Mkapa above the law?: Allegations

Kitila,

Swali gumu sana hili. Nimekuwa napiga vita swala la polisi kutumiwa na viongozi wa serikali (hata wastaafu) kwa mambo ya ajabu kama haya kwa muda sasa hapa.

Ni makosa makubwa, inaonekana walitaka hao vijana wasifie tu na kupiga vigelegele kuwa mkubwa kapita.

Pambaffff kabisa!

Unajua kuna mjumbe alisha wahi kusema hivi CHICHIEMU[CCM] isipo tumia dola nn kitatokea??yaani ijiweke kando kabisa na vyombo vya dola.
 
Hata kama Mzee Mkapa ni Mwizi(Hapa mahakama haijaamua) ila jua ya Kwamba bado ni Rasi Mstaafu tu..other thing reamin Constant.

Wewe unadhani kama angepita kiongozi mstaafu wa upinzani watu wakaanza kumzomea,viongozi wa juu wanatembea na mtoto wako huku wakimghasi..Polisi wakikaa kimya unadhani italeta picha nzuri??

Picha nzuri au mbaya inabakia kuwa picha na ni jukumu la mtazamani kuona kama anataka kuendelea kuiangalia au kugeuza shingo. Polisi wana jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao kama wamekuwa na haraka ya kukamata waliosema "Fisadi" kwa sababu ushahidi uko hadharani, kwanini imewachukua milele kukamata waliofanya "ufisadi" wakati ushahidi wanao na rahisi tayari kawaita ni wahalifu?

MKAPA FISADI!
 
Msaada mwingine kwa wanasheria, yapasa kusaidia hao vijana walishitaki Jeshi la vibaraka kwa kuwaweka kizuizini pasi kosa lolote! Wakileta kisingizio cha uzururaji then watuambie wametoa ajira ngapi baada ya kusababisha maisha ya vijijini kuwa magumu?!

TATIZO LA POLICE VIHELEHELE NDO HAO WAMEKURUPUKA TU KUWAKAMATA VIJANA PASIPOJUA KOSA LA HAO VIJANA JE WAKIULIZA WAMEFANYA KOSA GANI WATAISHIA KUSEMA TUNAFANYA UCHUNGUZI AU WAKABAMBIKIZIWA KESI.
TATIZO NI KWAMBA POLICE WETU WENGI NI VIHELEHELE TU YAANI HAPO WAMEFANYA KIHELEHELE KIFRONT FRONT KUWAKAMATA HAO VIJANA PASIPOKUAMBIWA.
 
Hii ni vita ya kisaikolojia dhidi ya Watanzania!
Ndugu zangu msije mkafikiri mafisadi ni wajinga na eti wata surrender!
Hiyo ni NDOTO!
Kuna watu hapa wanauliza kwanini apigwe mawe na kuna wale wanaouliza kwa nini vijana waswekwe ndani ilhali wana uhuru wa kufanya walichofanya? Hawakumdhuru wala kumtusi matusi ya nguoni or anything to endanger him!

Kwanini basi nasema ni suala la kisaikolojia?
Kwanza kabisa kitendo cha Mkapa kutembea mtaani kama vile bado na yeye ni raisi ni ujumbe kwa wananchi kuwa jamaa bado ana ka status ambako inabidi wawe makini la sivyo waswekwa ndani tu kama enzi zile alipokuwa akitoa orders

Tusisahau pia kuwa huyu jamaa amekaa madarakani kwa miaka kumi so ameshajijengea mtandao mzito ndani ya jeshi la polisi pamoja na credentials kutoka kwa jeshi la Wananchi kwani kabla hajaondoka aliwa mwagia mifadhila ambayo nilikuwa nikitia shaka kwani ni wazi inapelekea fikra kuwa ni namna yake ya kuji "postion" mara atakapotoka mdarakani ili kujilinda!

Maoni yangu hapa ni kuwa mahesabu yao ni very wrong kwa sababu History ime prove hivyo!
Kwa hali ilivyo kama hawata resolve hizi issues then kuna hatari ya machafuko!
Vile vile viongozi wetu sasa wamekuwa kama mungu watu na wako out of touch!
Pia wako radhi kututawala kimabavu!
Wameonyesha signs zote za kufanya hivyo! Na pia wameshawahi kufanya hivyo!

Aliyeko madarakani akiogopa kumshughulika aliyetoka madarakani kwa sababu either kuna links ambazo ni uncomfortable ama wanaona kuna hatari ya nchi kuyumba kama wakijaribu kumchukulia hatua mtu ambaye wanataka tuone kuwa bado ana heshima kwenye rank za uongozi wa Tanzania na ambaye pia ana wale wanaotaka awajibishwe ambao nao wako kwenye ranks kama hizo either kwenye taasisi za kijamii na kidini, ndani ya chama,serikali ama wastaafu! Pia wananchi walio wengi ambao nao wanataka kuona uwajibishwaji badala ya ubabe! Ndugu yetu huyu bado anaishi ikulu ya kufikirika na ana nguvu ya kuleta mgawanyo kwani ana mtandao wa nguvu!
Kazi ipo! Naona wananchi ndio tuwe waamuzi wa mwisho ili tuinusuru nchi yetu!
 
Tatizo hivyo vijitu vya usalama na polisi ni kama vijibwa fulani vikipewa amri vinakurupuka tu na kukamata watu sijui ndio shida ya kazi au ujinga waliofundishwa huko wanakofundishwa...Inatakiwa wajue zama za wa-tz kushangilia hata mambo ya kipuuzi zimepita siku nyingi sana nina imani vijana watatoka tu sana watawarusha kichura waseme kama wametumwa au ni wao wenyewe maana mafisadi wengi hawaamini kama wa-tz wameamka...

Ndio malipo ya matendo maovu hayo Mzee Ben.....alijifanya kamanda wa miavuli kudadadeki anatutia mchanga wa macho nadhani leo atagundua angalau kidogo kuwa watu wako serious...
 
Nasikitika kwa yaliyotokea maana ni kinyume kabisa na kauli aliyoitoa RAIS KIKWETE siku chache zilizopita mkoani Singida

namquote "VIONGOZI MSIOGOPE KUITWA MAFISADI...." unaweza kusoma hii thread http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12939

So vijana waachiwe mara moja kwa kuzingatia kauli halali ya RAIS JK.

Kikwete toa agizo mara moja na wape karipio KALI vijana wa Mwema waache kujikomba.
 
Wananchi wameshaamua. Wamechoshwa na ufisadi. Huwezi kumhemshimu kiongozi aliyekuibia. Angalia yaliyompata Moi shambani kwake baada ya Dec 27. Ilibidi akimbilie Ngurdoto.
Hayo hayo yatampata Mkapa na viongozi wa aina yake, hata kama wanasindikizwa na msururu wa magari mangapi.
 
Katiba ifanyiwe marekebisho ili tuhakikishe kuwa wanawatumikia wananchi na wala si maslahi ya watu wachache ama chama tawala!
Then pia tunatakiwa tuangalie upya training za wanausalama wetu kwa sababu vitendo vyao vinatia shaka!
Siwezi kushangaa wakishirikiana na mafisadi kwasababu wameshawahi kushirikiana na majambazi!
Ni lazima tuangalie upya mafunzo wanayoyapata pamoja na msisitizo wa katiba mpya mbayo inaweka bayana majukumu ya wanausalama hao wa namna ya kudeal na issue bila kukiuka haki za kibinadamu!

Siku hizi hata polisi wa kawaida wamegeuka kuwa traffic!
Na wakiwa na bunduki basi tena wanaona kama wana mamlaka juu ya uhai wako!
Badala ya kuwa walinzi wa wananchi..Wamekuwa msiba,kero na ugaidi kwa wananchi!
 
Naomba kuuliza wakuu:

Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?

Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.
 
Wananchi wameshaamua. Wamechoshwa na ufisadi. Huwezi kumhemshimu kiongozi aliyekuibia. Angalia yaliyompata Moi shambani kwake baada ya Dec 27. Ilibidi akimbilie Ngurdoto.
Hayo hayo yatampata Mkapa na viongozi wa aina yake, hata kama wanasindikizwa na msururu wa magari mangapi.

Mkulu Jasusi,

Hii ni point kubwa sana ambayo watu wanaisahau hapa. Kuna wale wanaobeza hapa kuwa hakuna chochote kitakachotokea kwa viongozi maana wataiba na kisha wataendelea na maisha yao wakichoma kuku na kutumbua vijisenti vyao.

Niliongea na rafiki yangu aliyeko bongo siku moja baada ya maelfu ya SMS kusambaa karibu Dar nzima kuwa Chenge amekunywa sumu. Utashangaa kusikia kuwa watu walikuwa wakisherehekea kifo cha Chenge na wengine wakimshukuru mungu (wanayemjua wao) kwa kulipiza kisasi.

Mafisadi wa ccm wanaweza kudhani kuwa sasa hivi wanashinda lakini taratibu chuki kubwa ya watanzania dhidi yao inajengeka na ni suala la muda tu mambo yatawabadilikia kama hawatabadilika.

Mfano wa Moi na yaliyompata baada ya uchaguzi wa kenya mwaka jana ni mfano mkubwa na muhimu sana.
 
Naomba kuuliza wakuu:

Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?

Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.

Well, kijana wa kawaida mlalahoi atakuwaje fisadi? Ni wazi kama ni kweli mazomeo hayo yalilengwa kwa Mkapa....
 
Kwani nani alimwambia kuwa vijana wanamsema yeye?

Inawezekana vijana walikuwa wanashangilia tu?

Kama basi na yeye anajijua kuwa ni FISADI kwa nini asitoke akajitetea?

Sasa naona tunapoelekea itabidi achague sehemu za kupita, la sivyo aende mahakamani au atoke aongee na wananchi watamuelewa.

Suala la kukaa kimya wakati anajua kuwa ni FISADI halitamsaidia.
 
Naomba kuuliza wakuu:

Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?

Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.

Mkuu kumbe ulikuwa umeishawahi kuuliza suala hili.
 
vijana wa kileo wamekuwa hawana adabu.

huo ndio ukweli na tukishindwa kukaza kamba kwenye malezi taifa litaelekea kubaya
 
Aaaahhhh!!! Big Ben huo ndio utamu wa utandawazi bwana....Baba ukifanya utumbo ndani ya nyumba kuna siku watoto wako mwenyewe watakuzomea ndio mambo yalivyo...Polisi si just watch dogs ni lazima kuna kibaraka wa huyo fisadi kawapa amri kukamata then kesho hao hao wanalia lia mishahara haitoshi mara nyumba za full suit (bati kila mahali) zina joto kumbe wanaosababisha hali ngumu wanawalinda wenyewe... Bravo na ni mwanzo mzuri message was sent and delivered correctly!!!Poleni vijana ndio gharama za mapambano hizo na sisi tutamzomea hata humu JF...

Kweli kabisa bana hawa watu lawa hawatakiwi kutetewa tena na vifull suit vyao nadhani waneridhika kukaa humo !@#$!~#%^&**(
 
Nasikitika kwa yaliyotokea maana ni kinyume kabisa na kauli aliyoitoa RAIS KIKWETE siku chache zilizopita mkoani Singida

namquote "VIONGOZI MSIOGOPE KUITWA MAFISADI...." unaweza kusoma hii thread http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12939

So vijana waachiwe mara moja kwa kuzingatia kauli halali ya RAIS JK.

Kikwete toa agizo mara moja na wape karipio KALI vijana wa Mwema waache kujikomba.
safi sana hebu ibold hii....
 
Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?
 
Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?

walikuwa wanamzomea Mkapa kuwa ni fisadi na next time Mkapa atafute magari kama yale waliyotumia makaburu kupambana na weusi kule south afrika kujikinga kwani watanzania watamponda mawe!
 
Nyani Ngabu,

Sikuhizi hapa Mbagala vijana humtania kila anayeendesha gari la thamani kama GX, VX etc kuwa ni FISADI. - ni utani tu.

Je unajuaje hakuwepo mtu wa aina hiyo jirani kapaki?

Wanajuaje kama haikuwa coincedence tu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom