Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

---Tanpower Resources ilisajiliwa 29/12/2004 na kupewa namba 51080 ikiwa na dhumuni kuu la kwanza kuchimba mkaa wa mawe nakuzalisha umeme, wakati huo Mkapa bado ana hisa na alijua sababu za kuanzishwa kwake. Wakati inasajiliwa wanahisa walikua ANBEM hisa 200,000 na aliyesaini ni Anna Mkapa, Devconsult ya Yona na Mwanae (hisa 200,000), Universal Tech (hisa 200,000), Choice Industries ya Mbuna (200,000) na Fosnik Enterprises ya Nicholus Mkapa na mkewe Foster wakiwa wameiga jina la kampuni ya baba na mama zao ya ANBEM (wao wakiwa na hisa 200,000) na aliyesaini ni Nico

-----Lakini jambo la hatari ni kwamba, kabla hata ya TANPOWER kusajiliwa ilikwishaanza kufanya kazi na Evans Mapundi akiwa Mkurugenzi wake, alifanya mawasiliano Desemba 15 na wakatembelea Kiwira Desemba 18 na 20, kwa baraka za Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona. Yona akiwa pia mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo.

----Mkapa na Mkewe kupitia ANBEM walijitoa TANPOWER Februari 21, 2005 ikiwa tayari hata mkataba wa ubia kati ya TANPOWER na Kiwira umekwishaandaliwa na Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini.... Hata baada ya Kujitoa, Mwanae Nico na mkewe Foster na baba mkwe wao Mbuna walikua ndani ya Kiwira.

----Ni mwaka huo ambao Yona na bosi wake waliitosa STAMICO na kuchukua eneo jingine lenye hazina kubwa ya mkaa wa mawe liitwalo Kabulo rig ambalo serikali ilikopeshwa USD milioni 50 kufanya utafiti. STAMICO hadi sasa wanalilia eneo hilo ambalo limechukuliwa na TANPOWER/Kiwira bureeeeeeeeeeeee

-----

I see... Hebu tujikumbushe kidogo:-

Mkapa1.jpg

Mkapa2.jpg

 
Invisible,

Thanks for page 1. Malizia basi na page 2, 3 na kuendelea... Maana utamu ndio ulikua unaanza kunoga atiiii...

Documents kama hizi zikionwa na jaji mwenye akili nzuri, nafikiri jaji atakua anajiinamia chini ya deski lake na kujichekea kwanza, then anarudi juu na kuendelea na kesi.

Hawa watu hawana aibu kabisa....
 
Posted Date::6/2/2008
Wanaomtetea Benjamin Mkapa waanza kushambuliwa
*Wabunge, wanasiasa wataka yeye ajibu
*Wasema tuhuma za nyaraka zijibiwe kwa nyaraka

*Wahoji Kiwira walikuwa wapi siku zote hizo


Na Muhibu Said


BAADHI ya wabunge na wanasiasa, wameiijia juu Kampuni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCP) kwa kukanusha kuwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ni miongoni mwa wamiliki wa mgodi huo, wakiitaka kampuni hiyo imwache ajibu tuhuma hizo yeye mwenyewe.


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema jana kuwa kitendo kilichofanywa na KCP, ni cha kuwapiga chenga wananchi kwa vile Mkapa ndiye aliyepaswa kujibu mwenyewe tuhuma za kujimilikisha mgodi huo alipokuwa madarakani.


Hata hivyo, Profesa Lipumba alisema majibu ya KCP, bado yana utata kwani sheria ya maadili ya viongozi, bado inamtaka aeleze mali alizonazo baada ya kuwa madarakani.


"Mbunge Aloyce Kimaro alipotoa tuhuma hizo bungeni, hakuwa akieleza kitu ambacho si sahihi. Mkapa anatakiwa atoe taarifa kamili mbele ya waandishi wa habari. Aeleze mali alizokuwa nazo wakati anamaliza kipindi chake cha uongozi na si kusubiri dakika za mwisho wamsafishe," alisema Profesa Lipumba.


Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa alisema kama ambavyo wao walitumia nyaraka kumtuhumu Mkapa hadharani kwamba, kinachotakiwa kufanywa naye, ni kujibu kwa nyaraka na si kutegemea watu wengine wamjibie.


"Kama tulivyomtuhumu kwa documents (nyaraka), tunataka na yeye atujibu kwa documents, lakini siyo masuala ya kujibiwa. Sisi hatusemi hivi hivi, tuna akaunti za Mkapa," alisema Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema) na kuongeza:


"Inashangaza kuona hata Sumaye alipotuhumiwa ana ng'ombe, Mkapa ndiye aliyemjibia kuwa ni mfugaji. Ni utaratibu ule ule wa kujibiana".


Dk Slaa alisema hata kama Mkapa alijiondoa wakati wa kununua Kiwira bado ukweli unabaki kwamba, kampuni yake ilishiriki kwa namna moja mchakato wa kuinunua. "Walikuwa wapi muda wote hadi leo watoe tamko hilo, hapa kuna walakini mkubwa," alisema Slaa.


Naye Wakili wa Mahakama Kuu, Juvenalius Ngowi aliiambia Mwananchi kwamba Kiwira walipaswa kuonyesha nyaraka na vielelezo badala ya maneno matupu.


"Ni muhimu wakatoa nyaraka, haya maneno matupu hayaingii akilini," alisema.


Alisema Kiwira pia wanapaswa kuwaambia wananchi kama Mkapa akiwa mwanahisa naye alishirikia katika maandalizi na je hisa zake alimuuzia nani?


"Ni lazima watuambie kwamba hizo hisa zake alimuuzia nani na kwa bei gani, kwa sababu anaweza akawa ameuza kwa bei kubwa kwa kujua kuna faida huko mbele," alisema.


Naye Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro alisema alichokisema bungeni ni sahihi na kwamba, mtu mwenye shaka na ukweli huo, aende kwenye Kitengo cha Usajili wa Makampuni (BRELA) Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.


"Waulizeni Wizara ya Nishati na Madini na BRELA. Lengo langu lilikuwa wengine wasirudie tatizo hilo," alisema Kimaro.


Jana, baadhi ya vyombo vya habari viliikariri KCP ikikanusha tuhuma kuwa Mkapa ni miongoni mwa wamiliki wa mgodi huo.


Badala yake, KCP ambayo inamiliki mgodi huo, ilisema Kampuni ya ANBEN inayomilikiwa na Mkapa na mkewe, Anna, ambayo awali ilikuwa sehemu ya Kampuni ya Tanpower, ilijitoa baada ya baadhi ya wanahisa wenzake kuwa na mpango wa kununua mgodi huo.


Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro alisema ingawa katika hati za umiliki (Articles of Association) inaonyesha kuwa Mkapa ni sehemu ya Tanpower, lakini baadaye alijitoa.


Aprili 25, mwaka huu, Kimaro, alimtuhumu bungeni Mkapa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Daniel Yona, kwamba walinunua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira (KCML), ulioko Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya kwa kificho.


Kimaro alisema mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na mkewe, Anna pamoja na Yona walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa mgodi huo kimya kimya.


Kimaro alisema hayo alipokuwa akichangia bungeni Muswada wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2007, uliowasilishwa bungeni mwezi Aprili.
 
We Kadampinzani nafikiri wewe ni cha Mkapa. kwa nini usiandike jina lako halisi kuwa wewe ni Mkapa? Je nikuuumbue zaidi
 
Huyu mafuru nampa poe sana. huwa anabururwa kwelikkweli. Sie mawakili tunamfahamu sana. Na mara nyingi huwa anapewa zile kesi mahakamani ambazo zinadalili za kushindwa.
Na huyu bwana Mbuna anajisikia sana. Nenda pakle askari Monument ktk duka la vipodozi vya Amos. Utakatishwa tamaa kumwona huyu ``mungu mtu``. Nilikoma na sikumpelekea kesi yangu kwake. Hajaokoko chochote ni kutafuta tu hela makanisani
 
Kwenye kipengele kifuatacho:

"It was resolved that 20,000 shares held by ANBEM LIMITED should be forfeited back to the company (i.e., TANPOWER RESOURCES LIMITED)."

Kwa neno la Kiingereza "forfeited" inaweza kuchukuliwa kumaanisha "surrendered" au "kutaifishwa" kwa Kiswahili. Kwa hiyo, kwa kifupi, nyaraka hii inathibitisha ukweli wa habari iliyoandikwa na "Daily News/UHURU" siyo?
 
Hold on a minute...

"As started earlier, Tan Power Resources Limited is a locally registered company formed by indigenous Tanzanians for purposes of investing in Tanzania's expanding energy sector"

... Indigenous Tanzanians ndio watu gani hawa?
... Yeye Waziri wa Madini alikuwa na uhusiano gani na hiyo kampuni ya Indigenous Tanzanians?
 
Hawezi kufa bila Raj Patel ku-sign death certificate, ya dig? As far as everybody is concerned, Raj Patel is supposed to be Nyani Ngabu's daddy and next-of-kin: for it was none other than Raj Patel who virtually (and single-handedly) invented "Nyani Ngabu"!

Na wewe mbona uko obsessed sana na Raj Patel? Kila kitu Raj Patel....Raj Patel...Raj Patel....dizaini unam-miss sana Raj Patel wewe.....
 
Smart as always Che Nkapa! he is always one step ahead of everyone, wonder why no one has said anything kumtetea before? It takes longer to get this kind of paper works done na sasa amefanikiwa kugeuza kibao. Nilishasema hapa kwamba asithubutu mtu kumpeleka mahakamani kwa maana angeangukia pua tu. Dawa ya watu kama hawa ni kupata Raisi Dikteta tu kama nilivyowahi kupendekeza, achanechane hayo makaratasi yao, awasweke ndani na kuturudishia wanyonge kile kilicho chetu bila hata kwenda mahakamani!
 
I see... Hebu tujikumbushe kidogo:-

Mkapa1.jpg

Mkapa2.jpg


Walitaka kutucheza kanyabwoya. Fisadi atumie jina lake na wadhifa wake kuwafisadi Watanzania mali yao ya mgodi wa makaa ya mawe halafu baada ya kuwa chini ya ownership ya fisadi, mkewe na Yona wajifanye kujitoa kama vile wao si shareholders tena wa KCM. Huyo mtoto wa fisadi Mkapa na mkwe wake wamefanya biashara au kazi gani ndani na nje ya Tanzania ya kuwawezesha kununua mgodi huo kwa shilingi milioni 700? Nani aliyeamua mgodi huo uuzwe kwa shilingi milioni 700 (ambayo ni less than 25% ya thamani halisi) badala ya thamani yake halisi ya shilingi bilioni nne? Mafisadi wameumbuka!!!
 
Hold on a minute...

"As started earlier, Tan Power Resources Limited is a locally registered company formed by indigenous Tanzanians for purposes of investing in Tanzania's expanding energy sector"

... Indigenous Tanzanians ndio watu gani hawa?
... Yeye Waziri wa Madini alikuwa na uhusiano gani na hiyo kampuni ya Indigenous Tanzanians?

Mkjj ondoa hiyo IT na uweke mafisadi, inakaa vizuri zaidi....🙂 Huyu Yona naona yeye ndiye aliyekuwa fisadi wa kuhakiki ufiisadi unakamilika kama walivyotarajia na walidhani wizi wao hautagundulika na Watanzania!!!! Duh!!!!
 
Posted Date::6/2/2008
Wanaomtetea Benjamin Mkapa waanza kushambuliwa
*Wabunge, wanasiasa wataka yeye ajibu
*Wasema tuhuma za nyaraka zijibiwe kwa nyaraka

*Wahoji Kiwira walikuwa wapi siku zote hizo.

Walikuwa wanafanya forgery za makaratasi na kupanga mikakati ya nini cha kuongea na nani awe msemaji wa fisadi Mkapa. Fisadi Mkapa ongeaaa!!!....uwazi na ukweli umeishia wapi tena!!? mbona unajikanyagakanyaga!!!!? Watanzania hatutaki kusikia yeyote yule anaongea kwa niaba yako tunataka kusikia wewe mwenyewe ukiongea na hayo utakayoongea yawe na vielelezo vya uhakika maana tunaweza kuomba vifanyiwe uchunguzi kama viliandikwa 2005 au ni karatasi ya juzi juzi.

Tunataka pia kujua ni nani walioshiriki katika mazungumzo ya kuingia kwenye mkataba kati ya KCP na TANESCO ambayo hatimaye yalizaa mkataba wa shilingi bilioni 326, pia kama walikuwapo wawakilishi toka wizara mama ya TANESCO. Tungependa kujua ni nani waliosaini mkataba huo kwa niaba ya TANESCO na nani alisaini kwa niaba ya KCP. Maana inasemekana mkataba huo ulisainiwa na makaburu wa Net Group kampuni ambayo iliingizwa kwa mtutu wa bunduki na Mkapa ili kuiendesha TANESCO pamoja na kupingwa na asilimia kubwa ya Watanzania wakiwamo wafanyakazi wa TANESCO.
 
Hizi habari za Mkapa kumiliki Mgodi wa makaa ya mawe zilianza kuandikwa magazetini miezi minane au zaidi iliyopita. Pia wajumbe wa kamati ya madini iliyoundwa na JK walitembelea mgodi na kushauri ifanyike probe nyingine ili kufuatilia umiliki halali wa mgodi huo. Hawa Kiwira, Mkapa, Wakwe zake walikuwa wapi siku zote hizi kuwafahamisha Watanzania kuhusu umiliki halali wa mgodi huu?

Posted Date::6/2/2008
Kwa nini Kiwira imechelewa kumsafisha Mkapa?
Mwananchi

HATIMAYE uongozi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira (KCP), umevunja ukimya juu ya kama Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kupitia kampuni yake na mkewe ya ANBEN, kuwa na hisa katika mgodi huo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Mtendaji Mkuu wa KCP, Fencis Tabaro, Kampuni ya ANBEN Mkapa ilijitoa kwenye ubia na kampuni Tanpower, ambayo ilinunua mgodi huo baada ya kubaini kwamba ina mpango wa kununua mgodi huo.

Sambamba na hili Taboro alikanusha kuwa Anna Mkapa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwira na kusisitiza kuwa mama huyo hana uhusiano wowote na kampuni hiyo.

Maelezo ya kiongozi huyo wa KCP yabainisha kuwa ingwa katika Hati ya Umiliki (Articles of Association) ya Tanpower inaonyesha kuwa ni sehemu ya kampuni hiyo, baadaye alijitoa hivyo, tuhuma zinazomkabili si za kweli.

Sisi kama sehemu ya jamii ya watanzania, tunaipokea taarifa hiyo kama ilivyotolewa, lakini kwa mashaka, kwa sababu muda mrefu umepita tangu Mkapa aingizwe kwenye tuhuma hizo nzito, ambao zimemvunjia heshima kwa kiasi kikubwa.

Hatukatai maelezo na ufafanuzi uliotolewa na Mtendaji Mkuu wa KCP, lakini hoja yetu ni kwamba, kwa nini ulichelewa kiasi hicho kutolewa? Je, anataka kuieleza jamii ya watanzania kwamba, hilo nalo lilihitaji utafiti na ushauri kabla ya kutoa taarifa kwamba hahusiki?

Jambo hilo limetukisitisha saa kwa sababu kuu mbili. Mosi ni urasimu wa kutoa taarifa sahihi juu ya sakata hilo na pili, kumchafua Rais Mstaafu, kwa sababu kama zingetolewa mapema, tuhuma hizo zisingefikia hatua hiyo.

Kitendo cha kumhusisha Rais Mstaafu kwenye tuhuma nzito kwama hizo, kimemshushia hadhi na kumwondelelea umaarfu aliojingea kwa kipindi kirefu ndani na nje ya nchi hii.

Sote tunasikia jinsi watu wanavyomtukana Mkapa, wakidai kuwa ni fisadi na hata baadhi ya wananchi walikamatwa na polisi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, baada ya kumzomea na kumtukana alipokuwa anapita kuelekea nyumbani kwake.

Hata kama watu hao walimvunjia heshima Rais Mstaafu, kama alivyosema Pinda alipoulizwa na waandishi muda mfupi baada ya tukio kwamba, lazima aheshimiwe kutokana na mafasi yake, tunasisitiza kuwa waliosababisha hali hiyo ni waliochelewa kutoa ufafanuzi, pengine na hata Mkapa mwenyewe.

Itakumbukwa kwamba licha ya kustaafu, bado Mkapa ana nafasi katika historia ya nchi yetu, hivyo kuacha tuhuma nzito kama hizo zimchafue kiasi hicho, ni sawa na kulichafua taaifa letu, kwa sababu hadhi aliyonayo kwa niaba ya nchi yetu katika jumuia ya kimataifa ni kubwa.

Tunachelea kusema kwamba, kama kweli Mkapa si mhusika wa katika kashfa hiyo, waliomchafua basi ni hao hao Kiwira na mlamlaka zinazohusika na suala hilo, kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa kueleza hayo mwanzoni kabisa.

Hoja yetu nyingine ni kwamba, kama Mkapa alijitoa kwenye kampuni ya Tanpower, ni lazima aliandika barua ya kufanya hivyo, kwa kuwa suala hilo linaingia kwenye taratibu za kisheria na kuvunja mkataba wa ushiriki, ambayo lazima iambatanishwe na waraka kwa kampuni hiyo. Je, barua hiyo ipo?

Tunasema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu wanahofu kwamba huenda suala hilo linazimwa kijanja ili umsafisha Rais Mstaafu.
 
..No doubts Mkapa na mafisadi wenzake wamecheza foul Kiwira na inabidi washughulikiwe kisheria lakini incompetency & stupidity ya waliopewa kazi kusimamia sheria zetu hawatafanya kazi kama kawaida,hayo ndio maisha ya bongo...uvunjaji wa sheria,rushwa halafu tunajiuliza kwa nini njaa na magonjwa vinatumaliza.
 
Kiwira yatamba umeme wake kuwa nafuu
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,June 03, 2008 @00:02

Kampuni ya Makaa ya Mawe na Nishati ya Kiwira (KCP), imetamba kuwa umeme wake utakuwa wa bei nafuu ambao utalipa faida kubwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

KCP pia imesema mkataba wake ambao wameingia na Tanesco kamwe hautakuwa mzigo kwa shirika hilo na kwa serikali. Akizungumza na gazeti mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro alisema mkataba walioingia na Tanesco ni kuliuzia shirika hilo uniti moja kwa senti tano, kiasi alichodai kuwa ni kidogo ikilinganishwa na bei za umeme wa kampuni nyingine.

"Kiwango hicho si tu kwamba ni cha chini, bali ni cha chini hata kwa Afrika Mashariki na Kati," alisema Tabaro wakati akijibu swali aeleze namna ambavyo wameingia mkataba na Tanesco. Alisema kiwango hicho cha bei ya umeme kilipendekezwa na serikali yenyewe wakati huo Waziri wa Nishati na Madini, akiwa Dk. Ibrahim Msabaha.

"Sisi tuliwapa kile ambacho serikali ilitaka, maana Dk. Msabaha alisema kama tusipokubaliana na bei hiyo, asingeruhusu mkataba na Tanesco kusainiwa," alisema. Mtendaji huyo alisema umeme wa makaa ya mawe gharama zake ni rahisi kama ulivyo wa maji ndiyo maana kampuni yao inaona ni vyema ikaiuzia Tanesco kwa bei hiyo ili shirika hilo litakapouza lipate faida.

"Ninavyojua mimi umeme wa gesi na umeme wa dizeli ni aghali na Tanesco inalazima kupata ruzuku kutoka serikalini ili imudu kununua kwa kampuni zinazozalisha umeme wa namna hiyo," alisema. Tanzania kwa sasa inatumia umeme wa maji ambao unaelezwa kuwa ni rahisi kuliko umeme mwingine. Pia inatumia umeme unaotokana na gesi na dizeli.

Kampuni ya IPTL inazalisha umeme wa dizeli, wakati Songas, Aggreko na Dowans wanazalisha umeme wa gesi. Licha ya kuwa na utajiri wa makaa ya mawe, Tanzania haikuwahi kufaidi nishati ya madini hayo. Tabaro alisema Tanesco itapata faida kubwa kampuni yake itakapoanza kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kwani itakuwa mara ya kwanza kununua umeme wa bei ya chini na kuuza kwa faida.

Alisema wanatarajia kuanza kuzalisha megawati 50 ifikapo Aprili mwaka 2010. Alisema Oktoba mwaka huo huo, kampuni yake itazalisha megawati 150 hivyo kufanya jumla ya megawati zitakazokuwa zinazalishwa na kampuni hiyo kufikia 200, umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya taifa.

Alisema kuanzia mwaka 2012 itaanza kuzalisha megawati zingine 200 hivyo kufanya umeme utakaotoka Kiwira kuwa megawati 400. KCP inamilikiwa na Tanpower kwa asilimia 85 na serikali ina hisa 15 tu mgodi huo uliuzwa kwa kampuni hiyo kwa Sh milioni 700. Katika kuhakikisha umeme wake unaingia kwenye gridi ya taifa, Tabaro alisema watajenga njia ya umeme ya 220kv kutoka Kiwira hadi Mbeya umbali wa kilometa 100.
 
Let me do some math here...BRELA offices are gutted down a few months ago, Ballali dies, KCL's CEO defends Mkapa (The CEO reports to the board of directors chaired by Mkapa's mzazi mwenzake) and now Sumaye comes out to defend him also...mmmh. Mimi si bingwa wa hesabu ila mlinganyo huu utakuwa rahisi kukokotoa!!!
 
Kwa nini Kiwira imechelewa kumsafisha Mkapa?
Jibu- Alikuwa mchafu sana na naamini bado si safi, sidhani kama ametakata!
 
Back
Top Bottom