DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 560
Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?
..that was a straight one! alizomewa yeye!
Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?
watan
kosa kubwa tulilofanya watanzania wakati wa ubinafsishaji ni kuwapa wahindi viwanda ..leo wamevigeuza magodown na havizalishi....bora tungewapa wazawa kama kina mugishangwe ,mengi....na wengine...
..je,umejiuliza kama hao wazazi nao wana adabu?
..we mama anapakuwa chakula anaweka mezani. baba kwa ulafi wake anawahi mapande yote mazuri ya nyama,tena karibia zote!. hao watoto kesho wakimwambia "baba acha ulafi" watakuwa na kosa gani?
..btw,muwe mnakumbuka kunawa mnapokula!
..unaongelea malezi? yapi? haya ya kuwafundisha watoto wetu jinsi ya kula rushwa na kujilimbikizia mali nyingi kwa muda mfupi?
..nani analipeleka taifa pabaya? baba/mama au mtoto?
mkapa yes...juu juu.
tangu lini mahakama zikahamia kijiweni!!???..alivyosema warioba leo sawa...kinga ya rais ni political..na kuliko kuendelea kumtuhumu tu wampeleke mahakamani haraka akajibu huko..sio kumzomea..
...na hili la kumdhalilisha ndio kikwete alilokuwa analitaka kama shukrani yake ....baada ya kumsaidia kumwangusha salim...,lakini si haki!!
mkapa anayo mazuri na pia anayo mabaya...kama kikwete anaona haya mabaya yana jinai ampeleke mahakamani haraka au kama hilo haliwezekani na akae kimya!!!!..yeye na watu anaowatumia kumchafua mtangulizi wake..ili tusipate muda wa kumuongelea yeye!!!
Kama bado Mkapa anahudhuria ibada ningeomba kujua ni kanisa gani?
Kuna kila sababu ya kuwashawishi waumini husika wamfukuze kanisani mpaka pale atakaporudisha mali aliyoiba yeye na washirika wake. Vita hii lazima iende mbali. Kile kiti cha enzi anachopewa kanisani lazima anyang'anywe. Kwani iliandikwa, "Nyumba yangu sio pahali pa wezi na wanyanganyi" maana nyumba ya ibada. Leo iweje mnyanganyi na muuwaji mkapa aruhusiwe kuingia kanisani? Ujumbe huu naomba umfikie paroko wa mkapa na mshikaji wake Polycarp Pengo.
Naomba fedha zote alizochangia kanisani arudishiwe kwani ni fedha haramu hazina baraka mbele ya mwezi Mungu.
Mkapa tubu dhambi umrejee muumba wako, wewe tayari ni mzee, unaumwa miguu, siku za kuishi ni miaka sabini , themanini ni bonasi.
Pengo, Pengo, Pengo sikusikii kabisa kuhusu huyu jamaa. Tuambie na lazima ueleze jamii moja kwa moja kwamba unayemsema ni Mkapa.
....well said ...tena over all the places in dar azomewe MASAKI...na pale hakuna kituo cha polisi karibu zaidi ya obay...hao polisi walijuwaje kuwa mkapa akipita atazomewa ili mara moja wakamate watu kijiweni...kama sio hao watu waliozomea ni planned na mwisho wa siku hakuna kesi....propaganda za kijinga kabisa za kikwete na cronies wake..inasikitisha sana,lowassa amezomewa mara ngapi ..mbona naye hawajakamatwa..thats propaganda!!.....mkapa asizomewe mjini au kwenye traffic lights na vijana waliokata tamaa ..azomewe, of all the places in dar, MASAKI..lets be serious jamani!!!
mkapa angemfanyia hivo mwinyi tungefika ..hivi mnayajua yaliyokuwamo kwenye ripoti ya warioba jamani!!!..ingefunuliwa mwinyi asingepona....dereva gani anaangalia nyuma tu...si tutagonga jamani!!!
nchi inaelekea ndiko siko kwa kuteka akili za wenye akili nyepesi!!!
Hata kama Mzee Mkapa ni Mwizi(Hapa mahakama haijaamua) ila jua ya Kwamba bado ni Rasi Mstaafu tu..other thing reamin Constant.
Wewe unadhani kama angepita kiongozi mstaafu wa upinzani watu wakaanza kumzomea,viongozi wa juu wanatembea na mtoto wako huku wakimghasi..Polisi wakikaa kimya unadhani italeta picha nzuri??
Ni rais mstaafu. Ni lazima tumuheshimu. we do not want to set a bad precedent. Kama anatuhumiwa wanaomtuhumu wampeleke mahakamani. Kumzomea haisaidii na ni kuvunja sheria!!
Je ikitokea wananchi wakaenda kanisa analosali halafu kuzomea wakati anaingia na kutoka kanisani, je waumini wakaamua kuanza kumnyooshea vidole mle kanisani watakamatwa?
..mamvi anafahamu vizuri hii kitu!
Maoni yangu ni kuwa sasa ni wakati wa kuanza kuangalia uwezekano wa kuchagua viongozi wapya pamoja na marekebisho makubwa ya kikatiba!
Wapya kabisa ambao hawajawahi kufanya kazi kwenye awamu zilizopita, na wala hawajuani na nobody alieko kwenye rank za uongozi!
Hapo taifa litazaliwa upya! Na maybe nuru mpya kuanza kuonekana!
Hawa viongozi wetu ni kama kabila la tofauti kabisa ndani ya Tanzania( or like aliens) ambalo liko absolutelly out of touch huku likilindwa na dola!
Na wao sio kama sisi hilo tusijidanganye! Wanajuana wenyewe kwa wenyewe na sasa ni wengi mno(from awamu ya kwanza till now) kiasi cha kufikia namba kubwa yenye uwezo wa kujenga tabaka la tofauti la kinyonyaji na kifisadi ndani ya Tanzania!
Ni wengi kiasi cha kwamba hata mafao wanayoendelea kuyapata(mara baada ya kustaafu) yamekuwa mzigo mwingine tena wa kifisadi wenye kuendelea kuwaweka mafisadi kwenye viwango vya juu in definetly in leau of the poor people's tax money and our own resources!
Hawa watu ni tofauti kabisa na hata mazungumzo yao yanaonyesha!
Halafu wasaidizi wao nao ni tabaka moja tu na ndio maana hata (wanapowaandikia hotuba zao) wanazotoa zinaonyesha kuwa wako dunia nyingine kabisa ya tofauti! Mfano wa ile ya Muungwana huko Singida!
Yani mtaani hawajui kabisa kinachoendelea!
Maisha yao yote wako serkalini halafu tunategemea walete mabadiliko!?
Tunaota!
Maoni yangu ni kuwa sasa ni wakati wa kuanza kuangalia uwezekano wa kuchagua viongozi wapya pamoja na marekebisho makubwa ya kikatiba!
RAIA MWEMA FRONT PAGE LEO SOMA, KWENYE MTANDAO WARIOBA ANAKILI VIONGOZI WETU NI DHAIFU,MZEE MUSHI SASA NI WAKATI WA KUKAMPENI JK TERM MOJA YAMTOSHA AKIONGEZA TU HAPENDEZI KWA AFYA YAKE.
Finally leo, Warioba naye anasema Mkapa aende mahakamani, ili mahakama iamue kama anayo hiyo kinga, na kesi zake zianze maana ni nyingi sana, heshima kwa Warioba kwa hili yaaani kusimama at the right political time ili kuhesabiwa!
according to the dataz, mkulu ana ishu nyingi sana za ufisadi, na hasa alizokuwa akizisaini dakika za mwisho wakati anaondoka, wabunge wengi wa kamati mbali mbali za bunge wanaojua ukweli nasikia wameanza kutishiwa kwa message za simu kuwa watauliwa au wataipata,
Naomba kuwaambia wale wanaotuma hizo message, kwamba you do not know what is coming your way, maana mngejua saa hizi mngeanza kutayarisha either kukimbia nchi, au mawakili wa kuwatetea, maana saa mbaya saa imefika ya ukombozi wa wananchi na mali za taifa ni lazima zirudi hata kama nusu maana tunajua mmeshazitumia sana!
Lakini at this stage, Yesuuuu na Maria! mahakamani hakukwepeki!