Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Phil,

Haiwezekani JK akapanga azomewe kisha washikwe.

Kumbuka kama upo Dar Ben anasafishiwa barabara za mjini hasimami kwenye traffic lights zozote. Check source zako vizuri kama Ben anasimama kwenye trafic lights. Halafu gari ni tinted hata kama anasimama watamuonaje?
 
Polisi mnatakiwa kuwa makini sana na kazi zenu. Mie sioni sababu ya kuwakamata hao vijana kwa sababu wemetumia demokrasia yao kuwakilisha kile ambacho wanaona ni sahihi. Yeye Mkapa hajawahi kukanusha kama anahusika kwa njia moja au nyingine kwa ufisadi. Mbona hamjaenda kuwakamata wahariri wa magazeti mbalimbali ambao wamekuwa wakimtaja Mkapa kama fisadi? Fanyeni kazi zenu kwa kufuata sheria na si kukurupuka. Nyie Polisi muulizeni kama Mkapa ni fisadi au la.
Angalieni msije mkaongeza chuki zaidi kwa wananchi mnapomtetea huyo fisadi.
 
Phil,

Haiwezekani JK akapanga azomewe kisha washikwe.

Kumbuka kama upo Dar Ben anasafishiwa barabara za mjini hasimami kwenye traffic lights zozote. Check source zako vizuri kama Ben anasimama kwenye trafic lights. Halafu gari ni tinted hata kama anasimama watamuonaje?

..INGIENI KWENYE MTANDAO ANGALIENI MAGAZETI Ya LEO....TIBAIGANA AMEKANUSHA VIKALI MKAPA KUZOMEWA..AMESEMA HUO NI UZUSHI
...sina la kuongeza,...kama kuna maswali yeye ahojiwe na waandishi!!!

kuhusu msafara wa mkapa ..ni nadra sana kumuona..mara nyingi huyu mzee siku hizi unaweza kumuona akipita ameongozana na zile RANGE ROVER zake mbili...yeye anakua mbele ...nyuma wanakuwa walinzi wake..kimya ..kimya...,sanasana utajua kuwa polisi wa barabarani wanayo taarifa kwa kuwa kila anapopita traffic light magari ya upande wake yanaruhusiwa...kama anavyofanyiwa IGP Au CDF..pamoja na kuwa anatakiwa kuwa na sweepers kila mahala...mara nyingi hutumia sweepers anapoenda kwenye officeal function...
 
Five arrested for anti-Mkapa slur

-As ex-president maintains reticent silence

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

POLICE in Dar es Salaam have arrested five young men for allegedly hurling insults and verbal abuse at former president Benjamin Mkapa.

The youth were reportedly nabbed on Monday this week in the city's Masaki suburb, while in the act of chanting anti-Mkapa slogans and hurling insults at the ex-president's passing motorcade.

Witnesses confirmed that the youngsters, who were sitting at a street corner, allegedly called the former leader ''Fisadi!...Fisadi...Fisadi!'' (Thief x 3) as the small motorcade passed them by.

It was not immediately known if the youth were arrested by police officers per se, or members of the former president's official security detail from the Tanzania Intelligence and Security Service (TISS).

Witnesses did confirm that the arrested suspects were whisked off to Oysterbay Police Station, detained and subjected to intense questioning for several hours, before finally being granted bail.

Contacted for comment, Kinondoni Regional Police Commander Jamal Rwambow denied reports that the young men were arrested specifically for hurling insults at the former president.

He said police have routinely been cracking down on jobless youths engaged in drug abuse and anti-social behaviour in various parts of the city.

The RPC said police have made several arrests of young men in the Masaki area in particular, allegedly caught in the act of smoking cannabis.

''I don't recall the arrest of anybody for insulting any public leader,'' Rwambow asserted.

Still, well-placed sources confirmed to THISDAY that in the statement of offence written at the police station, the men were accused of jeering the former president and hurling insults at his passing motorcade.

The arrested suspects were identified as Ayubu Masoud, Kagungi Shukuru, Hassan Ramadhani, Juma Rashid and Peter Steven - all residents of Masaki and Msasani areas in Kinondoni District.

Their case file was officially registered as OB/RB/8201/2008 at Oysterbay Police Station.

They were reportedly arrested at a street corner near the Masaki bus stand, within a neighbourhood dotted with the official residences of a number of cabinet ministers and other senior public officials.

It could not be immediately established yesterday if prosecution proceedings would be prepared against the youth for the alleged anti-Mkapa slurs.

The ex-president has recently dominated local newspaper headlines over allegations of corruption and abuse of public office during his 10-year term as head of state (1995-2005).

The allegations include doing business for his own private financial gain while at State House, and his dubious involvement in the 2005 privatization of the Kiwira Coal Mine.

Mkapa himself has so far declined to make any formal public comments on the widespread allegations against him.

However, the issue was recently raised in the National Assembly by members of parliament from both the ruling CCM and opposition camp, prompting Prime Minister Mizengo Pinda to announce an official government inquiry.
 
1
. ....TIBAIGANA AMEKANUSHA VIKALI MKAPA KUZOMEWA..AMESEMA HUO NI UZUSHI...sina la kuongeza,...kama kuna maswali yeye ahojiwe na waandishi!!!

2.
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

POLICE in Dar es Salaam have arrested five young men for allegedly hurling insults and verbal abuse at former president Benjamin Mkapa.

Tibaigana naye amepitwa na wakati hivi huko polisi hakuna vijana walioenda shule?

Tick!.....tick!.....tack!.....tack!.....tick!...taaaaaaaack!
 
Ningekuwa mshauri wake wa karibu huyu mzee wa Lupaso ningemwambia "Mzee katika hali kama hii si ujitwange shaba tu,mbona unakuwa mvivu wa kufikiri??....."
 
Kuzomewa Mkapa ni haki yake! Remember that, "The voice of people is the voice of God". Sio kuzomewa tu, hata akipita mtaani atachomwa moto. Kama anabisha, aongozane na Ali Hassan Mwinyi katika matembezi huru mtaa wowote TZ aone justice atakayopewa na "watu wenye hasira kali" wakati Mwinyi akiheshimika na kuchanganyika na watu bila wasiwasi.
 
ajue hawezi kuliziba jua kwa ungo

kwi kwi kwi kwi.... wewe mtu wa pwani....

Na hii umeitoa wapi? Naomba niitumie hii kwenye signature yangu kule kwenye forums zingine za kiafrika ninazotembelea.

Hii kali kabisa..

Huwezi kuliziba jua kwa ungo!... najaribu kutafsiri hii ili niiandike kwa kingereza.

Mkjj na wengine tafadhali nisaidieni kutafsiri hapa..

Huwezi kuziba jua kwa ungo .......
 
kwi kwi kwi kwi.... wewe mtu wa pwani....

Na hii umeitoa wapi? Naomba niitumie hii kwenye signature yangu kule kwenye forums zingine za kiafrika ninazotembelea.

Hii kali kabisa..

Huwezi kuliziba jua kwa ungo!... najaribu kutafsiri hii ili niiandike kwa kingereza.

Mkjj na wengine tafadhali nisaidieni kutafsiri hapa..

Huwezi kuziba jua kwa ungo .......
" there is noway you can eclipse the sun,with the help of a shield"
 
Kuzomewa Mkapa ni haki yake! Remember that, "The voice of people is the voice of God". Sio kuzomewa tu, hata akipita mtaani atachomwa moto. Kama anabisha, aongozane na Ali Hassan Mwinyi katika matembezi huru mtaa wowote TZ aone justice atakayopewa na "watu wenye hasira kali" wakati Mwinyi akiheshimika na kuchanganyika na watu bila wasiwasi.

spot on, jr.hiyo ni sawa na kuchumia kivulini"ufisidi"na kulia juani."ufisadi"heshma yoteeee...nje ya dirisha.😡
 
Nchi yetu ya ajabu sana. Unaweza kukuta hata hao polisi hawajui hao watuhumiwa wamevunja sheria gani! Hivi kuna sheria inayomlinda raisi kutozomewa na wananchi wake au kuitwa fisadi? I really hope our judges and magistrates are creative enough!

Wadanganyika kazi tunayo!
 
Their case file was officially registered as OB/RB/8201/2008 at Oysterbay Police Station.

Mkuu Lissu naamini vita sasa inakolea, mawakili wa kujitolea na wataalamu wa Katiba ya Tanzania mnaombwa kuwasaidieni hawa vijana ambao tayari wemeshabandikiwa kesi nyingine (UVUTAJI DAWA). Serikali hii inajitahidi kunyamazisha watu, vijana nikiwemo na mimi tunaamini MKAPA ni FISADI. Na kama si FISADI basi aje before Tanzania people akanushe. Kwa nini Mtaalamu wa habari anashindwa kuja kuongea na wanahabari wenzake kuhusu UFISADI??

Haya ni mambo ya KIJINGA polisi mnaacha ku-deal na watu kama Rostam, J. Patel, Mkono na fisadiz wengine mnakwenda ku-deal na watu ambao wanatetea haki yao. Vita ilishatangazwa toka kitambo kati ya FISADIZ and TANZANIANS. Tundu Lissu na wengineo ambao si wataalamu wa sheria, tuwape support hawa vijana ili wasinyamazishwe na serikali ya MAFISADI. Naamini JF tukianzisha mfuko maalimu for that case tutakuwa tumefikisha ujumbe kwa MAFISADI kuwa DAIMA HATUTANYAMAZA.

Mkuu INVISIBLE tafadhali tuwasiliane kama kutakuwa na mfuko wowote wa kuwasaidia hawa vijana kama wataamua kuwapeleka MAHAKAMANI
.
 
http://www.thisday.co.tz/News/3956.html

EYE SPY : His Excellency the ’fisadi’



Adam Lusekelo
DAR ES SALAAM

POLICE in Dar es Salaam have goofed again. They have arrested the wrong guys. They have arrested five young men for yelling unflattering things about former president, Ben Mkapa.

The thing is, you can�t tart up a thing reeking with stench, you just cannot do that. It will always stink. Our country is presently having a nasty rotting smell and there is nothing the entire Tanzania Police Force can do about it.

But I would pity the cops. The thing is the poor cops are confused. The guys were trained to save the rest of�us civilians from crooks and the bad guys, thieves and other nasties in society.

But it now turns out that the crooks are guys who were pretending to be our leaders. Now leaders (I call them rulers) should lead by example so that people can emulate their rectitude and goodness.

In Bongo it turns out that the rulers have also been found out to be thieves. They have been engaging in the shocking robbery of the Treasury and the central bank.

The police also know that they are also part of the people of Tanzania who have been robbed dizzy. They also get pay which is peanuts and have to be ’creative’ to make ends meet.

So they do not know what to do when the whole country knows and calls the crooks ’mafisadi’. There is not other name for thieves a thief is a thief! Period!

The thing is no one can force me to respect a robber. I was raised and told by my mum and dad to avoid bad company. To avoid crooks. How can you steal billions in a country where children sit on floors in classes?

How can you steal billions in a country where children die of malnutrition? How can you steal an entire coal mine and simply say it belongs to you? Just like that!

No. We will continue to call them ’mafisadi’. I am sure the police cannot arrest 35-plus million Tanzanians. The people will one day fight back. In fact they already have started fighting back by using their mouths and insulting the thieves, like what those young men did.

Instead of arresting the real thieves the police have resorted to childish bullying. The people will continue to resist the wanton rape of our resources.

The country is confused. Who is a real thief? The ruling CCM party is also mega-confused. Are the people who have bought their way into and bankrolled the party, their comrades with integrity or crooks engaged in unarmed robbery?

Youth CCM members in Tanga think a crook is just a crook. Those of Bariadi think that what their colleagues in Tanga say is just a load of rubbish.

To some of us a thug is just a thug. He belongs to a maximum security jail.

mailto: mbwene2@yahoo.com
 
Haya ndo matokeo ya kuiba na kujilimbikizia mali ya umma.

Bado viongozi hawajajua watanzania wa leo ni wanajua wameibiwa haki zao


Timing tu mwafrika wa kike unajua hii misafara ni ya kustukiza na sasa wameshajua kuwa moto umewaka wanapita kwa speed ya 120! hata ukirusha jiwe kazi bure!

Ila nadhani wangetega misumari wapate pancha kwa speed ya 120 lazma matokeo yawe mazuri🙂
 
Waliomzomea Mkapa wamekosea nini?
Salehe Mohamed



KATIKATI ya wiki hii kulikuwapo taarifa za kukamatwa kwa vijana wa Wilaya ya Kinondoni, hasa eneo la Kawe, kwa madai ya kumzomea Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwa kumuita fisadi.

Vijana hao waliona njia sahihi ya kufikisha ujumbe wao kwa Rais mstaafu huyo ni kwa kumzomea na kumwita fisadi, kwa sababu wasingeweza kupata nafasi ya kwenda Seaview kuzungumza naye.

Wangeweza vipi kuipata nafasi hiyo wakati hata vyombo vya habari ambavyo vina ukaribu na mwanasiasa huyo kila kukicha vimekuwa vikitafuta nafasi hiyo bila mafanikio, hivyo kuendelea kuandika matendo ya kifisadi aliyoyafanya kiongozi mstaafu huyo bila upande wa pili kujibu mapigo hayo.

Hivi sasa ni rahisi zaidi kupanga miadi ya Rais Jakaya Kikwete, na kuzungumza naye kuliko kuweka miadi hiyo na Mkapa, ambaye moja kati ya taaluma alizonazo ni uandishi wa habari, ambao unaeleza wazi kuwa mtu maarufu siku zote ni habari.

Habari yoyote iliyojificha ndiyo wananchi wana kiu nayo zaidi kuliko zile za kupikwa au kuandaliwa kwa lengo la kujisafisha au kuficha ukweli fulani ama kwa makusudi au bahati mbaya.

Vijana waliomzomea Mkapa walikuwa sahihi kwani hawaoni kama serikali yao ina juhudi za dhati za kumuwajibisha kiongozi huyo na wenzake waliotumia madaraka yao vibaya kwa kujineemesha.

Mkapa, aitwe nani kwa kuingia mikataba mibovu ya madini, kubariki uuzwaji wa nyumba za serikali, kuongeza mkataba wa TICTS kinyume na taratibu, kutowawajibisha watendaji wake walioelekea kulega lega katika kazi.

Tanesco kila siku hutoa sh milioni 146 kuilipa Kampuni ya Tanpower Resources Limited ambayo inaaminika kuwa inamilikiwa na Mkapa na Daniel Yona, ambao waliingia mkataba wa kinyonyaji wenye lengo la kujinufaisha zaidi.

Watanzania ambao wanaishi vijijini na hawapati huduma ya umeme kutokana na Tanesco kutokuwa na uwezo huo kwa sababu ya kulipa madeni mengi kwa kampuni zilizoingia mikataba mibovu wanamwonaje na watamwitaje Mkapa?


Si yeye na Mramba ndio walioidhinisha ununuaji wa rada ya kijeshi mwaka 2002, ambayo Tanzania ililanguliwa mara mbili ya bei halisi, yote hiyo ikiwa na lengo la kuchukua teni pasenti yao.
Bila shaka vijana wale hawakukosea kumwita Mkapa fisadi, si tunaona hata Marekani, Rais George Bush, anaitwa gaidi kutokana na sera ya kuzivamia nchi nyingine kwa kisingizio cha kupingana na ugaidi.

Mbona polisi hawakumkamata Dk. Slaa, Mrema, Mbowe, Mbatia, Kimaro na wengineo wengi wenye nafasi zao katika siasa ya nchi hii walioweka wazi na kutaja majina ya viongozi akiwemo Rais Kikwete wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Je, wanasiasa waliotaja listi ya viongozi mafisadi wapo juu ya sheria na hawaguswi, isipokuwa wale vijana wasio na mbele wala nyuma ndio wapo chini ya sheria na wanagusika kirahisi?


Kama utaratibu huu wa kuanza kuwakamata watu kwa kuwaita majina fulani wenzao umeidhinishwa, basi ni vema ukaanzia kwa viongozi wenyewe, kwani wao ndio vinara wa kuyakuza majina hayo.
Kwa mtindo huu kila mtu atakamatwa, maana hakuna hata mtu mmoja asiyetamka neno ufisadi katika nchi hii kwa hivi sasa.

Ingawa taarifa za kukamatwa kwa vijana hao kwa kutenda kosa hilo zimekanushwa na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, aliyebainisha kwamba, si kweli kuwa waliwakamata vijana hao kwa kosa hilo, bali inawezekana walifanya kosa jingine.

Alisema ni kawaida jeshi lake hufanya operesheni mbalimbali katika wilaya hiyo kwa lengo la kupunguza vitendo vya kihalifu, hivyo kuna uwezekano vijana hao walikutwa na makosa mengine na watu wakaamua kuyakuza mambo kwa kudai wamekamatwa kwa kosa la kumwita Mkapa fisadi.

Pamoja na majibu hayo, lakini bado kuna taarifa kuwa baada ya kuona jamii itakuja juu endapo itabainika wamekamatwa kwa kosa hilo, Polisi wameamua kubadilisha kibao kuwa waliokamatwa walikutwa na bangi.

Kama taarifa hizo ni za kweli, Polisi wamekosea na dhamira zao zitakuja kuwasuta au kuwashitaki siku za usoni, kwa kufanya uonevu kwa watu walio sahihi kuwaita majina wanayostahili watu fulani.

Mkapa analazimika kuitwa hivyo, kwani hakuna kumbukumbu zinazoonyesha alishawahi kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma zinazomkabili ili jamii ijue mbivu na mbichi, bali amekuwa kimya kwa kile kinachotafsiriwa kuwa watu wanaopiga kelele hawamkoseshi usingizi.

Ni kweli hizi ni kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji, lakini kwa muungwana ni lazima angalau angepaza sauti yake juu ya kile kinachosemwa juu yake.

Kulindana na kuoneana aibu kwa watendaji wa serikali hasa wanaofanya vibaya, ndiko kunakowasababisha wananchi kuanza kuwaita viongozi wetu majina ya aibu na ya kudhalilisha.

Serikali isipobadilika kuna kila dalili wananchi siku za usoni wakachukua hatua kali zaidi ya hizo na hata ikiwezekana kuwapiga mawe viongozi wa aina hiyo.

Waswahili walishaweka bayana kuwa usipoziba ufa utajenga kuta.

Salehe_mohamedi@yahoo.com

TANZANIA DAIMA
 
"POLICE in Dar es Salaam have goofed again. They have arrested the wrong guys"
quote of the week!
 
Back
Top Bottom