ni kweli kuna ajali lakini kuna siri kubwa sana kuhusu ajali zinazofanywa na haya mabasi. nasikia mwenye nayo ameanza tabia za kuhonga ili ajali zifichwe. last month nilisafiri na gari la sumry from mbeya kwenda dar, mabasi haya yana mwendo kasi ajabu, halafu hakuna ustarabu barabarani
sidhani kama atafanywa lolote kwa kuwa akina kova walikuwa wanaponea kwake pale mbya
WATU wawili wamefariki dunia baada ya basi la Kampuni ya Sumry walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Tunduma, mkoani Mbeya kupinduka.
Basi hilo T587 ARY Nissan, lilipinduka juzi, saa 8 mchana katika eneo la Kinyanambo A, mjini Mafinga, Wilaya ya Mufindi, baada ya kumgonga mwendesha baiskeli na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 23.
Akielezea tukio hilo, mmoja wa abiria aliyekuweo kwenye basi hilo, Rehema Mwakalonge (47) mkazi wa Mbalizi Mbeya, alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha baiskeli ambaye alikuwa akionyesha kuyumba barabarani.
Alisema baada ya mwendesha baiskeli huyo kukosa mwelekeo, dereva alijitahidi kumkwepa ilishindikana na kusababisha basi hilo lililokuwa kwenye mwendo kasi kupinduka.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Dk Deogratias Masawe, alisema majeruhi 23 ndio waliofikikshwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Hata hivyo, alisema hali za majeruhi watatu kati ya hao ni mbaya huku dereva wa basi hilo, Oscar Bango (43) amekatwa mguu mmoja kutokana na kupondeka vibaya katika ajali hiyo.
Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Crausy Mwasyeba, aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni mwendesha baiskeli aliyesababisha ajali hiyo, Tija Nyangwa (18), mkazi wa Kinyanambo B na Joyce Chikwanda (26), mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mwasyeba alisema basi hilo baada ya kumgonga mwendesha baiskeli liliangukia ubavu na kulala katikati ya barabara kuu ya Iringa -Mbeya.
Source:
Tz Daima