1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,336
- 8,061
sisi hatutaki
SUPU YA MAWE: Huko kwetu supu ya mawe ni pombe haramu ya chang'aa!
On a serious note, tafuta thread yangu yenye title "Ndoto ya matumaini ya Lowassa kuishia CC ya CCM"
Mpaka sasa hivi mikakati ya CCM ni kukata jina la Lowassa kwenye CC ya CCM. Vigunge wa CCM na hasa Mwenyekiti wao hawataki kabisa Lowassa awe next Rais wa JMT, kwasababu hawajui Lowassa atamfanya nini JK na Ridhwani baada ya kumtosa kwenye sakata la Richmond.
Mkulu alikwisha mwambia Lowassa aachane na ndoto ya Urais, lakini Lowassa akamwambia kwamba ni haki yake ya kikatiba hivyo amuache demokrasia ichukue mkondo wake ndani ya CCM, halafu Watanzania tutaamua.
Lakini pia baada ya muungano wa UKAWA kwa wale wachache wanaoipenda CCM, wanaona itakuwa ni mlima mkubwa kumnadi Lowassa mbele ya UKAWA kutokana na kashifa za ufisadi zinazo mzunguka. Zile zama ambapo mgombea wa CCM alipokuwa anapitishwa na mkutano mkuu wa CCM tayari ni Rais wa JMT zimepita.
Aidha pia kuna swala la afya ya Lowassa. It is un deniable true, kwamba afya ya Lowassa sio "NZURI" sana. Je, kama Lowassa atachaguliwa kupeperusha bendera ya CCM ataweza about four months grueling za kampeni? Na hasa wana CCM hao wakirejea matukio ya kuanguka kwa JK, ambaye relatively ana afya "nzuri" kulinganisha na Lowassa, tena mbaya zaidi kwenye kampeni zenye ushindani mkubwa katika historia ya nchi hii, ambapo sasa vyama vya upinzani vyenye nguvu vimeungana kuunda UKAWA.
CCM is now on DILEMA, wanataka kum contain Lowassa kwani akitoka CCM is a double edged sword to CCM, hata kama hatagombea URAIS kupitia UKAWA, lakini Lowassa akitoka CCM ndiyo hivyo CCM wanakipa a kiss good bye kiti cha URAIS wa JMT. Lowassa anafahamu hilo, CCM wanafahamu hivyo.
Mpaka sasa CCM wametegeneza mkakati mmoja, watapandikiza wagombea mamuluki wa nafasi ya rais, ili CC ya CCM itakapokata majina, yawe mengi including jina la Lowassa. Ili kama baadaye Lowassa atalalamika, ionekane hoja yake haina mashiko bali uroho wa madaraka, kwani CCM watakuja na propaganda mbona majina yaliyokatwa ni mengi tu, kwanini yeye Lowassa tu ndiye alalamike kama sio uroho wa madaraka. Akina Nape tayari wameshaandaliwa kwa kazi hiyo.
Kulingana na Katiba ya CCM, CC ya CCM itapendekeza majina yasiyozidi matano kwenda NEC ya CCM kupigiwa kura kwa waombaji wa nafasi ya URAIS. Majina matatu ya kwanza yatakayoshika nafasi ya juu kwenye kura za NEC yatapelekwa mkutano mkuu kupigiwa kura, kumpata mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM.
Hakuna vigezo vya wazi vinavyofahamika ambavyo CC ya CCM hutumia kupendekeza majina yasiyo zidi matano kwenda NEC kupigiwa kura. CC ya CCM ndiyo litakuwa the last nail on the coffin of Lowassa, kwani jina lake na majina mengine ya wana CCM wengi wao wakiwa waliopandikizwa yatapokatwa.
Mpaka sasa hivi majina yatakayopendekezwa na CC ya CCM ili priority order ni kama ifuatavyo
- Mizengo Kayanza Pinda (sitting PM)
- Prof Mark Mwandosya (alifanya Vizuri nyuma ya JK kwenye uchaguzi wa 2005)
- Jina moja la Mzanzibari (kudumisha muungano, bado jina hilo halijakubaliwa yapo 3 yanayotajwa)
- Dr. Asha Rose Migiro (gender balance, Prof Tibaijuka alikuwa awe mmojawapo lakini nafikiri sasa sakata la escrow limemtupa nje)
- ........................... (??) Hili bado ni kitendawili linajumuisha wana CCM wengi eg, Mwakyembe, Sitta, Membe, Magufuri, Nahodha, Karume Jnr,Wassira, Makamba Jnr etc lakini Lowassa si miongoni mwao. Hili jina litachaguliwa kutokana na upepo wa kisiasa wakati huo.
Naomba kuwasilisha
ndio tunataka
Lowasa hafai urais(tuwe waungwana na wakweli tu).
Na muarobaini wake ni huyu Mzee! Nasikia amekonga nyoyo za watu na amebomoa karibuni kambi zote!
Sio Lowasa ambaye hafai bali CCM haifai kuendelea kutawala.
Kama mnabisha basi endeleeni kuishabikia CCM na kumpata rais wa awamu ya Tano toka CCM muone kama amani ya hii nchi itadumu chini ya Katiba pendekezwa na waroho na walafi wa CCM.
Kikwete alijitahidi kuwa rais wa watanzania wote na kutaka kuwaletea watanzania katiba bora na usawa bila kujali udini ,ukanda na ukabila lakini hofu ya Chama cha Lusifa CCM ikaibuka na kuvuruga nia njema ya Kikwete na kumgeuka Jaji Warioba pamoja na watanzania waliotaka kuweka misingi bora ya Taifa hili kwa vizazi vijavyo.
CCM wameua misingi ya uwazi na Uwajibikaji na hakuna yeyote ndani ya CCM anayeamini katka uwajibikaji na sheria ya maadili. Kiongozi bora toka CCM ni yule anayeweza kuwagawa watanzania kulingana na dini zao.
Leo umaarufu wa Pinda ni kwa kuwa ni Mkatoliki na sio utendaji wala uadilifu.Lengo ni kupunguza kura za Dr.Slaa kwa kuwahadaa watu kuwa Slaa ni Padri hivyo waislam wasimchague.
Tumeona jinsi Pinda alivyomshawishi Mkurugenzi wa Benki ya Mkombozi ili kutakatisha fedha haram na kutoa sadaka ya fedha haram kwa kiongozi wa dini.
Mpaka sasa hatujasikia tamko lolote toka Baraza la maaskofu Katoliki kuhusiana na uchafu ulioasisiwa na Pinda akishirikiana na Kilaini kupaka matope Kanisa na taasisi yake ya kifedha iliyoonyesha jinsi kanisa hilo linavyotumia ukubwa wake kuhujumu uchumi wa taifa hili na kuwatumia BAKWATA kama chambo cha kuwapooza waislam huku mfumo mbaya ukiendelea kutawala.
Raisi wa nchi anachaguliwa na kakamati ka watu wachache ndani ya CCM.Fomula inayotumika ni ile ile ya zamu ya Wakatoliki na zamu ya waislam watakaoikumbatia BAKWATA.
Wakati umefika sasa kwa UKAWA kuja na sera bora zitakazoimarisha utaifa wetu na kupata viongozi bora wenye maono mapana zaidi. Tuwajenge watanzania kwenye misingi bora ya kuwapata viongozi kwa sera na uwezo.