LATRA Mkoa wa Arusha haya mateso ya usafiri wa King'ori na Kikatiti yataisha lini? Daladala zinaishia Maji ya Chai. Abiria wanateseka

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,156
Kuna daladala zimepewa leseni za kusafirisha abiria kutokea maeneo yafuatayo;
1. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kiong'ori
2. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kikatiti

Haya magari kwanza hayaanzii safari sehemu husika km nilivyozitaja hapo juu, mengi km si yote huanzia safari zao stand ndogo. Pili hayafiki mwisho wa safari yaani Kikatiti na King'ori, King'ori ndiyo kabisa hakuna gari linaenda kule. LATRA mkoa wa Arusha mnayafahamu yote haya ila kwasababu ya rushwa iliyokithiri hapo ofisini kwenu hamjishushulishi na mateso ya wananchi. Polisi trafiki wanajua vizuri ila kwasababu ya rushwa na kuwa magari mengine ni ya kwao hawaoni shida kutosimamia sheria.

Kwanini mtu akate leseni ya usairishaji ruti aliyoichagua yeye mwenyewe bila kulazimishwa na akipewa ruti anakuja kujipangia anavyotaka. Ile ni huduma kwa wananchi, watu tunaishi ndani ya nchi yetu kwa wasiwasi huna uhakika wa kufika unakoenda ingawa gari ulilopanda hata kibao chake mbele kinaonesha kinakotakiwa kufika. Badala yake madereva na makondakta ni wababe, wana lugha chafu kuliko unavyoweza kufikiri, anaweza kukujibu kuwa nenda mkokote kashtaki. Wakifika maji ya chai dereva anashuka mtakaa hata nusu saa au zaidi wakisubiri gari ya kuwafaulisha wanavyoita wao, hivi watanzania tumekuwa mizigo mpaka tufaulishwe? na wana lugha yao nyingine ya kusema tunawawauzia gari nyingine, kwanza huu ni udhalishaji wanaofanyiwa wananchi ndani ya nchi yao huru

Mkurugenzi mkuu wa LATRA CPA Suluo nchi hii inajua we ni mchapakazi umeiheshimisha LATRA, ila LATRA mkoa wa Arusha imeoza. Tunaomba msaada wako. Weka maafisa wako pale kituo cha maji ya chai tena watoke Dsm siyo hawa wa Arusha ambao wameshaoza na rushwa, afisa wa LATRA siyo wa kukaa ofisini wantakiwa wazunguke mitaani kuangalia changamoto wanazopata washika dau wao ambao ni abiria, changamoto zingine zinapata majibu on the sport.
Basi lolote litakalokamatwa limeishia Maji ya Chai lifutiwe leseni ya kwenda King'ori au Kikatiti apewe ruti yake ya kuishia hapo hapo Maji ya Chai na abadilishe kibao kuwa gari lake linaishia Maji ya Chai.
Ni serikali tu ndio itatusaidia, hawa wenye mabasi hawaridhiki labda mpaka wale mioyo ya binadamu wenzao, ni majuzi tu nauli iliongezwa, mwezi uliofuata mafuta yalipuangua bei, leo mtu anakuambia mafuta haya ni mashetani manyanayasaji, CPA Suluo wasaidie watanzania wenzako wanaoteswa. Unakuta basi lina abiria hata 10, anageuza. Nafikiri kisheria hata km kuna abiria moja anatakiwa afikishwe mwisho wa safari, hata km hakuna abiria gari linatakiwa lifike mwisho wa safari maana kuna abiria watakuwa njiani wanasubiri usafiri, wengine watakuwa vituo vya mbele inakoelekea gari, wengine wanalisunbiria aidha Kikatiti au King'ori.

Km watu hawataki kustaarabika wenyewe walazimishwe na sheria kustaarabika, mbona mambo hayapo nchi jirani za wenzetu? Tanzania kuna nini, lini tutastaarabika? Ni aibu! Kenya wametuacha mbali sana kwa ustaarabu ktk usafiri, kwanza hukuti hata abiria anayesimama. Nchi za Zambia, Zimbabwe, Uswatini ndiyo km uzunguni, bado South, Namibia. Baadhi ya nchi nimefika ustaarabu wao ni wa hali ya juu sana. Ukija huku kwetu utafikiri sisi sijui ni watu wa aina gani. Siku hizi madereva na makondakta wao Arusha hawavai uniform wamekaa kihuni huni tu, na mamlaka zipo. Arusha inatakiwa isafishwe kuna uozo kuazia jeshi la polisi k,itengo cha usafiri barabarani na LATRA. RTO wa Arusha na map-DTO wake wanafikiri wapo pale kula rushwa na kufanya biashara zao. Ondoeni hawa watu Arusha pelekeni huko mikoa mingine tena ya pembezoni mwa nchi, peleka wilaya km za Tunduru.
 
Abiria gani hao wanaoteseka? Maana kila siku naona ni wewe peke yako ndiye unayelia lia humu jukwaani! Nimekushauri ununue usafiri wako binafsi, hutaki! Wewe kutwa ni kulalamika tu.

Ukiona daladala zinakatiza ruti, ujue mbele ya hiyo ruti hakuna abiria wa kutosha! Na hivyo waningia tu hasara ya mafuta. Kungekuwa kuna abiria wa kutosha, zisingeishia njiani. Umeelewa sasa ewe kijana wa Lumumba?

Halafu hayo mambo ya sare achana nayo. Maana unachokitaka wewe abiria ni kufika safari yako salama na kwa wakati. Sasa hizo sare za makondakta na madereva zinakusaidia nini? Kama siyo ukuda tu na gubu!
Hoja ya jamaa ni ya msingi, hapa suala sio kuwaruhusu hao wenye mabasi kukatisha ruti kwasababu ya ukosefu wa abiria, kama hao LATRA walijua njia hiyo kuna ukosefu wa abiria kwanini wakatoa leseni?

Unakosea zaidi unapomtaka anunue usafiri wake binafsi, kwa hiyo kila penye kero ya usafiri nchi hii dawa yake ni kila mtanzania anunue usafiri wake binafsi?! Umemjibu kibinafsi sana sijui tatizo lako kwake ndio huo "ulumumba"

Suala la yeye kuwa analalamika kila siku pia halina msingi, kama kero ipo, na anayo sehemu ya kutoa kero yake sioni kwanini asifanye hivyo, wengine nao wenye kukerwa na hiyo issue watajua wapi wapeleke malalamiko yao.

LATRA wanatakiwa kufuatilia hiyo njia, waone kama abiria kweli wanakutana na hiyo kero, na kama wakikuta yapo mabasi hayafiki mwisho, dawa ni kuyafungia leseni, au kuyabadilishia leseni ya usafiri.

Lakini sio suala la kununua usafiri binafsi vinginevyo hao LATRA waondoke ofisini ili tujue hawapo abiria wajiongeze, sio wapo halafu hawatimizi majukumu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo kumshauri huyo kijana wa uvccm kununua usafiri wake binafsi ili kuepukana na hiyo kero, ni kosa!
Naona huu "UVCCM" unakupofua kifikra, jifunze kumjibu mtu bila kutazama id yake na kuinasibisha vile upendavyo, kinyume na hapo mchango wako kwake utakuwa chongo always.

Tatizo lolote lazima litatuliwe kwa njia ya muda mfupi na muda mrefu, kumpa mtu njia ya muda mrefu kutatua tatizo ambalo lingeweza kutatuliwa kwa muda mfupi sio sahihi, simply umempa jibu la kumkomoa ukaamua kuwalinda hao LATRA bila kujua, unawaacha waendelee kula mishahara ya bure!.

Au umempa pesa ya kununua gari?!
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kuna daladala zimepewa leseni za kusafirisha abiria kutokea maeneo yafuatayo;
1. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kiong'ori
2. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kikatiti

Haya magari kwanza hayaanzii safari sehemu husika km nilivyozitaja hapo juu, mengi km si yote huanzia safari zao stand ndogo. Pili hayafiki mwisho wa safari yaani Kikatiti na King'ori, King'ori ndiyo kabisa hakuna gari linaenda kule. LATRA mkoa wa Arusha mnayafahamu yote haya ila kwasababu ya rushwa iliyokithiri hapo ofisini kwenu hamjishushulishi na mateso ya wananchi. Polisi trafiki wanajua vizuri ila kwasababu ya rushwa na kuwa magari mengine ni ya kwao hawaoni shida kutosimamia sheria.

Kwanini mtu akate leseni ya usairishaji ruti aliyoichagua yeye mwenyewe bila kulazimishwa na akipewa ruti anakuja kujipangia anavyotaka. Ile ni huduma kwa wananchi, watu tunaishi ndani ya nchi yetu kwa wasiwasi huna uhakika wa kufika unakoenda ingawa gari ulilopanda hata kibao chake mbele kinaonesha kinakotakiwa kufika. Badala yake madereva na makondakta ni wababe, wana lugha chafu kuliko unavyoweza kufikiri, anaweza kukujibu kuwa nenda mkokote kashtaki. Wakifika maji ya chai dereva anashuka mtakaa hata nusu saa au zaidi wakisubiri gari ya kuwafaulisha wanavyoita wao, hivi watanzania tumekuwa mizigo mpaka tufaulishwe? na wana lugha yao nyingine ya kusema tunawawauzia gari nyingine, kwanza huu ni udhalishaji wanaofanyiwa wananchi ndani ya nchi yao huru

Mkurugenzi mkuu wa LATRA CPA Suluo nchi hii inajua we ni mchapakazi umeiheshimisha LATRA, ila LATRA mkoa wa Arusha imeoza. Tunaomba msaada wako. Weka maafisa wako pale kituo cha maji ya chai tena watoke Dsm siyo hawa wa Arusha ambao wameshaoza na rushwa, afisa wa LATRA siyo wa kukaa ofisini wantakiwa wazunguke mitaani kuangalia changamoto wanazopata washika dau wao ambao ni abiria, changamoto zingine zinapata majibu on the sport.
Basi lolote litakalokamatwa limeishia Maji ya Chai lifutiwe leseni ya kwenda King'ori au Kikatiti apewe ruti yake ya kuishia hapo hapo Maji ya Chai na abadilishe kibao kuwa gari lake linaishia Maji ya Chai.
Ni serikali tu ndio itatusaidia, hawa wenye mabasi hawaridhiki labda mpaka wale mioyo ya binadamu wenzao, ni majuzi tu nauli iliongezwa, mwezi uliofuata mafuta yalipuangua bei, leo mtu anakuambia mafuta haya ni mashetani manyanayasaji, CPA Suluo wasaidie watanzania wenzako wanaoteswa. Unakuta basi lina abiria hata 10, anageuza. Nafikiri kisheria hata km kuna abiria moja anatakiwa afikishwe mwisho wa safari, hata km hakuna abiria gari linatakiwa lifike mwisho wa safari maana kuna abiria watakuwa njiani wanasubiri usafiri, wengine watakuwa vituo vya mbele inakoelekea gari, wengine wanalisunbiria aidha Kikatiti au King'ori.

Km watu hawataki kustaarabika wenyewe walazimishwe na sheria kustaarabika, mbona mambo hayapo nchi jirani za wenzetu? Tanzania kuna nini, lini tutastaarabika? Ni aibu! Kenya wametuacha mbali sana kwa ustaarabu ktk usafiri, kwanza hukuti hata abiria anayesimama. Nchi za Zambia, Zimbabwe, Uswatini ndiyo km uzunguni, bado South, Namibia. Baadhi ya nchi nimefika ustaarabu wao ni wa hali ya juu sana. Ukija huku kwetu utafikiri sisi sijui ni watu wa aina gani. Siku hizi madereva na makondakta wao Arusha hawavai uniform wamekaa kihuni huni tu, na mamlaka zipo. Arusha inatakiwa isafishwe kuna uozo kuazia jeshi la polisi k,itengo cha usafiri barabarani na LATRA. RTO wa Arusha na map-DTO wake wanafikiri wapo pale kula rushwa na kufanya biashara zao. Ondoeni hawa watu Arusha pelekeni huko mikoa mingine tena ya pembezoni mwa nchi, peleka wilaya km za Tunduru.

Mkuu mjulishe Makonda atarudi hapo Arusha kutatua hiyo kero ya wananchi.
 
Aiseeh usafiri wa king'ori changamoto.
Ni either ushuke Kibaoni uchukue boda kwa 5000 na kirudi 7000.
Nimekwenda kule Desemba nikawahurumia tu wakaaji wa kule.
 
Sasa wewe naona unataka kunipangia cha kuchangia humu jukwaani! Kwani wewe ni msemaji wa mtoa mada? Vipi kwani, amekwambia hana hela ya kununulia gari? (By the way, katika maelezo yangu nimetaja usafiri binafsi! Hakuna mahali nimetaja anunue gari. Au kwa akili yako usafiri binafsi ni gari tu!!
Usi panic, mpe basi hiyo pesa ya bodaboda au bajaji kama unayo..

Kama hauna, wacha LATRA wafanye kazi yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kuna daladala zimepewa leseni za kusafirisha abiria kutokea maeneo yafuatayo;
1. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kiong'ori
2. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kikatiti

Haya magari kwanza hayaanzii safari sehemu husika km nilivyozitaja hapo juu, mengi km si yote huanzia safari zao stand ndogo. Pili hayafiki mwisho wa safari yaani Kikatiti na King'ori, King'ori ndiyo kabisa hakuna gari linaenda kule. LATRA mkoa wa Arusha mnayafahamu yote haya ila kwasababu ya rushwa iliyokithiri hapo ofisini kwenu hamjishushulishi na mateso ya wananchi. Polisi trafiki wanajua vizuri ila kwasababu ya rushwa na kuwa magari mengine ni ya kwao hawaoni shida kutosimamia sheria.

Kwanini mtu akate leseni ya usairishaji ruti aliyoichagua yeye mwenyewe bila kulazimishwa na akipewa ruti anakuja kujipangia anavyotaka. Ile ni huduma kwa wananchi, watu tunaishi ndani ya nchi yetu kwa wasiwasi huna uhakika wa kufika unakoenda ingawa gari ulilopanda hata kibao chake mbele kinaonesha kinakotakiwa kufika. Badala yake madereva na makondakta ni wababe, wana lugha chafu kuliko unavyoweza kufikiri, anaweza kukujibu kuwa nenda mkokote kashtaki. Wakifika maji ya chai dereva anashuka mtakaa hata nusu saa au zaidi wakisubiri gari ya kuwafaulisha wanavyoita wao, hivi watanzania tumekuwa mizigo mpaka tufaulishwe? na wana lugha yao nyingine ya kusema tunawawauzia gari nyingine, kwanza huu ni udhalishaji wanaofanyiwa wananchi ndani ya nchi yao huru

Mkurugenzi mkuu wa LATRA CPA Suluo nchi hii inajua we ni mchapakazi umeiheshimisha LATRA, ila LATRA mkoa wa Arusha imeoza. Tunaomba msaada wako. Weka maafisa wako pale kituo cha maji ya chai tena watoke Dsm siyo hawa wa Arusha ambao wameshaoza na rushwa, afisa wa LATRA siyo wa kukaa ofisini wantakiwa wazunguke mitaani kuangalia changamoto wanazopata washika dau wao ambao ni abiria, changamoto zingine zinapata majibu on the sport.
Basi lolote litakalokamatwa limeishia Maji ya Chai lifutiwe leseni ya kwenda King'ori au Kikatiti apewe ruti yake ya kuishia hapo hapo Maji ya Chai na abadilishe kibao kuwa gari lake linaishia Maji ya Chai.
Ni serikali tu ndio itatusaidia, hawa wenye mabasi hawaridhiki labda mpaka wale mioyo ya binadamu wenzao, ni majuzi tu nauli iliongezwa, mwezi uliofuata mafuta yalipuangua bei, leo mtu anakuambia mafuta haya ni mashetani manyanayasaji, CPA Suluo wasaidie watanzania wenzako wanaoteswa. Unakuta basi lina abiria hata 10, anageuza. Nafikiri kisheria hata km kuna abiria moja anatakiwa afikishwe mwisho wa safari, hata km hakuna abiria gari linatakiwa lifike mwisho wa safari maana kuna abiria watakuwa njiani wanasubiri usafiri, wengine watakuwa vituo vya mbele inakoelekea gari, wengine wanalisunbiria aidha Kikatiti au King'ori.

Km watu hawataki kustaarabika wenyewe walazimishwe na sheria kustaarabika, mbona mambo hayapo nchi jirani za wenzetu? Tanzania kuna nini, lini tutastaarabika? Ni aibu! Kenya wametuacha mbali sana kwa ustaarabu ktk usafiri, kwanza hukuti hata abiria anayesimama. Nchi za Zambia, Zimbabwe, Uswatini ndiyo km uzunguni, bado South, Namibia. Baadhi ya nchi nimefika ustaarabu wao ni wa hali ya juu sana. Ukija huku kwetu utafikiri sisi sijui ni watu wa aina gani. Siku hizi madereva na makondakta wao Arusha hawavai uniform wamekaa kihuni huni tu, na mamlaka zipo. Arusha inatakiwa isafishwe kuna uozo kuazia jeshi la polisi k,itengo cha usafiri barabarani na LATRA. RTO wa Arusha na map-DTO wake wanafikiri wapo pale kula rushwa na kufanya biashara zao. Ondoeni hawa watu Arusha pelekeni huko mikoa mingine tena ya pembezoni mwa nchi, peleka wilaya km za Tunduru.
Si alikuwepo Makonda huko hamjamalizana nae?
 
Aiseeh usafiri wa king'ori changamoto.
Ni either ushuke Kibaoni uchukue boda kwa 5000 na kirudi 7000.
Nimekwenda kule Desemba nikawahurumia tu wakaaji wa kule.
Mleta mada hazungumzii usafiri kati ya King'ori na Kibaoni. Anazungumzia ile route ya stand (mjimi) mpaka Kibaoni. Kuna confusion iko kwa Latra/Tanroads wanapotoa leseni/kuweka vibao vya barabarani; pale Kibaoni wanapaita King'ori, hilo ni kosa. So mleta mada analalamika daladala zinatoka mjin na kuishia Maji ya chai, au nyingine Kikatiti, badala ya kwenda mpaka King'ori.
 
Back
Top Bottom