Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

balaa hizo maana sumaye analipwa Ml 100 mwenzangu ohoo ... shauri yenu mtakuwa mashahidi mimi simo
 
Hii itakuwa janja ya mkapa ili wabunge wasiunde tume ya kumchunguza kwa sababu 'kesi itakuwa mahakamani'!!! Mafisadi safari hii watatafuta kila njia!!
 
Kitila Mkumbo,

Sam Nujoma Rd inaendelea kwa mwendo wa kusuasua mno,leo wakati natoka zangu Mbezi kuja mjini foleni ikaanzia Africana mpaka Mwenge kwenyewe,mtu unatoka nyumbani 05:50 a.m unafika Posta/Mjini 8:00 a.m!Kufika Mwenge nawakuta wachina na vibarua wao wana majembe na makoleo (as opposed to bulldozers,asphalt pavers and the like) wakijikongoja kujaza udongo na lami...damn it!!

Miundo Mbinu kwa kweli wa ovyo sana!!!

Hiyo barabara kwa kweli ni maumivu sana. Hiyo foleni ya leo asubuhi kidogo inisababishie ugonjwa wa moyo. Mimi niliwakuta vibarua wanabeba lami kwenye mkokoteni wa chuma, nilumhurumia yule kibarua kwa sababu hakuwa na gloves na mkokoteni wote inaelekea ulikuwa umepata moto kutokana na lami hiyo na alikuwa anapata taabu sana, matokeo yake lami ikawa inamwagika hovyo wka sababu mkokoteni ulikuwa unaangukaanguka kila mara jamaa alipokuwa anaungua mikoni! hawa nwachina watatuua
 
Rais (mstaafu) wa Tanzania Benjamin William Mkapa yuko katika mchakato wa mwisho kuyashtaki magazeti ambayo yamekuwa yakimwandama kwamba ni fisadi.

Habari kutoka ndani ya familia yake zinaeleza kuwa taratibu za kuyashitaki magazeti hayo zimekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kutolewa kwa taarifa za awali kwamba yeye na mkewe, mjasiriamali Anna Mkapa hawana hisa katika mgodi wa Kiwira.

Zaidi ya hapo inaelezwa kuwa magazeti yatakayoshikiwa bango ni Kulikoni, Thisday, Mwanahalisi, Mwananchi, Tanzania Daima, Majira na Mtanzania.

Mtoa habari huyo aliyeona makabrasha ya mashtaka hayo ameeleza kuwa kila gazeti litadaiwa bilioni mbili; akieleza kuwa anadai kiasi hicho kwa kuwa angalau kinalinganalingana na hadhi yake ndani na nje ya nchi.

Hivi majuzi kampuni ambayo ilinunua mgodi wa Kiwira wa kuzalisha makaa ya mawe iliibuka na kueleza kuwa Mkapa na mkewe hawana hisa eti kwamba walijitoa muda mfupi baada ya kugundua kuwa ilikuwa ikijiandaa kununua mgodi huo kwa bei ya kutupwa ya sh. milioni 700 (zililipwa 70 kwanza za kukopa kutoka Benki) wakati mgodi wenyewe ukiwa na gharama kubwa ya bilioni 4.

Mawakili sita wamejipanga kwa kazi hiyo, huku mmoja akiwa kutoka Afrika Kusini ambaye anaeleza kuwa mzoefu katika kesi zinazohusu kashfa kwenye vyombo vya habari.
MZEE KAANZA KUISHIWA UVUMILIVU SASA NDIYO SAFI AENDE MAHAKAMANI
 
Mimi nafikiri amechukua uamuzi wa busara sana. Madamu serikali yetu kwa niaba yetu imeshindwa kumshtaki acha yeye aende hukohuko ili ukweli ujulikane- kama sisi tukipigwa bao asafishike kiana, yeye akipigwa bao basi tumepona. Hii tabia ya kushtaki watu kwenye internet na kwenye vijiwe binafsi imeshanichosha. Tuna vyombo tumevitumie.

Nafikiri hizi kesi zikianze zitatusaidia ku-concentrate na yale wanayoyafanya akina JK. Nakubaliana na wale wanaosema kuwa tujifunze kuwaadabisha na kuwajibisha viongozi wetu wangali madarakani itatusaidia zaidi. Sasa hivi tunawapa easy ride akina JK; tunasubiri atoke tusikie amenunua Bagamoyo nzima ndipo tuanze.

BTW, kwa wale waliopo Dar, hivi barabara ya Sam Nujoma KM 5 iliyoanza kujengwa Januari 2006 imefikia wapi?


Hapo umesema Kitila maana tumeanza kushughulikia na mambo ya siku nyingi na kushindwa kuconcentrate na mambo yanayoendelea. Maisha yamekuwa magumu chakula kimepanda bei, mafuta yanapanda bei kila siku. Mkapa aende au apelekwe mahakamani ili ashughulikiwe huko na sisi tudeal na akina JK. Kwa mtazamo wangu tunastahili kumwangalia JK kama anafaa kuendelea 2010. Vyombo vya sheria na utawala vitusaidie kudeal na Mkapa na sisi tudeal na JK kisiasa
 
Nadhani walikuwa wana-update mafaili pale BRELA ili kumfutia umiliki wake kwa muda hadi hapo baadaye. Alipoona yametimia ndipo akaenda Lupaso na wao wakaambiwa tangazeni kukanusha taarifa hii kwamba "Mr Clean" ni saaaafi.
 
Hivi kweli BWM anadhani anaweza kuwanyamazisha watanzania millioni 40? kwa kutumia mahakama? mimi ninaamini ana kesi ya kujibu. Asidhani magazeti hayana mawakili pia. Kwa taarifa naomba wanasheria wa Tanzania muwe tayari kuyasaidia magazeti kama yana evidence. Hapa ni kila mtanzania kujitolea kufa na kuzikwa kupambana na mafisadi kutokea kila angle. Ni lazima tujue hata wao wamejipanga kunyamazisha jamii isiwapigie kelele. Hili halitawezekana. Hivi anaweza kuinyazisha na na JF? anaweza pia kuipeleka mahakamani? Na akifanya hivyo sisi na akina mkjj. invisible, painkiller tutasimama kueleza ukweli? je tunao ushahidi wakutosha?
 
Mkutano huo uliandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Leo Limited, inayochapisha gazeti la Tanzania Leo, Bw. Venance Rwegoshora, kukanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo, toleo la Machi 31 hadi Aprili 6, mwaka juzi, kuwa Bw. Sumaye, anamiliki akaunti iliyopo nje ya nchi, ikiwa na Sh. Trilioni 10.

Bw. Rwegoshora, alisema baada ya mchakato wa hoja kati ya kampuni hiyo na Bw. Sumaye kushindikana kupitia usuluhishi wa Baraza la habari, suala hilo lilifikishwa mahakamani, ilipobainika kuwa habari hizo zilikuwa za uongo, zilitungwa, zikapotosha na kutokuwa na msingi wowote.

Kutokana na hali hiyo, Mahakama Kuu iliamuru kufanyika kikao cha usuluhishi kati ya pande mbili hizo, na kukubaliwa masuala kadhaa, ikiwemo Tanzania Leo kumlipa Bw. Sumaye fidia ya Sh milioni 100, zitakazolipwa kuanzia kipindi cha kabla ya Desemba Mosi mwaka huu hadi juni mwaka ujao.

..naona waandishi wameamua kuficha aibu yao ambayo ni hiyo hapo juu.
 
pipo ol i can see twachezewa akili atiii as one of the members over here kamention huko nyuma,dat dis gov is very clever we ol focus on ibuaring makosa ya awamu iliyopita na madhambi yao ikiwemo madeal machafu yooote but look at how the things have gone,we are becoming very stupid maana laibuka hili moja,halijaisha wala patiwa ufumbuzi laibuka lingine n we forget the old one na kuanza hangaika na ongea bin pigia kelel hilo jipya,kesho likija lingine nalo twaacha la leo na kuanza ongelea hilo lingine by de tym twafika 2015...tutakua tumegusia gusia yoote na wengi wa watuhumiwa watakauwa wamekufa tayariii

we are not talkin abt scandal ya bot na majengo yake anymore...ile ilifukiwa zamaniiii,ikaja kuondoka kwa balali,tukapiga kelele wee,ikaja issue za karamagi na lowasa tukaacha balali na bot tukaja kwa el,after dat yakaja mengineyoooo now hata now we were pigiarin kelele mazingaombwe ya balali kupotea tumeongea weee now yamekuja ya sumaye na mkapa we don talk anymore abt hayo tumehamia ku discuss pensheni za watu na madili waliyoingia!we don even talk abt kesi ya chenge can u imagine??wat will b de next thing kutunyamazisha abt mkapa??u neva know....

ol i can see we deal with talkin abt the past wakati hata awamu ya sasa ina madudu kibaaaaoooo ila now tumekaa kimyaaa ka twanyolewa waitin tuje discuss miaka kumi na ushee bidae huko kuwa unaona na kikwete nae alifanya hivi!!

guys it high time tuanze ku tok abt wat shud be done ryt now tupate maisha bora kwa kila mtanzania as tulivyo ahidiwa na kuacha ongea abt the past cz it aint take us anywhere....
ni mawazo yangu tu hayo!
 
look mfano hai ni huu wa mjamzito kufia wodini kwa kukosa huduma yeye na kichanga,we might end up kusema siku yake ilifika lakini its too much and ingekua nchi zingine watu kibao walitakiwa wawajibishwe ikiwemo waziri husika which is the current issue lakini sie tumekali kuongea oohhh flani alifanya vile awamu ya tatu,ooh flani alifanya vile baada ya nyerere kufa....mambo kama haya ya sasa tutaja ya pigia kelele mwaka 2017 hukoo ohh mwakyusa hafai kuwa waziri mkuu kwa sababu mwaka 2008 alifanya.......akatakiwa kuwajibishwa!!
 
Mkapa anasubiri moto unafunga kila njia ndipo anaanza kukimbia? Amekwisha lazima aungue tu.
 
Kazi ipo mwaka huu msiuane tuu jamani...maana kila kitu kitakuwa wazi..........na ukwelii utajulikana....
 
..hivi wanaharakati, na wanasheria woote tulionao, hakuna mwenye ubavu wa kumpeleka mahakamani?

..where is Rev.Mtikila on this one? nakumbuka huyu alikuwa haishi kumnyanyasa Sumaye, tena akiwa madarakani. kwanini hamburuzi Mkapa mahakamani??

..mimi nadhani hili suala sasa liende mahakamani. kama mahakama italitupilia mbali on technicalities kama immunity, basi wanaharakati wanaweza kwenda bungeni kuomba hiyo immunity iondolewe.

..Suluhisho la sakata hii haliwezi kupatikana mitaani/ukumbi wa maelezo kwa Mkapa kujibizana na waandishi wa habari.
 
Nasema hivi Mlango wameufungua wenyewe sasa hivi kazi inakuja!... Na huyoTaharo ata hara kweli kweli maanake tunataka kwanza uthibitisho wa kila alichokisema, Nina hakika hana labda ziwe zimeghushiwa..
 
Nasema hivi Mlango wameufungua wenyewe sasa hivi kazi inakuja!... Na huyoTaharo ata hara kweli kweli maanake tunataka kwanza uthibitisho wa kila alichokisema, Nina hakika hana labda ziwe zimeghushiwa..

Mkandara.. hawa jamaa bado wanaishi zama za "Bosi kasema" halafu watu wanatakiwa wakae kimya. Usishangae Daily News ikija na kutuambia tumeshajibiwa na wenye mgodi hivyo tuache kuendelea kuuliza maswali.
 
Kuna mtu ananena anasema Sumaye kacheza deal ili kusafishwa na gazeti lile ni mali yake mwenyewe anajiandika , na kujishitaji na sasa anajisafisha baada ya kuona hilo Mkapa naye kaanza .Ni game hii wananchi .Mnakumbuka huko nyuma nilikuja na madai ya CCM kuanza kwa gharama yeyote kujisafisha watu wakasema Lunyungu ni mzushi ? Sasa mnayaona wenyewe hakuna cha magazeti kushitakiwa hapa ni kwamba wahariri wanalambishwa na kufanya deal .Rostam alijaribu akakwaa kisiki sijui ile kesi yake imeishia wapi.
 
Kuna mtu ananena anasema Sumaye kacheza deal ili kusafishwa na gazeti lile ni mali yake mwenyewe anajiandika , na kujishitaji na sasa anajisafisha baada ya kuona hilo Mkapa naye kaanza .Ni game hii wananchi .Mnakumbuka huko nyuma nilikuja na madai ya CCM kuanza kwa gharama yeyote kujisafisha watu wakasema Lunyungu ni mzushi ? Sasa mnayaona wenyewe hakuna cha magazeti kushitakiwa hapa ni kwamba wahariri wanalambishwa na kufanya deal .Rostam alijaribu akakwaa kisiki sijui ile kesi yake imeishia wapi.

nilidhani umepotea!! ukisikia mkapa tu basi huyoo unapop out !
 
Back
Top Bottom