SoC03 Namna Bora ya kuondoa au Kupunguza kabisa Ajali za Barabarani

Stories of Change - 2023 Competition

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Ajali za barabarani nchini Tanzania zimekuwa ni janga ambalo limekosa ufumbuzi na linaloendelea kugharimu maisha ya watanzania wengi na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.Licha ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa lakini pia ajali hizi zimekuwa zikiwaacha watu na ulemavu wa maisha vilevile kuziacha familia nyingi kwenye umasikini wa kutupa.Pamoja na jitihada za serikali kudhibiti miendendo ya madereva kwa kuweka miongozo inayosimamiwa na Sheria kali lakini bado jinamizi hili la ajali limeendelea kuyatafuna maisha ya watanzania wasiokuwa na hatia.Tarehe 30.8.2022 akisoma takwimu hizo mbele ya mkutano wa maofisaa wa Jeshi la Polisi ukiwa na lengo la kujitathimini uliofanyika Mkoani Kilimanjaro mjini Moshi,mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania(IGP) Camilius Wambura alisema ajali zimeongezeka kutoka ajali 858 Juni 2021 hadi kufikia ajali 955 Juni 2022 ikiwa ni ongezeko la ajali 97 sawa na asilimia 11.3;Kwa takwimu hizo inaonyesha namna gani hali inazidi kuwa mbaya.

Alisema “ Tathmini tuliyoifanya imebaini kwamba ongezeko hili limetokana na mwendo kasi na uzembe wa madereva wa vyombo vya moto, magari pamoja na biodaboda”

Basi kama hivyo ndivyo,nimeona nitoe mapendekezo ambayo yataisaidia Serikali namna Bora ya kuboresha ili kuweza kupunguza kabisa ajali za barabarani.

NINI KIFANYIKE?

1.SHERIA YA BIMA KUONGEZEWA NGUVU.

Pamoja na sheria nzuri inayohusu Bima lakini bado ina mapungufu makubwa mno,sheria hii ya Bima mara nyingi kama si mara zote inazipendelea sana vyombo vya moto,serikali jicho lake kwenye sheria hii ni kukusanya Mapato na wala si kuangalia maisha ya watanzania.
Watanzania wengi wafahamu kuhusu Bima na wala hawana elimu kabisa inayohusu mambo ya Bima,huwa najiuliza ni kwanini Serikali kupitia Idara zake haitaki kuwapa watanzania elimu hii ya Bima?,Ili uelewe na upate ufahamu wa jambo fulani ni lazima upatiwe elimu,hapa kwenye Bima naweza kusema ni kama Serikali imeamua kukaa kimya huku watanzania wengi wakipoteza maisha na kuwa walemavu.Ajali inapotekea watanzania wanabaki kusema “Kazi yake Mungu haina makosa” hata kama ajali hiyo ni uzembe wa dereva au kuharibika kwa chombo husika.

Naiomba serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani chini ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani,kuwepo na kitengo maalumu ambacho kitakuwa kinasimamia utekelezaji wa malipo kwa wahanga wa ajali.

Napendekeza kuwepo na kitengo maalumu cha kushughulikia fidia kwa wahanga kwasababu kumekuwepo na ukiritimba mkubwa mno wafiwa wakianza kufuatilia kuhusu malipo yatokanayo na Bima kiasi kwamba inapelekea ndugu hao kukata tamaa na kuacha.Bahati nzuri ni kwamba kwasasa hivi magari yote yanapaswa kukata tiketi za kielekroniki,hivyo naomba mfumo huu uunganishwe na kitengo cha jeshi la polisi usalama barabarani ili kubaini ni abiria wangapi wamepanda gari fulani na majina yao,hivyo hata ikitokea ajali basi iwe rahisi kuwatambua na wapewe malipo yao kwa haraka ndani ya siku 30.

2.KUWEPO KWA FAINI KALI AU KUFUNGIWA KAMPUNI HUSIKA.

Video hii ni kwa hisani ya mtandao wa YouTube

Hapa napendekeza kuwepo na faini kali au kufungiwa kabisa kwa makampuni yote ya usafirishaji yatakayogundulika kusababisha ajali kwa makusudi au kwa uzembe.
Sisi sote ni mashahidi ya kwamba,magari yanaporuhusiwa kuanza safari ile asubuhi kumekuwa na kufukuzana kusikokuwa na sababu za msingi,hii yote ni ufahari wa madereva tu kutaka kuonyeshana ubabe wa nani ni mkali wa kukimbilia kifo kuliko mwenzie.Naiomba serikali ikimfungia dereva basi mmiliki wa chombo husika alimwe faini kuanzia milioni 50 na kufungiwa kwa miezi 3 ili ajirekebishe,akifunguliwa atakuwa amejifunza kitu na asiporekebishika basi afungiwe moja kwa moja na kunyang’anywa leseni ya usafirishaji.

3.KUKOMESHWA VITENDO VYA RUSHWA.

Kama kuna jambo ambalo limeendelea kuyaweka maisha ya Watanzania rehani ni habari ya rushwa kwa maofisa wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na wale wakaguzi wa magari ya mikoani kabla hayajaondoka.Sote ni mashahidi kwa namna ambavyo Rushwa imekuwa ni sehemu ya maisha ya askari wetu,wao wanasema hiyo si rushwa bali ni “Fedha ya kubrashia viatu”;Kama hivyo ndivyo tusitegemee kuona ajali zinapungua ng’oo.
Abiria wanatoka stendi vizuri tu na gari ambalo inasemekana limetoka kukaguliwa,na Mungu ili awaepushe abiria hawa na ajali unakuta gari hilo kufika mbele kidogo baada ya kutoka stendi linaharibika palepale,sasa unakuwa unajiuliza maswali kadhaa,kama hilo gari lilifanyiwa ukaguzi na wakaguzi kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ni kwanini baada tu ya kutoka stendi mita 100 liharibike?,ila unakuja kugundua ni fedha ya kubrashia viatu ndiyo imeleteleza yote hayo.

4.KUJENGWE BARABARA ZA DHARURA(TRUCK RUNWAY RAMP)

Barabara hizi kwa nchi za wenzetu zimekuwa na msaada sana hasa pale gari inapotokea kufeli breki.Napendekeza serikali kufikiria kuanza kujenga barabara hizi hasa kwenye maeneo yote korofi na sehemu zenye miteremko mikali ili kukabiliana na wimbi la ajali zinazozuilika.Serikali ikitimiza wajibu wake kwenye suala la miundombinu nadhani hakutakuwa na wakumshika uchawi,tuache kujenga barabara kwa mazoea bali barabara zijengwe kwa teknolojia ya kisasa yenye lengo la kukomesha na kupunguza ajali.

5.SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Ukitazama Barabara ya njia nane kutoka pale Kimara hadi Maili Moja utagundua ya kwamba hakuna njia ya Watembea kwa miguu,hii kitu ni hatari sana kwa usalama wa watembea kwa miguu hivyo inawalazimu wao kutembea kando ya barabara nje ya ule mstari wa njano.Ni kwanini serikali haikujenga njia ya waenda kwa miguu pembezoni upande wa kulia na kushoto wa ile barabara?Napendekeza njia zote kubwa zitakazojengwa ziwe na sehemu ya watembea kwa miguu,siyo watembea kwa miguu wanakuwa wanajichanganya pamoja humo humo na magari kwani ni hatari kwa usalama wa watu wetu.

6.KUWEPO KITENGO MAALUMU CHA KUCHUNGUZA MIENENDO NA SPIDI ZA MAGARI KILA SIKU.

Kwenye kila gari kufungwe kifaa maalumu ambacho kitakuwa kinapeleka taarifa ya mwendo husika wa chombo kwenye kitengo hicho maalumu na palepale mwenye chombo au dereva wa siku hiyo atapigiwa simu na kufahamishwa mwenendo wake na kama atakaidi basi itapigwa simu kwa wilaya au mkoa husika na kuzuiliwa hicho chombo kisiendelee na safari.Hii naamini itasaidia sana kuliko sasa hivi ambavyo vyombo vingi vya moto vimefungwa spidi gavana “Ving’amuzi”,tukumbuke ving’amuzi hizi vinachezewa na wataalamu na kinakuwa kinalia na kupiga kelele tu ndani ya chombo husika lakini hakirekodi mwenendo wala nini.

7.KUFUNGWE KAMERA ZA KUREKODI MWENENDO WA SPIDI BARABARANI

Napendekeza pamoja na yote hayo mazuri yatakayofanyika lakini suala la Kamera ni muhimu sana kwasababu kuna watu inapofika usiku wao na spidi ni kama wamezaliwa tumbo moja,hii itasaidia sana hasa mijini ambako kumekuwa na ukorofi mwingi kwa wamiliki wa vyombo vya moto dhidi ya watembea kwa miguu.

Ni hayo tu.
 
UMUGHAKA nimekuita mara 3.
Umeandika kile kipo mawazoni mwangu mtani. Big up sana.
Thread kama hizi ngumu kupata wasomaji. Ulipaswa kuwa na 100+ votes.
 
🤔🤔🤔🤔🤔nikiangalia thread yako hii na the way unavoelezea maisha yako napata wakati mgumu kukuamini
 
View attachment 2616451

Video hii ni kwa hisani ya mtandao wa YouTube

Hapa napendekeza kuwepo na faini kali au kufungiwa kabisa kwa makampuni yote ya usafirishaji yatakayogundulika kusababisha ajali kwa makusudi au kwa uzembe.
Sisi sote ni mashahidi ya kwamba,magari yanaporuhusiwa kuanza safari ile asubuhi kumekuwa na kufukuzana kusikokuwa na sababu za msingi,hii yote ni ufahari wa madereva tu kutaka kuonyeshana ubabe wa nani ni mkali wa kukimbilia kifo kuliko mwenzie.Naiomba serikali ikimfungia dereva basi mmiliki wa chombo husika alimwe faini kuanzia milioni 50 na kufungiwa kwa miezi 3 ili ajirekebishe,akifunguliwa atakuwa amejifunza kitu na asiporekebishika basi afungiwe moja kwa moja na kunyang’anywa leseni ya usafirishaji.

3.KUKOMESHWA VITENDO VYA RUSHWA.

Kama kuna jambo ambalo limeendelea kuyaweka maisha ya Watanzania rehani ni habari ya rushwa kwa maofisa wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na wale wakaguzi wa magari ya mikoani kabla hayajaondoka.Sote ni mashahidi kwa namna ambavyo Rushwa imekuwa ni sehemu ya maisha ya askari wetu,wao wanasema hiyo si rushwa bali ni “Fedha ya kubrashia viatu”;Kama hivyo ndivyo tusitegemee kuona ajali zinapungua ng’oo.
Abiria wanatoka stendi vizuri tu na gari ambalo inasemekana limetoka kukaguliwa,na Mungu ili awaepushe abiria hawa na ajali unakuta gari hilo kufika mbele kidogo baada ya kutoka stendi linaharibika palepale,sasa unakuwa unajiuliza maswali kadhaa,kama hilo gari lilifanyiwa ukaguzi na wakaguzi kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ni kwanini baada tu ya kutoka stendi mita 100 liharibike?,ila unakuja kugundua ni fedha ya kubrashia viatu ndiyo imeleteleza yote hayo.

4.KUJENGWE BARABARA ZA DHARURA(TRUCK RUNWAY RAMP)

View attachment 2616395

Video hii ni kwa hisani ya mtandao wa YouTube

Barabara hizi kwa nchi za wenzetu zimekuwa na msaada sana hasa pale gari inapotokea kufeli breki.Napendekeza serikali kufikiria kuanza kujenga barabara hizi hasa kwenye maeneo yote korofi na sehemu zenye miteremko mikali ili kukabiliana na wimbi la ajali zinazozuilika.Serikali ikitimiza wajibu wake kwenye suala la miundombinu nadhani hakutakuwa na wakumshika uchawi,tuache kujenga barabara kwa mazoea bali barabara zijengwe kwa teknolojia ya kisasa yenye lengo la kukomesha na kupunguza ajali.

5.SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Ukitazama Barabara ya njia nane kutoka pale Kimara hadi Maili Moja utagundua ya kwamba hakuna njia ya Watembea kwa miguu,hii kitu ni hatari sana kwa usalama wa watembea kwa miguu hivyo inawalazimu wao kutembea kando ya barabara nje ya ule mstari wa njano.Ni kwanini serikali haikujenga njia ya waenda kwa miguu pembezoni upande wa kulia na kushoto wa ile barabara?Napendekeza njia zote kubwa zitakazojengwa ziwe na sehemu ya watembea kwa miguu,siyo watembea kwa miguu wanakuwa wanajichanganya pamoja humo humo na magari kwani ni hatari kwa usalama wa watu wetu.

6.KUWEPO KITENGO MAALUMU CHA KUCHUNGUZA MIENENDO NA SPIDI ZA MAGARI KILA SIKU.

Kwenye kila gari kufungwe kifaa maalumu ambacho kitakuwa kinapeleka taarifa ya mwendo husika wa chombo kwenye kitengo hicho maalumu na palepale mwenye chombo au dereva wa siku hiyo atapigiwa simu na kufahamishwa mwenendo wake na kama atakaidi basi itapigwa simu kwa wilaya au mkoa husika na kuzuiliwa hicho chombo kisiendelee na safari.Hii naamini itasaidia sana kuliko sasa hivi ambavyo vyombo vingi vya moto vimefungwa spidi gavana “Ving’amuzi”,tukumbuke ving’amuzi hizi vinachezewa na wataalamu na kinakuwa kinalia na kupiga kelele tu ndani ya chombo husika lakini hakirekodi mwenendo wala nini.

7.KUFUNGWE KAMERA ZA KUREKODI MWENENDO WA SPIDI BARABARANI

Napendekeza pamoja na yote hayo mazuri yatakayofanyika lakini suala la Kamera ni muhimu sana kwasababu kuna watu inapofika usiku wao na spidi ni kama wamezaliwa tumbo moja,hii itasaidia sana hasa mijini ambako kumekuwa na ukorofi mwingi kwa wamiliki wa vyombo vya moto dhidi ya watembea kwa miguu.

Ni hayo tu.
Ila mkuu hata watawala hawako serious na hili swala.., maana hata wao hufanya biashara kwenye hili tatizo. Kwa wale wahenga mtakumbuka kipindi cha Mkapa waliuza sana speed Gavana ikafika mda likafa, wakaja na suruhisho kwa njia ya Tochi lakini rushwa ikashinda, juzi juzi wamekuja naving'amzi navyo wakauza sana tu na sas hakuna anayevizungumzia, hapo kuna anayetaka kudhibiti ajali kweli., mtawala mtawala mtawala kuwa serious na maisha ya watu wako tafadhali.
 
Facts unazotema Kuna mda nahis we ni mtu upo kitengo ila upo vzr ku-narrate vitu
Nadhani kaka ni kipaji tu ndugu yangu,mimi ni mtu wa kawaida tu na maisha yangu niya kawaida,mimi ni Bodaboda na huwa nikiwaambia watu hawaamini!,nadhani kuhusu uandishi uenda ni kipaji tu ambacho Mungu kanijalia mkuu.
 
And your level of education mkuu? Maana uko vizuri sana ndugu.
 
Hapana mkuu nilisoma kawaida.

Nilisoma Tarime Secondary O level kisha nikafaulu nikapangiwa Tanga tech kusoma mchepuo wa PCB,kufika huko nikadata na mtoto mmoja wa kitanga nikajikuta hata kusoma nashindwa nikavurugwa na papuchi ya mtoto wa kitanga.
Hahaha hatari sana sikulaumu. Tunafanya makosa mtani.
Mimi niliwekeza hela katika umalaya umenigharimu sana. Nilikua mpaka nafahamika lodges za Sinza kama mteja muhimu.

Lakini, bado una nafasi ya kujiendeleza kama utaamua. Unaweza kufanya foundation course chuo kikuu huria. Ukifaulu unakua eligible kusoma degree na mkopo unaweza kuomba.

Hapo nyuma kulikua na program nzuri sana ya RPL chini ya TCU, bahati mbaya wakaifuta. Ingekufaa. Ungekua umepata bachelor degree yako mpaka tunavyoongea.
 
Nimechekea tumboni kusikia Papuchi ya dada yangu mtoto wa Kitanga kwetu
 
Back
Top Bottom