Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Francis Tabaro anailaumu serikali ya JK kwa kutosaidia kuisafisha kashfa ya BWM lakini nahisi kama anachokoza moto,hebu tusikie serikali itatoa jibu gani kuhusu hili maana lawama zimeelekezwa kwake! Ni nani katika serikali anatakiwa kulitolea ufafanuzi hili la Tabaro kutaka KCM isafishwe ili iweze ku-access mikopo kwenye mabenki?
 
---Tanpower Resources ilisajiliwa 29/12/2004 na kupewa namba 51080 ikiwa na dhumuni kuu la kwanza kuchimba mkaa wa mawe nakuzalisha umeme, wakati huo Mkapa bado ana hisa na alijua sababu za kuanzishwa kwake. Wakati inasajiliwa wanahisa walikua ANBEM hisa 200,000 na aliyesaini ni Anna Mkapa, Devconsult ya Yona na Mwanae (hisa 200,000), Universal Tech (hisa 200,000), Choice Industries ya Mbuna (200,000) na Fosnik Enterprises ya Nicholus Mkapa na mkewe Foster wakiwa wameiga jina la kampuni ya baba na mama zao ya ANBEM (wao wakiwa na hisa 200,000) na aliyesaini ni Nico

-----Lakini jambo la hatari ni kwamba, kabla hata ya TANPOWER kusajiliwa ilikwishaanza kufanya kazi na Evans Mapundi akiwa Mkurugenzi wake, alifanya mawasiliano Desemba 15 na wakatembelea Kiwira Desemba 18 na 20, kwa baraka za Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona. Yona akiwa pia mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo.

----Mkapa na Mkewe kupitia ANBEM walijitoa TANPOWER Februari 21, 2005 ikiwa tayari hata mkataba wa ubia kati ya TANPOWER na Kiwira umekwishaandaliwa na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.... Hata baada ya Kujitoa, Mwanae Nico na mkewe Foster na baba mkwe wao Mbuna walikua ndani ya Kiwira.

----Ni mwaka huo ambao Yona na bosi wake waliitosa STAMICO na kuchukua eneo jingine lenye hazina kubwa ya mkaa wa mawe liitwalo Kabulo rig ambalo serikali ilikopeshwa USD milioni 50 kufanya utafiti. STAMICO hadi sasa wanalilia eneo hilo ambalo limechukuliwa na TANPOWER/Kiwira bureeeeeeeeeeeee

-----
 
Halisi.. ndio hapo tunapotaka aende huko mahakamani... kesi hii itanoga kweli...nilisema watakapojaribu kutuzuga angalau wafanye jitihada za kutuzuga tukazugika~!
 
Alikuwa anasubiri magazeti mengi yamuandike ili apate mabilioon zaidi. Si umesikia kuwa atadai 2 billion kwa kila gazeti!!!!!!

Mahesabu yeke: kwa Magazeti 10 (10 x 2,000,000,000 = 20,000, 000,000 Tshs)

Sasa nimeamini kuwa kweli mzee anaishi kwa pensheni
 
Huyo Mkwe wake alipata wapi shiling 700 milioni za kununua KCM? Kazi gani aliyoifanya kumuwezesha kukusanya pesa zote hizo na kwa mduia gani?
 
Enyi watu kuweni na subira ktk maneno yenu! ya nini kukurupuka na maneno ,kama sisi tunamshitaki kwa sheria na yeye anashitaki kwa sheria hizo hizo hayo magazeti .Sasa yeye akiamua kwenda mahakamani sehemu muafaka ni busara zaidi kuliko wanaopiga kelele,na wengine tunao hapa wanadai tutasema mpaka kieleweke,damn take the necessary measure kama una envidence nenda mahakamani organize kama tuchangie mawakili ok,vielelezo si unavyo.Usibaki kuunganisha mambo ambayo mengine hayaonekani logic zake kama kiwira-balali-mkapa ,unaongea from undirected thinking.
Kumbuka kimya kingi kinamshindo mkuu and here we play by the rules not assumption or something na mjumbe mwingine katupa dokezo la tofauti ya sheria na haki.CAREFUL!
Tusikubali watu watuendeshe kwa personal conflit zao ,mtu akija na hoja za mafisadi tusieshie kusema tu ,let us go front line after gathering necessary inf. tusieshie kuwaita mafisadi tu haitusaidii kama mtu hana vielelezo tusimkublie mpaka vipatikane ingawa vinaweza patikana baade but some one cn't be convicted guilty unless otherwise proven.
 
Hii michezo ya maigizo ya "Tollywood" inafurahisha sana. Yaani "sterling" hakubali kuuwawa kabisa. Yaani kama picha flani la kimarekani vile. "Sterling" anapiga mkono kuanzia mwanzo mpaka mwisho bila kupigwa ngumi hata moja. Eti yeye akipiga risasi zinawaua wenzake, lakini za wenzake mia hazimpati. Very interesting.

Yaani napoangalia michezo michafu ya wanasiasa wetu mafisadi, naona kama naangalia "movie" la kimarekani. Ni lini hawa "masterling" watakubali kuuwawa? Ni lini watakubali risasi mia za maadui ziwapate? Huu usanii mpaka lini? Hii nguvu ya kutokusemwa wanaipata wapi?
 
Naota ndoto za alinacha?????

tukumbushane story ya alinacha. Alinacha alikuwa mtu mwenye ndoto nyingi za kuwa tajiri. siku moja akabuni mradi wa kuuza vyombo vya udongo, yaani vyungu, sahanim na vikombe. akawa amevipanga sokoni kusubiri wanunuzi katika mistari kadhaa. huku akajipa matumaini, nikuza mstari wa kwanza pale nitapata pesa nitajenga nyumba, ehee nanikuza mstari wa pili pale nitapata pesa nitanunua gari, naam ngoja....ehee. na nikuza ule mstari wa tatu nitaoa mke mzuri, sasa nitakuwa na nyumba, gari, na mke mzuri. lakini ole wake mke wangu aniletee za kuleta nitampiga hivi... akaanza kurusha mateke na kuvunja vile vyombo kuanzia mstari wa kwanza mpaka wa mwisho

ni wazi kuwa mkapa anaota alinacha, anaota mawakili wamsafishe, anaota magazeti kufungiwa, anaota kulipwa mabilioni, anaota makapa ndoto za alinacha

mwishomi mwa siku kesi aliyofungua mahakamani, ndiyo itakayommaliza, kama vile alinacha alivyoota. yeye kesi itamvunja vunja hadi hata lile tone la mazuri aliyiifanyia nchi litashaulika.

yetu macho, karibu mkapa, karibu ulingoni
 
Wanaomshauri Mzee Mkapa wanakosea sana,kila mtu anataka kuona Mkapa anakwenda Mahakamani.Kila kitu kipo wazi,(ushahidi wa kutosha upo) ataumbuliwa na wenzie aliokuwa nao serikalini.Lakini hali hii isihamishe juhudi za kutaka kujua pesa za umma za EPA zimeibiwa vipi?,hawa waungwana wamekuwa wajanja kukwepa maswala kwa kuzua habari mpya, moto moto.Wawakilishi wetu Bungeni wawe macho na hawa majangili,kila issue ipewe nafasi sawa ya kujadiliwa kwa uwazi.

Mkapa ni Fisadi,na kwa kuwa ameamua kwenda Mahakamani kila kitu kitakuwa nje!Anajivua nguo mwenyewe,wala msiwazibe macho watoto,waacheni waone sinema ya bure..Kuna ushahidi tosha wa yeye,Mrs,Nico na Mbuna Family kuhusika na Mradi wa kiwira.Judge Bomani na akina Zitto watakuwa mashahidi hapa,yale waliyoyaona Mbeya (Kiwira) yasiwe siri tena,kila kitu kiwekwe hadharani,ili hawa watu wahukumiwe kwa udhalimu wao.

Muungwana JK kama kweli utawala wako hauna Ubia usiwaonee haya hawa Majangili,acha sheria ichukue mkondo wake..Vinginevyo nawe utazomewa na kupigwa mawe kwa kuwalinda hawa wezi unaowaita wastaafu.Hivi serikali yako imefanya nini toka iingie Madarakani?kila siku tunaona kashfa mpya,kama nawe Uongozi umekushinda,achia ngazi si lazima umalize 10yrs,Historia itakuandika vizuri,kwa kuwa Rais wa kwanza kukaa madarakani Term moja..
 
Kuna watu wanakuwa baised hiyo kuchukua sehemu ya habari au kipindisha kabisa na kama ndio hivi basi kuna kazi.Na itafikia kipindi habari toka kwa mtu fulani mwenye negative attitude inabidi waachewe watu wa aina yake wajadili.Inakuwaje habari inavyoongelea taarifa mtu mmoja inakuwa tofauti.
Ni bora ziwe zinawekwa source kila mtu ameng'enyue kadiri awezavyo.
 
Mimi nafikiri amechukua uamuzi wa busara sana. Madamu serikali yetu kwa niaba yetu imeshindwa kumshtaki acha yeye aende hukohuko ili ukweli ujulikane- kama sisi tukipigwa bao asafishike kiana, yeye akipigwa bao basi tumepona. Hii tabia ya kushtaki watu kwenye internet na kwenye vijiwe binafsi imeshanichosha. Tuna vyombo tumevitumie.

Nafikiri hizi kesi zikianze zitatusaidia ku-concentrate na yale wanayoyafanya akina JK. Nakubaliana na wale wanaosema kuwa tujifunze kuwaadabisha na kuwajibisha viongozi wetu wangali madarakani itatusaidia zaidi. Sasa hivi tunawapa easy ride akina JK; tunasubiri atoke tusikie amenunua Bagamoyo nzima ndipo tuanze.

BTW, kwa wale waliopo Dar, hivi barabara ya Sam Nujoma KM 5 iliyoanza kujengwa Januari 2006 imefikia wapi?
 
Talking about backfire, sour grapes bwana naona mmepatikana sasa linyweni sasa mmelikoroga wenyewe hilooooo tena la motooooooooo!

Chaumbeya, heshima yako mkuu mbona unapotea sana brooo!

Sour grapes bwana kaaaazi kweli kweeeeeeeeeeeeli!

FMES,

Heshima mbele mkuu! Ama baada ya kutoa heshima zangu mbele, ningependa ufafanue mlengwa haswa ni nani na una maana gani kwa kutumia msemo wa "SOUR GRAPES"? Shukrani mbele mkuu!
 
Rais (mstaafu) wa Tanzania Benjamin William Mkapa yuko katika mchakato wa mwisho kuyashtaki magazeti ambayo yamekuwa yakimwandama kwamba ni fisadi.

Habari kutoka ndani ya familia yake zinaeleza kuwa taratibu za kuyashitaki magazeti hayo zimekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kutolewa kwa taarifa za awali kwamba yeye na mkewe, mjasiriamali Anna Mkapa hawana hisa katika mgodi wa Kiwira.

Zaidi ya hapo inaelezwa kuwa magazeti yatakayoshikiwa bango ni Kulikoni, Thisday, Mwanahalisi, Mwananchi, Tanzania Daima, Majira na Mtanzania.

Mtoa habari huyo aliyeona makabrasha ya mashtaka hayo ameeleza kuwa kila gazeti litadaiwa bilioni mbili; akieleza kuwa anadai kiasi hicho kwa kuwa angalau kinalinganalingana na hadhi yake ndani na nje ya nchi.

Hivi majuzi kampuni ambayo ilinunua mgodi wa Kiwira wa kuzalisha makaa ya mawe iliibuka na kueleza kuwa Mkapa na mkewe hawana hisa eti kwamba walijitoa muda mfupi baada ya kugundua kuwa ilikuwa ikijiandaa kununua mgodi huo kwa bei ya kutupwa ya sh. milioni 700 (zililipwa 70 kwanza za kukopa kutoka Benki) wakati mgodi wenyewe ukiwa na gharama kubwa ya bilioni 4.

Mawakili sita wamejipanga kwa kazi hiyo, huku mmoja akiwa kutoka Afrika Kusini ambaye anaeleza kuwa mzoefu katika kesi zinazohusu kashfa kwenye vyombo vya habari.


Mpango huu umeelezwa wapi? sidhani kama Mkapa ana ujasiri wa kwenda mahakamani. Binafsi siamini kama BWM ana mpango wa kwenda mahakamani, kwa sababu hawezi kwenda mahakamani.
 
Kama hakuwa mmiliki wa kweli, kwa nini imechukua muda mrefu hivyo kukanusha? Kuna kitu hakipo sawa hapa!
 
huyu nyani si nilisikia kafa ?

Hawezi kufa bila Raj Patel ku-sign death certificate, ya dig? As far as everybody is concerned, Raj Patel is supposed to be Nyani Ngabu's daddy and next-of-kin: for it was none other than Raj Patel who virtually (and single-handedly) invented "Nyani Ngabu"!
 
Back
Top Bottom