Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Umeongea kila kitu haswaaa.kwa kifupi wapo watu wachache huenda matamanio yao ni kuona vurugu nchini mwetu, la msingi wafahamishwe kuwa Watanzania hatuongozwi na maneno ya kuunga unga tuna Kiongozi imara na shupa yupo makini kutuvusha.
 
nimeielewasa sana hyo point ya 4, mimi siipendi ccm, unafiki unasumbua sana watu, wanaoikimbia ccm wanapaswa kuogopwa kuliko ccm yenyewe
 
Mwaka 2015, wewe na wenzio mlitaka JK apewe kipindi cha 3! JK mwenyewe akakataa. Leo mnataka kutoa ukomo wa Urais kwa Magufuli. Hivi hamuwezi kuishi bila kujikomba? Mbona watu wengi tu tunaishi bila kujulikana ama kujikomba?
.
Huwa inashanga sana.Wakati mwingine inakuwa vigumu kuamini kuwa hawa watu ni wasomi.
 
Ni kama huko akilini mwangu vile, niko nawaza kumbe nami naweza kumzidi japo sina PhD, Elimu yetu imeporomoka sana kama mwenye PhD anaandika hivi!!. na ndio maana nakutana na vijana waliomaliza kidato cha 4 lkn hawawezi kuandika milioni 1 kwa tarakimu.
Yaani ni majanga mkuu,watu wanasoma lakini hawaelimiki kabisa
 
1) Kwa Ushupavu wa Rais wetu, Watanzania tumeendelea na shughuli zetu zote, Hatuwazi Jambo moja tu la UCHAGUZI tuseme mazingira ya Corona, TANZANIA uchaguzi na kazi zote zinaendelea vilevile.

2) Tanzania ni nchi HURU, Watanzania tunafanya kazi zote bila uangalizi wa mtu yeyote toka kwa mabeberu, Hatuhitaji KIRANJA kutoka popote awe mwangalizi au MCHOCHEZI aseme ndio kilichofanywa au kilichosemwa kiwe na UHALALI.
KIRANJA wetu ni Rais wetu...
Ila wewe kaka noma kwa "propaganda" tu hujambo. Ni bahati mbaya wanaofahamu haya maigizo yako ya kila siku ni wachache saana bahati mbaya hata jiwe hajakustukia na juzi juzi kaingia mkenge kwa ulaghai wa kauli zako na kukurudisha katika ufalme wake...Unachokiongea ni tofauti na unachowaza rohoni mwako.....vice versa...is true
 
Nimemshangaa sana tena sana Msomi mwenye Phd na Waziri kusema kuwa Bungeni kuna Wabunge wa Upinzani eti ni kipimo cha kuwa Tanzania ina Tume Huru ya Uchaguzi. Napenda nimuulize waziri wetu hivi wanaposema Tume Huru anaelewa maana yake?

Inawezekana hajui ,Tume iliyopo iliyoundwa wa wanachama wa chama kimoja na ambao wanateuliwa na mwanachama wao na bado huyo anayewateua ni mgombea wa chama hicho hicho utaiitaje hiyo Tume ni Huru?

Ni suala la kutumia akili ndogo tu kujua Tanzania haina Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Mwigulu ni chagua la watu amezaliwa kuwatumikia watanzania

Mungu ambariki
 
Endelea kusifia Mwigulu ili utetee tumbo lako maana elimu mlizosoma nyie mnaojiita wasomi wa nchi hazijawakomboa kifikra kwani mnaamini bila siasa na kujikomba kwa binadamu mwenzio huwezi kuishi kwa kupata tonge...Jitu zima unakaa kutumia mda wako kutype unamsifia mwanamme mwenzako hata aibu huna..Njaa mbaya sana
Povu la Nini mtu katoa yake ya moyoni na kwa kweli kwa wale tuna nchi moja tu iitwayo Tanzania, yupo sahihi! Membe na kundi lake ni wahuni tu!
 
Mungu ni mwema sana, naamin kwa watanzania walio wengi hawawez kumbeza rais wetu kamwe. Amepitia changamoto za kutosha, but he is still firm katika uongozi wake. MUNGU ambariki sana walau nasi tuwe na mengi ya kuwa proud of as a nation!

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 
Nimemshangaa sana tena sana Msomi mwenye Phd na Waziri kusema kuwa Bungeni kuna Wabunge wa Upinzani eti ni kipimo cha kuwa Tanzania ina Tume Huru ya Uchaguzi. Napenda nimuulize waziri wetu hivi wanaposema Tume Huru anaelewa maana yake ? Inawezekana hajui ,Tume iliyopo iliyoundwa wa wanachama wa chama kimoja na ambao wanateuliwa na mwanachama wao na bado huyo anayewateua ni mgombea wa chama hicho hicho utaiitaje hiyo Tume ni Huru? Ni suala la kutumia akili ndogo tu kujua Tanzania haina Tume Huru ya Uchaguzi.
"Afrika ukishindwa unakuwa umeibiwa kura ukishinda unakuwa unahujaibiwa kura ,ukishinda kunakuwa hakuna tume huru ya uchaguzi ukishinda kuna kuwa na tume huru ya uchaguzi " rais kikwete
 
Mwigulu huitetei nchi, bali unajipendekeza kwa rais kwakuwa anaweza kukupa madaraka, ambayo yatakufanya ww, familia yako na ukoo wenu kuepukana na umasikini. Huna historia ya kuitetea nchi, bali siku zote umekuwa na utamaduni wa kukitetea ccm, maana huko ndio una nafasi ya kuepukana na umasikini. Isitoshe we sio mtu muadilifu, bali ni mtu wa siasa za chuki, ukatili na uhasama. Unajipa jukumu la kumtetea rais kwani kwa yale uliyoyafanya, cheo cha urais tu ndio kinaweza kukupa cover. Lakini kwa maneno marahisi ww sio mzalendo, bali ni muhuni mwenye madaraka ya kujipendekeza.
Hyu siku alipotemwa aliacha Yale maskafu aliporudi tu...akayavaa...
 
Hata Rais mstaafu, Mh. Mkapa, katika kitabu chake, aliongekea umuhimu wa kuundwa Tume huru ya uchaguzi. Hii ni ishara kuwa hii "taasisi" haiko huru!


Naye huyo alikuwa mnafiki, mbona alipokuwa madarakani alishindwa kuunda hiyo tume huru, kutoka tu madarakani anajifanya mwema sana kuandika habari hiyo ili ajaze kurasa za kitabu chake kufanya kiwe kikubwa ili kipande thamani, mjanja kweli huyo jamaa.
 
Hyu siku alipotemwa aliacha Yale maskafu aliporudi tu...akayavaa...
Madelu ni kibaka mmoja fulani aliyesogezwa karibu na Ikulu n' nothing else!!
Watz rejeeni yale mauaji ya Olasiti pale Arusha ndiyo mtajua hili Jinyiramba ni jitu la aina gani.....Over n' out!
 
1) Kwa Ushupavu wa Rais wetu, Watanzania tumeendelea na shughuli zetu zote, Hatuwazi Jambo moja tu la UCHAGUZI tuseme mazingira ya Corona, TANZANIA uchaguzi na kazi zote zinaendelea vilevile.

2) Tanzania ni nchi HURU, Watanzania tunafanya kazi zote bila uangalizi wa mtu yeyote toka kwa mabeberu, Hatuhitaji KIRANJA kutoka popote awe mwangalizi au MCHOCHEZI aseme ndio kilichofanywa au kilichosemwa kiwe na UHALALI.
KIRANJA wetu ni Rais wetu.

3) Inaudhi Sana, wasio Watanzania waisimange nchi yetu, walioko mbali waisimange nchi yetu, na walioko ndani WATUMIKE kuisimanga nchi yetu, yaani hatuoni kazi zilizofanyika tunaona tu hatuna tume huru???

4) NCHI YETU HATUJAWAHI KUFANYA UCHAGUZI BILA TUME HURU YA UCHAGUZI, MIJITU MINGINE ILIKUWEPO NDANI TANGU UJANA WAO HADI SASA, LEO NDIO WAONE HATUNA TUME HURU?? MLISHAISHI MAISHA YENU TANGU ASUBUHI, JIONI YENU MNATAKA KUTUHARIBIA AMANI YA NCHI YETU, VIJANA TUKO MACHO, "HATUTATUMIKA" HATUTARUHUSU TAMAA ZENU ZA MADARAKA KUVUNJA AMANI YA NCHI YETU.

WALIOWATUMA WAPENI TAARIFA kwamba TANZANIA IPO IMARA, na ina KIONGOZI wa Nchi IMARA zaidi ya JANA.

Pia soma:

Elections 2020 - Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?
Mwigulu Nchemba tokea uwe supastar (waziri wa fedha) huonekani humu. What's reason, au uko bize na kuhesabu pesa.
Afu mfanye kurekebisha hizi tozo za miamala sio poa. Yule mbunge zungu aliwaingiza cha kike.
 
Back
Top Bottom