Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

mkapa yes...juu juu.

tangu lini mahakama zikahamia kijiweni!!???..alivyosema warioba leo sawa...kinga ya rais ni political..na kuliko kuendelea kumtuhumu tu wampeleke mahakamani haraka akajibu huko..sio kumzomea..

...na hili la kumdhalilisha ndio kikwete alilokuwa analitaka kama shukrani yake ....baada ya kumsaidia kumwangusha salim...,lakini si haki!!

mkapa anayo mazuri na pia anayo mabaya...kama kikwete anaona haya mabaya yana jinai ampeleke mahakamani haraka au kama hilo haliwezekani na akae kimya!!!!..yeye na watu anaowatumia kumchafua mtangulizi wake..ili tusipate muda wa kumuongelea yeye!!!
 
Gembe amethibitisha tetesi kuwa JK is behind all of these games against his successor..

...........well said ...tena over all the places in dar azomewe MASAKI...na pale hakuna kituo cha polisi karibu zaidi ya obay...hao polisi walijuwaje kuwa mkapa akipita atazomewa ili mara moja wakamate watu kijiweni...kama sio hao watu waliozomea ni planned na mwisho wa siku hakuna kesi....propaganda za kijinga kabisa za kikwete na crinies wake..inasikitisha sana,lowassa amezomewa mara ngapi ..mbona naye hawajakamatwa..thats propaganda!!.....mkapa asizomewe mjini au kwenye traffic lights na vijana waliokata tamaa ..azomewe over all the places in dar MASAKI..lets be serious jamani!!!

mkapa angemfanyia hivo mwinyi tungefika ..hivi mnayajua yaliyokuwamo kwenye ripoti ya warioba jamani!!!..ingefunuliwa mwinyi asingepona....dereva gani anaangalia nyuma tu...si tutagonga jamani!!!

nchi inaelekea ndiko siko kwa kuteka akili za wenye akili nyepesi!!!!
 
Hawa wanawaonea, si mkuu Pinda alishasema majuzi Iringa vijana wasisite kumwita fisadi mtu yeyote anayetafuna mali ya umma! sasa hii imekaaje ina maana hawa Polisi wanakiuka maagizo ya mkuu Pinda?
Kumbe Mkapa bado anatafuna mali ya Umma..!
 
Hata mkapa mwenyewe angekuwa sio fisadi angejitokeza akaeleza what happened especially swala la kiwira coal mine na TICS, ingekuwa vizuri lakini kwa kuwa hajua atasema nini ndo maana hawezi kujitokeza kueleza chochote.

Lakini haya yote yana mwisho na mwisho wake unakaribia labda haache kutoka ndani, nayo pia hiko siku watu watavunja nyumba yake.
 
Kuzomewa ni suluhisho??Watu wgi waliochangia hoja hii wameone3sha kusifia sana suala la Mzee ben kuzomewa,ila suala la Muhimu na la Msingi ambalo linaweza kuwa mkakati ulio bora kuliko yote kuhusu ufisaid alioufanya Mzee Mkapa ni lipi?

Tujenge Hoja na siyo kusema Mzee alipata hiki na kufanya hivi,Je sheria zinasema Vipi kuhusu kushtakiwa kwa Rais Mstaafu??na kama Haiwezekani nini kifanyike ili jambo Ambalo wengi mnalitaka litimie??

Tusijengwe na mawazo mgando yenye Mwelekeo wa kimapinduzi,na mwiho kabisa sitaki mnichonganishe na Mwenyekiti wa Chama,sikusema Jk na Mipango dhidi ya Mzee Mkapa,ila kuna watu wana Nongwa na Mzee Huyu,hasa wale wenye wivu wa kijinga
 
Tujenge Hoja na siyo kusema Mzee alipata hiki na kufanya hivi,Je sheria zinasema Vipi kuhusu kushtakiwa kwa Rais Mstaafu??na kama Haiwezekani nini kifanyike ili jambo Ambalo wengi mnalitaka litimie??
Gembe, Watanzania wamekata tamaa baada ya kuona sheria hazitoi suluhu katika malalamiko yao dhidi ya aliyofanya Mkapa. Baya zaidi ni mfumo wa kutafsiri na kutekeleza sheria ambao kwa siku nyingi umehoziwa na wenye dola kiasi kwamba hata ulie machozi ya DAMU kama hawataki huwezi kufanya lolote (huwezi kutafsiri tofauti watakavyo au kubadiri)!!

Wakumbuke haya yametokea nchi nyingi, mwisho wake umekuwa kukata tamaa na kuchukua sheria mkononi (kumwaga damu)!!
 
...mkapa angemfanyia hivo mwinyi tungefika ..hivi mnayajua yaliyokuwamo kwenye ripoti ya warioba jamani!!!..ingefunuliwa mwinyi asingepona....dereva gani anaangalia nyuma tu...si tutagonga jamani!!!
Sasa tukiendelea kulindana tutafika?
Kama Mwinyi alikosa then Mkapa
akafumba macho basi alikuwa na lengo baya siku nyingi; alijua atajineemesha kupitia Ikulu na hivyo kwa kulinda mabaya ya Mwinyi kutasaidia ku'win' our sympathy!

Tukinyamaza tujue vicious cycle itaendelea milele maana ndicho atachorudia JK!!
 
Kitila,

Swali gumu sana hili. Nimekuwa napiga vita swala la polisi kutumiwa na viongozi wa serikali (hata wastaafu) kwa mambo ya ajabu kama haya kwa muda sasa hapa.

Ni makosa makubwa, inaonekana walitaka hao vijana wasifie tu na kupiga vigelegele kuwa mkubwa kapita.

Pambaffff kabisa!

KUKIRI UDHAIFU NI USHINDI. NA HUWA UNAKUWA HURU. KUNYAMAZA KUNA LETA UTATA MKUBWA WA MAWAZO KATIKA JAMII INAYOKUZUNGUKA. JK AMEOMBA TUMUACHE MZEE WA WATU APUMZIKE KWA KAZI NZURI ALIYOTUFANYIA WATZ. MIMI NAKUBALI MH JK. ILA TUNAMUOMBA BEN KAMA MTANZANIA MPENDA HESHIMA NA KUHESHIMIWA, AJITOKEZE AJIBU TUHUMA ZILIZO MBELE YAKE. NI MTU WETU TULIEPEWA NA BABA WA TAIFA, TUTAMSIKILIZA ILA SIO LAZIMA TUAMINI ATAKAYO SEMA. KUKAA KIMYA KUNAENDELEA KUMVUNJIA HESHIMA KATIKA JAMII YA WATZ. MWANZO NDIO HIYO YA KUZOMEWA BARABARANI. WHAT NEXT KAMA HAKUNA KAULI KUTOKA KWAKE??? KAMA STATE HAITAKI AJIELEZE KWA WATZ, BASI MSEMAJI WA STATE ASEME KWA NIABA YAKE ILI TUJUE WHAT IS CROPPING UP!!!
 
Mkuu nimekupata kabisa na nakubaliana na wewe
Lakini tatizo linakuja hapa, wananchi wanapofikia kuchuakua maamuzi yao mikononi ujue wamechoka na matatizo
Na sema haya kwa sababu, huyu jamaa kaamua kukaa kimya pamoja na shutuma zote bila kueleza ukweli, na wala serikali haijafanya lolote ili huyu jamaa aeleze ukweli wake kwa wananchi

Pili kwa nchi kama ya Tanzania, usitegemee kama kuna sheria au haki itatendeka kwa Viomgozi hao wa serikali, Pinda alisema mafisadi wanapesa sana hivyo kuwashughulikiwa ni ngumu sana na inaweza kusababisha serikali kuyumba
Kwa maana hii hakuna lolote litakalofanyika kwa huyu Fisadi BEN, so what next ni wananchi kufanya kama wanavyofanya kwa wananchi wengine walio wezi ambao wanapigwa na mawe mpaka kufa

Na ukweli ni kuwa kama kiongozi alifanya madudu wakati wa uongozi wake ni lazima afuatiliwe, hii kasumba ya kusema eti tusiangalie nyuma ni mbovu kabisa na itasabisha wizi zaidi, kwa sababu watajua wakimaliza hakuna wakuwauliza madudu yao

Mimi naona sawa kabisa kwa hayo yaliyotokea na hii ndio iwe kampeni ya kuwazomea na mengine yanayowezekana kufanyika kwa vibaka na wezi wengine yafuate pia, kama serikali inawaogopa na kuwaacha wakikla na kutanua na pesa zetu angali wananchi wanakufa kwa shida kibao, then what

Solution ndio hiyo mpaka serikali itakapoona umuhimu wa kufuata sheria kwa wananchi wote bila kujali, kiongozi, pesa, na mengineyo

Hili ni sawa,Ila tuliwazomea sana Mawaziri kipindi kile wanapita kutetea suala la buzwagi baada ya agizo la Mhe. Lowassa,Ila nini tulipata??nini kiliibadilika.

ikaja Mwaka huu,tukafanikisha Kumng'oa Karamagi,Lowassa ,Msabaha pamoja na kuangauka na wanasiasa wazee na waliofanya maovu katika serikali zilizopita,Mhe. Mramba na wengine.Je ni nini tulipata??

tukapigana kwa dhati na moyo mmoja,Chenge akadondoka,Je nini kimebadilika??

tumekuwa washaniki wa kufungwa magoli ya kisigino,na sasa tunashabikia hili la Mkpa,Je ndiyo itasaidia kuondoa Umasikini?Je ndiyo janja ya Serikali ya awamu ya nne kuwanyamaizsha wanachi??tuko tayari kwa haya mpaka lini??

Maswali sita nimeuliza ila la msingi ni kujipanga na kutumia haki tuliyonayo kuahkiksha tunaweka serikali iliyo makini na siyo serikali ya Unafiki iliyojaa urafiki ulio na Mashaka,na zaidi ya yote kinachoniskitisha ni urafiki wa Waandishi wa habari an wanasiasa,umetoka wapi??

tutafakari.
 
Watanzania tutafika?????hatuna na hatujui uhuru/haki yetu ............hatusomi na hatuwezi kuchambua katiba...tuna safari ndefu sana sana......na la mwisho ni waoga sana sana wa kujadili suala hata kama la haki yetu kwa uwazi..unafiki tuuu ndio umetujaaa...inaniuma sana
 
mkapa angemfanyia hivo mwinyi tungefika ..hivi mnayajua yaliyokuwamo kwenye ripoti ya warioba jamani!!!..ingefunuliwa mwinyi asingepona....dereva gani anaangalia nyuma tu...si tutagonga jamani!!!

nchi inaelekea ndiko siko kwa kuteka akili za wenye akili nyepesi!!!!

Kwahiyo tuyaache na tusiongee kitu??????propaganda zisizo na msingi kabisa hizi
 
Hili nim jizi tuu linapaswa hata kumwagiwa kinyesi maana limenifanya nashindwa kupata milo miwili kwa siku na badala yake napata nusu mlo kwa siku.

Kuna mwenye taarifa kuhusu hao vijana kama wameachiliwa ama bado wanashikiliwa na polisi na wapo kituo gani?

Mbona polisi hawakujitokeza kumkamata Dr slaa alipomwita Mkapa na Kikwete wote mafisadi? huu ni uonevu wa wazi walipaswa kumkamata Slaa na Lissu kwanza ndipo na wengine wafuatie wasiwanyanyase hawa vijana waliowasababisha wao kujikuta wapo kijiweni.
 
mfamaji hakosi kutapa
 
aaaaaaaaaaaa.... mshkaji unaniangusha TAJA JINA LA HOTEL WE DARE TO TALK OPENLY

Hilo jina kwa sasa linatunzwa kwa sababu za kiusalama! Hata hivyo kuna sehemu kibao tu bado Fisadi na mwizi mkapa anaweza kupatikana na akapata muziki mkubwa wa ..I work it out.. hadi ashangae!
 
Nchee Nkapa anakuja kunywa whisky hapa kwenye baa ya jirani yangu chacha ntakwambia ni baa gani ,kwani huwa siku hizi anakunywaga uswahilini , ajue kuwa JF ina mkono mpana sana.
 
KUKIRI UDHAIFU NI USHINDI. NA HUWA UNAKUWA HURU. KUNYAMAZA KUNA LETA UTATA MKUBWA WA MAWAZO KATIKA JAMII INAYOKUZUNGUKA. JK AMEOMBA TUMUACHE MZEE WA WATU APUMZIKE KWA KAZI NZURI ALIYOTUFANYIA WATZ. MIMI NAKUBALI MH JK. ILA TUNAMUOMBA BEN KAMA MTANZANIA MPENDA HESHIMA NA KUHESHIMIWA, AJITOKEZE AJIBU TUHUMA ZILIZO MBELE YAKE. NI MTU WETU TULIEPEWA NA BABA WA TAIFA, TUTAMSIKILIZA ILA SIO LAZIMA TUAMINI ATAKAYO SEMA. KUKAA KIMYA KUNAENDELEA KUMVUNJIA HESHIMA KATIKA JAMII YA WATZ. MWANZO NDIO HIYO YA KUZOMEWA BARABARANI. WHAT NEXT KAMA HAKUNA KAULI KUTOKA KWAKE??? KAMA STATE HAITAKI AJIELEZE KWA WATZ, BASI MSEMAJI WA STATE ASEME KWA NIABA YAKE ILI TUJUE WHAT IS CROPPING UP!!!

Mkapa amepewa nafasi nyingi za kujieleza lakini amekataa. Kuna baadhi ya waandishi wa habari kule Kenya walitaka kuongea naye kuhusu ufisadi wakati akiwa huko (kusulisha) akakwepa huku wasaidizi wake wakisema sio wakati muafaka.

Mpaka wakati huo ukifika, kwa sasa Mkapa ni mayowe tu na kuzomewa mpaka hapo sheria itakapochukua mkondo wake.
 
Nchee Nkapa anakuja kunywa whisky hapa kwenye baa ya jirani yangu chacha ntakwambia ni baa gani ,kwani huwa siku hizi anakunywaga uswahilini , ajue kuwa JF ina mkono mpana sana.

Acha kupotosha watu,Lengo lako ni lipi?huu ndio unafiki na habari za kufikirika.
 
Hili ni sawa,Ila tuliwazomea sana Mawaziri kipindi kile wanapita kutetea suala la buzwagi baada ya agizo la Mhe. Lowassa,Ila nini tulipata??nini kiliibadilika.

ikaja Mwaka huu,tukafanikisha Kumng'oa Karamagi,Lowassa ,Msabaha pamoja na kuangauka na wanasiasa wazee na waliofanya maovu katika serikali zilizopita,Mhe. Mramba na wengine.Je ni nini tulipata??

tukapigana kwa dhati na moyo mmoja,Chenge akadondoka,Je nini kimebadilika??

tumekuwa washaniki wa kufungwa magoli ya kisigino,na sasa tunashabikia hili la Mkpa,Je ndiyo itasaidia kuondoa Umasikini?Je ndiyo janja ya Serikali ya awamu ya nne kuwanyamaizsha wanachi??tuko tayari kwa haya mpaka lini??

Maswali sita nimeuliza ila la msingi ni kujipanga na kutumia haki tuliyonayo kuahkiksha tunaweka serikali iliyo makini na siyo serikali ya Unafiki iliyojaa urafiki ulio na Mashaka,na zaidi ya yote kinachoniskitisha ni urafiki wa Waandishi wa habari an wanasiasa,umetoka wapi??

tutafakari.

Unataka kujua nini kimebadilika? Wezi na majambazi wakubwa kama Manji, Jiitu Patel, Rostam Azizi na wengineo wameongeza ulinzi mara kibao ili kujilinda kwa vile hawajui siku wala saa ambayo watanzania watasimama kwa miguu yao, na kutumia mikono yao kudai kilicho chao - na hapo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno!
 
Back
Top Bottom