Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
Wajameni eeh,
Nimebahatika "kupata" mahala ka mtaji. Ni kiasi cha Shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.
Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida (i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake).
=======
Nimebahatika "kupata" mahala ka mtaji. Ni kiasi cha Shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.
Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida (i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake).
=======
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:
Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)
Jumla = Tsh 6,500,000/=
Baada ya Miezi 3;
UZALISHAJI:
Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.
MAPATO
Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=
Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=
Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi
BAADA YA MIAKA 5:
Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
kama una umri kati ya miaka 25 mpaka 35 nakushauri wekeza ktk misitu ya miti ya mbao(exortic) na nguzo za umeme,biashara ya nguzo za umeme kwa sasa inalipa ile mbaya,investment ktk misitu ya nguzo unafanya bila taabu hata kama uko Ulaya. Only risk takers can do it. Tz ardhi ni cheap sana.
Pili kama ungekuwa Dar ningekwambia jaribu Kitimoto,mzee hii kitu inalipa bila mgogoro,si umesikia tishio la mafua limepungua.Dar kinaliwa ile mbaya.Ng`ombe safi pia. Tatizo la kuku wa kienyeji wafugaji wadogo wadogo wengi mno si rahisi kupredict soko la uhakika.Tatu jaribu kufuga samaki,tilapia au nile perch,wanazaliana kwa kasi na soko lake ni kubwa sana kwa sasa.
Jenga Choo ya kulipia eneo la Kariakoo. Utakuwa na uhakika wa kurejesha gharama zako ndani ya muda mfupi kama ifuatavyo:
Wateja - Akina mama (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
- Akina baba (150 * 100/= * 30days) = 450,000/=
- Watoto/vijana/wanafunzi (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
JUMLA KWA MWEZI 1,650,000/=
Kwa mwaka (19,800,000), kwa miaka kumi (198,800,000/=).
Yaani baada ya miaka kumi utakuwa millionea mkubwa sana, na usisahau kurudi hapa JF na kutushukuru.
NB: Kumbuka, uzuri mmoja kwa biashara hii, haina suala la mvua wala kiangazi. Kila siku biashara inaenda.
Kwa ufupi nimekuwa ktk sector hii ya miti kwa muda mrefu sana. Naomba mchague wenyewe eneo mnalotaka nishushe data kati zifuatazo;
1; Ardhi ya bei poa iko wapi? na taabu za huko
2; mbegu zinapatikana wapi? na namna ya kuotesha?
3; Aina ya mti(mbegu,growth rate,soko,na sehemu ya kupanda ktk Tz)
4; Msimu mzuri na maandalizi yake.
5; overhead cost baada ya kupanda.
6; Field management.
Leo niwape item ya tatu tu,mimi nimeajiriwa,najaribu kutumia muda wa mwajiri kwa uangalifu.
Kuna miti mingi ila kwa sisi mizuri ni hii; mitiki(10, nje),milingoti boriti(8),milingoti nguzo (10), milingoti mbao (15),mikrismas(cyprus mbao) (25),
pines (12),ktk mabano ni miaka toka kupanda mpaka kuvuna. Soko la mitiki liko nje ya nchi,locally hakuna commercial market mpaka Kilombero wakijenga kiwanda mwakani. Mbegu zinapatikana kwa wakala wa serikali Morogoro,Iringa,Arusha,Tanga etc. Mbegu za mitiki ni ngarambe kuotesha, kilo moja ni Tsh 6000/ na ukifuata utaalam unapata miche 1000 hivi,lakini wajanja wanafanya kienyeji na wanapata zaidi au wanatumia suckers fulani hivi. Bei ya mche kwa sasa ni Tsh 500/ ya chini na 2000/ ya juu pale dar.
Pine/cyprus kilo moja ni Tsh 18,500/ na unapata miche 30,000 mpaka 35,000 inatosha eka hamsini ya miti ya mbao. Mlingoti kilo moja ni Tsh 22,500/ na unapata miche 120,000. Unapanda boriti eka 100 na unapanda miti ya mbao eka 200.
Utamu uko ktk boriti. Eka moja ni boriti 1200,bei ya boriti moja kwa leo hii ni Tsh 15,000/shambani.kwa hiyo eka moja iliyogharimu Tsh 70,000/ kununua ardhi mpaka kupanda itakupa 1200 x 15,000/=( ) toa gharama za fire break mara moja kwa mwaka. Hakuna kupalilia wala kumwagilia.
Mitiki peke yake inakubali pwani,mingine yote ni ktk nchi za baridi. Nimetoa kwa ufupi sana, ila tutaendelea kuelezana kidogo kidogo, item nyingine kesho.
Kwa Tanzania Mil. 10 unaweza kupata faida ya mwaka kama ifuatavyo:
1. Ukanunua used Corola na kuifanya taxi. Mradi huu unakuhakikishia a minimum net revenue ya Shs 2.92 mil per year (8000*365).
2. Hisa za TCC: 10mil. * 10% = 1 mil per year + annual appreciatiatin ya ?%
3. Gunia za mahindi June na kuuza December: 10 mil * 50% = 5mil
4. Ziweke deposit bank upate interest: 10 mil * 7% = laki 7
5. Anzisha ka-saccos kasiko rasmi (zikopeshe at interest): 10 mil * 17% = 1.7 mil
6. Nunua shamba, chimba kisima ufanye kilimo cha umwagiliaji: 10 mil * 2mil
7. NAENDELEA KUBUNGABONGO. WILL GET BACK TO YOU SHORTLY
Mradi mwingine mzuri wa bei nafuu ni mradi wa kukamua alizeti. Mwaka jana nilipata bahati ya kutembelea Singida kwa ziara ya kitume. Nikapata muda nikaenda mitaa ya sido. Nilitembelea viwanda vidogo vya kukamulia alizeti. Nikatafiti gharama za mradi wote ule. Kwa mujibu wa Sido,mtambo wenyewe unafikia Tsh 6,000,000/ kwa mwaka jana. Ila mitambo ya mitaani inaweza kuwa chini ya hapo. Gharama za jengo zinategemea sehemu.Ukiweza kufunga kimtambo hicho,mikopo ya upanuzi toka Sido ni mingi bila urasimu.
Wale jamaa wanatengeneza hela sio mchezo. Nimegundua pia kuwa watu wanarudi ktk matumizi ya mafuta ya nafaka sana na ukulima wa alizeti/ufuta unaongezeka sana.
Mr MBU think on this also
Uzuri wa IR ni huu,ardhi ipo,mvua zinanyesha sana,barabara zipo,wahehe wanaogopa kuiba cha mtu,wahehe hawabagui mgeni. Wewe fanya kilichokupeleka kwa utaratibu basi,halafu unaambiwa karibu tena. Wasichotaka, usiwadharau tu basi. Kazi wanafanya kwa kiwango cha kuridhisha ila baadhi ya vijiji tutapeli tumeingia.
Milingoti hasa Saligna na grandis,ina kuwa haraka na ni multipurpose yaani waweza kuuza kama nguzo za umeme,au boriti za kawaida au ukachana mbao.Wewe ukiwa na milioni moja inatosha kununua eka kumi na kupanda miche 6000 ya milingoti/pines ya mbao,kisha unaondoka kurudi zako mjini. Unakwenda huko june kuweka fireline na kurudi tena mjini. Baada ya miaka mitatu unaprun miti yako. Kwa hiyo mwendo ni huo.
Mimi na vijana wenzangu tumeunganisha nguvu na kununua eneo kubwa,tunaotesha wenyewe miche ya pines/mlingoti na kupanda ktk plots zetu. Mwaka huu tumepanda miti laki tatu kwa pamoja tuko sita tu. Ila mpaka sasa vijana waliopanda miti eneo lile tuko 24 hivi. Msimu ujao tutakuwa kama 30 jumla.
Wenzetu walikwama msimu huu kwa sababu mbalimbali. Tuna jirani mmoja kutoka Kenya yeye peke yake amepanda milingoti milioni nne. Yeye ardhi kapewa na serikali yetu tukufu. Usijali ndo hali halisi. Mmalawi mmoja kajimegea eka 1000 na amepanda miti.
Tafuta eneo kama ekari mbili mpaka nne chimba kisima kama ulivyoelekezwa na ikiwezekana tenganisha matumizi ya maji binafsi na maji ya biashara. uza maji kwa ajili ya kutafuta gharama za kuendeleza na kukuza mtaji zaidi, lakini ni vizuri ukafuga kuku wa mayai kama 700 ambao nauhakika hutakosa tray 25 kwa siku kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, tumia fuga ngombe wa maziwa wawili tu watunze vizuri wakupatie lita 20-30 kwa siku, hata kama mazima haya lipi unahitaji mbolea kwa ajiri ya mbogamboga na kupata bio gas pamoja na matunda achilia mbali kwa sababu maji unayo unaweza kuwa na bwawa dogo la samaki ukaanza kuvuna kila miezi minne mara baada ya kupanga na haya chini ndio mapato kwa miezi sita kwa kila mwezi.
maziwa 1,080,000.00 mbogamboga 600,000.00 mayai 4,500,000.00 maji 450,000.00 samaki 500,000.00 passion 400,000.00 jumla 7,530,000.00
Natengeneza mchanganuo ukikamilika nitwawasilisha kwenu, vinginevyo humu ndani kuna vibiashara na mawazo ya watu wengi nayaheshimu sana na yamenisaidia sana.
Kama muoga unaweza ukanunua ardhi kiasi wakati unajipanga.
Wazo linguine la nyongeza mkuu ni hili, uko nje ulipo, angalia yafuatayo,
1.viwanda vya kutengeneza vyakula vya kuku-kama wanaweza kununua dagaa kutoka Tanzania.
2.Viwanda vyakutengeneza vyakula vya mifugo, na dawa za viatu kama kiw-ulizia kama wanaweza kununua mashudu ya alizeti kutoka tanzania
3. Viwanda vya kutengeneza viatu, mikoba, mikanda n.k- ulizia kama unaweza kuwa uzia ngozi za wanyama kama ngombe.
4. Viwanda vya kutengeneza taa za umeme, balb- ulizia kama wanaweza kununua kwato na pembe za ngombe.
Ukisha pata soko lake la uhakika, rudi jamvini kuomba watu wa kushirikiana nao ili kuongeza mtaji.bidhaa zote nilizo eleza kwa apa Tanzania zinapatikana sana. hivyo ukiomba watu wa kushirikiana nao uenda ukawapata na mimi naweza kuwa mmoja wapo kwa kuongeza zingine 10milion. na hivyo ukapeleka hata kwa kuanzia angalau contena moja.
ndo hayo tu mkuu. ubarikiwe
km sio mzoefu itakukata tu
1om sio pesa
Dodoma pameshakuwa pagumu
kwani biashara ni za Msimu
Mimi nipo Mjini kati na nina nyumba napangisha kwa ajili ya biashara kodi ni 300,000 hivyo kwa mwaka lazima utangulize 3.6m je shelves na mali zitatoka uweze kunilipa kodi ya 2016 nakushauri tuliza munkari na uanze na mtaji mdogo zaidi kwani wamekuuliza hela yote umeipata wapi ghafla, ni heri uwe na mali ya 10m kuliko cash (km ni kiinua mgongo watu wanamalizahata 70m kwa mwezi)
- Mazao ni Msimu kuanzia Julai hadi Novemba
- Kulima nako ni Msimu kuanzia Novemba hadi April
- Kuuza pembejea unatakiwa uleta majembe na mbegu uuze kuanzia Oktoba hadi Januari na mvua inyeshe!
- Guest sasa hivi ni kichaa 10m haiwezi nunua pagale ukajenga na kuweka maji umeme na vitanda
- Biashara ya maji na juice za azam ni kiamgazi km Oktoba hadi januari wakati wa joto kali
karibu Dodoma
Mdau rasomaka;
Angalia mazingira unayoish, km inawezekana anzisha biashara ya bodaboda za mkataba (miez 10 baada ya hapo inakuwa ya kwake huyo dereva, matengenezo n jukumu la dereva)
Kwa 10 millions unanunua pkpk 4 (pkpk moja inauzwa around 1.8 mil san lg inapendwa zaid, ingawa zpo nyngne za bei pungufu)
Na kila pkpk kwa siku inaingza sh. elfu 10, baada miez 6 kila pkpk imeshajrudshia hela yake ya manunuz ile miez mi4 ilyobak faida. (Mwisho wa mkataba kila pkpk inazaa nyingine)
Biashara n kupata faida, kutanuka na kuzaa biashara nyingne.
Ukikusanya hela ya pkpk 4 kwa miez 3 (1,200,000×3=3600,000/=) ni hela ambayo unaweza kununua pkpk ya matairi matatu (bajaji) ya mizigo/maji ambayo itakuletea kipande kwa siku sh. elfu 15 ( kwa mwez lak 4 ukiondoa matengenezo)
Au kuamua kununua pkpk nyngne tena na kupanua wigo mkubwa wa bzness ambapo mpk pkpk za kwanza znaisha mkataba wake, ztakuwa zmeshazalisha nyngne nyingi.
Pia kwa hela unayokusanya unaweza kubuni biashara nyngne kutokana na eneo unaloish.
Changamoto:
Kila biashara haikosi changamoto, kwa pkpk changamoto kubwa ni kuibiwa/kutoroka na pkpk.
Mkataba uwe wa maandishi kwa m/kt wa mtaa ikiwezeka hata polisi mnaandkshiana ili kuwe na usalama.
Bodaboda ya mkataba n nzur kwa wote, tajiri na dereva, dereva anafaidika kwa kuwa baada ya kumalza mkataba anaimiliki inakuwa yake hivyo atakuwa makini na ataitunza. Matengenezo n jukumu lake.
Bodaboda za kipande kwa kila siku n majanga sana, dereva akishaona imechoka anaiacha na kutafuta nyingne mpya.
Ni hayo mawazo yangu nawasilisha.