Mkapa above the law?: Allegations

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,549
40,204
Imeripotiwa hivi karibuni kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Taifa Bw. Ben Mkapa kwamba yeye hakubaliani na uamuzi wa Mahakama ulioruhusu uwepo wa wagombea huru.

Binafsi sijafurahishwa kuwa hakuna mwandishi aliyeamua kumhoji Mkapa kwa kina inakuwaje yeye na chama chake wamejiweka kuwa ni walinzi wa sheria zetu na katiba yetu badala ya mahakama? Haya mambo ya kudharau mahakama kwa wazi namna hii yatatufikisha pabaya!

Na tuangalie ni yepi mabaya yaliyotendeka chini ya utawala wa Mkapa sasa!
 
You are right on the money on this one!

Ni uamuzi wa wananchi kuamua kama ni sawa kwa rais wao wa zamani, kujenga Mansion Lushoto, kujenga upya ile mansion Sea View, Mansion Mpya kule Msasani, na kununua mansion South Africa kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, alio-retire!

Mungu amrehemu Mwalimu Julius Kambaraga Nyerere, kwani huyu alikuwa ni a TRUE LEADER NA MKOMBOZI WA WANANCHI!

Aluta Contunua, na Stay Tuned................Tunaendelea!
 
Mwanakijiji
You are loosing your direction and mind. Mkapa kama mwenyekiti wa chama cha siasa au kama mtanzania mwingine ana uhuru wa kutoa msimamo wake na mawazo yake au ya chama. Kudharau mahakama ni kutofuata maamuzi ya mahakama. Let us look the other side of the coin, kama mahakama ingekataza mgombea binafsi viongozi wa vyama vinavyounga mkono mgombea binafsi vingekuwa na uhuru wa kutamka kutofurahishwa na maamuzi ya mahakama. Huko siyo kuzalau mahakama.

Mimi binafsi naunga mkono wagombea binafsi kwa sababu siyo haki kwa mtu ambaye hakubaliani na sera za chama chochote kumkataza asigombee nafasi ya uongozi katika jamii. Ingawa tukiangalia ukweli itakuwa ni vigumu sana ka mtu mmoja kuuza sera zake bila kuwa na chama. Mimi sielewi ni kwa nini CCM wanapinga kwani naamini wagombea binafsi ni + kwa CCM. Tutegemee utitiri wa wagombea na mara nyingi kwenye hali kama hiyo ni + kwa CCM. Lakini hiyo siyo sababu ya mimi kuunga mkono ila naamini ni haki kwa kina mtu kuogombea uongozi bila kujali itikadi.
 
Huyu Mkapa alikuwa haambiliki katika utawala wake. Kila kitu yeye aliona ndiye anajua kuliko wote.

Maoni yangu kama CCM itatumia UBABE WAKE KUMKATAA MGOMBEA BINAFI BASI TUNAWAOMBA HAO MIUNGU MTU ANGALU WAANZE KWA KURUHUSU WAGOMEA BINAFSI WA NGAZI ZA CHINI HADI UBUNGE NA SIYO URAIS!

ILA KUMBUKENI HATA KANU ILIKUWA POWERFUL HUKO KENYA LAKINI SASA IKO WAPI?!

CCM FUATENI HAKI NA MASLAHI YA TAIFA. KAMA MNAMKATAA MGOMEA BINAFSI KWA MASLAHI YA TAIFA NI VEMA LAKINI KAMA NI KWA MASLAHI YA WACHACHE IKO SIKU MTAHUKUMIWA! KUMBUKENI HATA MAKABURU CHNI YA DE KLER WALIFIKIA MAHALI WAKAONA NO WAY NI VEMA TUMUFUNGULIE MANDELA NA TUACHANE NA UBAGUZI WA RANGI!

KWA HIYO KUWENI MAKINI VIONGOZI WETU WA CCM! WAPINZANI NAO ACHANENI NA KUPIGA KELELE TU REKEBISHENI MAKOSA YENU KAMA KWELI MNATAKA ANAGALU KUONGEZA IDADI YA WABUNGE BUNGENI! LAKINI NYIE MNALILIA KWENDA IKULU TU ! KUFANYA NINI?
 
Mzee Mkira,

As long as upinzani unaendelea na huu unyonge wanao uonyesha, CCM wataendelea tu kuwavuruga wananchi, kumbuka hata huko SA, na Kenya mabadiliko yalitokana na ushupavu wa upinzani kuanzia ANC, na NARCO sio kwamba walilala tu na kusubiri magazeti ya Mtanzania Daima yaweke agenda chini, HAPANA!

Nakuanza kazi wakakti tu wa uchaguzi wa rais, huku wakifukuzana kugombea ruzuku, na kwenda bungeni kukusanya marupurupu makubwa bila ya kuuliza WHY? hela za kodi ya wananchi zinachezewa bila ya responsibility?

As of the rest, ubarikiwe!
 
Jamani,

BM kazungumza kama mwenyekiti wa chama. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, mawazo yangu yananituma kusema upinzani waungane, sio lazima wawe chama kimoja ila wasimamishe mgombea mmoja kila eneo, waache kushindana wao kwa wao.

Ujinga wao ndio ulinifanya niendelee kubakia CCM. Mimi ni CCM damu, na naamini CCM itabadilika in next 09 years!

Sam, mawazo yako msumari! safi sana hiyo!

Kidumu chama cha Mapinduzi!

Na kitadumu MILELE!
 
sam said:
Mwanakijiji
You are loosing your direction and mind. Mkapa kama mwenyekiti wa chama cha siasa au kama mtanzania mwingine ana uhuru wa kutoa msimamo wake na mawazo yake au ya chama. Kudharau mahakama ni kutofuata maamuzi ya mahakama. Let us look the other side of the coin, kama mahakama ingekataza mgombea binafsi viongozi wa vyama vinavyounga mkono mgombea binafsi vingekuwa na uhuru wa kutamka kutofurahishwa na maamuzi ya mahakama. Huko siyo kuzalau mahakama.
Mimi binafsi naunga mkono wagombea binafsi kwa sababu siyo haki kwa mtu ambaye hakubaliani na sera za chama chochote kumkataza asigombee nafasi ya uongozi katika jamii. Ingawa tukiangalia ukweli itakuwa ni vigumu sana ka mtu mmoja kuuza sera zake bila kuwa na chama. Mimi sielewi ni kwa nini CCM wanapinga kwani naamini wagombea binafsi ni + kwa CCM. Tutegemee utitiri wa wagombea na mara nyingi kwenye hali kama hiyo ni + kwa CCM. Lakini hiyo siyo sababu ya mimi kuunga mkono ila naamini ni haki kwa kina mtu kuogombea uongozi bila kujali itikadi.

Sam kama umenisikiliza vizuri utagundua kuwa tatizo langu, ni hii kawaida ya baadhi ya viongozi wetu (wawe madarakani au la) kufikiri kuwa wao ni sehemu nyingine ya mahakama! Ni jambo moja kutoa maoni yako kuhusu kutofuraishwa na maamuzi fulani lakini ni jambo jingine kuonyesha upinzani dhidi ya mahakama. Sifikiri kuwa Mkapa alikuwa anatoa maoni yake tu, bali pia alikuwa anajaribu kuonyesha kuwa mahakama haijui inachofanya! Hili ni tusi kwa nchi yenye utawala wa sheria.

Madai yake ya kuwa Tanzania bado hatujakomaa kufikia kuwa na wagombea huru ni kebeki iliyojaa dhihaka kwa Watanzania. Hivi ni lini tutakuwa tumekomaa!!? Ni sawa atoe maoni, lakini kama hakufurahishwa na uamuzi wa mahakama si chama kikate rufaa!!!?
 
Mwanakijiji,
Mie nimemwelewa BWM alivyotoa maoni yake ingawa mwingine anaweza kuona kama ni mbabe. Kwanza chukulia hali halisi ya wabongo, elimu, flow of information, na uelewa wa siasa. Chukulia kuwa 90 percent plus ni watu wenye elimu ya chini. Economy is something else. Halafu kwa stage kama hii ya Tanzania bado kuna flagmentation ya udini, ukabila, ambao una-kuwa backed up na ukosaji wa elimu na flow of information. I may classify you as liberal, but lazima tuangalie vile vile upande wa conservatives.
Ingawa ni vizuri kwa mgombea binafsi, risk bado zipo! Raisi anayeshinda ndiyo huchagua mawaziri, theorectically ndiye mwenye madaraka ya kupanga mikakati ya mwelekekeo wa nchi. Madaraka kwa rais ni makubwa mno kwa nchi kama yetu. Tuangalie pande zote mbili. BWM can be right!
 
IO, kama tatizo ni hilo dawa si kukataza wagombea huru bali kuweka mazingira ambapo wagombea huru wanaweza kushirika katika nafasi mbalimbali za uongozi! Na tunaposema wagombea huru sio kwa nafasi ya urais peke yake hata madiwani, wabunge, au viongozi wa mitaa!! Ni wajibu wa serikali kuja na njia au mtindo mzuri ambapo hata wagombea huru wanaweza kujaribu nafasi zao za uongozi!
 
Duniani Kote vyombo vya habari vimekuwa vikitoa mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuikosoa serikali pale inapofanya vibaya?

Vyombo vya habari vinaweza kuchochoa kasi ya kukua kwa maendeleo ya kiuchumi lakini pia inawapo vyombo hivyo vitafanya kazi zake vibaya vinaweza kuzorotesha kasi hiyo.

Sehemu mbalimbali duniani vyombo vya habari vimekuwa vikitoa mchango mkubwa katika kujenga uchumi na kufichua mambo mabaya yanayofanywa na watawala hasa wale wanaozitumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao binafsi.

Nikirudi hapa nchini kuwa muda mrefu baadhi ya wana habari wamekuwa wanafiki wa kushindwa kuisaidia serikali pale inapokwenda kombo wakati uleule na kusubiri mpaka kiongozi muhusika anapotoka madarakani na kuanza kushambulia kwa kumuona kuwa si lolote si chochote.

Mfano nzuri ni kile kinachotokea hivi sasa kwa baadhi ya waandishi wa habari kuiona awamu ya rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa si Lolote si chochote na haikufanya lolote la maana katika utawala wake.

Ikizingatiwa kwamba ni baadhi ya waandishi haohao katika zama hizo walithubutu kuandika makala na habari mbalimbali ambazo ziliutukuza utawala wa awamu hiyo na kuuponda utawala ra rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi.

Hao ndio baadhi ya waandishi wa habari wa Tanzania awanaopenda kusifu pale Serikali inapokuwa madarakani lakini ikidondoka wanasahahu na kuanza kuponda kile kilichofanywa na serikali hiyo.

Huo utakuwa ni unafiki uliopindukia na utakuwa hausaidi chochote kwani yule ambaye anapondwa hayupo tena madarakani hivyo ni kupoteza muda bure bila mantiki yeyote.

Mimi nafikiri ni vema vyombo vya habari vikatambua kwamba hakuna serikali yeyote duniani ambayo imeweza kuleta maendeleo yote bila utegemezi kutoka serikali tangulizi.

Nakumbuka alipokuwa katika ziara yake huko Dubai miezi takribani miwili aliyopita rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipata fursa ya kuzungumuza na Watanzania wanaoshiti katika nchi za falme za kiarabu kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini

Rais aliwaeleza wazi Watanzania hao kwamba serikali yake haiwezi kubeza juhudi zilizofanywa na waliomtangulia katika kuifanya Tanzania ifikie hatua iliyopo hivi sasa.

Nakumbuka rais waliwaambia Wafanyania hao kwamba serikali yake katu haitobeza juhudi zilizofanywa na watangulizi waliomwachia nchi kwani kufanya hivyo ni kujiingiza katika matatizo makubwa ya kiutawala.

Rais akasema unaposhika madaraka ukaiona kuwa wewe ndiye mjuzi na wenzako si lolote si chochote basi ujue unajipalia makaa kwani wenzako nao kuna walilolifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kauli hiyo ya rais Kikweteinakwenda sambamba na hali ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya watu kuona kwamba serikali ya rais mstaafu Mkapa si lolote si chochote na hiyo yamedhihirishwa na baadhi ya wana habari katika makala zao.

Kwanini mabaya hayo yaanze kuchambuliwa hivi sasa wakati ameshaondoka madarakani? Kwa nini baadhi ya waandishi hao wasithubutu kushika kalamu zao na kushauri katika kipindi hicho hicho?

Waandishi wa habari wana uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa kwani wanaelewa matatizo ya wananchi wanaelewa shida za wananchi na wanaelewa kero za wananchi.

Cha msingi hapa ni waandishi wa habari kuwa wa kweli, kuacha uwonga, kuacha kujikomba na kujipendekeza badala yake tukae chini na tuangalie namna gani tutaisaidia serikali katika kupambana na kero mbalimbali za wananchi na kuondoa ufisadi pale tunapoushuhudia.


Na Hamis Dambay - RAI
 
Ninakubaliana na wewe, LAKINI LABDA WALIOGOPA KUFUNGWA AU KUFUNGIWA! JAMAA ALIKUWA ANATISHA AU D...

LAKINI UHURU UKIWEPO BILA VITISHO NINADHANI WAANDISHI WASIPOUTUMIA HUO UHURU. BASI WAMELAANIWA TU!
 
Hii ni speech nzuri.

Ni vizuri kama wanachama wote wa CCM wa eneo husikika watashiriki katika kura za maoni za kuchagua wagombea uongozi.

kuhusu hela je ni kweli watatekelza hili na kuachana na hela za wizi? au majambazi kama. nilivyowahi kuskia huko Moshi jimboni mwa waziri wa sasa. Kuna tajiri mkubwa na jambazi aliyefadhili kampeni zake?

CCM watatumia kipimo gani kujua hizi ni "dirty money" na zile ni "clean money"

Anyway, this is a good move JK keep it up and keep overhauling the Party.

1995 JKN aliwahi kusema "CCM kimekokora hadi KONOKONO NA KWAMBA KAZI KUBWA NA NGUMU NI KUJISAFISHA ILI KUWEZA KUWEKA KONOKONO NJE YA CHAMA".

KAZI KWAKO MR CHAIRMAN TUSAFISHIE CHAMA. PIA MKITEKELEZA VIZURI ILANI YENU HUO NI MTAJI NA HELA ZENU ZA UCHAGUZI UJAO WA 2010. NA SIYO KUANZA KUKUSANYA HELA KUANZIA SASA SASA KAMA UNAVYOSHAURI. HELA ZA KUFANYIA NINI?!!

KAZI KUBWA ULIYO NAYO NI NA MTAJI MKUBWA NI KUENDELEA KUWABANA WAKURUGENZI NA WAZIRI MKUU WAKO WACHAPE KAZI KWA NIA MOJA YA KUFANIKISHA ILANI YENU. BAADA YA HAPO KAITKA UCHAGUZI WA 2010 MTATUMIA 20% YA HELA MLIZOTUMIA KATIKA UCHAGUZI WA 2005.


LAKINI KAMA MNAFANYA BLA BLA BASI MTATUMIA FEDHA MARA NNE YA MLIZOTUMIA KUWANUNUA WAPIGA KURA 2005!!Shun dirty funds, CCM told

CASSIAN MALIMA in Musoma
Sunday News; Sunday,August 13, 2006PRESIDENT Jakaya Kikwete has told the ruling Chama Cha Mapinduzi party (CCM) to distinguish between contributions from upright institutions and individuals and those from criminal elements.

The president, who is also National CCM Chairman, repeated the remarks at various rallies he addressed last week in his tour of Mara Region.

He said that much as the party welcomed contributions and donations from members and supporters, it must differentiate between ‘clean money’ and ‘dirty money’.

Mr Kikwete said for the party to be held in high esteem, its sources of revenue should be untainted.

He warned party leaders to be careful, lest the party’s coffers would be beefed up by ‘dirty money’ given as contributions by drug barons and other crooks.

The president has advised that the only way to avoid doubtful money from bankrolling CCM is for the party leadership at all levels to conceive and implement sustainable economic projects.

He further advised the party and its members to start saving now and mobilise other resources in preparation for the 2010 general elections.

“We should start preparing for the next elections now by pooling our resources together,” Mr Kikwete advised at Kasuguti Village in Bunda District on Friday.

He also underscored the need for the party to review the nomination process for its candidates at general and local elections.

Mr Kikwete concurred with Mara elders who faulted the present nomination process, saying it had loopholes that may lead to nomination and election of weak candidates.

The elders had lamented to him that under the present nomination system, candidates with financial muscle, but with little other qualifications stood a better chance of winning.

‘The newly introduced primaries at different levels proved to be no solution as others seized the opportunity to lock out some potential voters. So, this issue can be discussed and we can reach a collective decision on a better system by 2010,’ Mr Kikwete assured them.

Meanwhile, President Kikwete has agreed in principle to divide Tarime District into two.

He was addressing a public rally at Bukama Village, Rorya Division, in Tarime District, yesterday.

The president was on the last leg of his five-day tour of Mara Region.

During the tour, the president hosted African Development Bank President Dr Donald Kaberuka and former Ghanaian head of state, Mr Jerry Rawlings who visited him at the Musoma State Lodge.
 
Ndugu Mzee Benny Mkapa huko uliko vijana wa RO watakuletea hii habari ama wapambe wako hapa mkekani.Mimi leo nimeamua kukuuliza wewe Mzee wangu baada ya kuona kimya kimekuwa kirefu. Mwaka jana ulipokuwa Geneva ulilia juu ya hospitali zetu kukosa vyandarua .Muda huo huo Nabii ndugu JK rais wetu sasa alikuwa Arusha na mshukaji wake EL wanachangisha mapesa ya kampeni .

Wakati unaomba net kwamba Tanzania ni masikini Arusha JK na EL walichangisha 200M plus . Nikajiuliza sikupata majibu hadi sasa .Sasa Mzee BM yule Mama Sharon alitoa 6mUSD na wengine wakaingia mifukoni na kutoa chochote ,je zile pesa uliipa hospitali gani hapa Tanzania ?Au uliwapa kikundi gani ? Mbona hatujasikia ukizisemea pesa kama inavyo kuwa kawaida ya misaada Mzee wangu BM? Naomba mnisaidie watanzania huenda mna habari na kilicho endelea baada ya juhudi zile pale Geneva .
 
Mzee Shughuli,

Sidhani kama ni 6Mio Usd, soma extracts toka kwenye net mbalimbali hapa chini:

Friday :January 28, 2005
Sharon Stone Raises $1 Mil in 5 Minutes for Africa


Kudos to actress Sharon Stone who stood up at the World Economic Forum in Davos, Switzerland at the World Conference and raised $1 million in 5 minutes for poverty-stricken Africa.

Seizing her chance during a heavyweight debate on how to tackle poverty in Africa, Stone stood up in the middle of the crowded hall to offer an immediate personal pledge of 10,000 dollars -- then challenged others to follow suit. It rather undercut the big-name panelists, who included Britain's finance minister Gordon Brown, Brazilian President Luiz Inacio Lula da Silva and the billionaire Microsoft chairman Bill Gates.

"Could you please stand up, President Mkapa needs help today," she called, referring to Tanzanian leader Benjamin Mkapa who was also on stage, and whose country is among the poorest in the world...."So if you would help children in his country stop dying today, I would appreciate that and I think he would too." The money would be donated to the Global Fund for AIDS, Malaria and Tuberculosis, she added.

Stone also gave $10,000 of her own to the effort. Bill Frist, moderator of the panel, congratulated her efforts at the end, but she had to fight her way there:

U.S. Senate Majority Leader Bill Frist, R-Tenn., was moderating a session on anti-poverty efforts when Stone stood to address a panel that included Microsoft founder Bill Gates and the presidents of Brazil and Tanzania.

"Please identify yourself," said Frist, perhaps one of the few men on the planet who couldn't visually identify the sultry star of such hit movies as "Basic Instinct" and "Casino." "Sharon Stone," she said dryly, proceeding to announce that she was giving $10,000 on the spot to help Tanzanian President Benjamin William Mbaka's anti-malaria efforts.

As Frist tried to steer the conversation back to poverty, Stone talked over him, urging people to stand up and give to Mbaka. (emphasis supplied) "People are dying in his country today," she said. The surprised senator yielded to the spike-haired movie star.

Mbaka, a large, round man, grinned widely as roughly three dozen people stood to be counted and have their pledges written down. After a few minutes, Frist announced that more than $1 million had been pledged.


Source:Sharon Stone Raises $1 Mil in 5 Minutes for Africa - TalkLeft: The Politics Of Crime

Kamchango kangu kadogo kuweka mambo sawa.

Wenu FD
 
Inawezekana hesabu zimekosewa lakini sasa jamani total yake ni ngapi na zilienda api ndiyo maana Mzeeshughuli Bwana akauliza kuna mwenye nyeti ?
 
Fikiraduni,
You are a man of facts. Lakini nilidhani baada ya Geneva mzee wetu angeitisha press conference pale Dar kusema "jamani tumechangiwa kiasi hiki na tutakielekeza kwenye hospitali hizi na hizi. Lakini kimya! Ndo maana watu wanajiuliza, eti
 
Hivi nyinyi hamjipendi? Mnawezaje kumhoji aliyewahi kuwa Rais wa JMT? Je hamjui kuwa yote aliyoyafanya akiwa madarakani hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhoji? Hivi kweli mnategemea angewaambia fedha zimeenda wapi.. achekwe?
 
Angalau kuelezwa kwamba akizipata na akazifanyia nini.Maana Mzee kama kaacha Nchi akiwa mtumishi mwema basi ni vyema hata kila kidogo alicho kipata kwa jina la Tanzania akakisema ama ni vibaya ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom