Takwimu zinaonesha kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO) umeeleza kuwa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia vifo vya watu Milioni 41 kila Mwaka Duniani sawa na 74% ya vifo Ulimwenguni.

Hayo yamebainishwa katika Kongamano la Mabalozi wa Usalama Barabarani lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dangote Mkoani Mtwara, leo Ijumaa Oktoba 13, 2023.

Meya wa Mji wa Mtwara, Shadida Ndile akimuwakilisha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika ufunguzi wa Kongamano hilo amezungumzia changamoto mbalimbali na jinsi ambavyo mamlaka zinafanya katika kujali afya za watu.

Ameeleza kuwa Kongamano hilo ni siku muhimu kukumbushana umuhimu wa hatua za kuchukua ili kupunguza madhara ya ajali za barabarani.

Ameeleza Takwimu za WHO zinaonesha kuwa kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani Duniani, sawa na Watu 3,700 kwa siku na watu 100,350 kwa Mwezi, huku Afrika ikiwa na wastani wa 20% ya ajali zote Ulimwenguni.

Amesema “Waathirika wakubwa wa ajali Nchini ni Abiria na watembea kwa miguu, ndio maana Umoja wa Mataifa umeweka nia ya kupunguza ajali za barabarani kwa 50% kufikia Mwaka 2030, hilo halitawezekana bila ushirikiano wa Wadau na Serikali za nchi husika.

“Kwa Tanzania magonjwa yasiyo yakuambukiza yanachangia vifo kwa 33% ikiwemo ajali za Barabarani, magonjwa mengine ni kama ya Moyo, Kisukari, Saratani, changamoto ya akili na magonjwa sugu ya mapafu, ambapo visababishi vikuu ni pamoja na tabia ya ubwete na vyakula visivyo na afya.

“Kwa kutambua tabia ya ubwete, WHO imeweka shabaha ya kuongeza ushughulishaji mwili kwa 10% ifikapo Mwaka 2023 ili kuondoa hali ya ubwete.
ZZA.JPG

ZZ1.JPG
“Kufikia malengo hayo mkakati mmoja wapo ni ni kutengeneza mazingira ya kushughulisha mwili kwa kutembea kwa miguu, kufanya mazoezi na kuendesha baiskeli.

“Bahati mbaya Barabara zetu hazijawa rafiki na salama kwa wanaotembea kwa miguu, hivyo mpango ni kuboresha mazingira ya kufanyia mazoezi ili kuepuka madhara yanayowakuta wanaofanya mazoezi kando ya barabarani.

“Wizara ya Afya itashirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani kufanikisha marekebisho ya Usalama Barabarani tangu ilipoishia Juni 2021, pia Wizara hizo zitashauriana kuona mchakato w akuridhia michakato ya Umoja wa Mataifa kuhusu Usalama wa Barabarani.
ZZ2.JPG

“Wizara itaangalia uwezekano wa kusaidia Jeshi la Polisi kupitia Mamo ya Ndani kwa ktafuta fedha au wafadhili katika kutafuta vifaa hitajika kama vile vidhibiti mwendo na kupima ulevi kwa madereva.

“Pia Serikali itaendelea kuimarisha hospitali na vituo vya afya zinapopita Barabara kuu ili kuwa tayari na kupokea majeruhi pindi zinapotokea ajali.

“Ameshauri maderava kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa au kupitia katika njia za watembea kwa miguu, kuzingatia Sheria wakati huohuo watembea kwa miguu nao wazingatie usalama.

Takwimu za ajali
Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Michael Deleli ametoa takwimu za ajali za Mwaka 2022 na 2023.

Kwa kipindi cha miezi 9 kwa Mwaka huu 2023 kuna ajali 1,334 ni ongezeko la ajali 30 ukilinganisha na kipindi kama hichohicho kwa Mwaka 2022, kuna ongezeko la 2.5% ya ajali za barabarani

Ajali hizo zimesababisha vifo vya watu 1,198, ukilinganisha vifo zilivyotokana na ajali, Mwaka 2023 kuna ongezeko la vifo 30 sawa na 2.8%

Majeruhi wa Januari hadi Septemba 2023, ni 1,833, ukilinganisha na Mwaka 2022 kipindi cha miezi 9 kama hiki kuna ongezeko la majeruhi 98 sawa na 5.6%.

Ajali za Pikipiki
Ajali ndani ya miezi 9 (Januari hadi Seotemba 2023) zilikuwa 339 ukilinganisha na Mwaka 2022 kulikuwa na ajali 352, tumepunguza ajali 13 sawa na 3.7%, ambapo waliofariki ni 263.

Takwimu za vifo vilivyotokana na ajali ya pikipiki Mwaka 2022 kwa muda wa miezi 9 kuna ongezeko ya vifo 27 sawa na 11%.

Majeruhi wa ajali za Pikipiki Mwaka 2023 ni watu 252 ambao waliripoti taarifa zao kwenye vituo saw ana pungufu ya 5% ukilinganisha takwimu za Mwaka 2022

Askari wa Barabarani hawawezi kumaliza ajali wao peke yao bali kunahitajika ushirikiano wa Wadau mbalimbali katika suala la utii wa Sheria.

Waathirika wakubwa katika ajali nyingi za vyombo vya moto ni abiria saw ana 60% tofauti na makundi mengine.
ZZ34.JPG

ZZ4.JPG
 
Pia usisahau kwamba kila Sekunde kuna mtoto anazaliwa Duniani

Husipokufa kwa ajali utakufa kwa maradhi. Kufa ni Pie, haikwepeki kwa sababu wote tumekuwa programmed kufa baada ya muda fulani.

Ukifa wewe, unatoa nafasi kwa kiumbe kingine kuzaliwa. Uwezi kukwepa kifo, as long as ukikuwa na mwanzo lazima utakuwa na mwisho.
 
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kati ya Januari hadi Septemba 2023, kulikuwa na matukio ya Ajali za Pikipiki 339 zilizosababisha Vifo vya watu 263

Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Michael Deleli amesema Majeruhi walioripoti taarifa za Ajali kwenye Vituo katika kipindi hicho ni 252

Waathirika wakuu katika ajali nyingi za Vyombo vya Moto ni Abiria ambao ni 60% tofauti na makundi mengine yanayoathiriwa na Ajali hizo

Soma Takwimu zinaonesha kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani
 
#JFDATA: Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kati ya Januari hadi Septemba 2023, kulikuwa na matukio ya Ajali za Pikipiki 339 zilizosababisha Vifo vya watu 263

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma
Ndio mtaji wa wanasiasa huo. Wao na familia zao wametulia wanapanda V8
 
#JFDATA: Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kati ya Januari hadi Septemba 2023, kulikuwa na matukio ya Ajali za Pikipiki 339 zilizosababisha Vifo vya watu 263

Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Michael Deleli amesema Majeruhi walioripoti taarifa za Ajali kwenye Vituo katika kipindi hicho ni 252

Waathirika wakuu katika ajali nyingi za Vyombo vya Moto ni Abiria ambao ni 60% tofauti na makundi mengine yanayoathiriwa na Ajali hizo

Soma Takwimu zinaonesha kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma
Bora niende msituni kulima mahindi kuliko kuendesha bodaboda ,yaani kugeuka kuwa kilema WA maisha au kufa Bila sababu Ni dakika mbili tu ....
 
#JFDATA: Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kati ya Januari hadi Septemba 2023, kulikuwa na matukio ya Ajali za Pikipiki 339 zilizosababisha Vifo vya watu 263

Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Michael Deleli amesema Majeruhi walioripoti taarifa za Ajali kwenye Vituo katika kipindi hicho ni 252

Waathirika wakuu katika ajali nyingi za Vyombo vya Moto ni Abiria ambao ni 60% tofauti na makundi mengine yanayoathiriwa na Ajali hizo

Soma Takwimu zinaonesha kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma
Bado asilimia 60 ya ajali hizo ni za kukanyagwa kichwani na lori.
 
Ila imerahisisha sana usafiri,shida ni elimu ya barabarani na wao kujithamini kwamba uhai wao ni muhimu.Sasa unakuta pikipiki imetolewa side mirror,kavaa ndala mregezo ,suruali boxer iko nje kweli atahimili mikiki ya barabarani!Maana yake mtu wa hivyo hata akili haijakaa sawa,chochote barabarani kitakuwa kipengere.
 
Ni hatari sana tatizo ajira za kueleweka hazipo Hali inayopelekea vijana kujiajiri kupitia hiyo kazi
 
Ila imerahisisha sana usafiri,shida ni elimu ya barabarani na wao kujithamini kwamba uhai wao ni muhimu.Sasa unakuta pikipiki imetolewa side mirror,kavaa ndala mregezo ,suruali boxer iko nje kweli atahimili mikiki ya barabarani!Maana yake mtu wa hivyo hata akili haijakaa sawa,chochote barabarani kitakuwa kipengere.
Wajinga kama nyie ndio wapumbavu msiojielewa.

Vifo vya watu 200 mnaona kawaida.

Wenzenu Israel wamevamia Gaza Kwa watu wao 200 kuuawa kwenye tamasha la muziki ila nyie mapumbavu vifo vya watu 200 unaona ni kawaida eti unasema bodaboda zimerahisisha safari.

Nyani wew

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
#JFDATA: Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kati ya Januari hadi Septemba 2023, kulikuwa na matukio ya Ajali za Pikipiki 339 zilizosababisha Vifo vya watu 263

Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Michael Deleli amesema Majeruhi walioripoti taarifa za Ajali kwenye Vituo katika kipindi hicho ni 252

Waathirika wakuu katika ajali nyingi za Vyombo vya Moto ni Abiria ambao ni 60% tofauti na makundi mengine yanayoathiriwa na Ajali hizo

Soma Takwimu zinaonesha kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma
Hiyo idadi ya vifo bado ni ndogo sio kwq rafu wanazozifanya hawa madogo kama ni idadi ya Tanzania hiyo idadi ya vifo ni ndogo sababu hawa madogo wa boda wanazalisha sana wanawake
 
Bodaboda ni hatari sana ...Kuna maamuzi wafanyaga wakiwa barabarani,ndo yanayowagharimu sana, lakini ajali nyingine wanasababishiwa na waendesha magari

Kuna siku nlikua nimepanda boda kuelekea mwenge tulivofika pale karibu ghorofa la nobble centre kuna gar ikatu push tukadondoka pembeni ,Nashukuru Mungu hatukuumia sana ilikua n michubuko tuu,

Note:
Sio kila ajali ya bodaboda inasababishwa na uzembe wao ,nyingine ni za uzembe wa waendesha magari
 
Back
Top Bottom