Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Kuna ajalimbaya imetokea maeneo ya milima ya Sekenke Kijiji cha Shelui ambapo basi la Zuberi Trans liliokuwa likitoka Mwanza kupata ajali majira ya saa 5 asubuhi na kuua zaidi ya watu 30 baada ya kutumbulia mtoni.

Tunaelekea mwisho wa mwaka ambapo ajali nyingi hutokea. Mungu awape nafuu walionusurika.



Daaa kwa kwelihao wote wanaosafiri jamani mwisho wa mwaka huu inabidi wawe makini sana tena sana jamani.....Pia mwenyezi mungu ailaze roho za marehemu mahali pema peponi
 
Ukweli ni kuwa basi hilo la Zuberi lenye nambari za usajili T 677 AGJ limepinduka baada ya break zake kushindwa kufanya kazi.

waliokufa katika ajali hii ni 17 na wengine 35 wamejeruhiwa na basi lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza, lililala Singida kutokana na magari kukwama katika barabara hiyo.

Dereva ambaye hajafahamika, usiku kabla ya ajali alilalamika kwa askari wa usalama barabarani kuwa basi hilo ni bovu na kwamba breki zake zilikuwa hazifanyi kazi sawasawa, lakini abiri walimshupalia na ikabidi eti hiyo asubuhi aanze safari.

Ni kwamba baada ya kufika katika mlima huo na kuanza kuteremka, breki za gari zilishindwa kufanya kazi na katika kuliokoa akalipeleka kilimani lakini likavuka kilima na kutumbukia kwenye kurongo ambali urefu wake unakadiriwa kuwa kilometa hamsini.

end
end

Mungu alaze roho za marehemu wote mahalipema peponi!!! Pole kwa familia za marehemu, walio jeruhiwa na Taifa zima.
Ndugu zangu niwakati mwingine tena ambao unatukumbusha umuhimu wa usalama wetu na nijinsi gani tunawajibu wa kudumusha usalama huo.
Kama wewe ni mtengeneza magari na unajua kwamba hiligari halina breaks kamili, lazima ujue kwamba wanaopanda ni jirani zako, ndugu zako na hata watu baki. Nilazima kuhakikisha kwamba tuna fanya tunalotakiwa kufanya kwa manufaa ya watu wengi kwasababu hauwezi kujua labda mmoja wa watu aliye fariki ni dactari ambaye angemtibu na kuokoa maisha ya mtoto wako ambaye ataungua na moto kwa bahati mbaya baadaye. Sina maana kwamba watu fulani wana umuhimu zaidi ya wengine, ila nimfano tu wa jinsi tulivyo kua "connected" katika njia moja ama nyingine. Kama yaliyo semwa nikweli, nasi abiria lazima tuwe na jukumu katika usalama wetu. Mtu kasema gari ni bovu bado mna mlazimisha kuwapeleka, huku nikuto kuangalia vitu katika mtazamo thabiti. Serikali lazima iwashitaki wanao miliki gari hili na kutoa mfano kwa watu wote kwamba hata kama abiria watalazimu uwapeleke, wewe ndio mwenye uamuzi wa mwisho. Hivyo jukumu hilo ni lako la kurudisha nauli zilizo lipwa kama gari haliko katika hali nzuri. Kampuni hii ama mmiliki huyu lazima atozwe faini kubwa sana kama fundisho. Na kama abiria watakuwa wanalazimisha au kufanya fujo wakati gari haliwezi kuwapeleka washitakiwe.
Tunajua mabasi gani yanayo endeshwa katika hali ya hatari na mbio zisizo na msingi, lakini bado tunapanda tu. Well the chances are 50/50, 50% get there safe,50% die on the road, that is the reality, which one we wannt to increase is up to us.Nchi gani hii isiyo nautawala washeria zinazo fuatwa!!!! Just let me run this nchi for six months you will see!!! Mungu awabariki walio umia wapate nafuu na RIP wote waliofariki. Samahani kama nimemuudhi mtu kwa kuandika hivi.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake!
 
Dah, poleni wafiwa na poleni sana majeruhi.........hivi hizi hadithi za kusema abiria walilazimisha dereva kuendesha gari hata dereva alipodai kuwa breki zake haziko sawa.........zina ukweli?......au ndio kuamisha lawama!!......sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu akiambiwa gari bovu atalazimisha dereva aendeshe tu........na hata dereva mwenyewe akiendesha atakuwa na matatizo fulani..........

Watu hawa walikuwa na 'usongo' wa safari kwa sababu kabla ya kufika Singida, walikwama kwa siku mbili njiani kutokana na ubovu wa barabara kutokana na mvua. Inaelekea walipoambiwa na dereva kuwa gari ni bovu, walichokuwa wanafikiria ni kuendelea kukwama zaidi njiani na ndio maana inaelekea walimlazimisha dereva kuendelea na safari. taarifa nilizonazo ni kuwa trafiki walilichukua gari na kulipeleka gereji, lakini walipondoka tu, kabla halijatengenezwa walimlazimisha dereva waondoke.
Kinachoshangaza ni kuwa ilikuwaje dereva, ambaye alikuwa anajua uzito wa tatizo, alikubali 'kulazimishwa' na kuendesha gari?
 
Duh!
Kwa kweli nasikitika sana uamuzi wa dereva. Sijui hata aliamuaje kwenda. Sipati picha kabisa. Lakini nadhani ni ushauri wa abiria wazoefu wa hiyo safari kwa hilo basi. Nakumbuka siku moja natoka Mbeya nikiwa nimepanda Basi la kutoka Tunduma. JIna silitaji maana yote yanafanana. Mwendo ni mdundo yote! Hiyo basi ukikaa seat ya mbele utaona jinsi ambavyo magari madogo yanapisha njia kabisa!
Sasa kufika sehemu inaitwa Igawa, mama mmoja alilalamika sana kuhusu mwendo. Kilichofanyika pale ni kwa abiria kuchangishana hela na kumpatia huyo mama nauli na kumwambia atafute basi la mwendo anaotaka! Wakati huo nauli ilikuwa 20,000 lakini walimpatia 78,000/=. Just imagine.
Sikushangaa kabisa siku ya Mechi ya Tanzania/Mozambique qualification ya World Cup basi hilo hilo likachinja abiria wote. Nalikumbuka sana siku aliposhushwa mama. Ni basi hilo hilo. Na siyo kwamba wameacha. Mwendo pale pale mpaka leo hii
 
Imetolewa mara ya mwisho: 25.11.2008 0008 EAT

• Ajali zaua 25 papo hapo

*Zahusisha mabasi ya Zuberi, Sai Baba na Fuso
*Abiria 84 wajeruhiwa, 50 walazwa Dom, Singida
*Basi la Zuberi labiringika korongoni Sekenke

Hillary Shoo, Singida na Flora Amon, Dodoma
Majira

ZAIDI ya watu 25 wamekufa na wengine 84 kujeruhiwa ambapo 50 wamelazwa katika hospitali za Singida na Dodoma baada ya mabasi mawili kupata ajali tofauti katika mikoa hiyo.

Katika ajali ya Singida, watu zaidi ya 20 walipoteza maisha na 35 kulazwa katika hospitali ya Iramba, huku ajali ya Dodoma walikufa watu watano na 15 kulazwa katika hospitali ya Mkoa ya Dodoma.

Wakati ajali ya Singida ilitokea juzi saa 2.30 asubuhi katika Mlima Sekenke ilihusisha basi la Zuberi lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ya Dodoma ilihusisha basi la Sai Baba lililokuwa likitoka Dodoma kwqenda Dar es Sakaam na kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso.

Basi la Zuberi ni aina ya Scania lenye namba T 677 AGJ wakati la Sai Baba ni namba T 700 ADK na lori la Fuso ni namba T 870 ASK.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la tukio jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Bibi Celina Kaluba alisema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa basi hilo na mwendo wa kasi.

Kamanda Kaluba alisema hadi jana idadi kamili ya watu waliofunikwa na basi hilo ilikuwa haijajulikana vizuri kutokana na ugumu wa kazi ya uopoaji ambapo basi hilo lilipinduka na kuporomoka kwenye korongo na kulala chali.

Hata hivyo, Kamanda Kaluba alisema hadi juzi saa 10 jioni idadi ya abiria waliokuwa wamekufa ilifikia 17 na kazi kubwa ilikuwa ni namna ya kuligeuza basi hilo ambalo limepinduka chali huku zana zinazotumika zikiwa duni, hali iliyofanya kazi ya uopoaji kuwa ngumu.

Akisimulia chanzo halisi cha ajali hiyo Kamanda Kaluba alisema imetokea kutokana na ubovu wa basi hilo na ubishi wa abiria wakimlazimisha dereva kuendelea na safari huku wakijua kuwa basi hilo lilikuwa likihitaji matengenezo.

Alisema baada ya mabishano makali dereva wa basi hilo, ambaye alinusurika katika ajali na kukimbia, aliamua kulipeleka gari hilo kituo cha Polisi kwa ajili ya ukaguzi.

"Baada ya ukaguzi tuliwaamuru walipeleke gereji iliyopo eneo la Namfua mjini hapa lakini baadae tukasikia kuwa abiria walimlazimisha dereva kuendelea na safari," alisema Kamanda Kaluba na kuongeza kuwa basi hilo lilikuwa na matatizo kwenye 'kompresa' na breki.

Alisema majina kamili ya waliokufa bado hayajajulikana lakini kazi inaendelea kwenye eneo hilo na majina kamili ya marehemu na majeruhi yalitarajiwa kupatikana jana baada ya kazi hiyo kumalizika.

Mmoja wa majeruhi aliyenusurika kwenye ajali hiyo, Bw. Ahmad Seleman mfanyabiashara wa Mwanza, alidai kuwa mara baada ya kufika kwenye mlima huo mkali, aliona basi likiwa katika mwendo mkali.

"Baadaye lilipanda kwenye kilima kikali kwa kasi na kujikuta likitumbukia kwenye korongo kubwa la mlima huu, kwa kusema kweli dereva pale hakuwa na ujanja, kwani mwendo ulikuwa mkali mno, we fikiria kupanda kwenye kile kilima si mchezo," alisema.

Akizungumza kwenye eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw. Parseko Kone, alisema alisikia kuwapo kwa ajali hiyo akiwa kwenye ziara ikabidi kuahirisha na kwenda eneo la tukio hilo saa 3 asubuhi jana.

Hata hivyo, Bw. Kone alisema tayari ameagiza tingatinga kutoka kampuni ya kichina ya CGC iliyoko Isuna kwenda Sekenke kusaidia kuligeuza basi hilo ili kuopoa miili zaidi iliyokandamizwa kwenye korongo hilo.

Bw. Kone alisema vifaa vinavyotumika ni duni, hivyo kazi ya kuopoa miili ni ngumu, lakini aliwapongeza vijana wa Shelui kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha miili hiyo inaopolewa yote ili kupata idadi kamili.

"Kwa kweli hii ni ajali mbaya sana kutokea katika mkoa wangu, huwezi kuamini kama kuna watu wamepona kwenye ajali hii, inanisikitisha sana," alisema kwa masikitiko Mkuu huyo wa Mkoa, huku machozi yakimlengalenga.

Nako Dodoma, Flora Amon anaripoti, kwamba watu hao watano walikufa papo hapo na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea Manchali.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Godfrey Mtey, aliwaambia waandishi wa habari hospitalini hapo jana kuwa walianza kupokea maiti na majeruhi jana saa 7.30 mchana.

Dkt. Mtey alisema kati ya watu watano waliokufa ni mmoja tu ndiye aliyetambuliwa kwa jina la Bw. Seleman Hassan, mkazi wa Tanga ambapo wengine wanne majina yao bado hayajafahamika.

Aliwataja walijeruhiwa kuwa ni Bw. Miraji Omar (17) mkazi wa Kiteto, Bw. Michael Kibisa mkazi wa Chinangali, Bibi Scholastica Zakaria, Bw. Jonas Jefunila wa Maili mbili, Dodoma, Bw. Zacharia Mgalo (30), mkazi wa Dar es Salaam, mtoto Erasto Peter miezi 9, wa Mpalanga na Bw. Baraka Mlumba wa Ihumwa.

Wengine ni Bw. Maneno Ngomai (29), Bw. Mahomanyika, Bibi Mariam Senyo (23) mkazi wa Chadulu, Dodoma, Bw. Shaaban Mustapha (14) wa Vingunguti Dar es Salaam, Bw. Yohana Seterina (26) wa Dar es Salaam, Bw. Shaaban Bakari (10) wa Kiteto na Bw. Haruna Saimon wa Majengo, Dodoma, Bibi Feli Nemsudi (28) wa Arusha na Bw. Alikadi Emmanuel (32) wa Singida.

Alisema jumla ya majeruhi 49 walifikishwa hospitalini hapo na kati yao 34 walitibiwa na kuruhusiwa na aliongeza kuwa waliolazwa wamevunjika mbavu, miguu na mikono.
 
Imetolewa mara ya mwisho: 25.11.2008 0008 EAT

• Ajali zaua 25 papo hapo

*Zahusisha mabasi ya Zuberi, Sai Baba na Fuso
*Abiria 84 wajeruhiwa, 50 walazwa Dom, Singida
*Basi la Zuberi labiringika korongoni Sekenke....

Alhamdulillah!
Inna Lillah Wa Inna Ilayhe Rajiun

Hakika sisi ni wa M'Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea

To God we belong and to Him is our return

Tunawapa pole zetu wafiwa na kuwatakia unafuu na uponaji wa haraka majeruhi wote na ni juu yetu kusubiri wakati wa matatizo na kumuomba M'Mungu kutunusuru na mabalaa ya kila aina.

Amin!
 
Watu hawa walikuwa na 'usongo' wa safari kwa sababu kabla ya kufika Singida, walikwama kwa siku mbili njiani kutokana na ubovu wa barabara kutokana na mvua. Inaelekea walipoambiwa na dereva kuwa gari ni bovu, walichokuwa wanafikiria ni kuendelea kukwama zaidi njiani na ndio maana inaelekea walimlazimisha dereva kuendelea na safari. taarifa nilizonazo ni kuwa trafiki walilichukua gari na kulipeleka gereji, lakini walipondoka tu, kabla halijatengenezwa walimlazimisha dereva waondoke.
Kinachoshangaza ni kuwa ilikuwaje dereva, ambaye alikuwa anajua uzito wa tatizo, alikubali 'kulazimishwa' na kuendesha gari?

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

Hii ajali ni mfano mwingine wa jinsi sisi wenyewe tusivyothamini maisha yetu. Abiria wanamlazimisha dereva aendeshe gari bovu! Abiria wanamuhimiza dereva aongeze spidi! Abiria wanamnunulia dereva pombe!

Hatujipendi.
 
Kinachoshangaza ni kuwa ilikuwaje dereva, ambaye alikuwa anajua uzito wa tatizo, alikubali 'kulazimishwa' na kuendesha gari?

Kwa kawaida mazoea hujenga tabia, inawezekana kabisa kuwa amewahi kuendesha likiwa na tatizo kubwa kama hilo na bado wakafika Mwanza. Yaani ni sawa na mtu ambaye amecheza bila salama mara zaidi ya moja bila kuathirika, atazoea tu kucheza hivyo akiamini kuwa atapita tu bilia kuathirika kama alivyopita kabla. Kuna hitaji kubwa sana la kuhakikisha tunaboresha mfumo wetu wa udhibiti ili usitegemee hisia za watu tu!
 
Mlio karibu na magazeti ya Bongo tupeni majina ya waloofariki/umia.
 
Hii ajari imeshatokea nani wa kulaumiwa hapa?
Abiria au dereva?
Na mala nyingi abiria huwa ndo chanzo cha ajali kwa kushabikia mwendo au kulazimisha hata mahali ambapo hapawezekani angalia sasa wamegharimu maisha yao.
POleni wafiwa wote na poleni majeruhi wote wa ajali hizi.
 
Hii ajari imeshatokea nani wa kulaumiwa hapa?
Abiria au dereva?
Na mala nyingi abiria huwa ndo chanzo cha ajali kwa kushabikia mwendo au kulazimisha hata mahali ambapo hapawezekani angalia sasa wamegharimu maisha yao.
POleni wafiwa wote na poleni majeruhi wote wa ajali hizi.

Tunaanza kumlaumu dereva......huyu ndiye mwendeshaji wa gari.......!
 
Hapo gari lilipopatia ajali kuna msitu ambao mheshimiwa rais kipindi akiwa ziarani Singida alizindua hifadhi hiyo. Pia kuna korongo kubwa tuu. Kusema kweli magari ya kuja safari ndefu wanakwenda mwendo mbaya
 
Ukweli ni kuwa basi hilo la Zuberi lenye nambari za usajili T 677 AGJ limepinduka baada ya break zake kushindwa kufanya kazi.

waliokufa katika ajali hii ni 17 na wengine 35 wamejeruhiwa na basi lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza, lililala Singida kutokana na magari kukwama katika barabara hiyo.

Dereva ambaye hajafahamika, usiku kabla ya ajali alilalamika kwa askari wa usalama barabarani kuwa basi hilo ni bovu na kwamba breki zake zilikuwa hazifanyi kazi sawasawa, lakini abiri walimshupalia na ikabidi eti hiyo asubuhi aanze safari.

Ni kwamba baada ya kufika katika mlima huo na kuanza kuteremka, breki za gari zilishindwa kufanya kazi na katika kuliokoa akalipeleka kilimani lakini likavuka kilima na kutumbukia kwenye kurongo ambali urefu wake unakadiriwa kuwa kilometa hamsini.

end
end
Pole wafiwa wote. Inna Lyilah wa inailah raajun

Unajua hapa ndio ninapo lalamikia mfumo mzima wa usalama barabarani. Kwanza kabisa kwa nini basi liruhusiwe kutoka kituoni kama halina brake?

Nategemea owner wake atasimamishwa mbele ya pilato na kujibu mashitaka ya kuwa bila kukusudia kwa watu hawa 17. We need tough law, na tukiwa na sheria nzito haya mambo ya kipuuzi yatapungua.
 
Mmoja wa waliotuacha ni mwachuo wa UDSM...MUNGU AWAREHEMU..
 
TAFADHALI TUKUBALIANE KUPAMBANA NA TATIZO SUGU LA AJALI NYINGI ZA BARABARANI AMBAZO KWA MUDA MREFU HUWA NYINGI SANA KILA MWEZI DISEMBA.
NAJIULIZA ,
KWA NINI AJALI ZA BARABARANI HUWA NYINGI DISEMBA?
NASHAURI,
WAOMBAJI TUOMBE MUNGU NA WATU WOTE TUJIEPUSHE NA VISABABISHO VYA AJALI.

Exaud J. Makyao
0784347001
 
Ajali nyingi zinakwepeka. Naambiwa ukitoka Dar au Morogoro kuelekea Mbeya, gari kugonga ng'ombe, mbuzi, n.k ni jambo la kawaida kutokea.
 
Tuomwombe Mungu atuepushe na hizi ajali.
Kufunga na kuomba ni jambo linalowezekana.
 
Tuomwombe Mungu atuepushe na hizi ajali.
Kufunga na kuomba ni jambo linalowezekana.

Mkuu
Mungu huwa haepushi uzembe, la sivyo nae atakuwa mzembe. Tuache uzembe, tufuate sheria na wasimamizi wa sheria wafanye kazi yao. Ina maana mataifa yenye ajali chache duniani huwa wanafunga na kuomba mungu kuliko Tanzania?
 
Back
Top Bottom