeleka nchi ya ahadi sasa kweli kama siyo kudanganyana ni nini? Hivi nchi kama TZ ya mwisho kwa umasikini duniani (apologetics watakuja kupinga na kusema eti sisi si wa mwisho ila ni wa tano toka mwisho!) Can we realy afford spending such amount kwa pango la mtu mmoja? Na kesho tunapeleka bakuli kuomba misaada?

Its nonsense kusema eti cheo cha spika sijui kina hadhi...hivi ni nani kazi yake haina umuhimu? jiulize una daktari, mwalimu, polisi nk..wote hawa wana umuhimu wao katika taifa letu..na ni dharau za kazi kama hizi zinazowafanya watu wakimbilie siasa maana huko ndo wanathaminiwa-kwa kuiba....Nenda kwa wenzetu hivi unajua Chancellor Merkel..ingawa ana nyumba ya ofisi..bado anaishi kwenye apartment yake na familia yake ambayo alikuwa nayo hata kabla ya kuwa waziri miaka ya 90s?? Na apartment iko mtaani kabisa..anaishi na wananchi wengine..

Tuache ndoto za alinacha kuongelea maendeleo na upupu mwingine..kwa porojo tuu. Nilishasema taifa letu linasalitiwa na wasomi kama mimi na wewe...na hawa peasants mpaka waje wapate akili..it will take time..na ukweli ni kwamba hakuna mwenye huruma wala interests na matatizo yao..

Aliyeturoga waafrika alishakufa.. Inauma lakini mi nadhani mtu kama mkapa angeswekwa lupango kama Maddof for the rest of his life! Agrrrr..........
 
Mimi nafikiri kutokana na uhalisia wa mambo hasa ktk sisi tulio chini ya jengwa la sahara si vyema mfumo unaotumiwa na nchi za magharibi na si tukautumia kama ulivyo,ni wazi sisi linapokuja swala hasa la kujipimia tunashindwa kujipimia haki ,tunashindilia junia hadi na kichwa juu.

Nimawazo yangu Bunge watunge sheria zingine zote na bajeti wapitishe zingine zote lakini inapokuja sheria zinazowahusu wao kiundwe chombo kingine ambacho kitakuwa kinawatungia sheria wabunge na kuwapa bajeti stahiki, yani kipime kazi wanayofanya kulingana na wafanya kazi wengine, ugumu wa kazi na mazingira ya kazi yao na wapewe kinachowafaa.
 
Huyu Sheikh ndo Nabii wa akina JUNIUS!!!

Kwanza huyu sheikh anaShirki ambayo katika dini ya kiislamu haitakiwi. Pili nilimuona LIVE siku hiyo kupitia kwa Msaidizi wake ALIUUNGA MKONO WARAKA HUO!

Sasa huyo mwandishi na bwana Junius sijui wanataka kupindisha nini hapa,

Kuchanganya Mahakama ya Kadhi na WARAKA ni sawa na kuchanganya maji na Chuma ukitegemea vita ungana!!

Hata Bakwata wameunga mkono WARAKA huo!
 
Wakuu,

Naomba tuangalie yafuatayo kabla ya kuhitimisha :

Nafasi ya nyumba ...yaani ipo kwenye kiwanja chenye ukubwa kiasi gani. Kwa kutizama picha hiyo nyumba imejengwa karibu sana na ukuta, haina nafasi mbele sijui kwa nyuma.
Nyumba ina accessories muhimu kama Swimming pool na ya ukubwa gani?, Jakuzi? au (ndo mojawapo ya iliyonunuliwa na Million 200).
Nyumba ina ka kiwanja cha basket au ina Gym?
Angalia mengineo, ipo close na bahari au eneo lisilo na nyumba karibu na hapo kuwa na hewa safi.

Nyumba ambayo ina sifa nilizotaja hapo juu ninayojua ililipiwa kodi ya Dollar 6000 tena ilikuwa kampuni inamkodishia Expatriate wa ngazi ya juu.

Uzoefu wangu unaniambia kuwa kati ya nyumba NNE ninazozijua ambazo wamepangiwa washkaji zangu wa kigeni kwenye eneo la Masaki bei ni USD 3000 mpaka 5000 USD.

Jamani sijaona zaidi ya USD 6000. Sasa hii mi sijui. Halafu pia kupangisha nyumba kwa THIRD PARTY WAS UNPROFESSIONAL kwa nchi kama Tanzania (sector ya agency ni changa), kwasababu for sure Margin inaongezeka. Ninaamini wafanyakazi wa Bunge wana uzoefu...

Ila kabla ya kuingia NDANI naweza kusema HAPO VALUE FOR MONEY HAMNA.

Asanteni
 
Huyu Sheikh ndo Nabii wa akina JUNIUS!!!

Kwanza huyu sheikh anaShirki ambayo katika dini ya kiislamu haitakiwi. Pili nilimuona LIVE siku hiyo kupitia kwa Msaidizi wake ALIUUNGA MKONO WARAKA HUO!

Sasa huyo mwandishi na bwana Junius sijui wanataka kupindisha nini hapa,

Kuchanganya Mahakama ya Kadhi na WARAKA ni sawa na kuchanganya maji na Chuma ukitegemea vita ungana!!

Hata Bakwata wameunga mkono WARAKA huo!
Mkuu, nilichounga mkono kwa Yahya Husein ni uhuru wake wa kutoa maoni kama watanzania wengine, hayo mengine ni yake mwenyewe usinihusishe nayo, Nabii wangu mm ni Muhammad (s.a.w), ambaye ndo kigezo kwangu, Upo!!
 
Mkuu, nilichounga mkono kwa Yahya Husein ni uhuru wake wa kutoa maoni kama watanzania wengine, hayo mengine ni yake mwenyewe usinihusishe nayo, Nabii wangu mm ni Muhammad (s.a.w), ambaye ndo kigezo kwangu, Upo!!


Sipo na washabikia UTABIRI WA MAMBO YA MBELENI, ambayo kwenye dini ya kiislamu hairuhusiwi!
 
Kwaujumla Shekhe amenasa kwenye mtego uleule, amesikia tetesi za kwenye vijiwe vya kahawa kuywa waraka ni mbaya bila kutuonyesha ubaya wake, huyu niwa kariba moja na mzee Seif Sharif Hamad, wanafiri wajibu wa kanisa nikusoma biblia tu, ? wanakosea hata kama wanayo haki ya kujieleza bila kuathiri uhuru wangu, fikra zao zimejaa mawazo kua Kanisa katoliki ni chanzo cha maendeleo yao duni kijamii, makisahau historia zilizoleta athari ktk mazingira yao duni.
 
Wakuu,

Naomba tuangalie yafuatayo kabla ya kuhitimisha :

Nafasi ya nyumba ...yaani ipo kwenye kiwanja chenye ukubwa kiasi gani. Kwa kutizama picha hiyo nyumba imejengwa karibu sana na ukuta, haina nafasi mbele sijui kwa nyuma.
Nyumba ina accessories muhimu kama Swimming pool na ya ukubwa gani?, Jakuzi? au (ndo mojawapo ya iliyonunuliwa na Million 200).
Nyumba ina ka kiwanja cha basket au ina Gym?
Angalia mengineo, ipo close na bahari au eneo lisilo na nyumba karibu na hapo kuwa na hewa safi.

Nyumba ambayo ina sifa nilizotaja hapo juu ninayojua ililipiwa kodi ya Dollar 6000 tena ilikuwa kampuni inamkodishia Expatriate wa ngazi ya juu.

Uzoefu wangu unaniambia kuwa kati ya nyumba NNE ninazozijua ambazo wamepangiwa washkaji zangu wa kigeni kwenye eneo la Masaki bei ni USD 3000 mpaka 5000 USD.

Jamani sijaona zaidi ya USD 6000. Sasa hii mi sijui. Halafu pia kupangisha nyumba kwa THIRD PARTY WAS UNPROFESSIONAL kwa nchi kama Tanzania (sector ya agency ni changa), kwasababu for sure Margin inaongezeka. Ninaamini wafanyakazi wa Bunge wana uzoefu...

Ila kabla ya kuingia NDANI naweza kusema HAPO VALUE FOR MONEY HAMNA.

Asanteni

Mkuu hapo ndipo wengi tunaposhindwa kuelewa. Kama value for money hakuna, basi si kosa kusema yafuatayo:
1. Wahusika wote walioshughulikia suala hilo wameibia serikali. Fedha ya walipa kodi imeibiwa na huo ni ufisadi. Kwa maana hiyo bunge kama taasisi lina kashfa ya matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.
2. Kwa vile hiyo nyumba haikuwa na samani, bei yake ilitakiwa iwe ndogo zaidi. Kwa hiyo wametumia mwanya huo kuiba pesa au kufanya matumizi yasiyo ya lazima kununua samani wakati wangedai mwenye nyumba aziweke kwa gharama zake mwenyewe. Hiyo ni kashfa ya pili kwa taasis.
3. Mhusika anayeishi humo (Spika, awe ni Sitta au mwingine) ana kosa la kimaadili (moral ofense) la kukubali matumizi mabovu ya pesa za umma hata kama sheria inatoa mwanaya wa namna hiyo. Kwa hiyo hawezi kukwepa lawama (binafsi) kwenye hii kashfa.
4. Hoja kwamba wengine wanalipiwa na kutendewa hivyo na kwamba haijavunjwa sheria haifuti kosa la matumizi mabovu ya pesa za umma. Inaonesha moral iresponsibility ya wahusika wote (Taasisi, yaani Bunge na Mzee wetu mpendwa Sitta).
5. Kwa hili Sitta amekuwa mfano na mahali pa kuanzia (stepping stone) katika mjadala mpana wa matumizi mabaya ya pesa za umma yanayofanywa na viongozi wa wetu. Tunaomba tupate data za wengine ili tuendelee. Labda siku moja dua za kuku zitampata mwewe😕.
 
Back
Top Bottom