Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Halafu tabia ya kuita mtu fisadi bila ushahidi, ni upungufu wa akili na zaidi ni tamaa tu nyinyi mwategemea mi nikae Ikulu kwa miaka kumi, wakati huu wa biashara huria nitoke bila kitu mna akili nyie, fanyeni kazi acheni wivu anaechagua watu na kuwapa madaraka makubwa ni nani? vyie vipi acheni tule nchi yetu hii kama wewe huna chanel hama nchii! Ebo!

unasound kama mkapa mwenyewe! ebo
 
nani Mwenye Ushahidi Kuwa Mkapa Amekasirishwa Na Hiyo Bag Party Mlioiandaa Huko Masaki? Maana Hakuna Malalamiko Yake Polisi Wala Kampuni Ya Manyasi, Waulizeni Hao Waliondaa Hiyo Bag Party Ikoje Sherehe Yao Na Wao Waende Lupango Wakati Mualikwa Hana Analolijua,HIYO DEAL MKAA IMEWABAMBA WENDAWAZIMU SASA WANAWEWESEKA,mtu timamu hana sifa za kuzomea na ndio maana hata wataalamu wa sheria hawakuona sababu ya kuipa nguvu ya kisheria tabia ya kiendaazimu ya kuzomea?

Acheni Uhuni Wa Butiku ,eti Mnajipaka Upupu Kisha Mpakazie Majirani Kuwa Wamewamiminia ?!!! Hekima Gani Hiyo Wakuu; Kama Mnataka Aseme Nendeni Mahakamani Jamani Tena Uzuri Jk Kateua Majaji Tele Wapya Hawana Rehema Za Benja Ktk Kufikia Hapo
 
jamani nani mwenye taarifa ya maendeleo hawa vijana na kesi hii? nakumbuka kamanda alisema hakuwepa kazini na akifika atakuwa kwny pos ya kujua mhii kesi, je ameshahojiwa tena?
 
nani Mwenye Ushahidi Kuwa Mkapa Amekasirishwa Na Hiyo Bag Party Mlioiandaa Huko Masaki? Maana Hakuna Malalamiko Yake Polisi Wala Kampuni Ya Manyasi, Waulizeni Hao Waliondaa Hiyo Bag Party Ikoje Sherehe Yao Na Wao Waende Lupango Wakati Mualikwa Hana Analolijua,HIYO DEAL MKAA IMEWABAMBA WENDAWAZIMU SASA WANAWEWESEKA,mtu timamu hana sifa za kuzomea na ndio maana hata wataalamu wa sheria hawakuona sababu ya kuipa nguvu ya kisheria tabia ya kiendaazimu ya kuzomea?


Naona sasa umeanza kujiita mtaalamu wa sheria hapa JF

Acheni Uhuni Wa Butiku ,eti Mnajipaka Upupu Kisha Mpakazie Majirani Kuwa Wamewamiminia ?!!! Hekima Gani Hiyo Wakuu; Kama Mnataka Aseme Nendeni Mahakamani Jamani Tena Uzuri Jk Kateua Majaji Tele Wapya Hawana Rehema Za Benja Ktk Kufikia Hapo

Uhuni wa Butiku? ccm mnajipaka vinyesi wenyewe na wala usilaumu wana JF kwa hili. Rudini Butiama kuomba radhi maana kibao kinaanza kugeuka taratibu!
 
Jamani Mkapa huyu chinga kwanza ni mla rushwa hili linathibitika ktk ununuzi wa radar pili ni FISADI pia ni mtu alie liingiza Taifa letu hasara kubwa kwa kuingia ktk mikataba mibovu ya IPTL,SONGAS na mingineyo,tatu kajimilikisha mgodi wa Kiwira mwisho wa siku Taifa limekosa ma trillions ya hela sasa inatakiwa ashikwe na apelekwe eneo la wazi kama pale National Stadium halafu apigwe risasi hadi kufa ili iwe funzo kwa marais wengine watakao kuja
 
Raha kweli hapa wakuu, maana mpaka gembe anapopendekeza gaidi bila kujali kuwa sharia ya ugaidi ipo tayari maungoni mwetu TZ ni hatari sana. Kumekucha Tz
 
Kwi kwi kwi kwi,

Mkulu Gembe, hayo ya kumwaga tindikali inabidi ufanye peke yako!
ila hiyo ya kuzomea mbona rahisi, midomo mali yetu, tumechoka kupelekeshwa, watazomewa tu!
 
Hii ni vita ya kisaikolojia dhidi ya Watanzania!
Ndugu zangu msije mkafikiri mafisadi ni wajinga na eti wata surrender!
Hiyo ni NDOTO!
Kuna watu hapa wanauliza kwanini apigwe mawe na kuna wale wanaouliza kwa nini vijana waswekwe ndani ilhali wana uhuru wa kufanya walichofanya? Hawakumdhuru wala kumtusi matusi ya nguoni or anything to endanger him!

Kwanini basi nasema ni suala la kisaikolojia?
Kwanza kabisa kitendo cha Mkapa kutembea mtaani kama vile bado na yeye ni raisi ni ujumbe kwa wananchi kuwa jamaa bado ana ka status ambako inabidi wawe makini la sivyo waswekwa ndani tu kama enzi zile alipokuwa akitoa orders

Tusisahau pia kuwa huyu jamaa amekaa madarakani kwa miaka kumi so ameshajijengea mtandao mzito ndani ya jeshi la polisi pamoja na credentials kutoka kwa jeshi la Wananchi kwani kabla hajaondoka aliwa mwagia mifadhila ambayo nilikuwa nikitia shaka kwani ni wazi inapelekea fikra kuwa ni namna yake ya kuji "postion" mara atakapotoka mdarakani ili kujilinda!

Maoni yangu hapa ni kuwa mahesabu yao ni very wrong kwa sababu History ime prove hivyo!
Kwa hali ilivyo kama hawata resolve hizi issues then kuna hatari ya machafuko!
Vile vile viongozi wetu sasa wamekuwa kama mungu watu na wako out of touch!
Pia wako radhi kututawala kimabavu!
Wameonyesha signs zote za kufanya hivyo! Na pia wameshawahi kufanya hivyo!

Aliyeko madarakani akiogopa kumshughulika aliyetoka madarakani kwa sababu either kuna links ambazo ni uncomfortable ama wanaona kuna hatari ya nchi kuyumba kama wakijaribu kumchukulia hatua mtu ambaye wanataka tuone kuwa bado ana heshima kwenye rank za uongozi wa Tanzania na ambaye pia ana wale wanaotaka awajibishwe ambao nao wako kwenye ranks kama hizo either kwenye taasisi za kijamii na kidini, ndani ya chama,serikali ama wastaafu! Pia wananchi walio wengi ambao nao wanataka kuona uwajibishwaji badala ya ubabe! Ndugu yetu huyu bado anaishi ikulu ya kufikirika na ana nguvu ya kuleta mgawanyo kwani ana mtandao wa nguvu!
Kazi ipo! Naona wananchi ndio tuwe waamuzi wa mwisho ili tuinusuru nchi yetu!
Kama ujumbe wangu ulivyotabiri hapo juu before ndio yanayoendelea hapa!
Ok then JF we'll try!
 
Nasikitika kwa yaliyotokea maana ni kinyume kabisa na kauli aliyoitoa RAIS KIKWETE siku chache zilizopita mkoani Singida

namquote "VIONGOZI MSIOGOPE KUITWA MAFISADI...." unaweza kusoma hii thread http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12939

So vijana waachiwe mara moja kwa kuzingatia kauli halali ya RAIS JK.

Kikwete toa agizo mara moja na wape karipio KALI vijana wa Mwema waache kujikomba.

Pia msisahau hiyo link hapo juu ambapo Mh Rais aliwataka wasiogope wala kujali kuitwa mafisadi na ni wazi kuwa wameshajipanga upya kutudhibiti!
Nawaonea huruma wale wanaoimiliki hii Jambo Forums kwa sababu lazima na wao wako kwenye severe hard times!
Either kwa vitisho..Ama kwa kupenyeza rupia!
Na kama JF ikimshinda shetani kwa niaba ya Watanzania then kuna mwanga!
 
Ni rais mstaafu. Ni lazima tumuheshimu. we do not want to set a bad precedent. Kama anatuhumiwa wanaomtuhumu wampeleke mahakamani. Kumzomea haisaidii na ni kuvunja sheria!!
 
Hii kesi nzuri sana, na haiwezi kufika kokote.

Kwa sababu hawa vijana wakipelekwa mahakamani tu hapo hapo ndipo mitandao yote ya Civil Society inayojali maendeleo ya Tanzania inapotakiwa kuwatetea, na kumuita Mkapa mahakamani ajibu shutuma za vijana.

I would love Slaa on their defence and Mkapa on the stand.

Mkapa anaweza kuwaambia wawaachie tu kwa kuua soo mambo yasije yakawa mabaya zaidi in a popular uprising.

Hawa vijana hawafungiki, wakiwafunga watawafanya kuwa martyrs na popularity ya Mkapa itaanguka chini zaidi, ataonekana siyo tu fisadi bali ni fisadi mkandamizaji.

Hawa polisi nao wanajishaua tu huenda hawakutumwa wala nini, njaa zao tu na kujifanya vijibwa vya wakubwa, hawana principle wala nini.

Speaking of incidents za maskani na polisi,I will never forget kitambo niko maskani waiting for my results siku polisi walipokuja kwenye kijiwe chetu Upanga kutaka kutu harass, wakaanza zao.


Polisi- "Nyinyi mnafanya nini hapa"

Sie "tumepumzika nyumbani"

Polisi "Wewe unakaa wapi?"

Kijana1 "Hapo nyuma"

Polisi "Na wewe?" (arrogantly)

Kijana2 "Hapo Nyuma"

Wakamfikia mtoto wa kishua mwenyewe sasa

Polisi "Na wewe?"

Mtoto wa kishua "Mimi nakaa kwa Ben"

Polisi "Kwa Ben, Ben gani huyo"

Mtoto wa kishua "Ben huyo huyo wa Jamhuri ya muungano, kwani kuna Ben wangapi tena"
Polisi (attitude imebadilika katika U Turn ya 180 degrees "Haa hapana wazee, siyo hivyo unajua ni katika kujuana tu, eenh ni katika kujuana tuu"
Jamaa kuanzia siku hiyo maskani hawakuigusa, hamna sheria hamna morals hamna principles, ni uonevu na upendeleo tu.
Pundit hii kali but true!
 
Si watu walitaka mkapa aende mahakamani?

Naona sasa anaweza kujipeleka mwenyewe. Vijana wakitaka kuprove kuwa ni FISADI data ziko za kumwaga tu.
Vijana wamemchokoza Ben ama Ben ndio kawachokoza Vijana?
Je vijana watajibu mapigo?
 
Hata kama Mzee Mkapa ni Mwizi(Hapa mahakama haijaamua) ila jua ya Kwamba bado ni Rasi Mstaafu tu..other thing reamin Constant.

Kuwakamata hao vijana, wamefanya kitu kinaitwa "escalation", wamepandisha none-issue kuwa ishu na ndo maana tunaijadili hapa, na imeenea kote na bila kujua washambatiza Mkapa jina hilo sasa ni rasmi kabisa BMF (Benjamin Mkapa Fisadi). kama wasingewakamata hao vijana, hatungekuwa tunazungumzia hilo wala hakuna mtu angejua zaidi ya hao vijana na majirani wachache. does not say much about the "intelligence of the intelligence".

Kwa level ya hadhi ya Mkapa, na kwa jinsi tuhuma dhidi yake zilivyo, hawezi kutarajia anymore kuoshwa na mahakama. itaonekana kama "a bad joke". Ishu ni ya kisiasa zaidi, kwamba hearts and minds za watanzania haziko naye tena. No game changer there. kwa kukurupuka walivyofanya, polisi "hawajamtendea haki Mkapa" (ingawa wametutendea haki sisi) kwa maana kwamba keshahukumiwa kisiasa na kwenye public, na binafsi naamini asingependa iwe hivyo.

Kuhusu ukimya wake pia amepoteza mchezo. alitakiwa kui-handle ishu ya ufisadi kisiasa kwa kuicheck mapema. Na ndio maana hata hizo efforts zake za kusuluhisha Kenya hazijampa credit yoyote, wala hakuna anayekumbuka hayo. The only game in town ni UFISADI wake tu. lakini pengine hakuwa na kete yoyote ya kucheza isipokuwa "wait and see". si unajua kuzidiwa tena...

Wewe unadhani kama angepita kiongozi mstaafu wa upinzani watu wakaanza kumzomea,viongozi wa juu wanatembea na mtoto wako huku wakimghasi..Polisi wakikaa kimya unadhani italeta picha nzuri??

Polisi wetu basically don't care about "picha nzuri". polisi wa TZ wanafanya kazi kwa "kuonekana wanafanya kazi", kufurahisha wanasiasa na wasije onekana hayo yametokea na wao wakiwa hapo karibu. Did you actually say "KIONGOZI MSTAAFU WA UPINZANI?" acha utani! kiongozi wa upinzani anapokea mkong'oto wa nguvu kutoka kwa polisi, leo atetewe tu hivihivi? mbona akizomewa ni good news kwa waheshimiwa, proof kwamba upinzani hauna dira! On the other hand, huenda polisi wamewakamata hao vijana kama namna ya uwekezaji, kwamba baadae itabidi wanavijiwe wenzao wawachangie jero jero ili waachiliwe. Not a very bad bargain ukizingatia hali ngumu ya bongo.
 
Ni rais mstaafu. Ni lazima tumuheshimu. we do not want to set a bad precedent. Kama anatuhumiwa wanaomtuhumu wampeleke mahakamani. Kumzomea haisaidii na ni kuvunja sheria!!

Chausiku,

Hivi nani anatakiwa kumpeleka Mkapa mahakamani? Kikwete amesema kuwa mzee aachwe apumuzike kula vijisenti vyake vya wizi. Kwa hiyo wananchi wa kawaida wamebakiwa na nini then!

Kufanya life ya mzee kuwa hell ili asipumuzike. Kuzomea sio kuvunja sheria na so far ndiyo silaha pekee watanzania wenye uchungu na nchi yao wamebakiwa nayo.
 
hao mapolisi wakamkamate basi na Mbunge Aloyce Kimaro

Yeah hapo umenena kwa nn yule hawajamweka ndani wkt ndo aliyechambua mambo yote pale mjengo mbona hakamatwi??wanawaonea hawa vijana.Kweli mnyonge mnyongeni Lakini ipo siku....
 
Ni rais mstaafu. Ni lazima tumuheshimu. we do not want to set a bad precedent. Kama anatuhumiwa wanaomtuhumu wampeleke mahakamani. Kumzomea haisaidii na ni kuvunja sheria!!

yeye mbona kutuheshimu na kuacha maisha ya kina mama wajawazito na watoto kuendelea kupotea kila siku mahospitalini

yeye mbona kutuheshimu maisha ya watoto kataka mashule ya serikali kuwa na huduma mbovu na viwango vidogo vya elimu ikiwa pamaja na shida ya usafi wanazo pata watoto wetu

yeye mbona kutuheshimubarabara zute zimeendelea kuharibika kila siku mazao yanaharibika mashambani na maisha ya wakulima yanazidi kudidimia

yeye mbona kutuheshimu, swala la umeme linazidi kuwa gumu na wananchi tunakaa giza hata mara naada ya kupata uhuru takriban nusu karne iliopita

zaidi ya yote hatuheshimu watanzania kwa kuamua kukaa kimya wakati tunamtaka aje mbele yetu na kujibu maswali na kizungu zungu hiki
 
Tuandamane,
Unaonesha TAbia ya Ubinafsi na tabia ya kuonekana wewe ndio unaweza kusema bila kupingwa na mtu yeyote,siku zote Jf tumekuwa mstari wa mbele kueleza mabaya ya serikali na kusifia machache mazuri.

Naweza kuwa upande wa Mafisadi,ila mafisadi sio ambo wewe unawawafahamu kwa ufahamu wako,manaa ufisadi una maaana nyingi.

Naomba nisisitize na kutilia mkazo jambo moja la Muhimu,siyo kwamba napenda Mabaya aliyoafanya Mkapa,ila nachosisitiza hapa ni nini kifanyike ili aweze kushitakiwa.siyo kuzungumza tu,tunajua fika kwamba maneno bila vitendo ni swa na kazi bure.

tufikirie nini cha kufanya,tupo hapa kw ajili ya watanzania wenzetu,tukianza kulalamika ooh afanywe hivi katika thread hii haitaisaidia sabau thread itaneda itaisha na habari mpya itakuja kuendelea.

Cha msingi tufanye nini,na hatua zipoi zifuatwe,sipendi kuanzisha jambo na likaishiakulaumu tu bila kuchukua hatua madhubuti.

Mwafrika wa kike,Tupo pamoja kwa point yako ya hapo juu.ila naomba uungane na mimi kutafuta tiba ya udgalimu alioufanya Mzee Mkapa,jambo nalopingana nalo ni la kumzomea,ambalo ni sawa na mtu mwenye mawazo mengi ya masiha,anakwenda kunywa pombe ili aondoe Mawazo na pombe inapokwisha anarudi katika khali yake ya kawaida.

Tuandamane,nitaendelea kuquote unachokiandika sababu siko hapa kwa ajili yako na wala sijalipwa na mtu yeyote.

Kwenye highlight inaonyesha huyu ni mwenzao!
Kweli kujificha usoni pa ukweli ni vigumu!
Haya karibu jf na tuendelee!
Wananchi vs fisadis!
 
yeye mbona kutuheshimu na kuacha maisha ya kina mama wajawazito na watoto kuendelea kupotea kila siku mahospitalini

yeye mbona kutuheshimu maisha ya watoto kataka mashule ya serikali kuwa na huduma mbovu na viwango vidogo vya elimu ikiwa pamaja na shida ya usafi wanazo pata watoto wetu

yeye mbona kutuheshimubarabara zute zimeendelea kuharibika kila siku mazao yanaharibika mashambani na maisha ya wakulima yanazidi kudidimia

yeye mbona kutuheshimu, swala la umeme linazidi kuwa gumu na wananchi tunakaa giza hata mara naada ya kupata uhuru takriban nusu karne iliopita

zaidi ya yote hatuheshimu watanzania kwa kuamua kukaa kimya wakati tunamtaka aje mbele yetu na kujibu maswali na kizungu zungu hiki

Kama mahakama na polisi wamekaa kimya huku Kikwete AKA Vasco Da Gama akizunguka dunia unategemea wananchi wafanye nini?
 
Back
Top Bottom