Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Lowassa kama anatambua ukawa wana hoja za msingi, kwamba ukawa kama ilivyo muungano wao wamedhamiria kuwasemea wananchi, siyo dhambi yeye kuiunga mkono ukawa
 
Japo ambalo si la siri kwamba kambi zote za wagombea uraisi CCM zinamuogopa sana Lowassa, hivyo kuna kila aina ya jitihada ya kuhakikisha jina la Lowassa halipitishwi kugombea nafasi ya uraisi.

Huku wapinzani wakijipanga kukata jina lake lakini Lowassa yeye anaendelea na mikakati yake ikiwa ni pamoja na kugawa fedha kama njugu kwani anaamini yeye ni raisi wa Tanzania 2015-2025 "PIGA UA"

Lowassa anatishia kukiua chama (CCM) endapo hata pitishwa kugombea uraisi.

Wakati huo huo, endapo jina la Lowassa halitapitishwa CCM wanyetishaji wetu wanasema mkakati wa Lowassa kugombea kupitia UKAWA kwakuwa tayari ana mtaji wa wanaCCM wengi hivyo ni rahisi kwake kushinda nafasi ya uraisi.

Inasemekana kuwa tayari Lowassa ameshaanza mazungumzo ya chini chini na viongozi wa UKAWA lakini bado hawajafikia makubaliano rasmi.

By: SUPU YA MAWE

UKAWA wasimkatae akija kama mwanachama au kugombea jimbo la Munduli lakini si cheo cha uraisi. Kwa nini aje mwisho kisha apewe ugombeaji wa uraisi? Maana yake shida yake ni urais walasi upinzani! Alikuwa na nafasi nzuri sana muda wote kuingia upinzania hawezi tena. Pili hana jipwa Lowasa, alisha zeeka apumzike huyu.
 
Last edited by a moderator:
Vyovyote itakavyokuwa Lowasa bado anabaki kuwa mwanasiasa mwenye nguvu sana ndani ya nchi yetu kwa sasa. mtaji wa watu (social capital):confused2: alionao kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii hivyo hata akienda ukawa na asilimia nyingi za kushinda.
 
Turufu ya EL ni moja kuanika ukweli kabla ya May 2015 kuhusu Richmond na iwe inam implicate JK, atawin. UKWELI TUPU
 
ukiona mtu anamsifu mtu mchafu kama Lowassa ujue yeye ni mchafu zaidi raisi ajaye chaguo la watanzania ni DR Slaa pekee yake hana skendo za wizi kama ccm
 
Nashangaa watu wanavyomnadi EL huyu hawezi kuwa rais wa Tanzania pamoja na njugu zote anazomwaga, watakula na kuvimbiwa kama JK alivyovimbiwa wizi kwa miaka 10 iliyopita. Hana jipya. wakuu endeleeni kufaidi hizo njugu kutoka Voda phone hazina mwenyewe. Kiini cha kuvuruga shirika la simu Tanzania.
 
Nashangaa watu wanavyomnadi EL huyu hawezi kuwa rais wa Tanzania pamoja na njugu zote anazomwaga, watakula na kuvimbiwa kama JK alivyovimbiwa wizi kwa miaka 10 iliyopita. Hana jipya.

Duh! Umenichekesha sana mkuu, hasa huyo aliyevimbiwa kwa miaka kumi. Umetisha sana.
Ova
 
Nashangaa watu wanavyomnadi EL huyu hawezi kuwa rais wa Tanzania pamoja na njugu zote anazomwaga, watakula na kuvimbiwa kama JK alivyovimbiwa wizi kwa miaka 10 iliyopita. Hana jipya. wakuu endeleeni kufaidi hizo njugu kutoka Voda phone hazina mwenyewe. Kiini cha kuvuruga shirika la simu Tanzania.

Lowasa atahangaika sana lakini uraisi utakuwa ndoto kwake
 
Back
Top Bottom