Nyerere, alimjua Mkapa tena nje ndani, tena kwa karibu sana,
kwa sababu alikuwa akimjua Lowassa kwa karibu sana, ingawa hakuwa mtoto wake wala ndugu yake, wala kiongozi aliyefanya naye kazi kwa karibu, mpaka akamkatalia urais, sasa iweje kuwa hakumjua Mkapa aliyekuwa waziri wake wa nje?
Watanzania inabidi tukubali ukweli, kwamba tumekuwa wajinga for too long, ndio maana tunakazania kuitangaza JF kwa nguvu zote tulizonazo, ni kwa sababu tunajaribu kuamshana kutoka kwenye usingizi mzito sana tulionao, Mkapa alikuwa Elimu na Sayansi, nani aliyekuwa hajui kilichokuwa kikiendelea huko betweeen Mkapa na Mahalu? Eti mnasema Mwalimu, alikuwa hamjui Mkapa? Wakuu tunaambiwa kuwa kipindi cha Mwinyi, hata Usalama walikuwa wamechoka na kuamua kumpa Mwalimu, info zote za serikali na ndio maana wakampa hata za Lowassa, na za Ikulu kuwa pango la kufanyia biashara haramu, sasa mnataka kutuambia kuwa kwenye hizo info hazikuwepo za Mkapa?
Mwalimu, alimpigia makelele Mwinyi, kuwa ni mwizi, lakini hakutuomba msamaha wananchi kwa kutuchagulia kiongozi mbovu, the next thing akarudia tena mchezo wake na kutuchagulia Mkapa again mambo yakawa yale yale, lakini akanyamaza kimyaa, sasa leo maa-pologists mnasema hakumjua Mkapa? Eti Mwalimu hakujua kuwa CCM ilishindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 kule visiwani?, sasa kama alijua hilo how could you put past him kuwa hakumjua Mkapa? Mbona hakusema kitu kwenye ishu ya Zanzibar kama kweli alikuwa ni malaika kama wengi hapa mnavyotaka tuamini? hivi wakuu kweli tunaelewa maana ya siasa na mwanasiasa au tunabahatisha tu?
Wewe kweli ni rais wa nchi, watoto wako wote wanasoma bongo, waziri wako wa nje watoto wake wanasoma US toka wakiwa watoto wadogo, tena in the middle ya siasa ya ujamaa, wakati wananchi wanakula njano na foleni ya kipande cha sabuni mbuni, halafu unasema kuwa humjui waziri wako wa nje? Vijana hebu muache haya masiala, wewe kweli unaamini kuwa Mkapa aliandika mali zake zote? wananchi wa bongo tulikuwa tumelala sana usingizi, matokeo yake tukaruhusu aliyeamka Mwalimu na alioamka nao kina Mkapa, kutuchezea na bado tunaendelea kuchezewa, ndio kwanza tunajaribu kuamka, lakini bado kazi ni nzito saana ya kuamshana, ndio maana ni lazima tuitangaze JF kwa nguvu zote, maana huwezi ingia hapa ukaendelea kulala!
Mwalimu, alale pema peponi, lakini alikuwa akimjua tena vizuri sana Mkapa, kuliko hata sisi wananchi, lakini tunasahau kuwa Mwalimu, alikuwa ni mwanasiasa, alikuwa pia akiangalia legacy yake ambayo ilishamiri sana under Mkapa, Nyerere Foundation imewika under urais wa Mkapa, na sio Mwinyi, hebu nyie Nyerere apologists tuambieni zile shillingi millioni 300 ambazo Mkapa alikuwwa akitoa kwa hiyo foundation alikuwa akizitoa wapi? au under what budget? Mwinyi, na kundi lake walikataa kata kata kumpa Mwalimu hizo hela, na kuna wakati Mwalimu, alikuwa bado ana demand kusafiri kwenye ndege ya rais na Mwinyi alikuwa akikataa, lakini yote haya aliyafanya under Mkapa, kwa hiyo si kweli kabisaa kuwa kwa kumchagua Mkapa, Mwalimu alikuwa hajui anachofanya no way wakuu!
Tunasema kuwa Mwalimu, hakuwa mfisadi, lakini hakuwa na tatizo na mafisadi waliokuwa wakimsujudia, Mkapa included, kusema Mwalimu, hakumjua Mkapa ni very naive thinking kama sio kujua what makes siasa na wanasiasa, to be politicians, siasa sio dini wakuu au charity, siasa ni utawala na power ndani yake, na pia tukumbuke kuwa power siku zote huwa ina-corrupt hata wachungaji kina Mtikila!