Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mzee Es said:
The main thing is, ".....then the gun went off accidentally killing......", tuitoe hukumu kabla ya kesi,

Tafiti iachie mahkama iamue kama ni kweli hiii kesi ipo!


Haya kati yangu na wewe nani anaonekana kumtetea huyu mzee ambae hii ni wikiendi yake ya kwanza akiwa ndani pengine tangu baada ya uhuru?

tusiwachoshe watu na malumbano yako yasiyo na msingi.

I have to know when to quit kwa vile umeshawahi kusema unaishi ili ulumbane....

Naam narejea tena ijapokuwa huyu inasemwa ni mwanajeshi mstaafu taratibu za kimsingi kabisa ni kwamba you only use CHA MOTO wakati ukiwa katika hostile environment na pia ikiwa unataka kufanya self defence.

My heart goes to the familly ya wafiwa na kama kuna aliedhurika mwingine yeyote,

Habari za kwenye uhuru www.uhuru.info zinasema kwamba Ditopile aliondoka katika eneo la tukio lakini polisi walimkamata, kakamatwaje?
 
Habari haikuwa kamili na tayari ulishaanza kutoa hukumu, sasa habari ni kamili na utaona kuwa hata mtoa mada alighafirika pale aliposema kuwa ilitokea accidentally, na sasa tunajua kuwa sivyo ilivyokuwa,

na respect kwa mtoa mada, maana habari ilipotoka hata kuna baadhi washikaji walioko Dar walikuwa hawajui, nimewapigia wakawa wanshangaaa, kwa hiyo bravo mzee kwa breaking news,

Mzee tafiti, wewe what ever you want nipo imara hunitishi bro, sitishiki na usalama mbuzi, uliza toka BCS wembe wangu ni ule ule!
 
Ni kweli watu wanalewa madaraka na sasa imefika kikomo. Hawa maRC ndio wanaotakiwa kuchunga maisha ya Watanzania sio kuyaondowa kwa uchungu wa vitu visivyokuwa na maana.

Hili linanifanya nilikumbuke jambo linaloniumiza kichwa sana ambalo linawachwa liendelee bila kukemewa nalo ni kuua watu kwa njia ya mob justice na wauaji kufikiria kuwa kitendo hicho wanachofanya ni sawa, na hakuna mtu anayecondemn unyama huu. At least juzi nimesoma kuhusu wanajeshi wawili waliotiwa ndani kule kigamboni kwa kumuua mtu waliyemtuhumu kuwaibia vishillingi kwenye guest house. Kutiwa hawa wanajeshi ndani kungefanyika kwa wale wote wanaowauwa watu kwa kuwatuhumu kuwa ni wezi kwani baadhi ya muaji hayo yanasikitisha sana ukichukuliwa thamani ya hivyo vitu wanavyotuhumiwa kuviiba na ukizingatia ukweli kuwa pengine hata huko kuiba kwenyewe hawakufanya. Mwingine walimtowa msikitini alikokwenda kutafuta kujiokoa maisha juzijuzi tu waka muua. Jamani inakuwaje watanzania tunatowa thamani uhai wa watu hata kufikia kuuwa hadi kuchoma watu moto hadi kufa eti kwa sababu tu wameiba kicell phone au wamenyofowa kioo cha gari?! Watu hawa wanauawa kinyama kwa kupigwa mawe na kuchomwa moto kwa kudhaniwa tu kuwa wameiba vijidubwasha hivi visivyokuwa na maana nasi tunanyamaza tu. Matokeo yake ni haya ya akina Dito. Hizi ni dalili tu za jinsi tusivyohishimu uhai wa watu hivyo inabidi tujirekebishe na kuacha kuchukuwa sheria mkononi. Mambo ya mob justice yakomeshwe kabisa na wale wote wanaoua watu kwa kuchukuwa sheria mikononi mwao, wawe viongozi au walalahoi, wafikishwe mahakamani jamani kujibu tuhuma na kupewa haki wanayostahili. Huyu Dito achukuliwe hatua hizo na wengine wote pia. Huu uuaji wakubeba sheria kwenye bastola, mawe, matairi ya gari na njiti za viberiti UKOME. Ni unyama huu.
 
In fact sheria ya Tanzania kwa kosa la mauaji ya kukusudia kama alivyofanya Ditopile ni kunyongwa mpaka ufe. Kuna watu wengi wamenyongwa kwa makosa hayo ya kuua kwa kukusudia ikiwa ni pamoja na mauaji yanayotokana na kupigania mwanamke halafu katika huo ugomvi mmoja wa wagonvi akauwawa.

Ngoja tuone "mtoto wa mjini" Ditopile atashughulikiwaje. Miezi michache Mkuu wa Wilaya alimpiga mwananchi (http://jamboforums.jamboo.co.tz/showthread.php?t=399) na hakuna hatua inayojulikana kuwa imechukuliwa na serikali dhidi ya mkuu huyo wa Wilaya, sasa leo Mkuu wa Mkoa kaua mtu, na kama hakuna kitakachotokea then by extrapolation Raisi wa nchi ataua ukoo mzima bila lolote kufanyika.
 
Ditotipile umefanya kitendo KIBAYA!!

NA WEWE UNASTAHILI HUKUMU HIYO HIYO!

HAPA SASA NDIPO WAKATI MWINGINE NINAPOONA LABDA MAHAKAMA YA KIISLAMU CHINI YA KADHI INATAKIWA!

JK TUNAKUSUBIRI TUONE KAMA UTAACHA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE!

NILIWAHI KUSIKIA MAMA MMOJA MKUU WA WILYA ALIPGIA WATU MAKOFI LAKINI SIJAJUA AMECHULULIWA HATUA GANI HADI SASA. SASA HILI LA HUYU MHUNI NI BAYA ZAIDI.
 
Theories theories theories are applied in philisophy
In Maths we apply LOGIC
In Law (learned bros and sis) are applying "beyond reasonable doubt" thing.

Hapa wooote tuna doubts, so????, ipo chance, a remote chance ya kumnasua Dito.

Ndivyo itakavyokuwa.

FD
 
Haha, yani mawazo yangu najua ni NEGATIVE na wachangiaji wengine!

Kama umewahi kusafiri na hizi daladala za Dar au kuendesha gari binafsi hapa Dar huenda ukaniunga mkono katika nitakayoongea hapa.

Nimerejea jijini nikasikia habari ya huyu Mzuzuri kufanya kitendo hiki SIKUSHUTUKA. Nilitarajia kitu hiki kutokea siku moja japo sikujua lini na nani atafanya.

Inashangaza kuona mkuu wa Mkoa kafikia uamuzi huu lakini ngoja nami niseme nionavyo.

Ningekuwa mimi pia, NINGEMTWANGA RISASI. Msishangae kwa kauli hii ila huwa inatokea mtu unapoteza ile akili ya kuwa kuna sheria unaamua ku-act Starling wa picha.

Usafiri wa Dar:-

Kuna ka mchezo flani hivi wanaita kuchomekea. au kumpiga pasi mtu. Hii imewahi kunitokea mara kibao wakti naendesha kijidude changu mi naita gari (Suzuki) nikitoka kazini kuelekea mitaani baada ya uchovu. Dereva wa kipanya (daladala) alinichomekea nikajikuta nadumbukia kwenye mtaro kisha akakimbia bila hata ya samahani! For God, ningekuwa na risasi ningemtungua!

FD nadhani wewe upo Dar unanipata namaanisha nini. Siku nyingine nilikuwa kwenye daladala nikitokea Mwenge (kabla vunjavunja haijashika hatamu). Nakumbuka ilikuwa saa 4 usiku. Gari lilikuwa linatangaza nusu safari ili mkifika mbele litangaze route nyingine. Humo kondakta alithubutu kusema wote humu ni mademu tu! Kisa watu tumemwambia kwanini atangaze anaishia Sinza Madukani wakti gari yake ni ya Kariakoo. Fikiria mzee mzima nilikuwa na wife ndani humo. Dah, hasira ziliniwaka lakini niliwaachia abiria wengine wamrekebishe. Walimjibu kwa kujibizana lakini naamini kama vipi wangekuwa na silaha wengine wangemdungua tu!

Nakumbuka siku si nyingi kuna kondakta alimsukuma mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Azania (ili asipande gari yake kwakuwa ni hasara). Alimsukumiza na akaanguka kisha tairi ya gari hilo (ya nyuma) ikampitia na kumuua papo hapo. Kilichofuatia ilikuwa ni wanafunzi kuandamana na kuzitwanga mawe daladala zipatazo 19 na kuondoa vioo kwa hasira baada ya kuona mwenzao kauwawa kikatili vile. Hawa wangekuwa na bunduki naamini wangewadungua makondakta na madereva wa daladala!

Kwa wanaoujua usafiri wa daladala wa Dar unakera sana hasa kamchezo ka kuchomekea! Yani wako radhi wakuue wewe kwa kisingizio kuwa wamebeba raia wengi na wewe ni mmoja hakuna hasara sana. Najua hapo yawezekana ndipo palipomkuta mzee mzima Ukiwaona, akajikuta bila ajizi anafanya kweli! Huyu mura hajaishi na waswahili naona, hakuwahi kuchomekewa.

TATIZO:- Silaha hizi wanazopewa watanzania kadhaa hazitumiki vile wamepewa watumie. Aidha kuna matendo kama hayo mengi ingawa watu wanatumia mawe kufanya mauaji, wengine moto, wengine vitu kama hivyo. Ni hasira, watanzania inabidi tuwe wenye subira na kupunguza hasira. Pole zake Mzuzuri, ajue wengine tumezoea na tukichomekewa huwa tunavumilia na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na kifo!

Huyu hukumu yake ndogo tu... Auaye kwa upanga nae afe kwa upanga! Akikuchomekea mchomekee! Mzuzuri atunguliwe pia... :)
 
Bwana Mkira chonde chonde usituletee habari za mahakama´ya Kadhi katika ili suala la Ditopile. Kwani uliambiwa Mahakama kuu imeshindwa kutoa hukumu?. Please usitumie kesi ya Ditopile kuteletea mahakama za Kidini, lazima uelewe kwamba Tanzania aina dini. Kama unataka mahakama ya kadhi ianzisheni kwa katiba ya BAKWATA na sio kubomoa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa matakwa ya watu wachache.Kesi ya Bwana DITO iachie mahakama kuu.Mahakama za kidini hazina nafasi Tanzania na wala hatuziitaji.
 
Kichuguu,

Ni kweli usemayoi
Kaanza Mkuu wa wilaya kupiga mtu, kafuata RC kuua mtu, huko nyuma mtoto wa Rupia, mtoto wa kingunge kinje na waziri mmoja alishawahi kugonga na kuua (nafikir alikuwa Kilontsi, plse correct me if im wrong), hawa wote wana peta, believe me.

Watu tuliowaweka kwa kura nyingi madarakani, tena huyu Ditopile kada mzuri tu wa CCM wanatuua, maskini Watanzania sie, sijui tukimbilie wapi

Eee Mola wetu sikia Kilio chetu, wanatuua kwa risasi, kutugonga na magari yao, kwa kutotupa elimu, kwa kutusababishia umaskini na hatimaye maradhi IPTL na mengineyo meengi, Eee Mola tunakuomba uibariki nchi yetu na hawa watu wapate haki yao mbele yako
 
Dito kisha tengenezewa mazingira ya kupunguziwa adhabu,his was murder,pure and simple,lakini mtasikia atashtakiwa for manslaughter,which carries a much lesser sentence(could be even less than 10 yrs) Kitendo cha Tibaigana kusema kuwa 'kaua bila kukusudia' ana maana hio ni manslaughter.

Kwa wale ambao wanadhani anaweza kuokolewa,wasijidanganye,kesi ya mauaji especially kama hii ambayo kiongozi kaua raia mpiga kura akiwa 'sehemu' yake ya kazi,hata raisi anaikimbia.Leo hii Waziri wa Serikali za Mitaa ambaye ndio bosi wa ma RC kishasema sheria itafuata mkondo wake,hilo kwa kifupi ni tamko la serikali.

Mimi ningependa kupingana na wOrM anayeunga mkono kitendo hicho.

Moja,no matter what,nobody has the right to take the life of another,period!

Pili, jaribu kwanza kujiweka kwenye nafasi ya muendesha daladala...i.e,unaamka saa kumi na moja asubuhi na kumaliza kazi saa tano usiku,hapo tumeongelea muda tu.Sasa basi,fikiria muda wote huo unaufanya kwa kupita njia ileile kwa masaa zaidi ya 18,kwenda na kurudi,with all the traffic,heat,fatigue and so forth,jaribu hata na gari ndogo tu uone ugumu wake.. Katika muda huo, umetukanwa matusi aina yote unayoyajua,umetishiwa kupigwa mara nyingi tu,kugombana na abiria waogoma kulipa,huku traffic police nae ana yake on top of that,ni lazima ukamilishe hesabu kwa mwenye basi! Tusisahau kuwa hawa ni binadamu,wanaotegemewa na familia zao ambao wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana.Ukilielewa hilo,(ambalo Ditto kwa kuwa ni mtoto wa mjini kama anavyojiita mwenyewe,na alishakiuwa RC wa Dar analielewa vizuri sana)hutaweza hata kutukanana nao,utaona ni upuuzi na kujipotezea muda.
Huyu bwana asingekuwa dereva wa daladala leo hii angekuwa hai.Kilichomponza mpaka akapoteza maisha yake sio wizi,ubakaji,ujambazi au utapeli,bali ni KAZI YAKE halali.Na aliyemuua,probably alikuwa anakwenda Bagamoyo kujipumzisha na kimwana wake(maana taarifa zinasema kulikuwa na abiria wa kike kwenye gari).Na ilikuwa ni weekend.

Kwa kifupi ni kwamba,Ditto ndio kishajimaliza kisiasa,maana definatelly atakuwa convicted,Tibaigana was pretty specific on that,maana alisema 'mheshimiwa aliua bila kukusudia'...sio kwamba inasadikiwa aliua.In that sense kishakuwa criminal,na hawezi kuajiriwa tena.Msamaha wa raisi ndugu zangu huawahusu wauaji,wabakaji,kesi za madawa ya kulevya. Huyu ni muuaji,msamaha wake ni Mungu tu!

Pia ningependa kugusia kwenye hili la kusema kagonga kioo mpaka risasi ikajifyatua...thats bullshit!Hata kama angegonga kioo na hakutaka kumdhuru ule mtutu ungeelekea juu,ili incase of anything dereva wa daladala asidhurike,hilo moja na pili hata kwenye movie jamani muwa tunaona mtu akigonga kitu hiwa anatumia kitako(butt) kama kweli hadhamirii kumdhuru mlengwa.And what happened to that thing they call safety?Na risasi ilikuwa inafanya nini kwenye chamber,alikuwa anategemea kuvamiwa?Being an ex soldier,he has all the answers.Kwangu mimi,i dont care yeye ni nani,that was murder tena premeditated!
 
Wakati wa JK kujionesha ni kiongozi ndio huu!! ameshindwa kwenye maswala ya mikataba.. je ataweza kwenye kutetea haki!?
 
wOrM said:
Ni mawazo tuu...

Miaka minne iliyopita nilikuwa hapoa Dar kusalimia ndugu. Nikiwa nazinguka mtaa wa Samora kutafuta bidhaa za kibongo nikagongwa kwa nyuma na kijana mmoja, siyo dereva wa daladala; yaliyonipata wakati huo ni sawa kabisa na yaliyomkuta mtoto wa mjini Dito. Sote mimi na yeye tulitelemka kutazama uharibifu na kwa bahati nzuri mimi nilikuwa na karandinga (gari kubwa kidogo) kwa hiyo hakukuwa na uharibifu wowote, ila yeye gari yake ikawa ilipinda bonnet. Sasa yule kijana anataka kunijia mimi juu eti kwa nini nilikuwa nimesima wakati akiona kabisa kuwa tulikuwa kwenye foleni. Nikamwuliza kuwa kwani ulitaka niruke magari yaliyoko mbele yangu? Akanyamaza na kulalamika kuwa gari la watu sijui atafanyaje. Nilimwambia tuite polisi waje kupima ajali kususdi akadai insurance lakini akakataa na kuondoka na gari lake huku bonnet likiwa limepinda. Nikahisi kuwa pamoja na kuwa gari hilo alikuwa kaliazima, kijana huyu hakuwa na leseni hivyo hakutaka kukaribiana na polisi.

Ninachotaka kuongezea kuwa kuna madereva wengi ambao eidha hawana leseni au wana leseni lakini hawana uwezo wa kuongoza magari kwa makini na mara nyingi wanaendesha wakati mawazo yao hayako barabarani.

Baada ya hayo, hata kama dereva wa daladala aliyeuawa alikuwa na makosa, bwana Ditopile hana mamlaka ya kuwa mwendesha mashtaka, hakimu na mnyongaji papo kwa papo. Yeye ni raia kama sisi sote na anatakiwa afuate sheria za nchi kama wengine. Ni matumaini yangu kuwa sheria itachukua mkondo wake na Bwana Ditopile naye atanyongwa kama vile alivyonyongwa Bwana Mwamwindi kwa kumwua Mkuu wa Mkoa Dr. Kreluu mwaka 1971.
 
Swali je risasi ilitoka kwa bahati mbaya au alidhamiria hapo sasa ndipo tutakapoana ukomavu wa sheria za tanzania na vyombo vya dola
 
Huyu Ramadhani Mwinshehe Ukiwaona Ditopile Mzuzuri si ndio yule yule aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar miaka ya 90? Namkumbuka kwa kauli zake za dharau na Utoto wa mjini.Kwani kuna kipindi huko Kinondoni kulikuwa na ugomvi kwenye uchaguzi,kwa sababu wazawa wa Dar walikuwa wanalalamika kuwa watu wa kigoma wanataka madaraka Dar.Ditopile alisema "Dar ina wenyewe watoto wa mjini,haiwezi kuongozwa na watu wenye matongotongo,waliokuja kwa treni".Pia kuna kipindi huko nyuma alifumaniwa ugoni huko Upanga ,na bila aibu alisema "Hakuna mwanamume lijali anayeogopa kufumaniwa".Sasa kauli zote hizo zinaonyesha dharau na kutoogopa Binadamu wenzio hata Mungu!Sasa ni zamu yake aende huko Lupango akawaone watoto wa mjini haswa! ambao bila shaka watamshika ma***!.Bado tunangoja kauli ya serikali kuhusu hili jambo!
 
Hahaha, nashukuru bro Zanaki kwa kunipinga. Ni kweli uongeayo lakini kumbuka nilitoa hitimisho kwa kutoa hukumu (japo mi si hakimu) ya kumdungua kama alivyofanya.

Wasiwasi wangu ni
1. Dereva wake kugeuziwa kibao kuwa ndio alifyatua risasi katika kumlinda boss.
2. Mheshimiwa ashadaiwa 'aliua bila kukusudia' (kitu ambacho napingana nacho kabisa kwani kitendo cha kutoa silaha anamaanisha KADHAMIRIA. Hapo wanasheria ndo hunikata maini kabisa! Sheria za nini sasa kama vitu vingine viko wazi kiasi kile? Unatoa silaha, ni wazi unataka kuitumia. Kama ni kisu maanake wataka kuchinja mura!
3. Ni wazi hataupata ukuu wa mkoa tena, lakini kama mwenzangu Mwawado alivyosema hapo juu '... "Ditopile alisema "Dar ina wenyewe watoto wa mjini,haiwezi kuongozwa na watu wenye matongotongo,waliokuja kwa treni".Pia kuna kipindi huko nyuma alifumaniwa ugoni huko Upanga ,na bila aibu alisema "Hakuna mwanamume lijali anayeogopa kufumaniwa"...'
Sasa hapo kakangu elewa huyu ni mbabe!

Nasikitika even JK is not above the law. But I doubt our lawyers wakaichelewesha kesi hii au kuifanya isahaulike masikioni mwa watanzania na unaweza kukuta hukumu yake inatoka 2015! (Hahahaha... Nothing imposible in Tanzania... Nothing!)

Yangu mie macho!
 
wOrM said:
Nasikitika even JK is not above the law. But I doubt our lawyers wakaichelewesha kesi hii au kuifanya isahaulike masikioni mwa watanzania na unaweza kukuta hukumu yake inatoka 2015! (Hahahaha... Nothing imposible in Tanzania... Nothing!)

Kuna Kesi ya mauaji ya changudoa mmoja nadhani akiitwa Modesta (correct me if am wrong) ilifutwa kienyeji tu bila maelezo yoyote. Kwa hiyo tusubiri mambo yatakavyokuwa.

Kwa jumla mimi ninataka Ditopile anyongwe kama vile Mwamwindi alivyonyongwa kwa kumpiga risasi Mkuu wa Mkoa. Mambo ya watu kuuana kiubabeubabe tunataka yakome tuishi kwa amani.
 
Mimi ntakuwa na msimamo tofauti kuhusus suala hili

KWA NINI TUSISUBIRI UAMUZI WA MAHAKAMA KABLA YA KUMHUKUMU?

Afterall according to law the man is still innocent until proved otherwise

au mnasemaje?
 
DrWHO said:
Mimi ntakuwa na msimamo tofauti kuhusus suala hili

KWA NINI TUSISUBIRI UAMUZI WA MAHAKAMA KABLA YA KUMHUKUMU?

Afterall according to law the man is still innocent until proved otherwise

au mnasemaje?

Hiyo ni kweli kabisa kuwa mahakama ndiyo itakayoamua kama huyu mheshimiwa ana hatia na adhabu gani apewe kwa kosa hilo. Tatizo letu ni pale mahakama zinaposhindwa kuendesha haki kwa watu wote. Ukiangalia kwenye posts za nyuma utaona mifano mingi tu ambapo viongozi na matajiri wamekuwa wanaachiwa na mahakama hata kama makosa yao yako wazi

Katika kesi hii kinachotakiwa ni upande wa mashitaka (yaani serikali) kuionyesha Mahakama kuwa Ditopile alifanya kosa hilo na alikuwa na nia ya kulifanya. Ushahidi utakaotakiwa ni pamoja na taarifa ya kipolisi (yaani serikali) kuonyesha kuwa marehemu aliuwawa na risasi iliyofyatuliwa na Ditopile ikiwa imelengwa kwake. Ushahidi mwingine utakaotakiwa ni silaha iliyotumika kufanya mauaji hayo. Mwishoni Mahakama itatakiwa iambiwe kama kulikuwa na motive yoyote kwa Ditopile kufanya kosa kosa hilo.

Kwa taarifa zilizopatika kutoka vyanzo mbalimbali ni kwamba huyu jamaa alishikwa red-handed akifanya hilo kosa. Abiria wa kwenye dala dala la marehemu na dereva wa Ditopile mwenyewe walimwona Ditoplie akifanya kosa hilo; silaha iliyotumika kufanya kosa hilo imeshikwa na inajulikana kuwa ni mali yake; mtu aliyeuwawa anajulikana na kuna ripoti za kipolisi kuonyesha kuwa alikufa kutokana na mejeruhi ya risasi iliyopigwa kichwani mwake kutoka kwenye bunduki ya Ditopile baada kufyatuliwa na Ditopile mwenyewe; motive inajulikana kuwa ilikuwa ni kutokana na aksident ndogo ya barabarani iliyomhusisha marehemu na mtuhumiwa.


Kwa hiyo kama sheria haitapindishwa, ni imani yetu kuwa mahakama itamkuta na hatia ambayo adhabu yake ni kunyongwa.
 
DrWHO
Hata wakati tunasubiri uamuzi wa mahakama tunayo haki ya kulijadilia hili suala. Si eti?
 
Back
Top Bottom