Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,890
ndiyo hivyo.. mtu atusaidie tu.. kwa sababu hofu yangu ni kuwa hili la Spika lina zaidi ya suala la matumizi. Kuna zaidi ya malipo ya dola 10,000 kwa mwezi au magari. I really want to know what is this about.. maana haya mapambano ya fronts nyingi kweli.
Kuanzia mshahara na marupurupu, Spika analipwa sawa na Jaji Mkuu.
Bila kujadili kiwango cha kodi ya nyumba (kwamba dola 8000 ni sahihi au hapana), ukweli ni kwamba Spika wa sasa hana nyumba (official residence) maana iliyokuwepo Dar aliuziwa Msekwa (kupitia mama Ana Abdala ambaye alikuwa Waziri) na iliyokuwepo Dodoma aliuziwa Msekwa kupitia yeye mwenyewe.
Baada ya kupata uspika, alipangiwa nyumba ya kukaa katika quota za manaibu mawaziri pale Kijitonyama. Wabunge (Kamati ya Uongozi) ikakataa na kuona ni udhalilishaji wa Bunge. Ikaamuliwa apangiwe nyumba.
Sheria ya manunuzi ndio hutumika katika kupata huduma kama hizo ambapo spika hahusiki katika zabuni. Kumlaumu Sitta katika hili sio sahihi. Suala la msingi ni kuangalia kama kuna 'value for money' katika huduma hiyo na nyumba ni ya nani? Ilipatikanaje? Sheria ya manunuzi ilifuatwa? Nyumba za jirani na nyumba hiyo 'rent' yake ni hiyo hiyo? Ninadhani hayo ndio masuala ya msingi ya kujiuliza badala ya kupeleka akili zetu zote kwa 'individual' anaeitwa Samwel Sitta.