Mgomo wa madaktari - Updates

Mgomo wa madaktari - Updates

:A S 465:I wish mgomo ungeliendelea hadi 2015 ili magamba wakose cha kujitetea kwa wananchi. wakimaliza madaktari waalimu, wauguzi, wafanyakazi wa reli, nk.
Waswahili walituasa kuwa "KIBURI SI MAUNGWANA" sasa kiburi cha JK kutomuwajibisha Mponda na naibu wake, vifo kwa watz.:eyebrows:
 
Habari nilizozipokea sasa hivi kwa njia ya SMS kutoka kwa doctor mmoja pale Mhimbili zinasema hivi,nanukuu,"Hii ya sasa ni bab kubwa responce ni 100% MPAKA EMERGENCY,intern ndio wamemaliza kikao chao cha kupeana moyo na specialist ndio wanaanza Russian culture nw..together we can make it" mwisho wa kunukuu sms niliyoipokea.

My take; hivi serikali ina shindana na madaktari kwa ajili ya maslahi ya kisiasa? au inatakiwa kulinda afya za wananchi wake?
Maana kama mawaziri wamelalamikiwa na ni kweli wameshindwa kuwajibika kwa nini waendelee kuwepo hapo?na je inawezekanaje kupokea malalamiko ambayo kimsingi wao ndio wanalalamikiwa na kisha wakayafanyia kazi?
Nawasilisha wadau

rais hawezi give up kirahisi namna anapgopa kuzarauliwa make akiwapiga chini kesho walim nao watataka minister wao ajiuzulu then; wafanya biashara, uchukuzi etc ila sie wa kipato cha chini tukubali tu yaishe
 
rais hawezi give up kirahisi namna anapgopa kuzarauliwa make akiwapiga chini kesho walim nao watataka minister wao ajiuzulu then; wafanya biashara, uchukuzi etc ila sie wa kipato cha chini tukubali tu yaishe
ufinyu wa kufikiri....
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

Hilo ndo tatizo la watu weengi badala mtibu tatizo mnakimbilia kusema migomo inasababishwa na vyama vya siasa hebu tutajie chama gani ndo kinahamasisha madr wagome!muwe mnatafuta solution ya matatizo na sio kukimbilia kusingizia vyama vya siasa.
 
madaktari mnataka tufe mfaidi nchi? Tutaweza kweli kuwapa kila mtakachokitaka? Wekeni utu mbele mtupe huduma
 
Sikuwahi kuhisi kuwa Mponda na Nkya wanagharama kubwa hivi serikalini mpaka JK aliponionyesha.....
Kama JK ndiye amewakatalia kujiuzulu basi amewaondolea utu na heshima mbele ya Watanzania na jumuiya ya wasomi Duniani. Nani atawaona ni watu tena? Nani atawaheshimu?
 
Kuna Mitanzania mingine ina wivu wa Kike (Mkapa) na inawaonea wivu Madaktari wetu kwa kuiendesha Serikali yetu na kuinyima usingizi. Hii haijawahi kutokea kwa Serikali ya CCM ukiacha wale Machalii walitaka kumuua Nyerere na kumpindua enzi za akina Ngaiza sijui na yule Comandoo aliyeuawa.

Kama Madaktari hawataki kufanya kazi kwani ni lazima?

Nchi huru hii na hakuna anayesema Rais analazimishwa kumfukuza Waziri wa Afya kazi.

Hapa mambo yako wazi, au Madaktari warudi kazini au Waziri na jamaa zake watemwe kwenye vyeo vyao.

Mbona hamuwashupalii hao watu wanaokataa kuachia ngazi? Sisi pia hatuwashupalii. Poleni mtakaofiwa katika hii vita na poleni mtakaoteseka katika hii vita. Ukishakufa, hata kama maiti yako itatupwa kama Umbwa na kusahauliwa palepale kama vile huna ndugu (Makassy) basi wala hujali maana mwili umebaki pekee na Roho imeshajiondokea.

Mnaowaonea wiFu Madokta, haki ya nani mchukue tu Kamba, ila ziwe nene za kutosha na imara pia - MJINYONGE.
 
Hivi kiapo chao si ni kulinda maisha???? Sasa unalinda maisha ya wagonjwa kwa kuwaacha wafe? So kama Serikali haiwasikilizi, nani aanaathirika na mgomo huu, ni viongozi wa serikali kweli? Huyu Jack and Jill kakosa nini? Shame on you. Mwogopeni Mungu aliyewapa talanta yake na nyinyi mnaifukia!
Hivi talanta anayo daktari tu? Mafisadi wao ndio wana talanta ya kuiba tu ndio maana wanaiba kila siku huku tukikaa kimya kwa kuwa wanatimiza wito wao?
 
Kinachonishangaza ni jinsi ambavyo watu humu ndani wanona kuwa Madaktari wana haki kwa kila wanachokisema. Tunajua umuhimu wao katika jamii lakini wao wasijione kuwa bora kuliko watumishi wengine serikalini. How do you demand kwamba Waziri lazima aondoke na unataka kweli aondolewe? This is holding the government at ransom. walitaka Mtasiwa na KM waondoke wakaondoka, tena masikini KM akampoteza mama yake in the process. Ndugu zangu Madaktari, mgomo si suruhisho la kila kitu. Hebu fikiria roho za maskini wangapi wanakufa kwa sababu ya migomo yenu. Hamna hata Kwaresma nyinyi? Hiki mnachokifanya ni kwa manufaa ya nani kama sio nyinyi na matumbo yenu? Mna tofauti gani na mafisadi? I hate ufisadi lakini hili mnalolifanya ni well out of control and I will never support this. Doctors must be declared as enemy number one of the common mwananchi! Mkielezwa mnaanza kubwaga matusi humu, well sishangai kwani kama mnaruhusu watu kufa mahospitalini ili mifuko yenu itune, then matusi is just a drop of water in the indian ocean. As we stand, Doctors wanalipwa kuliko cadre yoyote serikalini; mnataka mlipwe kama wabunge????? For this one, doctors you sack!!!
How much?
 
taarifa zilizonifikia kutoka vyanzo vya kuaminiaka bugando wamebandika tangazo likisomeka hivi

"kutokana na serikali kutokuwa tayari kushughulikia madai ya madaktari ipasavyo sisi madaktari tumesikitishwa sana. Kuanzia leo tarehe 7 machi 2012 saa 2; 00 asubuhi,madaktari wa hospitali ya bugando tunasitisha kutoa huduma zote mpaka hapo serikali itakaposhughulikia madai hayo.
Jumuiya ya madaktari bugando (intern,registrars,residents)
nakala kwa wakuu wa idara,utawala bmc"

muhimbili
emd-kitengo cha wagonjwa wa dharura kimefugwa

opd-wagonjwa wamejaa lakini hawaoni

thetre hazifanyi kazi na maspecialist wapo russian culture to put last nail in the coffin

amana
total tools down

temeke
total tools down

mbeya
wanaendelea pale walipoishi maana mgomo kama kawa

ifakara
total tools down

kcmc
madaktari kutoa tamko muda si mrefu

ikulu kuna mkutano mkubwa unaendelea nitato updates bdae

mungu wangu!!!!!!!!
 
Mob psychology ime wa-affect madaktari wetu. Natoa ushauri kila mmoja atafakari ni nini anachogomea hasa kama yeye binafsi bila kutegemea vikao vyao wanavyokaa kupeana molali! Kama ni maslahi yake hayajatekelezwa au ni kuto kujiuzuru kwa mawaziri au vyote viwili. Na ukiangalia dai la kuto kujiuzuri/kutowajibishwa mawaziri imemeza madai yao yote ikiwemo ya masilahi yao. Sasa wawe makini katika madai yao wasije wakawa wanatumiwa na kundi fulani bila kujijua? na hii ndio madhara ya mob psychology. Nawashauri waonane na wataalam wapate ushauri?

Divide and rule method. Nadhani mbinu imegonga ukuta.
Nenda kajipange upya. Uje kivingine!!
 
Mara tu baada ya uchaguzi mkuu kumalizika na Jakaya kuingia Ikulu, chama fulani cha siasa kilitangaza kwamba kitahakikisha nchi yetu haitawaliki tena. Hivyo sintashangaa kuona haya yanayotokea. Lakini wanaokufa kwa kukosa huduma za madaktari si CCM pekee yetu bali Watanzania wote.

Mkuu emu uwe clear kidogo. Je hicho Chama ndicho kipo nyuma na haya mamigomo?? Je hicho chama ndicho kinaiba madawa, vitanda na vifaa vya mahospitali?
 
Ina maana hili suala la madaktari halina ufumbuzi?
 
well well well..........nitapenda kuona reaction ya serikali kwenye hii dhahma...........
 
Back
Top Bottom