Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,831
Katika suala lililoitikisa fani ya sheria na utoaji haki ni tukio la miaka 17 iliyopita kutokana na mlolongo wa matukio yaliyojiri baada ya kufunguliwa mashitaka ya mauaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wa wakati huo, Ukiwaona Ditople Mzuzuri baada kumpiga risasi dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33) mwaka 2006.
Pia, soma=> Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala
Kesi ya mshitakiwa huyo ilisababisha mahabusu katika magereza ya Dar es Salaam na kwingineko, kugoma kuingia kwenye magari kwenda mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kesi zao. Mgomo huo wa siku tano haukuwahi kutokea nchini.
Upelelezi wa kesi dhidi ya Ditopile ulichukua miezi minne tu hadi mashitaka kubadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya kutokusudia, na hivyo kupewa dhamana.
Hilo liliwakasirisha sana mahabusu wengine waliokuwa wakingojea kesi zao (pamoja na zile kesi za mauaji), ambazo baadhi yao walikuwa mahabusu kwa miaka kadha. Walitaka nao wafanyiwe uharaka wa namna hiyo katika kuchunguza kesi zao, la sivyo dhamana ya Ditopile ifutwe.
Askari kanzu wakimpeleka Athumani Ukiwaona Ditopile Mzuzuri lupango mara baada ya kusomewa shtaka la mauaji mbele ya hakimu mkazi, Michael Lugulu mahakama ya Kisutu November 06, 2006.
Kesi ya Ditopile ili-trend kwa matukio mengi ikiwemo ndugu wa Ditopile kuwarushia maneno na kuwafanyia vurugu ikiwemo kuwamwagia maji waandishi wa habari waliokuwa wanafatilia kesi hiyo kwa madai ya 'kuishikia bango'. Baada ya tukio hilo kesi ya Ditopile ilitawala 'Front Page' zote za magazeti makubwa na prime ya TV stations 'waandishi wakilipa kisasi'
Pia kapteni Ditopile akiwa mahabusu, alipata bahati ya kutembelewa na Rais aliye madarakani wakati huo, Jakaya Kikwete akisema ni rafiki yake wa siku nyingi.
Ndani ya miezi minne uchunguzi ulikamilika na kesi yake ikabadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia kwenda mauaji bila kukusudia.
Baada ya kesi kubadilishwa, Ditopile alitoka nje kwa dhamana.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri huko nyumbani kwake Upanga. Kulia ni Mariam Ditopile mtoto wa marehemu na nyuma ya Rais ni mtoto wa Rais, Rashid Chodo Kikwete.(April 21, 2008)
Hata hivyo, mwaka 2008 ikiwa bado kesi yake haijapata hukumu, kapteni Ditopile aliaga dunia katika hoteli ya Hilux mkoani Morogoro akiwa na mke Mdogo. Sababu ilitajwa kuwa mshtuko wa moyo.
Pia, Soma=> Ukiwaona Ditopile afariki dunia