Nina mtaji wa milioni kumi; nifanye biashara ipi kati ya hizi nilizochagua?

Ze_Papirii

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
419
818
Habari ya muda huu wakuu, poleni na majukumu ya kila siku. Mimi kama kijana nimeamua rasmi kujikita kwenye kufanya Biashara maana ndiyo ndoto yangu ya siku nyingi sana.

Binafsi nimepambana hapa na pale nimebahatika kupata mtaji wa Tsh Milioni 10 hivyo nmeamua kujikita rasmi kwenye Biashara na kwa kufikiria nimepata mawazo ya Biashara 4 ambazo binafsi ninazipenda na kuzimudu..

1. BIASHARA YA KUUZA VYOMBO VYA MAJUMBANI
-Hapa nitahusisha uuzaji wa vyombo mbalimbali ambavyo vinatumika kwenye majukumu ya kila siku majumbani kama (Masufuria, Hotpots, Vijiko, Visu, Madeli, Ndoo za maji, Mabeseni, Chupa za Chai, Viti & Meza za plastic, Majaba etc)

2. BIASHARA YA NGUO NA PRODUCTS MBALIMBALI ZA WATOTO(0-3YEARS)
-Hapa itahusisha kuuza products mbalimbali za watoto wachanga hadi miaka mitatu(3) kama vile (Nguo, Nepi, Viatu, Kofia, Neti, Beseni za kuogea, Toys km Vigari & Midoli, Poda & Sabuni za watoto etc)

3. BIASHARA YA BIDHAA MBALIMBALI ZA UREMBO NA VIPODOZI VYA WANAWAKE
-Hapa nitahusisha bidhaa kama(Perfumes, Rasta, Lotions, Poda, Hereni, Lipstics, Cheni, Nguo za ndani,Madela etc)

4. BIASHARA YA VIFAA MBALIMBALI VYA UJENZI WA NYUMBA NA VIFAA VYA ELECTRONICS
Wakuu naombeni USHAURI kwa uzoefu wenu ni Biashara ipi hapo yenye return kubwa na bidhaa zake ni more Liquid (Rahisi kuuzika kwa haraka) na ni sehemu gani naweza kupata hzo bidhaa kwa urahisi na Bei nafuu kwa DAR ES SALAAM na changamoto pia za hyo biashara husika na kama itapendeza Location nzuri ya kufanya hyo biashara kwa DAR.

NINAWASILISHA KWENU WADAU KWA USHAURI.
 
Hongera sana kwa WAZO la kuanzisha BIASHARA.

Naamini ktk Uchambuzi wa Biashara kwa kuandaa proposal.. ukizileta kwa njia hii wale wataalam wa analysis watakujibu kiusahihi.

Hapa tutatumia hisia kwa wingi.

For me: Biashara ya vitu vya Ujenzi naona ipo poa..
 
Ukishindwa biashara zote hizo.
Fungua day care uwe mwalimu au meneja.
Kuna bi mkubwa mstaafu Serikalini ameanzisha day care yake ya kihali ya chini, kutokana na muitiko wa ile idea yake pale mtaani kwa sasa ana uhakika wa kupata watoto 40 hadi 50 kwa siku, then hapo kila mtoto kwa siku anaenda na elfu 1 ya chakula na mwisho wa mwezi elfu 30 kama ada, bibi anakula pension yake kiurahisi mno
 
Back
Top Bottom