KV LONDON
JF-Expert Member
- Jul 18, 2012
- 903
- 242
Mkuu upo?
Mbowe kauza chama na wanachama...
Inakuhusu nini, si ubaki na CCM yako
Mkuu upo?
Mbowe kauza chama na wanachama...
LOWASSA NI NGUMU KUINGIA UKAWA KAMA ILIVYO KWA NGAMIA KUPENYA KTK TUNDU LA SINDANO"lowasa for presidential 2015"via CCM
LOWASSA NI NGUMU KUINGIA UKAWA KAMA ILIVYO KWA NGAMIA KUPENYA KTK TUNDU LA SINDANO"lowasa for presidential 2015"via CCM
dr slaa hawezi kukubali kumwachia lowasa agombee badala yake.
Say it again...
Here I can say it again. UKAWA wamerukwa na akili kumpokea Lowassa.
Haya tuendelee na mjadala!
Sibonike Ukawa wamerukwa na akili kama ulivyotabiri!
Babu Chodo mapepo yamehamia Ukawa!
Tuendeleza mjadala baada ya October tuone kama wamerukwa na akili au la!
Hata kama atahongo billions viongozi wa ukawa hawawezi kumpendekeza na hawawezi kumkubali by any means. Hauziki huyo
LOWASSA NI NGUMU KUINGIA UKAWA KAMA ILIVYO KWA NGAMIA KUPENYA KTK TUNDU LA SINDANO"lowasa for presidential 2015"
Huyu ni mwiz tu
Mtu anayeshindwa kuitetea ccm japo Arusha Tu hatumtaki.
hatutaki viongozi waliowahi kuliingizia taifa hasara ndo waje huku never on earth, labda awe mwanachama wa kawaida tu na sio kugombea nafasi yoyote ya uongozi vinginevyo arudi huko huko kwa chama chake cha mashetani
Lowasa akija UKAWA mimi natoka , amechafuka , hana na wala hajawahi kuwa na fikra mpya , ndio maana hadi leo anaamini kwamba rushwa itampeleka ikulu .
Haiwezekani maana hana sifa za upinzani.hatutaki UKAWA iwe tawi la ccm
Lowasa awezi kujiunga na wahuni
ukawa hawawezi mkaribisha mwizi! wezi wenzie wamshindwe sa ukawa itakuaje???
Mwizi ni mwizi tu.
Mtoa mada umeongelea Lowassa 'kugawa pesa kama njugu' ili awe rais. Nakukumbusha kuwa UKAWA haihitaji mgombea mwenye sifa kama hiyo! Na siyo mgombea tu, bali haihitaji hata mwanachama wa kawaida tu kuwa na hiyo sifa ya kutoa rushwa.
UKAWA wasimkatae akija kama mwanachama au kugombea jimbo la Munduli lakini si cheo cha uraisi. Kwa nini aje mwisho kisha apewe ugombeaji wa uraisi? Maana yake shida yake ni urais walasi upinzani! Alikuwa na nafasi nzuri sana muda wote kuingia upinzania hawezi tena. Pili hana jipwa Lowasa, alisha zeeka apumzike huyu.
Ukawa wakimpokea lowassa ntaipigia kura ccm
sisi hatupokei watu wachafu
Lowasa atahangaika sana lakini uraisi utakuwa ndoto kwake
Sikiliza wewe FISI, mimi sio ukawa wala sisiemu. Nachotaka ni rais bora, sasa mnyonya mapvmbu ya EL kama wewe unakuja na upumbafu eti EL for presidency, unahitajika kupelekwa mirembe, kwamba hujui EL ni worse than JK??
Kuona hili hauhitaji kuwa na certificate, diploma au shahada zingine. Wala hauhitaji hesabu au science nyingine kujua kuwa hafai, haiwezekani anatumia pesa nyingi hivi kutaka kuwa rais. Na kwa taarifa yako, huyu hata sisiemu hakatizi. Mtamremba sana na kukisi mapvumbu yake, ila hamna kitu. Sidhani kama sisiemu ni wapumbavu kama wewe na team yako.
Nashangaa watu wanavyomnadi EL huyu hawezi kuwa rais wa Tanzania pamoja na njugu zote anazomwaga, watakula na kuvimbiwa kama JK alivyovimbiwa wizi kwa miaka 10 iliyopita. Hana jipya. wakuu endeleeni kufaidi hizo njugu kutoka Voda phone hazina mwenyewe. Kiini cha kuvuruga shirika la simu Tanzania.
Lowasa hafai urais(tuwe waungwana na wakweli tu)!
Yani huyo Lowasa yeye ni spacial kiasigani, hata atoke ccm asubuhi, jioni aingie Ukawa nakupewa nafasi ya juu kiasihicho!!.
Ivi huko UKAWA ndo wanapokea mafisadi
ukawa hatutaki mapepo!! huko huko
Kama UKAWA lengo lao kuu ni kushinda uRais tu (kiasi cha hata kumtumia mtu kama Lowasa), basi HAWATUFAI! Nchi inahitaji marekebisho makubwa sana kisiasa. Watu kama Lowasa (na wenzake huko CCM) wanawakilisha uozo unaolitesa taifa letu leo hii.
Ni wazi Edo ana nguvu kubwa sana kwenye chama hicho kuliko yeyote yule. La kulielewa nyie wote ni kuwa iwe iwavyo Lowassa hawezi kujiunga upinzani.
Kwa7bu hzo bora CCM ife kuliko kumweka huyu mtumwa wawahindi. Inaniuma sn kuona watu timamu mnamsafisha mtu alie tuingza kwenye hasara kubwa wakati wapo watu wasio fungamana na makundi jaman huyu mzee hafai
EL ni kielelezo cha vyote ambavyo ukawa wanapinga. Haitawezekana kumpokea kwa vyovyote vile. Labda kama ukawa watakuwa wamerukwa na akili.
Huyu mwizi aje ukaws ili iweje?
UKAWA ya wapi,hatutaki majizi sisi
Utadhani ulikuwa kichwani mwangu Mkuu, hakuna sababu yoyote ya huyu fisadi kukaribishwa UKAWA.
Aje ukawa kutafuta nini?aiseh tuheshimianeg
Uliyeleta mada ni mkereketwa wa ACT.Kwa taarifa yako,Ukawa haiitaji mtu anayeitwa mamvi.Kumkubali mtu mzee huyu ndani ya ukawa ni kama kuchambia mfuko wa Rambo.
lowassa akija ukawa naachana na siasa!
Yani hilo gamba ndio lipeperushe bendera ya ukawa? Hamjiewi kumbe!
Wewe unachokifanya hapa ni kuwa blackmail ccm wampitishe LOWASA tu na wala huna lolote. Lowasa hakubaliki UKAWA. Na kwa uroho wake wa madaraka alionao, si ajabu kweli jamaa likahamia chama kingine ili ligombee uraisi. Huu ni wehu.
UKAWA WAKIMSIMAMISHA LOWASA, SISI HATUWAPI KURA. Hatuwezi kupoteza muda wa kupigia kura fisadi lilokubuhu eti kwa kuwa kuna wajinga kadhaa wanalipigia kampeni.
Ninaimani kwa usafi na umakini wa UKAWA, hawawezi kufanya kosa kubwa kama hilo. UKAWA kumsimamisha fisadi lowasa ni kuwasaliti na kuwatukana Watanzania nchi nzima waliosimama macho yao yakiwa UKAWA huku wakiwa wamefungamanisha mikono yao pamoja!.
Na wewe mleta mada usirudie kuwaelekezea UKAWA mifereji ya maji machafu!. Hayo yamalizeni huko huko ccm.
UKAWA hakuna nafasi ya mafisadi aende zake huko. UKAWA hawawezi kufanya makosa ya kipumbavu ya kumkaribisha huyu fisadi.
Chama gani kimeshikwa vibaya? Ila team lowassa wanamuhangahikia mzee wa richmond lakini watambue hawezi kuwa Rais JMT.
Mtakuwa vichaa mwaka huu Ukawa hakuna nafasi ya watu wachafu bora aende kubaki huko mafisadi wenzake huko ccm.
amechelewa sana sisi kina gogo la shamba tulimshauri kuachana na ccm tangu 2014 lakini hakutuelewa hivyo kwa sasa hakuna chama kitakachomkubali maana amekuwa ni mzigo pamoja na pesa zake
Kuungana na mchawi ili mmpige anayekuibia mke ni ujingaaa sana, kwa sababu maana yake ni moja tu kuwa umeamua kuwa mchawi pia
Akija Naondoka akapokelewa naondoka.
Ukawa wakichukua hili fisadi nitaamini kweli ni wasaka tonge na ntaacha siasa, naanza kupambana na mwanasiasa yeyote bila kujari anatoka chama changu teno nitafanya jino kwa jino
Lowasa hakuna Chama kilichotayari kumpokea.aanzishe chama kipya.hakuna Chama kilicho tayari kuungana na fisadi.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, nakubaliana na wewe, hata mimi ningependa kuwasikia, kwanza waliosema hili haliezekani, baada ya kuwezekana leo wanasemaje?!. Kuna waliosema hili likitokea watahama, limetokea lakini hadi leo hawajahama, jee bado wanasubiri nini?!, ila pia kuna waliosusa na kuamua kujinyamazia kimya, tungependa kuwasikia leo wanasimama wapi?!.Kwenye hii mada kuna michango ya watu ambayo ningependa leo watueleze wamebadili mawazo vipi... ama waliamini walichokisema humu au hawakukiamini.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, nakubaliana na wewe, hata mimi ningependa kuwasikia, kwanza waliosema hili haliezekani, baada ya kuwezekana leo wanasemaje?!. Kuna waliosema hili likitokea watahama, limetokea lakini hadi leo hawajahama, jee bado wanasubiri nini?!, ila pia kuna waliosusa na kuamua kujinyamazia kimya, tungependa kuwasikia leo wanasimama wapi?!.
Pasco
Pasco, hakuna hata sehemu moja ambapo qualities, principles and standards za CHaDEMA na UKAWA zimekuwa compromised kwa ujio wa Lowasa. Ninachokiona ni behavioral na attitudes transformation kutoka ufisadi kwenda uzalendo kwa hao immigrants kitu kinachoongeza ukubwa na uimara kwa jeshi la UKOMBOZI. Sanasana Makamanda wenyeji waongeze nguvu kwenye growth management.
Kwa hiyo, UKAWA bado haijabadilika. Msimamo ni ule ule kwamba hawapokea mafisadi. Dr. Slaa alisema, mtu atakapotaka kujiunga na ukawa, akatoa maelezo na vielelezo vya kueleweka watamwelewa.
Na ukumbuke kwamba ufisadi ni tabia chafu ya kishetani dhidi ya binadamu na kamwe si jina wala sura ya mtu.
Unatakiwa kufahamu yafutaatayo kwamba binadamu hubadilika na mazingira. Ccm inazalisha na kudumisha ufisadi, UKaWA inasafisha na kuwaweka watanzania katika msimamo sahihi wa kujenga nchi inayobeba agenda na maslahi ya Wananchi.
UKAWA haihitaji na KAMWE HAITAHITAJI MAFISADI kwa sababu kufanya hivyo ni kusaliti dhamira na Watanzania. Lakini UKAWA inakazi moja ya kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania katika ngazi zote kwa maana ngazi ya mtu binafsi, serikali na mifumo yake hadi ngazi ya uhusiano wa kimataifa.
Kila mtu sasa anayependa kufahamu, anaelewa namna gani Lowasa amegeuka kutoka unyang'au aliokuwa aki advocate akiwa ccm na sasa ameamua kuungana na Watanzania kuleta ukombozi sahihi. MFANO, WAKATI YUKO CCM ALIKUWA MSTARI WA MBELE KURARUA RASIMU YA KATIBA YA JUDGE WARIOBA NA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE UHARAMIA WA KUUNDA KATIBA YA CCM ITAWALE NCHI NA BILA HAYA KUHAKIKISHA KATIBA PENDEKEZWA INAPITSHWA KWA UBARADHURI WA WAZI.
LEO HII, LOWASA ANASEMA, SASA AMEAMUA KUIKOMBOA TANZANIA KUTOKA MATESO YA CCM NA ANASIMAMIA MISINGI YA UKAWA IKIWEMO KATIBA YA JUDGE WARIOBA. Mtu anapobadilika, hata kama ni jambazi sugu, anapoamua kushirikiana na binadamu katika kuhakikisha usalama wa raia, ni akili gani iliyomakini itakayozidi kumkataa mtu huyo?
Kama vile jambazi akijirudi, anavyoweza kushirikiana na raia kubainisha na kuangamiza mitandao ya ujambazi anavyostahili kukubaliwa, kupewa ushirikiano huku akiongozwa kwamba asije akakiuka maadili ya jamii kwenye hiyo operation, vivyo hivyo, Lowasa UKaWA imemkubali kwa kujitoa kwake, na uwezo wake wa kuiua ccm kwa kushirikiana na makamanda na Watanzania katika ujenzi wa Tanzania mpya.
Paul Mtume alikuwa kinara katika "MATESO YA KANISA LA KWANZA, wakati ule aliitwa Saul.". Kama vile Lowasa ccm alivyoshiriki katika uharamia wakuua Tanzania, Saul yule yule alishiriki tena akiwa kiongozi wa mauaji ya Mtume Stephano.. Kanisa lilitawanyika na kutawanyika kwa ajili ya adha ile na Sauli akiwa na kibali cha serikali aliwafuatia ili kuendelea kuwamaliza Wakristo..
Alipokuwa akienda Damesk, alikutana na NENO likambadilisha. Sauli akaenda kwa Wakristo akieleza yaliyompata na kwamba sasa alikuwa akihtaji Mwongozo sahihi ili awe Mkristo Halisi. Wakristo wale walimwogopa kwanza hapo awali. Kama vile Lowasa, kuna wengi waliona anakwenda UKaWA kuwamaliza Watanzania kama vile SAuli alivyoenda Kanisani awali.
Lakini ni Mkristo gani ambaye anahitaji kupewa maelezo juu ya kazi aliyoifanya Paul ya kueneza habari za Mungu katika Kristo Yesu?
Lowasa vile vile hajakataa kushiriki uchafu alipokuwa ccm, lakini sasa yuko na watu safi wakimwongoza na kumpa maarifa zaidi ya Ukombozi sahihi wa Mtanzania. Ikiwa watu kama Saul au hata majambazi sugu yanapobadilika hukubalika na kupewa nafasi sahihi katika jamii, kwa nini MNALAZIMISHA LOWASA ASIPEWE NAFASI YA KUFANYA ANAYOWEZA KUYAFANYA KATIKA UKOMBZI WA NCHI?
Kumbukeni UKAWa inakwenda kubadilisha kila mtu aishi Kizalendo bila kujali anataka ama hataki. Sasa kama mmoja wa mafisadi ameamua kwa hiyari yake kuwa Mzalenddo, kuayaacha matendo ya ufisadi na kuanza sura mpya kwa kuungana ya jeshi la Wakombozi wa nchi, kwa nini asikubaliwe kubadilika?
Hamwoni yeye ni heri kuliko mafisadi yaliyobakia ccm yanayojiapiza kufa na tai shingoni bila kujua hatari inayowangojea ya kubadilishwa kwa nguvu bila ridhaa yao?
UKaWA haijengi taifa la matabaka. Inalengo ya kuwaunganisha Watanzania wote waungane na kujenga nchi kwa umoja chini ya mfumo mpya wa UKAWA na si kulazimisha migawanyiko na malumbano yenye misuguano isiyokuwa na tija.
Yeyote anayetaka kwa hiyari yake kujiunga na jeshi la UKOMBOZI ukawa anakaribishwa na anahaki yake na kushiriki ukombozi na ujenzi wa taifa jipya kwa kutumia uwezo na vipaji vyote walivyonayo kwa maslahi y anchi.
Yule anayeng'ang'ania kuendeleza ufisadi kama jk & familiy, na wengineo kama kina chenge, na wale wanufaika wa ccm, hawataachwa waendelee na ufisadi. Watalazimika kuwa Watanzania wema na watalazimika ushirikia ujenzi wa nchi chini ya UKaWA.
Wewe nkwingwa ulioteshwa na mizimu?Hakuna mtu mwenye uwezo wa kumkataa Lowasa ndani ya ukawa wengi ni waganga njaa tu.
Mkuu,Wapiga kura wanaojitambua na wenye mapenzi ya kweli na Tanzania kamwe hawawezi kupoteza kura zao kwa huyu fisadi mgawa rushwa katika nyumba za ibada.
hatutafukua makaburi.Mkuu umeshatoka au unasubiri Lowasa aje UKAWA Ndo utoke?