Bi. Senti 50
JF-Expert Member
- Apr 17, 2007
- 287
- 12
Wana ndugu, tangu Waziri Mkuu aje na utaratibu wa kubadili matumizi ya barabara ya Morogoro na nyingine ili kupunguza msongamano, upande mmoja imerahisisha watu kuingia na kutoka katikati ya jiji. Hata hivyo, matokeo yake hasi ni kuwa ajali za waenda kwa miguu zimeongezeka (kwa mujibu wa Kamanda Kombe). Watu wengi waliozoea kuvuka kwa kuangalia kushoto, kulia, tena kushoto, sasa wanajikuta wanakutana na magari toka kulia! Sasa, Waziri mkuu abebeshwe lawama za kuja uamuzi wa haraka bila kuangalia athari zake na bila ya kuwaandaa wananchi hasa watoto wa shule ambao huvuka barabara mara nyingi. Je, atakubali lawama?
Asante.
Asante.