Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Kutokana na vyama vyote vinavyounda UKAWA kuamini wanamgombea wa kupeperusha bendera ya urais,nashauri wamtafte mtu ambae si CDM,CUF,NLD wala NCCR ila wamvizie lowasa akikatwa jina lake CCM. E.L atatupa ushindi 90% kwa sababu anakubalika na watanzania walio wengi.vyama hivi vinavyounda ukawa vijadiliane kutafta mgombea mwenza kama ni lipumba,slaa au yeyote wanaemwamini anauzika pia kwa wananchi..ni hayo tu.
UKAWA tegemeo la watanzania
 
Kutokana na vyama vyote vinavyounda UKAWA kuamini wanamgombea wa kupeperusha bendera ya urais,nashauri wamtafte mtu ambae si CDM,CUF,NLD wala NCCR ila wamvizie lowasa akikatwa jina lake CCM. E.L atatupa ushindi 90% kwa sababu anakubalika na watanzania walio wengi.vyama hivi vinavyounda ukawa vijadiliane kutafta mgombea mwenza kama ni lipumba,slaa au yeyote wanaemwamini anauzika pia kwa wananchi..ni hayo tu.
UKAWA tegemeo la watanzania

Ni vema ungeshauri Lowasa atinge UKAWA kwa kujiamini kuliko kusubiri kuombwa
 
Shaka na EL bado iko palepale, alijihuzuru kulinda serikali na CCM isianguke, sio kulinda maslahi ya wananchi, hivyo alisaliti wananchi, hii iko kwenye hotuba yake ya kuachia ngazi. Ni msaliti fulani huyu wa UMMA, ndo maana ataungana na ZZK katika orodha ya wasaliti TZ
 
Joto kuelekea uchaguzi mkuu 2015 linazidi kupanda. Kati ya mtu anayetajwa sana kugombea katika nafasi ya urais ni Edward Lowassa. Pamoja na tafiti nyingi rasmi na zisizo rasmi kuonesha kuwa EL anaongoza kwa kuaminiwa na kupendwa na watanzania wengi, CCM inaonekana kwa siri na kwa dhahiri kutokumhitaji Lowassa. Na kwa kuwa Lowassa anataka kuwatumikia watanzania na watanzania wanamhitaji yeye.. Ni ushauri wangu kuwa, kama CCM wakimzingua abadili uelekeo na kuelekea UKAWA ama Chama kingine chochote. Nina imani EL atashinda 2015 iwe kupitia CCM, ukawa ama Chama kingine chochote.
kwanini wamzingue?nani anaweza mzengua master wa chase ktk ccm
 
Wakati Yeye Akijipanga Na Critics Wake Nao Wanajipanga ktk Kumwangusha Na Kwa Taarifa Nilizonazo Tena Za Ndani Jikoni Ni Kwamba Piga ua Rais Ajaye Wa Tanzania Ni Kati Ya Watu Hawa :

1. Sospeter Muhongo.....15%
2.Stephen Wassira.....20%
3. Jaji Augustino Ramadhani.....5%
4. John Magufuli.........60%

Makamu Wa Rais Iwe Isiwe Amepangwa Kuwa Mzee Samuel Sitta

Waziri Mkuu Ni Kati Ya Hawa Wafuatao:

1. Asha Rose Migiro ( Ila Kama Atagombea Ubunge Na Kushinda )....5%
2. Mark Mwandosya ( Ila Kama Atathibitisha Sumu Ile Imemtoka )....5%
3. Hussein Mwinyi..........70%
4. Harrison Mwakyembe......20%

NB. Endapo Hii Itabadilika Basi Mjue 100% UKAWA Wanashika Hatamu Na Padre Wangu Wilbroad Slaa Kuwa Rais Wangu Mpya.
Kwa katiba ipi? Maana kwa katiba iliyopo Rais na makamu wote haiwezekani watoke upande mmoja wa Muungano na pia Waziri Mkuu ni kiongozi Mkuu wa Serikali juu ya masuala ya Tanzania bara (Tanganyika), hivyo hawezi kutoka Zanzibar kwa katika ya 1977.
 
Wakati Yeye Akijipanga Na Critics Wake Nao Wanajipanga ktk Kumwangusha Na Kwa Taarifa Nilizonazo Tena Za Ndani Jikoni Ni Kwamba Piga ua Rais Ajaye Wa Tanzania Ni Kati Ya Watu Hawa :

1. Sospeter Muhongo.....15%
2.Stephen Wassira.....20%
3. Jaji Augustino Ramadhani.....5%
4. John Magufuli.........60%

Makamu Wa Rais Iwe Isiwe Amepangwa Kuwa Mzee Samuel Sitta

Waziri Mkuu Ni Kati Ya Hawa Wafuatao:

1. Asha Rose Migiro ( Ila Kama Atagombea Ubunge Na Kushinda )....5%
2. Mark Mwandosya ( Ila Kama Atathibitisha Sumu Ile Imemtoka )....5%
3. Hussein Mwinyi..........70%
4. Harrison Mwakyembe......20%

NB. Endapo Hii Itabadilika Basi Mjue 100% UKAWA Wanashika Hatamu Na Padre Wangu Wilbroad Slaa Kuwa Rais Wangu Mpya.

Hv kwani M'kyembe yeye ile sumu ilishamtoka kwani!
 
Uliyeleta mada ni mkereketwa wa ACT.Kwa taarifa yako,Ukawa haiitaji mtu anayeitwa mamvi.Kumkubali mtu mzee huyu ndani ya ukawa ni kama kuchambia mfuko wa Rambo.
Balale mkuu, mimi ACT na ushabiki wa siasa za vyama niliziacha kitambo saaana. Mimi siku hizi nipo na mtu. Na ndio maana kama umeisoma vizuri thread yangu nimemshauri Lowassa akiona CCM inamzingua, ahamie UKAWA au aende Chama kingine chochote. Nina imani, watu watamfuata huko huko atakapokuwa
 
Unawezaje kumshabikia na kumzungumzia mwizi!?.Kuliko huyo jamaa bora hata ya Wasira kwa ma CCM.
 
WAZIRI mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameanza kuwaandaa wafuasi wake kwa uwezekano wa kujiunga na mojawapo ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Raia Mwema limeelezwa.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata kutoka katika kambi ya mgombea huyo zinaeleza kuwa amepiga marufuku mazungumzo yoyote ya kutafuta mbadala wake ndani ya CCM na kutaka nguvu yote ielekezwe kwake.

Gazeti hili limeelezwa kuwa wapo watu walio ndani ya kambi yake wanaoamini kwamba anahitajika mwanasiasa mwingine ndani ya kundi hilo ambaye anaweza kuvaa viatu vya Lowassa endapo CCM itaamua kumkata au kuendeleza adhabu yake ya kutofanya shughuli za siasa aliyopewa na chama chake.Hata hivyo, kundi hilo linadaiwa kuwa na wakati mgumu kwa madai kwamba Lowassa hataki kusikia chochote kuhusu suala hilo.

"Anasema yeye ndiyo Plan A, Plan B na Plan C. Kama, kwa sababu yoyote ile, CCM itaamua kumpitisha mgombea mwingine na si yeye, yuko tayari kujiunga na Ukawa lakini si kubaki ndani ya chama."Hili ndilo jambo linalotusumbua sana kwa sasa. Hakuna vita ambayo ina mpango mmoja tu. Lazima muwe na mpango zaidi ya mmoja. Huku Pwani wanasema ukienda kuteka maji wakati wa ukame, ni muhimu uwe na ndoo na kidumu cha kushika mkononi.

"Kwenye kutembea na ndoo mtu unaweza kujikwaa na maji yote yakamwagika na kile kidumu cha mkononi ndiyo kikakuokoa. Sasa huyu bwana hataki kusikia habari ya kidumu. "Anataka twende kutafuta maji na ndoo moja tu ambayo ni yeye. Hili linatupa shida kidogo kwa sasa," alisema mbunge mmoja wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni mtu wa karibu na mtarajiwa huyo.

Katika kambi ya Lowassa, kuna majina ya wanasiasa vijana ambao wanatajwa kuwa tayari kuvaa viatu vyake endapo CCM itaamua tofauti na matarajio yao. Miongoni mwa wanasiasa wanaotajwa kuwa katika kambi ya Lowassa na ambao kambi inayotaka Plan B inawapendekeza ni Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

Miongoni mwa wanaotajwa, Dk. Nchimbi anaelezwa kuwa na nguvu zaidi kutokana na ukweli kwamba ndiyo mwenye ushawishi zaidi ndani ya chama kutokana na ukweli kuwa amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwa zaidi ya miaka 10. Kimsingi, kwa upande wa Tanzania Bara, hakuna mwana CCM aliyedumu katika Kamati Kuu ya chama hicho kwa muda mrefu kuliko Nchimbi miongoni mwa waliomo sasa, ukimwondoa Rais Jakaya Kikwete.

Anasema Mbunge huyo: " Tunajaribu kumshawishi Lowassa akubali kuwa akikosa yeye, basi apatikane mtu ambaye ataweza kuyafanya yale aliyopanga kuyafanya kupitia CCM. Kwa sasa, hili hajakubaliana nalo," kilisema chanzo hicho cha gazeti hili ambacho hakikutaka kuwekwa jina lake wazi. Hata hivyo, kwa vile Ukawa si chama cha siasa, kama Lowassa ataamua kuhama CCM, ni lazima ajiunge na mojawapo ya vyama vinavyounda Ukawa ambavyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na National League (NLD).

Akizungumzia taarifa hizo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kwa sasa hawataki kujihusisha na mambo ya ndani ya CCM na badala yake wanaangalia namna ya kukishinda kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
"Sisi sasa hivi lengo letu kubwa ni kuijenga Ukawa kitaasisi na kuifanya iwe tishio katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

"Kamanda, sitaki kuzungumza kama tutampokea au hatutampokea Lowassa kama akiamua kuhamia Ukawa. Mambo ya CCM waachie CCM wenyewe. Mimi nakuhakikishia kuwa wakati wa uchaguzi ukifika; CCM wamweke Lowassa, au Membe, sijui Makongoro Nyerere ama yeyote mwingine, Ukawa itashinda tu kwenye uchaguzi huo," alisema Mbowe kwa kujiamini.

Juhudi za kuwapata wenyeviti wenza wengine wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia na Emmanuel Makaidi hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni juzi Jumatatu. Kwa sasa, Lowassa na wanasiasa wengine watano ndani ya CCM wako katika kifungo cha muda usiojulikana walichowekewa na chama chao kutokana na madai ya kukiuka taratibu za chama hicho.
Wanasiasa wengine walio katika kifungo hicho ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira; Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe; Ngeleja na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.Ilivyokuwa chaguzi mbili zilizopita.


Chanzo: Rai Mwema
 
Back
Top Bottom