Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

mTz

JF-Expert Member
Aug 20, 2006
282
21
The regional commissioner of the Tabora Region Ukiwaona Ditopile Mzuzuri has been arrested under suspicion of shooting dead in the head a Dala-Dala Driver last night.

News that reached TZUK.net from a very credible source in Tanzania say that Ditopile's vehicle was hit by the DalaDala that sped off after the incident, Ditopile's driver gave chase and the Daladala finally stopped.

However when Mzuzuri's driver went out to ask the Daladala driver as to why he failed to stop after the occurence the Daladala Driver kept silent while his Daladala windows were up and car locked, having failed to make any progress the driver returned to his car and reported this to his Boss.

At this point Mr. Mzuzuri got out of the car with a Pistol in hand and started challenging the driver verbally as to why he did not stop after the accident but got no response. Now with a pistol in hand Ditopile started banging on the driver's window, the gun accidentally went off shooting and killing the Daladala driver in the head and splitting his head apart.

=======
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji

Ditopile Mzuzuri.jpg

Ukiwaona Ramadhan Ditopile Mzuzuri

Na Muhibu Said

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ramadhan Ditopile Mzuzuri, ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za mauaji ya raia kwa kutumia bastola yake jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, zinaeleza kuwa Ditopile anatuhumiwa kumuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), mkazi wa Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam kwa kumpiga risasi kichwani.

Ditopile anatuhumiwa kumuua dereva huyo juzi saa 2.30 usiku, katika njia panda ya barabara ya Kawe na Bagamoyo, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kuchukizwa na hatua ya gari lake kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu. Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.Gari hilo lililigonga gari aina ya Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva wa Ditopile, Nassoro Mohamed (42), mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo, mkoani Pwani.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.

Walisema wakati dereva huyo akiendelea kulikagua gari hilo, Ditopile naye alishuka na kuungana na dereva wake katika ukaguzi huo.Walisema baada ya kuona uharibifu huo, Ditopile, alimfuata marehemu na kumtaka ashuke katika gari alilokuwa akiliendesha ili aende kushuhudia uharibifu uliotokea na kisha waende polisi.

Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu, alimweleza Ditopile kuwa ajali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya na kumwomba msamaha kwa tukio lililotokea.Walisema mkuu huyo wa mkoa, hakukubaliana na utetezi huo na badala yake aliendelea kumwamuru marehemu ashuke kwenye gari na kumtaka akaeleze maneno hayo polisi.

Mashuhuda hao, walisema marehemu alipoona Ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali, aliamua kufunga kioo cha gari kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo.Walisema kitendo hicho kilimuudhi Ditopile ambaye alichomoa bastola aliyokuwa nayo na kuanza kuitumia kugonga kwenye kioo cha gari la marehemu huku akimsisitiza kushuka katika gari.

Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu aligoma kutii amri hiyo ya Ditopile na ndipo alipomfyatulia risasi iliyopenya kwenye kioo cha gari na kufumua kichwa cha marehemu. Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika eneo hilo muda mfupi baada ya tukio hilo, alishuhudia mwili wa marehemu ukiwa umeegemea kwenye kiti cha dereva huku damu na ubongo vikiwa vimetapakaa ndani ya gari alilokuwa akiliendesha. Tukio hilo lililozua hofu, lilisababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa watu, wakiwamo madereva na abiria waliokuwa wakisafiri katika njia hiyo, kutokana na mlio wa risasi.

Watu waliokuwa kwenye magari, walishuka na kuanza kukimbia ovyo katika sehemu mbalimbali wakidhani kuwa eneo hilo limevamiwa na majambazi. Watu pekee waliobaki katika eneo hilo, ni dereva anayedaiwa kuwa wa Ditopile na mwanamke ambaye hakuweza kufahamika mara moja ambaye anadaiwa kuwa alikuwa katika gari lililokuwa limembeba Ditopile.

Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.

Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana.

Dakika chache baadaye, polisi waliobeba silaha wakiwa ndani ya magari matatu aina ya Lond Rover Defender, walifika katika eneo hilo. Akielezea tukio hilo, Kamishna Tibaigana, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku katika eneo hilo na gari lililombeba Ditopile, lilikuwa na abiria wawili; akiwamo Ditopile mwenyewe na mtu mwingine ambaye hajafahamika.

Alisema wote walikuwa wakitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo."Mara baada ya ajali hiyo kutokea, magari hayo yalisimama. Dereva Nassoro Mohamed alishuka na kwenda kuangalia gari lake ili kubaini lilivyoharibika/kugongwa, aliliona limepata madhara kidogo upande wa nyuma," alisema Kamishna Tibaigana na kuongeza:

"Wakati Nassoro Mohamed akiendelea kuangalia, alishuka mheshimiwa Kapteni Ukiwaona Ramadhani Ditopile Mzuzuri ili naye aende kuona uharibifu uliotokea. Baada ya kuona uharibifu uliotokea alimtaka dereva wa Isuzu Journey, Hassan Mbonde, ashuke ili naye aone uharibifu uliotokea kisha waende polisi kutoa taarifa."Dereva wa Isuzu Journey alikataa kushuka kwenye gari lake na badala yake alifunga kioo cha dirisha la mlango wake kisha alifunga mlango na ku-lock kwa ndani.

Mheshimiwa Ditopile Mzuzuri baada ya kuona dereva amefunga mlango, alisogelea dirishani na kutoa bastola yake na kuanza kugonga dirisha kwa kutumia bastola yake, huku akimwamuru ashuke ndipo ghafla alifyatua risasi moja ambayo ilivunja kioo cha dirisha na kumjeruhi Hassan Mbonde kichwani na alifariki dunia papo hapo," alisema Tibaigana katika maelezo yake kwa waandishi wa habari.

Tibaigana, alisema baada ya tukio hilo, dereva Mohamed, aliendesha gari lake na kuondoka sehemu ya tukio akiwa na abiria wake wawili. "Mtuhumiwa Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri amekamatwa na anaendelea kuhojiwa. Pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Kamanda Tibaigana.

Asubuhi jana, watu walimiminika katika Kituo cha Polisi Kawe kwa ajili ya kuandikisha maelezo yao juu ya jinsi walivyoshuhudia tukio hilo.Baadhi walisimulia kuwa katika tukio hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alipiga risasi mbili ambapo moja ilimkosa marehemu na nyingine ndiyo ilimuua papo hapo. Daladala aliyokuwa akiendesha marehemu Mbonde ilikuwa imeegeshwa katika kituo hicho cha polisi na baada ya baadhi ya watu kutoa maelezo, walitakiwa kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Nyumbani kwa marehemu kulikuwa na watu wachache huku mvua ikiendelea kunyesha na wengi wao walikuwa wakijadili tukio hilo. Marehemu Mbonde ameacha watoto wadogo watatu. "Hii inatakiwa Rais aunde Tume kama ilivyokuwa kwa Zombe, hivi hivi hakutakuwa na haki," alisema muombolezaji mmoja.Watu hao walishikwa na hasira na kutaka kuwavamia waandishi waliokuwa msibani hapo baada ya redio moja kutangaza kuwa marehemu alikufa katika ajali.

Habari zilizopatikana msibani hapo zilieleza kuwa marehemu Mbonde atazikwa leo saa saba mchana katika makaburi ya Kawe.
 
Of all the things Ditopile is accused to have done, hii ndio kubwa sana na kwa kweli we have to see anaweza kujibabadua vipi.

Maswali ya haraka haraka kwangu ni haya:

1. Is he licensed to keep/possess a gun?

2. Why was he in possession of a gun at a public place kama hivi?

3. Does he understand his restrictions to keep a gun?

4. Kwa nini asiripoti kituo cha polisi au kuchukua namba za dala dala husika na kukabidhi mamlaka husika.

5. Dereva wa mkuu wa mkoa ambae yupo out of his jurisdiction, [dito ni mkuu wa mkoa wa tabora, hii incident kwa source zangu naelewa kwamba imetokea Dar es salaam] anaruhusiwa kufanya 'police chace'?

6. For that matter is he allowed to do a chace after all?

Kwa kweli huu ni mtihani mkubwa kwa Mzee JK kwa vile huyu naambiwa ni mwanamtandao mkubwa...
 
Ni kweli huyu Bwana Ukiwaona kaua, Hivi huu uungu mtu utakwisha lini kule nyumbani? kweli inasikitisha sana sana
 
Invisible even me I'm shocked, actually it is unbelievable. After getting this piece of info I scanned all Tanzania newspapers to get further clarification with no avail and I hope wanabodi waliopo Bongo watatuhabarisha zaidi. Kama ni kweli itakuwa ni test case nzuri sana ya kuona kama haki itatendeka.
 
Hivi Tanzania kumekuwa mahali pa hatari mpaka watu wanatembea na Silaha? Hili ni jaribio kubwa kwa Utawala wa sheria Tanzania.
 
Kamanda wa Kaanda ya polisi maalum ya Dar es saalam amethibitisha na kasema kwamba ni kweli ameuwa na anashikiliwa na polisi na hivyi karibuni atafikishwa mahakamani.
 
The main thing is, ".....then the gun went off accidentally killing......", tuitoe hukumu kabla ya kesi,

Tafiti iachie mahkama iamue kama ni kweli hiii kesi ipo!
 
Mzee Es, sawa "the gun went off accidentally Killing" je na uyo Dreva wa daladala alikuwa na silaha yeyote au?

Je sheria ya usalama barabarani inaruhusu, kama ukigogwa na gari jingine na jamaa akakimbia unaruhusiwa umfukuze mdeni wako mpaka umpate au utoe taarifa polisi?

Je ni wakati gani unaruhusiwa kutumia silaha unayomiliki kisheria?

Ni hata ukikwaruzana na muuza nyanya sokoni unatakiwa uitoe na kumtisha au kumfyatulia risasi.Je hata kukiwa na verbally conflict unaruhusiwa kutoa silaha na kumtishia adui yako ambae hana hata panga?

Kwa wale wanaofaamu sheria ya kumiliki silaha na sheria ya usalama barabarani naomba wanaisaidie kunielewesha zaidi.
 
Hakuna hata swali moja katika maswali niliyouliza linahusiana na hukumu, maybe kuhusu connection yake na wanamtandao which is a fair assessment.

Nimemsikia TIBAIGANA katka bbc hivi punde akisema huyu jamaa bado yupo selo tangu jana na atafikishwa mahakamani hivi karibuni.

TUnataka sheria ichukue mkondo wake ,hizi accidentally went off air huoni kwamba ni PR inaanza kutumika kufanya damage repair, let him have his day in court...

I feel for him as someone close to me lakini hapa hakuna kumuangalia nyani usoni, nimeshakaa nae katika vikao kadhaa mzee DITO mcheshi, mwingi wa maneno, chekibobu licha ya umri wake nk lakini hapa NO sheria ichukue mkondo!
 
It is terrible! I cant believe am reading this, it is like I am just dreaming!

Sasa tuone hiyo sheria kama itauma kweli. Tulimsifia sana JK jinsi alivyohandle ile kesi ya Sinza; nafikiri huu ndio mtihani mkubwa zaidi kwa JK kuliko ule wa Sinza.
 
Mzee Es,

Uncle huyu jamaa kenda mbali sanaa. Huwezi kutishia na bastola na kisha kuua kwa kisingizio cha bahati mbaya.
Kwanza kabisa ktk kesi za mauaji, ku-withdraw bastola ina maana moja tu unataka kuitumia!

Pili huwezi kuondoa safety ikiwa huna kusudio

Na mwisho huwezi kuielekeza kwa mtu ikiwa kidole chako hapo ktk trigger na kudai bado bahati mbaya.
Kuua kwa bunduki na hasa bastola hakuna bahati mbaya unless mtu huyo ni mtoto mdogo asiyejua anachofanya.

Huyu, mshikaji kaua na haki lazima isimame!
 
Hapana we are all reacting, kuotkna na kichwa cha mada, na kama ni kweli hiyo sentesi ambayo sikuiandika mimi ni very important kisheria kuliko the whole sagga,

kisiasa, yes it ok kumwaga emmotions, as you can see michango ya hii mada, lakini kama ni kweli huyu jamaa ameua kwa makusudi, basi Mzee Malecela was right alipomzuia JK asimpe ukatibu mkuu wa CCM,

Halafu ni muhimu kpata habari zaidi na tutazipata tu au tumneshaanza kuzipata, my sympathy kwa ndugu wa marehemu dreva wa dala dala ambaye ni very easy kumsahau kwenye hii hype ya Ditopile!
 
Mkandara maneno yako ni sahihi kabisa, why on earth atoe bastola wakati yule dereva hakuonekana kumtishia usalama Mh. Dito kama ninavyoquote hapaHowever when Mzuzuri's driver went out to ask the Daladala driver as to why he failed to stop after the occurence the Daladala Driver kept silent while his Daladala windows were up and car locked, having failed to make any progress the driver returned to his car and reported this to his Boss.

Hata kama Dito alikuwa tu na nia ya kupiga mkwala, sasa ndio hivyo tena ameshaharibu. Generally kuna tendency ya watu wenye bastola kutishia watu, mimi nimeshahudia kwenye maulevi jamaa wakizichomoa. If the case is well handled it can serve as a lesson kwa wote wanaown silaha.
 
kuna options mbili tu!! aidha tutashuhudia sheria ikifuata mkondo (kama kesi ya Zombe na wenzake au we will witness the "grand illusion" of all times!!!
 
Kutokana na hiyo isu ilivyo kaa, ditopile ataachiwa huru na ataendelea na kazi yake, ila kwa hao polisi waliomuweka sero, ndio watakiona chamoto, unajua mkuu wa mkoa ni apointee wa rais kwahiyo ana presidential power, kilichotokea ni kuwa aligongwa na daladala, kwahiyo yeye kama mkuu wa mkoa alikuwa anakazi mbili, kwanza ni self defence halafu pili nikumkamata mtuhumiwa, yaani kwa jinsi isu hao waliomuweka ndani ditopole watakiona cha moto.
 
Someni gazeti la mwananchi, limeandika vizuri zaidi hii saga kuliko hiyo habari iliyopo kwa kiingereza kwenye Tzuk.net. Na-paste hapa for clarity purposes

Mkuu wa Mkoa Ditopile akamatwa kwa mauaji

Na Muhibu Said

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ramadhan Ditopile Mzuzuri, ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za mauaji ya raia kwa kutumia bastola yake jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, zinaeleza kuwa Ditopile anatuhumiwa kumuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), mkazi wa Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam kwa kumpiga risasi kichwani.Ditopile, anatuhumiwa kumuua dereva huyo juzi saa 2.30 usiku, katika njia panda ya barabara ya Kawe na Bagamoyo, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kuchukizwa na hatua ya gari lake kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu.Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.Gari hilo lililigonga gari aina ya Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva wa Ditopile, Nassoro Mohamed (42), mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo, mkoani Pwani.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.

Walisema wakati dereva huyo akiendelea kulikagua gari hilo, Ditopile naye alishuka na kuungana na dereva wake katika ukaguzi huo.Walisema baada ya kuona uharibifu huo, Ditopile, alimfuata marehemu na kumtaka ashuke katika gari alilokuwa akiliendesha ili aende kushuhudia uharibifu uliotokea na kisha waende polisi.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu, alimweleza Ditopile kuwa ajali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya na kumwomba msamaha kwa tukio lililotokea.Walisema mkuu huyo wa mkoa, hakukubaliana na utetezi huo na badala yake aliendelea kumwamuru marehemu ashuke kwenye gari na kumtaka akaeleze maneno hayo polisi.

Mashuhuda hao, walisema marehemu alipoona Ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali, aliamua kufunga kioo cha gari kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo.Walisema kitendo hicho kilimuudhi Ditopile ambaye alichomoa bastola aliyokuwa nayo na kuanza kuitumia kugonga kwenye kioo cha gari la marehemu huku akimsisitiza kushuka katika gari.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu aligoma kutii amri hiyo ya Ditopile na ndipo alipomfyatulia risasi iliyopenya kwenye kioo cha gari na kufumua kichwa cha marehemu.Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika eneo hilo muda mfupi baada ya tukio hilo, alishuhudia mwili wa marehemu ukiwa umeegemea kwenye kiti cha dereva huku damu na ubongo vikiwa vimetapakaa ndani ya gari alilokuwa akiliendesha.Tukio hilo lililozua hofu, lilisababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa watu, wakiwamo madereva na abiria waliokuwa wakisafiri katika njia hiyo, kutokana na mlio wa risasi.

Watu waliokuwa kwenye magari, walishuka na kuanza kukimbia ovyo katika sehemu mbalimbali wakidhani kuwa eneo hilo limevamiwa na majambazi.Watu pekee waliobaki katika eneo hilo, ni dereva anayedaiwa kuwa wa Ditopile na mwanamke ambaye hakuweza kufahamika mara moja ambaye anadaiwa kuwa alikuwa katika gari lililokuwa limembeba Ditopile.Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana.

Dakika chache baadaye, polisi waliobeba silaha wakiwa ndani ya magari matatu aina ya Lond Rover Defender, walifika katika eneo hilo.Akielezea tukio hilo, Kamishna Tibaigana, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku katika eneo hilo na gari lililombeba Ditopile, lilikuwa na abiria wawili; akiwamo Ditopile mwenyewe na mtu mwingine ambaye hajafahamika. Alisema wote walikuwa wakitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo."Mara baada ya ajali hiyo kutokea, magari hayo yalisimama. Dereva Nassoro Mohamed alishuka na kwenda kuangalia gari lake ili kubaini lilivyoharibika/kugongwa, aliliona limepata madhara kidogo upande wa nyuma," alisema Kamishna Tibaigana na kuongeza:

"Wakati Nassoro Mohamed akiendelea kuangalia, alishuka mheshimiwa Kapteni Ukiwaona Ramadhani Ditopile Mzuzuri ili naye aende kuona uharibifu uliotokea. Baada ya kuona uharibifu uliotokea alimtaka dereva wa Isuzu Journey, Hassan Mbonde, ashuke ili naye aone uharibifu uliotokea kisha waende polisi kutoa taarifa."Dereva wa Isuzu Journey alikataa kushuka kwenye gari lake na badala yake alifunga kioo cha dirisha la mlango wake kisha alifunga mlango na ku-lock kwa ndani. Mheshimiwa Ditopile Mzuzuri baada ya kuona dereva amefunga mlango, alisogelea dirishani na kutoa bastola yake na kuanza kugonga dirisha kwa kutumia bastola yake, huku akimwamuru ashuke ndipo ghafla alifyatua risasi moja ambayo ilivunja kioo cha dirisha na kumjeruhi Hassan Mbonde kichwani na alifariki dunia papo hapo," alisema Tibaigana katika maelezo yake kwa waandishi wa habari.

Tibaigana, alisema baada ya tukio hilo, dereva Mohamed, aliendesha gari lake na kuondoka sehemu ya tukio akiwa na abiria wake wawili."Mtuhumiwa Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri amekamatwa na anaendelea kuhojiwa. Pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Kamanda Tibaigana.Asubuhi jana, watu walimiminika katika Kituo cha Polisi Kawe kwa ajili ya kuandikisha maelezo yao juu ya jinsi walivyoshuhudia tukio hilo.Baadhi walisimulia kuwa katika tukio hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alipiga risasi mbili ambapo moja ilimkosa marehemu na nyingine ndiyo ilimuua papo hapo.Daladala aliyokuwa akiendesha marehemu Mbonde ilikuwa imeegeshwa katika kituo hicho cha polisi na baada ya baadhi ya watu kutoa maelezo, walitakiwa kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Nyumbani kwa marehemu kulikuwa na watu wachache huku mvua ikiendelea kunyesha na wengi wao walikuwa wakijadili tukio hilo. Marehemu Mbonde ameacha watoto wadogo watatu."Hii inatakiwa Rais aunde Tume kama ilivyokuwa kwa Zombe, hivi hivi hakutakuwa na haki," alisema muombolezaji mmoja.Watu hao walishikwa na hasira na kutaka kuwavamia waandishi waliokuwa msibani hapo baada ya redio moja kutangaza kuwa marehemu alikufa katika ajali.

Habari zilizopatikana msibani hapo zilieleza kuwa marehemu Mbonde atazikwa leo saa saba mchana katika makaburi ya Kawe.
 
Mkandara,

You are very right, Ditopile ni Mwanajeshi, jambo la usalama wa silaha analijua sana, hivyo alikuwa anajua fika lililokuwa likiendelea. Hapa ni sheria tu ichukue mkondo wake.

Pole sana kwa wafiwa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom