Wewe unachokifanya hapa ni kuwa blackmail ccm wampitishe LOWASA tu na wala huna lolote. Lowasa hakubaliki UKAWA. Na kwa uroho wake wa madaraka alionao, si ajabu kweli jamaa likahamia chama kingine ili ligombee uraisi. Huu ni wehu.
UKAWA WAKIMSIMAMISHA LOWASA, SISI HATUWAPI KURA. Hatuwezi kupoteza muda wa kupigia kura fisadi lilokubuhu eti kwa kuwa kuna wajinga kadhaa wanalipigia kampeni.
Ninaimani kwa usafi na umakini wa UKAWA, hawawezi kufanya kosa kubwa kama hilo. UKAWA kumsimamisha fisadi lowasa ni kuwasaliti na kuwatukana Watanzania nchi nzima waliosimama macho yao yakiwa UKAWA huku wakiwa wamefungamanisha mikono yao pamoja!.
Na wewe mleta mada usirudie kuwaelekezea UKAWA mifereji ya maji machafu!. Hayo yamalizeni huko huko ccm.