Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
...Kuelekeza tuhuma moja kwa moja kwa polisi kwa ajali za mabasi sio sahihi
...Kuna tamaa binafsi(madereva,makondakta na wenye mabasi) kuna ubovu wa mabasi, kuna matatizo ya barabara zetu, uchovu, ulevi, uzembe wa watu wengine watumiao barabara zaidi ya mabasi na sababu nyingine chungu nzima. Hivyo kabla ya kunyosha kidole na kupanyuka ni vema ukaangalia kwa kina ni vitu vingapi vinavyosababisha ajali.
Sina takwimu za kiutafiti juu ya sababu za ajali za mabasi. Lakini kuna moja nalijua:
Sababu moja ya msingi ya Wananchi kufa kwenye mabasi ni Wananchi.
Umeshasikia dereva amegeesha chupa ya bia pembeni ya gia huku anaendesha na Wananchi waangalia ?
Dereva anashindana, anaendesha upande wa kulia wa barabara mbele kuna kuna curve au mshuko hamuoni kuna nini kinakuja halafu Wananchi wamekaa tu!
Unamuogopa dereva kumwambia utatuua? Au kuomba kushushwa pale pale unapoingia kwenye basi ukaona chupa ya bia imefunguliwa kabla ya safari ? Au kuripoti kwa mmiliki wa mabasi kwamba tajiri umeajiri wauaji ? Au kuripoti kwingine?
Abiria tunaogopa kumkoromea dereva?