Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Natowa pole kwa majeruhi wote na pole nyingi sana kwa wafiwa wote. "Inna Li-Llahi wa Inna ILlahi Rajiun"
 
duh.. katika wiki kama hii habari hii ni nyongeza ya machungu yetu. Poleni sana wafiwa, majeruhi... ila Singida nako..~
 
Bwana alitoa na leo ametwa jina lake lihimidiwe na kila goti lipigwe kwake. Roho zao zipumzike kwa amani .
 
Bwana alitoa na leo ametwa jina lake lihimidiwe na kila goti lipigwe kwake. Roho zao zipumzike kwa amani . Lakini hapo Singida kunanini jamani? mara Basi la Mohamed Trans limewaka moto mara watoto wameuwawa kinyama why? kwanini? tujiulize jamani,ikiwezekana huyo Kamanda wa polisi wa Mkoa kashindwa kazi aachie ngazi,SAA 4.30 USIKU MABASI HAYATAKIWI KUENDELEA NA SAFARI VIPI HILI LILIKUWA LINAENDELEA NA SAFARI KAMA KAWAIDA? Manyoni kuna trafic pale,wameliruhusu vipi kwa muda huo?.
 
bwana alitwaa na bwana amechukuwa


mola awape malazi mema peponi.


ila nnauliza habari kama hizi kuwekwa kwenye siasa ni sawa?


jee hakuna haja ya kuanzisha sehemu yake maalum ya misiba na majanga ya taifa?

nnauliza kwa nia nzuri na nikiwa na uchungu wa kufiwa na watanzania wenzangu, ila nnaomba muongozo
 
Poleni sana,Ni matumaini yangu,serikali itawapa fidia watu wote waliopata ajali.
 
Mungu awarehemu marehemu wote, na majeruhi wapate ahueni haraka. Hizi ajali zisizokwisha kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na MAFISADI, kwani chanzo cha kuwa na barabara mbovu na madereva wasioheshimu sheria ni rushwa iliyozaa ufisadi usiomithirika.
 
Hivi Watanzania tutaendelea kutoa pole mpaka lini? Haiwezekani tatizo moja linajirudia na kujirudia lakini kama nchi hakuna jambo la maana tunalochukua kupambana na hizo ajali. Tutaendelea kulia mpaka lini?

Pole kwa waliofiwa na pia walioumia. Tunawaombea mupate nafuu haraka iwezekanavyo.
 
Hakuna ajali nzuri na haiwezi kuwa mbaya sana ,maana kama ingekuwa mbaya sana basi dunia nzima ingeliskia na kujua.
 
Mwenyezi Mungu awape Nguvu na subira Ndugu,jamaa katika kipindi hiki kigumu cha Msiba.
Poleni sana Wa Tanzania.
 
Nimeambiwa Sumry kwenda Mbeya limepata ajali Makambako na kuna mtu/watu wamefariki.

Wenye taarifa zaidi tafadhali tujulisheni.

Mungu awasaidie wote waliopata ajali hiyo. Hizi ajali zinasikitisha sana.
 
ni kweli kuna ajali lakini kuna siri kubwa sana kuhusu ajali zinazofanywa na haya mabasi. nasikia mwenye nayo ameanza tabia za kuhonga ili ajali zifichwe. last month nilisafiri na gari la sumry from mbeya kwenda dar, mabasi haya yana mwendo kasi ajabu, halafu hakuna ustarabu barabarani

sidhani kama atafanywa lolote kwa kuwa akina kova walikuwa wanaponea kwake pale mbya
 
Back
Top Bottom