Mtanyooka tu na propaganda zenu!

Zama zimebadilika. Hakuna kutekana tena wala kubambikiana kesi za uhujumu uchumi.
Miaka minne hii isiwafanye msherehekee kupindukia.Narudia hakuna Uhuru usio na mipaka.Na kumbuukeni kwamba 2025 kuna uchaguzi,na Samia atakuwa mgombea tu kama wengine na ni lazima apitishwe na Chama.
 
CAG katumwa sio bure. Report gani ile kila kitu kibaya. Sijasikia jambo zuri lolote kwenye hiyo report. Kwa nn ofisi ya makamu wa raisi na bunge hakuna!!
MAtaga tuko na JPM forever.
Kazi ya CAG si kutafuta mazuri yaliyofanywa na serikali,
 
Mkuu, CAG si chama kipya cha siasa wala si tume maalum iliyotumwa kumchunguza JPM. Labda kama umeanza kuona report zake mwaka huu.

Huyu yupo miaka yote na report za miaka yote ziko hivihivi. Na hata mwakani atafyatua report nyingine.
Sawa kabisa..

Shida Ni pale ambapo katika report ya MWAKA huu Kila kinachoitwa wizi, anatajwa JPM, marehemu ambaye hawawezi hata kumuhukumu.

Siamini Kama report imemtaja jina kwamba ye ndo kachukua pesa hizo, ila ni tafsiri tu ya wasikilizaji wa report hiyo.

Nadhani watendaji wa JPM ambao bado wapo madarakani sasa, wanajaribu kufichia maovu yao kwa marehemu.

Ni Kama vile wanajaribu kutengeneza hukumu hewa.
 
Ulitakiwa kusema umeridhika na si kutujumuisha wote kuwa tumeridhika na wezi wa magufuli na wanaccm wengine
Wizi unaozungumziwa wa Magu ni hadithi za vijiweni mkuu,hauna hard evidence.Na kwanza mwizi hawezi kufanpya aliyofanya Magufuli.Tuhuma dhidi yake ni fabricated zikichangiwa na chuki binafsi na husuda.Wanao mchukia Magufuli ni waliofaidika na awamu ya tatu na nne na impostors wa mabeberu.
 
Kangi Lugola na Andengenye kwenye ile scandal ya kutia taifa hasara kutolewa kazini tu kulitosha kuwawajibisha?

Wangapi kwa kesi ndogo za kusukwa wameenda lupango kwa kesi za economic sabotage?

Hawa ilikuaje wakarudi uraiani na mwingine kulamba cheo tena?

Inafikirisha kusema awamu ile iliziba mianya ya rushwa kumbe ndio awamu iliyokubuhu kwa rushwa!
 
Miaka minne hii isiwafanye msherehekee kupindukia.Narudia hakuna Uhuru usio na mipaka.Na kumbuukeni kwamba 2025 kuna uchaguzi,na Samia atakuwa mgombea tu kama wengine na ni lazima apitishwe na Chama.
Mimi ni mwanaCCM,hivi karibuni SSH atakuwa mwenyekiti wa chama. Kwa utamaduni wa CCM na vyombo vya dola ambavyo anacomand,kuna wa kumzuia SSH kuwa mgombea? Kama unadhani kuna wa kumzuia utakuwa unaota ndoto ya mchana!
 
1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyo hivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!....
Jisemee mwenyewe bwana, usiwasemee watanzania wote!. Ondoa SISI, andika MIMI!!
 
1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyo hivyo kwa sababu tuna macho ya kuona...
Rubbish Nonsense.

Ndiyo unayo haki na mawazo yako lakini usijumuishe WaTz wote.

Who are you kutupangia mawazo yetu.

Kaunge ukoo Chato.

Atakumbukwa kwa uharibifu wa Umoja Upendo na Uhuru wa WaTz
 
I believe Watanzania wengi wana mtizamo kama wangu,na ndio maana maombolezo ya Magu yakawa historical.Hivi mmeshaona lini maombolezo watu wakatandika nguo zao barabarani.Ni Bwana Yesu peke yake alipata mapokezi ys namna hiyo.

Kwanza hamna hata aibu,yaani mnawa betray Watanzania wazi wazi.Ajabu sana.
We chizi kweli! Unalingia maombolezo?

Hata marehemu Ruge alijaza watu na nguo walitandika!
 
Mimi ni mwanaCCM,hivi karibuni SSH atakuwa mwenyekiti wa chama. Kwa utamaduni wa CCM na vyombo vya dola ambavyo anacomand,kuna wa kumzuia SSH kuwa mgombea? Kama unadhani kuna wa kumzuia utakuwa unaota ndoto ya mchana!
Mkuu sina hakika kama hakuna wa kumzuia so far,ila kwa utendaji huu ambao tumeshauona,hatafaa kupeperusha bendera ya CCM tayari kwa 2025.Kama CCM itakuwa imesahau tatizo la 2015 lililoletelea Magu kuingia kwenye kinyanyiro cha Urais,kitakuwa chama kisichojifunza kutokana na makosa na kisichojali mustakabali mzima wa Watanzania,isipokuwa watu wachache.
 
MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM!!

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijimga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga, wavivu
wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.
Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.
#TutakukumbukaDaimaJPM.

MAGUFULI ANAISHI MIOYONI MWETU...
 
MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!...
Hii ni takataka
 
Mataga wameanza kutaga! Na bado.

Fisadi ni fisadi tu...alianza tangu akiwa waziri kipindi cha Mkapa.

Alichofanikiwa ni kuziba watu midomo tu na ubabe. Wacha tujue ukweli wote kumuhusu sasa.

Mungu, fundi!
 
Back
Top Bottom