Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,484
- 40,012
Tatizo ambalo tumeliona kwenye historia ya "Tanganyika" tunaliona kwenye hili vile vile. Kuna mambo ambayo hayana utata kwamba yametokea. Yapo kadhaa ambayo hayana ubishi:
1. Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya makubaliano na taasisi za kidini kwa ajili ya huduma za kijamii.
- Mwaka 1991 Julai - Serikali iliingia makubaliano na taasisi ya kidini ya Aga Khan katika kile ambacho kiliitwa "Accord of Cooperation". Mkataba huu uliboreshwa zaidi na Mkapa mwaka 2001 ambapo taasisi ya Aga Khan ilipewa hadhi ya kidiplomasia. Na katika shughuli zake kama zilivyo za Kanisa hailipi kodi. Makubaliano haya ndio yaliifungua Aga Khan kwa namna ya pekee kuweza kuingia nchini na kujishughuliisha na shughuli mbalimbai - za faida na zisizo na faida (na kwa uelewa wangu katika zote hailipi kodi - niko tayari kusahihishwa). Aga Khan ni taasisi ya dini ya Kiislamu inayoongozwa na Imam Aga Khan mkuu wa madhehebu ya Ismailiya. Kwa Tanzania ni Aga Khan ndiye aliyekuwa muasisi wa taasisi ya East African Muslim Welfare Society ambayo imekuwa ikitajwa mara kwa mara. Kwa hiyo. Mkataba wa 1991 uliingiwa chini ya Rais Muislamu mzee Mwinyi na uliboreshwa mwaka August 2001 chini ya Mkapa Rais Mkatoliki. Wote wawili hawakuona tatizo la serikali kuingia ushirikiano na taasisi ya kidini. Ikumbukwe katika maboresho ya 2001 yaliwapa kinga watendaji mbalimbali wa Aga Khan nchini kama mabalozi (though limited immunity).
Mwaka 1992 - serikali hiyo hiyo ikaingia mkataba na makanisa ambao umejadiliwa hapa. Ikumbukwe wakati Serikali ya Mwinyi inaingia mkataba na Makanisa kuhusiana na huduma za kijamii tayari ilikuwa imeshaingia mkataba na Taasisi ya Kiislamu kwa ajili ya suala la huduma za kijamii vile vile. MoU hautoki kinga yoyote ya kidplomasia kwa watendaji wa makanisa kama ilivyo kwa Aga Khan.
Mwaka 2004 - SErikali ya Benjamin Mkapa (Mkatoliki) iliikabidhi rasmi majengo ya serikali ya kule Morogoro kwa taasisi binafsi ya Muslim Development Trust ambayo yamegeuzwa kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu. Majengo ya serikali kupewa bure taasisi moja ya kidini lingeweza kusababisha mgogoro kwenye nchi nyingine lakini katika Tanzania hakukuwa na tatizo kwani ilijulikana chuo hicho kitawafaa Watanzania wote. Wanafunzi wanaosoma shahada ya Ualimu hapo MUM wanalipiwa na serikali na kwa kadiri ninavyojua - nitasahihishwa - kiasi kikubwa cha kuweza kuendesha Chuo hicho Kikuu kinatokana na wao kupokea wanafunzi wa Ualimu ambao wanalipiwa na serikali.
Haya yote yanatuambia nini?